Dr slaa si lolote si chochote

Dr slaa si lolote si chochote

Kamuulize rais wako kuwa Dr.Slaa ni nani atakwambia kwa kinagaubaga.Gamba wewe,umetumwa kuja kutupotezea muda hapa JF?

Hii thread ni kwa ajili ya kujua watu wanaojiita Great Thinkers wa JF kwa kusoma vichwa vya threads tu. Tutawajua wengi sana leo.
 
Anapaishwaaa weweeeeeeeeeeeeee nani Dr Slaa lazima zije thread kama 100 kwa siku impact ni kwamba wengi wanamfahamu na kujenga ukaribu naye kwa njia nyingine magamba wanajimaliza wenyewe nyum huko hizo propaganda zilifanya kazi sasa hivi wananchi waelewa sana
 
Leo ndo nimeamini kwamba JF gt ni wachache mno wengi ni wakurupukaji..Nashangaa sana wanao mtukana mkuu Sangarara
 
Someni post kabla ya kuporomosha matusi,hi inaonyesha ni jinsi gani baadhi ya wana jf ni wakurupukaji.
 
Ndugu yangu umenena vyema ila tu kusema Dr Slaa si chochote si lolote kama umemkosea vile kwa walio wengi ila umeeleweka Tuangalie zaidi ya Kumfikiria Dr Slaa peke yake. ila tu mkuu Dr Slaa ndiye tunatakaa atutengenezee njia 2015 kama Mungu akimjalia afya na uhai afyeke msitu akipewa msaada na watu kama akina mwaKyembe, then tutaandaa wengine wa kumpokea mbele ya safari, wapo watu wasafi akina Mnyika na wengine wengi tu...

UNAJUA KELELE ZOOOTE HIZI WATU WANAWAZA HIVI IKIWA RAIS NDIYE DR SLAA ITAKUWAJE...............JARIBU KUFIKIRI NA KUWAZA TU THEN UKIPATA JIBU NDIO UTAELEWA KWA NINI CCM HAWAISHI KUMTAJA NA KUMFIKIRIA DR SLAA KULIKO WATU WOTE SI KUNA PROF LIPUMBA MBONA HATAJWI! NI KWA SABABU YEYE SIO TISHIO MKUU...
 
Kajizungusha na kujiumauuma sana aise...
 
ni ajabu mashambulizi na mitusi anayoelekezewa Sangarara bila hata watu KUSOMA katikati ya mistari kuona alichowasilisha.Hii ni USHABIKI au UZUZU?
 
thread ndefu pointless!!
Kwa wewe ulioshiba ni pointless, hila kwangu mimi hohe hahe hiyo ndio hali halisi, chuki niliyonayo dhidi ya ccm itaendelea kwa muda mrefu sana hata baada ya kuondoka madarakani 2015.
 
Mkuu Sangarara hebu edit hiyo heading ya thread yako.
 
Kwa wewe ulioshiba ni pointless, hila kwangu mimi hohe hahe hiyo ndio hali halisi, chuki niliyonayo dhidi ya ccm itaendelea kwa muda mrefu sana hata baada ya kuondoka madarakani 2015.

Ungekuwa na chuki na CCM usingemshambulia doctor! Yaani wewe kweli niliposoma heading kuwa dr. Slaa sikuweza kusoma thread yako tayari heading yako ilishanichefua! pole kama wewe ni kamanda mwenzangu, ila jifunze kutafuta heading inayoendana na habari!
 
Umetumwa na watu wa CCM,kila njia mnajitahidi kumchafua Mh.Dk.Slaa.Mmenunua mamluki kwa pesa za watanzania wampake matope,uzuri baada ya kufanya mnatangaza.Hata wasira alisema ataimaliza Chadema kabla ya 2015.Na wengine wanatuita malimbukeni tunaotumbulia nyongo humu,acha iwe hivyo.Mbona watoto leo wanaelewa mimba ikoje,inapatikanaje,tunaelekea ktk kizazi cha watoto wachanga wenye uwezo kama watu wa umri wa miaka 40.
 
Ulichosema ni kweli kabisa,Watanzania tunamambo mengi ya kujadili haya ya binafsi kuhusu viongozi tuwaache na maisha yao.Hakuna msafi ulimwenguni na kila mtu atahukumiwa kwa matendo yake,hatuna sababu ya kumtukana au kumtuhumu mtu kama hakuna udhibitisho.Tusonge mbele na mambo mengine.La pili waandishi wa habari pia wasikurupuke kumwandika mtu kwa mabaya ili wauze gazeti siyo sahihi,waache pia kama mtu hana ushahidi basi wasiandike habari ili mradi kumchafua mtu.
 
Leo ndo ntajua who are great thinkers hapa!!
 
Ungekuwa na chuki na CCM usingemshambulia doctor! Yaani wewe kweli niliposoma heading kuwa dr. Slaa sikuweza kusoma thread yako tayari heading yako ilishanichefua! pole kama wewe ni kamanda mwenzangu, ila jifunze kutafuta heading inayoendana na habari!

ukisoma thred yangu utagundua nilikua sikuandikii wewe, the message is meant for some other guys. bye
 
Mkuu Sangarara hebu edit hiyo heading ya thread yako.
Heading haina tatizo, ukifuatilia utagundua wale nilio maanisha ujumbe uwafikie, wamesoma wameelewa na kuondoka kimya kimya.
 
Back
Top Bottom