Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,502
- 911,254
Gazeti la Tanzania Daima la leo limemkariri mgombea Uraisi kupitia Chadema ya kuwa akiwahakikishia mashabiki wake ya kuwa atashinda kwa kishindo na yakuwa wapigakura safari hii wamemkubali awe Raisi wao wa tano wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Namna ya pekee ya kuikamilisha azma hii ni sote kesho tusijivunge tujitokeze kwa wingi tukapige hizo kura za kudai mabadiliko ya mfumo wa uongozi wa nchi hii..tukachague katiba mpya ambayo itaturuhusu tushiriki kikamilifu katika ujenzi wa nchi yetu badala ya sera hizi za CCM za kutegemea wafadhili hususani marekani waje watufanyie kazi za kuijenga nchi yetu wakati uwezo tunao na nia tunazo za kujiendeleza wenyewe........Hivi kama wageni wakiwa ndiyo tumewaweka mstari wa mbele katika ujenzi wa taifa letu kama JK alivyodai jana kwenye mdahalo wake je hata hilo soko la ajira tutaambulia kitu au ni wageni tu ndiyo watakao kuwa wakitesa?.......