Dr Slaa Tafadhali Kutana na Maalim Seif

ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,543
550
Najua CUF na Chadema ni vyama tofauti sana na vyenye malengo tofauti. Hata hivyo ukweli ni kwamba Chadema tunawahitaji sana CUF kwa ajili ya kufanikisha mambo mengi. Kwanza ni swala la katiba, CUF wameshika sehemu nyeti maana bila wao katiba haiwezi kupita maana wana zaidi ya 1/3 ya bunge la katiba na referandum pia. Ila kuna mambo chadema na cuf wanakubaliana na hasa serikali tatu na tume huru ya uchaguzi. Pia pamoja na tofauti zilizopo, tunaweza kukubaliana na CUF wao wakatoa mgombea mwenza uchaguzi ujao. Bado ccm wana mbinu za kushinda hivyo umoja ni muhimu sana. Namshauri Dr Slaa baada ya uchaguzi wa uzini akutane na Seif kuangalia uwezekano wa kushirikiana angalao kwenye katiba. Nadhani ndugu zangu mnaona busara kwa hili, nadhani Dr Slaa ataona busara ya ushauri wangu
 
Sikubaliani na hoja yako. Chadema iendelee kusimama kama Cdm. CUF ni mwali wa mtu tukijiunga nae ni sawa na kujiunga na Magamba. Untaka tuwe wake wenza? Kamwe hatupikiki chungu kimoja na CUF. Waliyotufanyia ni mengi na mabaya ysiyosahaulika. Mara ngapi wametutukana bungeni hadi kutoa tafsiri ya neno Tundu? Nasema CDM wakiungana na CUF mi najitoa kwenye chama nibaki mtanganyika huru asie na chama.
 
Mimi ni mwanachadema damu ila siasa hazipo hivyo, Cuf ni adui lakini kama unaweza kumtumia wakati wa shida hakuna tatizo ndio siasa zilivyo. Tutaihenyesha sana CCM kwenye katiba tukisimama na CUF maana wao wana nguvu kuliko chadema kwa maana ya katiba . Wao kwa kule znz hakuna kinachoweza kufanyika bila wao maana watahitaji 2/3 wa wazanzibari. Tukizungumza nao kuna baadhi ya mambo tutakubaliana na tusimame nao dhidi ya ccm. Kama chadema imekubaliana na ccm kuhusu mswada nini kitatushinda kukutana na kukubaliana na cuf kuhusu mambo fulani?
 
Najua CUF na Chadema ni vyama tofauti sana na vyenye malengo tofauti. Hata hivyo ukweli ni kwamba Chadema tunawahitaji sana CUF kwa ajili ya kufanikisha mambo mengi. Kwanza ni swala la katiba, CUF wameshika sehemu nyeti maana bila wao katiba haiwezi kupita maana wana zaidi ya 1/3 ya bunge la katiba na referandum pia. Ila kuna mambo chadema na cuf wanakubaliana na hasa serikali tatu na tume huru ya uchaguzi. Pia pamoja na tofauti zilizopo, tunaweza kukubaliana na CUF wao wakatoa mgombea mwenza uchaguzi ujao. Bado ccm wana mbinu za kushinda hivyo umoja ni muhimu sana. Namshauri Dr Slaa baada ya uchaguzi wa uzini akutane na Seif kuangalia uwezekano wa kushirikiana angalao kwenye katiba. Nadhani ndugu zangu mnaona busara kwa hili, nadhani Dr Slaa ataona busara ya ushauri wangu

Ibange bwana wewe mawazo yako mkuu duh.KAFU wanaitaka Pemba yao na wala si Zanzibar sasa tukaseme nawatu wanataka wilaya iitwe Nchi ?Watu wa jino kwa jino ?
 
@ibange. waache CUF siku ikifika wao wawe wa kwanza kuitafuta CDM. hawa jamaa agenda zao zinaishia Zanzibar na zaidi Pemba.
 
Wakuu hakuna adui wa kudumu wala rafiki wa kudumu kwenye siasa ila tunaweza kumtumia adui kupata maslahi ya kudumu na sio sasa tu! Hata tukifanikiwa kuchukua dola bado tunaweza kuangalia vipaumbele kadha wa kadha kwa ajili ya mustakabali wa chama na taifa bila kutanguliza uadui wameweza usa ,obama VS hillary during the presidential campaign but walikuja kuwa obama AND hillary kwenye suala muhimu kwa ustawi wa america!! Tukija kumpata na mh lipumba akiwa clean tusimuache pia! Naunga mkono hoja!!
 
