Dr Slaa Tafadhali Kutana na Maalim Seif

kuungana au kushirikiana sio lazima kukutana na kukaa pamoja busara na hekima ndio vinahitajika kwamba yale mambo ambayo CUF wanayasimamia na CDM wakiona na kuhakikisha ni kwa maslahi ya watanzanania na hayakiuki sheria na muongozo wa chama wanaweza kuyaunga mkono kadhalika na CUF hivo hivo ila hili la kukaa na kuzungumza ni gumu kidogo kwa kuwa CUF tayari wapo kwenye coalition government na ccm so kukubaliana na cuf automatically ni kukubliana na ccm, mbona uchaguzi uliopita cdm walisimama wenyewe bado wkashinda viti vingi?? mbona Igunga cuf waliinga cdm hadharani na kwa nguvu zote lakini bado cdm ikashika nafasi ya pili so cdm fight alone!
Mimi nina nia njema kabisa. hakuna chama kimetopiga vita kama nccr. Kuna jamaa anaitwa sungura aliandika makala gazeti la rai akieleza kuwa ni afadhali ccm kuliko chadema, hayo ndio yalikuwa mawazo ya mbatia na mvungi. Lakini leo tumezungumza. Mimi nazungumzia hasa swala la katiba kuwa kushirikiana na cuf ili tupate nguvu kubwa ni muhimu. Kwani chadema tunataka nini zaidi tukipata tume huru ya uchaguzi, serikali ya tanganyika nk. Lakini ni ukweli kuwa bila cuf hatutaweza ku achieve haya na pia uzuri cuf wanakubaliana na chadema kuhusu haya. Kwa maana nyingine cuf wakiikataa katiba haitapita, chadema pia tunaweza kupata 1/3 tukaipinga ila wanaweza kuchakachua.

Msingi hasa wa hoja yangu ni kuwa chadema akiweza kuwa win cuf itawabidi ccm wa compromise mambo mengi ili katiba ipite, nadhani mmenielewa wandugu wapenzi
 
Dr. sii mtu wa kuburuzwa kiivyo, huyo sharf akiona inafaa asimamie maslai ya taifa ikimpendeza zaidi alinde ndoa yake. Chadema walipambana na CCM,na CUF bado wakashinda hivyo tunayo nafasi tutashinda kwenye haya mengine haipo shida. what is cuf after roo cuf inakufa muda sii mrefu.
 
Najua CUF na Chadema ni vyama tofauti sana na vyenye malengo tofauti. Hata hivyo ukweli ni kwamba Chadema tunawahitaji sana CUF kwa ajili ya kufanikisha mambo mengi. Kwanza ni swala la katiba, CUF wameshika sehemu nyeti maana bila wao katiba haiwezi kupita maana wana zaidi ya 1/3 ya bunge la katiba na referandum pia. Ila kuna mambo chadema na cuf wanakubaliana na hasa serikali tatu na tume huru ya uchaguzi. Pia pamoja na tofauti zilizopo, tunaweza kukubaliana na CUF wao wakatoa mgombea mwenza uchaguzi ujao. Bado ccm wana mbinu za kushinda hivyo umoja ni muhimu sana. Namshauri Dr Slaa baada ya uchaguzi wa uzini akutane na Seif kuangalia uwezekano wa kushirikiana angalao kwenye katiba. Nadhani ndugu zangu mnaona busara kwa hili, nadhani Dr Slaa ataona busara ya ushauri wangu
Kuunganisha nguvu ni suala zuri lakini kwa kutumia hoja ulizoziweka, nadhani ni wazo baya.
Suala la Katiba ni vema vyama vya siasa vikafanya lobying tu lakini tukaachiwa wananchi kuamua katiba tunayoitaka. Kama Vyama vya siasa ndivyo vitakaachwa viamue aina ya katiba inayiotakiwa, hatupata katiba itakayotufaa wananchi. Hivyo, kuunganisha nguvu za Chadema an CUF katika suala la katiba, ni kuwanyang'anya wananchi uhuru wao wa kujiandikia katiba wanayoitaka. Ni vema katiba hiyo isitokane na ushawishi kubwa wa vyama vya siasa.
Pili, mimi ninaamini katika chama kujiimarisha kama chama. Chadema, CUF,. CCM, NCCR, TLP, CCK au chama kingine chochote cha siasa kilipoanzishwa, kilikuwa na malengo yake, kikiamini kuwa sera zake na itikadi ndivyo vinavyofaa zaidi kuongoza nchi. leo hii inapotokea ukaona kuwa kumbe alicho nachio mwingine ni bora zaidi ya cha kwako hivyo njia bora ni kuungana naye, ni njia mojawapo ya kukiri kuwa kumbe zile sera na itikadi zako si mujarabu. kwangu mimi, vyama kuungana na namna ya kukiri udhaifu. Chama kama kinatakiwa kisimamie sera na itikadi zake na kijijenge chenyewe. Iwapo kitafanikiwa kufanya hivyo na kuchukua madaraka, kitakuwa chama imara sana.
lakini pia, pendekezo la Chadema kufanya kazi pamopja na CUF inapaswa litolewe pale tu ambapo mtu ataelewa sawasawa CUF ni nini na Chadema ni nini
 
