Malafyale
Platinum Member
- Aug 11, 2008
- 13,913
- 11,327
Rais duniani anachaguliwa kwa misingi mikubwa miwili;kwanza anapimwa kwa sera zake endelevu kuhusu uchumi na mikakati yake ya kuuimarisha na mbili anapimwa kama anaweza kuongoza vyema majeshi ya nchi yake kwa dhana ya u-Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama!
Lk toka kampeni hizi zianze,wagombea wa vyama vya upinzani akiwemo Dr Slaa huwa wanawaeleza tu Wa TZ jinsi CCM na serikali yake ilivyoshindwa kuwakomboa WaTZ kiuchumi hata huwa wanawaeleza wa TZ watawafanyia nini kiuchumi wakishinda;lkn sijapata soma sehemu wakieleza wao wana utafouti gani na Rais JK kama watashinda U-Rais na kuwa Amiri-Jeshi Mkuu!
Kuna mambo mengi ya kuwaeleza waTZ tofauti yenu na JK kama mkishinda u-Rais na kuwa Amiri Jeshi Mkuu;kwanza ni kuhusu majeshi yetu kwenda Comoro mwanzaoni mwa 2008 ambapo Jeshi letu lilipelekwa Anjoun kwenda kuwachapa waasi wa jeshi la Comoro chini ya Kanal Mohamed Bacar aliyetangaza kumuondoa Madarakani Rais Sheikh Ahmed Sambi!Baada ya ushindi wa jeshi letu Rais JK akaenda Comoro na kushangiliwa sana na wa Comoro waliojipanga mitaani wakimsubiria
Vita vya Comoro vilikuwa vita vya ndani vya nchi hiyo hata Rais Thabo Mbeki akiwa bado yupo madarakani alivipinga wazi wazi kule Adis Ababa,wapinzani wanaweza wakajenga hoja nzuri hapo hasa kwa vile Comoro nao wapo hoe hae kiuchumi,basi ni nani aliyefadhili vita hivyo?Je tulipaswa kwenda Comoro kwenye matatizo yao ya ndani?
Pia jeshi letu lipo Lebanon kulinda amani na au ama tayari lipo Darfur-Sudan au lipo karibu kwenda huko kwenye sababu zile zile za kulinda amani ;mbona kuna nchi zaidi ya 52 Barani Afrika,kwa nini kila siku sisi ndiyo jeshi lienda kwenye kulinda amani?Dr Slaa ongelea suala hili na wananchi watataka kujua sera zako zina utofauti gani na Rais JK kwenye kuongoza majeshi yetu!
Hata kuhusu kulipukia mabomu wananchi wa Mbagala napo kunaweza kuongelewa kwenye mikutano ya kampeni;sidhani kama ni vyema hadi leo ghala za majeshi ziwe karibu na nyumba za raia.Tunataka kujua wagombea wengine wana sera gani tofauti kuhusu zile za CCM zinazoweka silaha nzito karibu na makazi ya watu na hivyo kuhatarisha maisha yao!
Hints yangu:Ni vyema Dr Slaa akatuhaidi kuwa akishinda atabadili katiba ili ni Bunge tu liwe na uwezo wa kutupeleka vitani tofauti na sasa ambapo Rais tu kwa uamuzi wake akiamua anaweza akayapeleka majeshi yetu vitani popote pale duniani!