Dr. Slaa: Natishwa

Dr. Slaa: Natishwa

Hilo jina ni lake na hiyo account ni yake, nachofurahi mwenyewe katuonya tuwapuuze nyie mnaosema account hiyo sio yake

Hilo jina haliwezi kuwa lake na account siyo yake, mtaeleweka mwaka huu! Ila picha ni yake
 
Hakuna mtu binafsi aliye maarufu kuliko chama.
Hayo maneno waambie Bavicha wenzako.

Mbowe ni zaidi ya Chadema na ndiyo mmiliki halali wa Chdema.

Anachosema sema Mbowe ndiyo kauli ya Chadema.
 
Nimemsoma twiter, anasema kweli usalama wake u mashakani. Na amesisitiza kuwa akipata ulinzi alio uomba kutoka kwa mashirika ya kimataifa atasema ukweli kwa vyombo vya habari. Na amesema wazi kuwa Mwenyekiti wa Chadema na baadhi ya wanachama walikwenda kwake kumshawishi arejee, ikashindikana hivyo kumtaka akae kimya nayo bila shaka imeshindikana, na kwa mtazamo wangu inawezekana kabisa ndio sababu kubwa iliyo pelekea kuugua ghafla kwa mwenyekiti wa Chadema..hapo bado Dr. hajamwaga -----, mtajikuna mpaka mpauke
 
Slaa abaki cdm au aondoke cdm yote sawa...... sisi adui yetu watanzania ni ccm na mfumo wake
 
Katika hatua nyingine, mmoja kati ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyekuwa akiwania kuteuliwa na chama hicho kupeperusha bendera kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu, Makongoro Nyerere, amesema Chadema kitapata wakati mgumu kumsafisha mgombea wao wa urais, Edward Lowassa.

Makongoro na Lowassa ni miongoni mwa makada 32 wa CCM waliokatwa majina yao na Kamati Kuu ya chama hicho mjini Dodoma mwezi uliopita.

Akizungumza na Raia Tanzania jana, Makongoro alisema uamuzi wa Lowassa kuhamia Chadema ni wa kidemokrasia na haki ya kila Mtanzania. "Huo ni uamuzi binafsi, uheshimike. Lakini chama chake kipya kitapata wakati mgumu sana kumsafisha kutokana na tuhuma za ufisadi anazoandamwa nazo.

"Chadema walikubalika mioyoni mwa wananchi kutokana na hoja ya ufisadi dhidi ya Lowassa. Hiyo sabuni au brashi ya kumsafisha haipo hata Nakumatt," alisema Makongoro, mmoja kati ya wanaCCM wachache waliokuwa wakimnyooshea kidole Lowassa wakati wa kusaka wadhamini ndani ya chama hicho.

Kuhusu uamuzi wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa kuachana na siasa, Makongoro alisema hilo si jambo jema hata kidogo. "Tuna muhitaji. Taifa linamuhitaji. Wanasiasa wa aina yake wanatakiwa kuendelea kutoa mchango kwa mustakabali mwema wa taifa letu. Ninamshauri asiache siasa, aje CCM tujenge taifa," alisema.

Imeandikwa na WAANDISHI WETU, Dar

Raia Tanzania
 
Huyu naye ni wa kupuuza! Watoto wa marais wa kwanza wanakula shavu ikulu yeye anabaki kutapatapa tu na ufisadi wa Lowassa, senzi typn kabisa! Atuache na Lowassa wetu sisi mengine sasa hivi hatujadili kabisa tuna kazi moja tu mbele yetu "KUMNG'OA CCM"
 
Pole zake. Anaona kuwa ana ufahamu kuliko wale woote waliokwenda kumsindikiza?? Kama ni kukatwa nadhani walimwonea sana Maakongoro. Wangemdanganya hata afikie 5 bora afadhali. Lakini kamati ya maadili wakaanza na jina lake kwanza ndio wengine wakafuata. Kweli, mtoto wa muasisi wa hilo lichama, na bado anang'ang'ania hilo lichama. Nasema Pole zake.
Hayo si mahaba ni utumwa. Ajifunze kwa Pinda, Urais wa njoziiiii
 
Makongoro ndo walewale akna kinana,magufuri,jk,nae hajitambui hayo sio yakusema mbele yetu sisi wachambuzi au kwa vile mtoto wa muasisi wa taifa ndo kibuli eti.
 
Raia Tanzania = Uhuru = Mzalendo = Habari Leo. Yameshindwa kumnadi Magufuli.
 
Moderator kwanini huyu Abunuas hafungiwi? Tusipotezewe wakati...

kwanza ufahamu, kuwa kufungiwa hapa kwangu sio tatizo na wala sipotezi chochote. lakini kwenye post yangu iliyofuata nimetoa angalizo kama hii sio verified ID ya Slaa basi mods waiondoe kabisa na hata sio kuunganisha kama walivyofanya.
baada ya maelezo haya endelea ku-rap.
 
Back
Top Bottom