naöndoa shilingi ktk hii hoja, cuf ni almarehemu cdm itajiungaje nayo? Mfano mzuri ni wakati wa mapitio wa marekebisho ya mswada wa kukusanya maoni cuf kwa kutambua nafasi yao(mke wa *******) hawakuongea hata mmoja
Waliacha wanaume tu wakazungumza, so jamani tuwaache huko jikoni.
gumza
 
Wakuu hapa pana utata sana. Unajua kwa tamaduni za kiafrika, mwanaume kwenda kuongea na mke wa mtu wakati mumewe yuko hai na mbaya. CUF walishaolewa na CCM. CHADEMA wakishanogea na ****** ambaye ndie mume mkubwa wa CUF ndo wamemaliza.
Nawasilisha
 
Islamophobia ni ugonjwa hatari
sana. Ugonjwa huko siku nyingi
sana ila kwa miaka ya hivi
karibuni umekuwa ukikua kwa
kasi ya ajabu sana. Aliyeathiriwa
na ugonjwa huu huwa anaogopa UISLAM na vitu vyote
vinavyohusiana na UISLAM.
Mfano, mtu anayeumwa
ISLAMOPHOBIA akiona mtu
amevaa kofia ama kanzu ama
hijabu, mtu huyu huwa anaogopa sana na huwa anateseka sana
katika nafsi yake. Au mgonjwa
wa islamophobia akisikia kuwa
waislam wanataka kuanzisha
mahakama ya kazi basi yee
huwa hapendi na maumivu humsonga moyoni mwake.
Wagonjwa wa islamophobia
huwa hawapendi kuona uislam
ukienda mbele ama sharia za
kiislam zikifuatwa.
Mengi kuhusu ugonjwa wa ISLAMOPHOBIA soma hapa: 1. Islamophobia - Wikipedia, the free encyclopedia (kiswahili soma hapa: Google Tafsiri)

Baambie habo bajamaa benyewe ndio badini hasa habo bakatoliki benyewe banaudini sana ndio maana banadhania kila mutu kama bao bambieee...
 
Wakuu hapa pana utata sana. Unajua kwa tamaduni za kiafrika, mwanaume kwenda kuongea na mke wa mtu wakati mumewe yuko hai na mbaya. CUF walishaolewa na CCM. CHADEMA wakishanogea na ****** ambaye ndie mume mkubwa wa CUF ndo wamemaliza.
Nawasilisha

kila forum ukiingia ukitaka kuwafaham waunga mkono cdm ni wale wote wenye kaida ya kukosa hoja na kutumia matusi fatilieni hilo mtakubaliana nami,hilo lina maana gani,ni kwamba wote mashaka pamoja na viongozi wao,naoma kutoa hoja...
 
Wazo hili ni zuri lakini kwa sasa haliwezi kuwa la muhimu kwa sababu; kwanza kwa jinsi CUF ilivyo sasa haiwezi kuwa mshirika wa kuaminika ktk mchakato mzima wa katiba mpya wakati wanashirikiana kwa karibu na ccm, pili CUF haiwezi kuwa mshirika mwenye nguvu ktk kuunda katiba wakati amekubali kuunda SUK Zanzibar wakati ni kinyume cha katiba ya muungano iliyopo i.e hawana uzalendo, tatu CUF walishirikiana bega kwa bega na ccm kupitisha mswada ambao ulipingwa vikali na wadau mbalimbali nchini i.e walizingatia maslahi yao na sio ya taifa, nne mwelekeo chanya unaoonekana haujaletwa na ushirikiano wa kivyama bali umakini na umadhubuti wa CHADEMA ndio umetufikisha hapa. Kwa kuzingatia hayo basi kama CHADEMA itathubutu kushirikiana na CUF itakuwa imejitumbukiza ktk safari ya kuelekea iliko CUF. Nadhani umefika wakati tukubali kuwa sio kila nchi imefanikiwa kidemokrasia kwa kuendekeza ushirikiano wa vyama vya upinzani. Vyama vya Republican na Democratic havijafika pale kwa kushirikiana na vyama vinavyokufa ambavyo vimegeuka ni vya kijimbo badala ya kitaifa.
Chonde chonde! viongozi wa chadema msithubutu kutafuta kushirikiana na CUF, endeleeni kufanya kazi na wananchi wanaiona kazi yenu.
 
