Ndugu wana JF
natoa ushauri huu nikiamini kwamba natimiza wajibu wangu kama raia naependelea kuona Jamii yetu ikipiga hatua za kimaendeleo.
Kwamba DR SLAA ni kama watu wengine wote waliopo na waliokwisha tangulia mbele ya haki,hata yeye ipo siku, hata labda sekunde ijayo kwa heri au kwa hila maisha yake yanaweza kukatika na kurejea mavumbini ambako ndio asiri yetu sote, na zaidi hawezi kufanya kitu chochote kilicho nje ya uwezo ambao umewekewa mipaka na Mwenyezi Mungu, zaidi anaweza akayafanya yale ambayo yako ndani ya uwezo karibia wa kila mtu.
Nasema hivi si kwa nia ya kumchuria, bali ni katika hali ya kukumbushana uhalisia wa maisha haya, hasa kwa sababu siku za karibuni nguvu ya kutaka kuuaminisha UMA wa watanzania kwamba yeye ndio tatizo umeshika kasi kwa hari ya hali ya juu sana, kwakwamba, hasa katika makorido ya watalawala wa CCM ni kama sasa ndio wanaamini kwa dhati kabisa DR SLAA ndio tishio la utawala wao katika nchi yetu.
Mimi niseme kwa dhati kabisa, kwamba hata kama huyu mzee ataamka kesho na kusema yeye na siasa basi, hii haitosababisha kwa namna yoyote ile watanzania tuanze kuona matatizo tuliyonayo ni mafanikio, haitasababisha tukione chama cha mapinduzi kama kinauwezo wa kutokwamua hapa tulipo, wala haitakuwa mwisho wa kumkumbusha rais kikwete kutekeleza ahadi zake ukizingatia ahadi ni deni, wala haitasababisha mibarabara inayotandazwa rami kwa pesa za misaada na mikopo ya hiana kuacha kubanduka rami mara tu wakandarasi wanapoondoa vifaa vyao eneo la ujenzi, na wala haitafuta maovu ambayo tunaamini kwamba kwa muda mrefu yamekuwa yakifanywa na ama chama cha mapinduzi, serikali yake ama wateule wake kutoka kwenye kumbukumbu zetu.
Hivyo ni bora, badala ya kuendelea kutumia muda mwingi kumuandama, CCM ingejielekeza kutekeleza ahadi zake kwa dhati, na kama imeshindwa ije ituambie wananchi kwamba kazi waliyoiomba imekuwa ngumu kwao ili tujue tunafanyaje, sababu mpaka sasa kuna mamilioni ya watu wamekaa wanategemea kuona ahadi hizi zinatekelezwa ili waweze kufanyia kazi fursa zinazoambatana na mambo hayo.
kwa Mfano, watu wa Kigoma, wanasubiri kuona mji wao unakuwa na hadhi ya dubai ili waweze kutumia fursa hiyo kufanua biashara, watu wa mwanza na bukoba wanaweka pesa zao wakisubiri meri mpya ziwa victoria wakiamini usafiri salama utawahakikishia ufanisi katika biashara zao, kuna wagonjwa wengi maeneo mbali mbali nchini wanaishi kwa imani wakiamini muda si mrefu hospitali zao za wilaya zinakuwa za rufaa na kuweza kupata matibabu ya uhakika, na mengine mengi.
Ahadi huleta matumaini na pale zisipotekelezwa hukatisha tamaa, na matokeo yake ufuta kabisa imani ambayo mtu aliweka kwa mtoa ahadi, na mbaya zaidi kinachofatia ni kudharauliwa, na labda ndio maana viongozi wengi wa serikali na ccm wamekuwa wakizomewa na kudhihakiwa kama vile vikojozi.
Waswahili wanasema heri nusu shari kuliko shari kamili, nikiamini wanamaanisha kwamba, kwa mfano, kama umetoa ahadi ya kujenga hospitali za rufaa na ukashindwa basi jenga japo dispensary utaeleweka, kwani nyie Mungu Bwana si binaadamu kama sisi, mbona hata sisi tunashindwa kufanya mambo mengi tu? lakini sio unaahidi kutuletea bajaji ya kubebea wajawazito alafu badala ya kutuletea bajaji unakuja ama kutuongeza ahadi nyingine tena au kutuambia mtoto wa DR SLAA sijui mke wake kafanya nini na nini? Haisaidii kitu ni maongezi tuuuuuuu ambayo hayatuletei unafuu wa aina yoyote sana sana tukirudi kwenye maswala ya msingi tunalazimika kushirikia msimamo ule ule, kwamba hapana hawa ni kama matapeli, sasa basi.