CUF wadini sana, wanataka jamhuri ya Kiislam ya Pemba, CDM wanataka jamhuri ya umoja na mshikamano ya Tanzania chini ya serikali 3. Sasa kujichanganya na KAFU ni sawa na kuweka ndimu kwenye maharage
 
CUF wadini sana, wanataka jamhuri ya Kiislam ya Pemba, CDM wanataka jamhuri ya umoja na mshikamano ya Tanzania chini ya serikali 3. Sasa kujichanganya na KAFU ni sawa na kuweka ndimu kwenye maharage

Yaani unanikumbusha gazeti lao la Mzalendo jinsi lilivyo na udini. Tuwe makini sana na hawa wajamaa wanavyosema ni wanachama wa CDM si kweli na kwa nini wanataka Dr Slaa amtafute Sefu amwambie nini? Sasa tunaanza kupata majibu ya kwa nini Lipumba amekimbia, kumbe alisoma nyakati akajua Kafu kwisha kazi.
 
CUF wadini sana, wanataka jamhuri ya Kiislam ya Pemba, CDM wanataka jamhuri ya umoja na mshikamano ya Tanzania chini ya serikali 3. Sasa kujichanganya na KAFU ni sawa na kuweka ndimu kwenye maharage

Islamophobia ni ugonjwa hatari
sana. Ugonjwa huko siku nyingi
sana ila kwa miaka ya hivi
karibuni umekuwa ukikua kwa
kasi ya ajabu sana. Aliyeathiriwa
na ugonjwa huu huwa anaogopa UISLAM na vitu vyote
vinavyohusiana na UISLAM.
Mfano, mtu anayeumwa
ISLAMOPHOBIA akiona mtu
amevaa kofia ama kanzu ama
hijabu, mtu huyu huwa anaogopa sana na huwa anateseka sana
katika nafsi yake. Au mgonjwa
wa islamophobia akisikia kuwa
waislam wanataka kuanzisha
mahakama ya kazi basi yee
huwa hapendi na maumivu humsonga moyoni mwake.
Wagonjwa wa islamophobia
huwa hawapendi kuona uislam
ukienda mbele ama sharia za
kiislam zikifuatwa.
Mengi kuhusu ugonjwa wa ISLAMOPHOBIA soma hapa: 1. Islamophobia - Wikipedia, the free encyclopedia (kiswahili soma hapa: Google Tafsiri)
 
usiku mwema.

kuungana au kushirikiana sio lazima kukutana na kukaa pamoja busara na hekima ndio vinahitajika kwamba yale mambo ambayo CUF wanayasimamia na CDM wakiona na kuhakikisha ni kwa maslahi ya watanzanania na hayakiuki sheria na muongozo wa chama wanaweza kuyaunga mkono kadhalika na CUF hivo hivo ila hili la kukaa na kuzungumza ni gumu kidogo kwa kuwa CUF tayari wapo kwenye coalition government na ccm so kukubaliana na cuf automatically ni kukubliana na ccm, mbona uchaguzi uliopita cdm walisimama wenyewe bado wkashinda viti vingi?? mbona Igunga cuf waliinga cdm hadharani na kwa nguvu zote lakini bado cdm ikashika nafasi ya pili so cdm fight alone!
 
umefikiri vyema rafiki yangu lakini ni lazima uweze kuifahamu cuf ya seif vizuri kama uinataka kushirikiana nao.kwanza n unapaswa kukumbuka kuwa cif na ccm waliwazomea chadema na kuwatukana wakati walipotoka njee ya ukumbi wa bunge kupinga madudu ya sheria ya mabadilko ya katiba mpyaa.hii inaonyesha kuwa kwa kujua au kutokujua cuf wamewekwa makwapani kwa ccm wakiwatumukia na kupewa mkate wao wa kila siku hivyo siaminim kama wapinzani wenye malengo wanaweza kushirikiana na cuf.hata suala la mgombea mwenza haliwezekani kwani cuf wanadaiwa kukubali matokeo ya uraisi mapema kabla hayajatangazwa ilimradi tuu wapewe umakamu sasa watu wa aina hiyo huwezi kushirikiana nao,wao wanataka kipande cha slesi wakati wewe unataka mkate mzima.Naomba niwasilishe
 
Back
Top Bottom