Yaliyosemwa yote humu ndio hali halisi.. hapa ndipo tulipofikia Watanzania wenzangum kiasi kwamba leo tunatengana kwa Uzanzibar, Upemba , Uislaam na Ukristu ni hali halisi ya Watanzania hivyo Dr.Slaa na Chadema hawawezi kabisa kufanya muafaka na CUF kwanza hawatakubali hata kuonana naye wanamwita Padre!.

CUF wanaamini Chadema ni chama cha Wakristu na ndio sababu wanazozijenga kwa nini waliondoa makubaliano yao na CDM kujiunga na CCM kwa faida ya Wazanzibar (madai yao)..Na Chadema wanaamini CUF ni chama na Waislaam na Wapemba. Hapa ndipo tulipofikia na hizi siasa za majitaka hivyo hakuna sababu kabisa kukutana. Kwa mtaji huu Imekula kwetu na CCM itatawala milele - najua sana mtasema Mkandara hafai ktk maswala haya kwa sababu tu nasema yale ambayo hamtaki kuyasikia, lakini ndio ukweli ambao unauma sana lakini ndio ulosimama!
 
Chadema kipo kwa ajili ya Kanisa tu wala musidanganye watu ccm na chadema ni chama kimoja wote wapo kwa ajili ya kanisa kama kweli chadema ni chama makini kwa nini basi hawajawahi hata siku moja kudai tume huru ya uchaguzi. kwasababu wanajuwa siku kanisa litakapo choka na ccm nchi wanapewa wao. Tume ya uchaguzi ni kanisa, Jeshi ni kanisa, Usalama wa Taifa ni kanisa sasa Chadema wanawasiwasi gani wao kazi kubwa utawasikiya na ufisadi basiiiiiiiiiiii.
 
A strong politician should reach out to his enemies and opponents. Hakuna mtu alikuwa mbaya kwa Mandela kama Butelezi. Dr Slaa atatudhihirishia kuwa atakuwa rais mzuri atakayeweza kuwaunganisha watu kama atakuwa na guts za kuzungumza hata na maadui zake
 
Najua CUF na Chadema ni vyama tofauti sana na vyenye malengo tofauti. Hata hivyo ukweli ni kwamba Chadema tunawahitaji sana CUF kwa ajili ya kufanikisha mambo mengi. Kwanza ni swala la katiba, CUF wameshika sehemu nyeti maana bila wao katiba haiwezi kupita maana wana zaidi ya 1/3 ya bunge la katiba na referandum pia. Ila kuna mambo chadema na cuf wanakubaliana na hasa serikali tatu na tume huru ya uchaguzi. Pia pamoja na tofauti zilizopo, tunaweza kukubaliana na CUF wao wakatoa mgombea mwenza uchaguzi ujao. Bado ccm wana mbinu za kushinda hivyo umoja ni muhimu sana. Namshauri Dr Slaa baada ya uchaguzi wa uzini akutane na Seif kuangalia uwezekano wa kushirikiana angalao kwenye katiba. Nadhani ndugu zangu mnaona busara kwa hili, nadhani Dr Slaa ataona busara ya ushauri wangu

kwa nini usiseme "maalim tafadhali kutana na DR. Slaa??'"
 
Sikubaliani na hoja yako. Chadema iendelee kusimama kama Cdm. CUF ni mwali wa mtu tukijiunga nae ni sawa na kujiunga na *******. Untaka tuwe wake wenza? Kamwe hatupikiki chungu kimoja na CUF. Waliyotufanyia ni mengi na mabaya ysiyosahaulika. Mara ngapi wametutukana bungeni hadi kutoa tafsiri ya neno Tundu? Nasema CDM wakiungana na CUF mi najitoa kwenye chama nibaki mtanganyika huru asie na chama.
hapo RED ndipo unapo dhihirisha udhaifu wako ulipo si rahisi kuwa unayoyapenda tu ndiyo yanatendeka ndani ya chama chak. Kumbuka pia kuwa hakuna adui wala rafiki wa kudumu ndani ya siasa
 
Chadema kipo kwa ajili ya Kanisa tu wala musidanganye watu ccm na chadema ni chama kimoja wote wapo kwa ajili ya kanisa kama kweli chadema ni chama makini kwa nini basi hawajawahi hata siku moja kudai tume huru ya uchaguzi. kwasababu wanajuwa siku kanisa litakapo choka na ccm nchi wanapewa wao. Tume ya uchaguzi ni kanisa, Jeshi ni kanisa, Usalama wa Taifa ni kanisa sasa Chadema wanawasiwasi gani wao kazi kubwa utawasikiya na ufisadi basiiiiiiiiiiii.
Nadhani unachanya mambo badala ya kusema TAIFA unasema kanisa hata hivyo si kosa lako angalia hapa

user-offline.png
Kifoi

Join Date: 12th May 2007
Posts: 36
Rep Power: 456
 
Back
Top Bottom