Dr.Slaa na Kinana sasa kuripoti kwa Zitto

Dr.Slaa na Kinana sasa kuripoti kwa Zitto

Hakuna tabu ila CCM hawako tayari kwa hili kwahiyo Zitto awe na Uhakika atakwamishwa tu! Lakini mwenye wajibu wa kuvikagua vyama vya siasa si msajili wa vyama na msajili ndo anakaguliwa na Mkaguzi mkuu wa serikali, maana Vyama vya siasa viko chini ya hiyo taasisi ya msajili wa vyama vya siasa!

Sasa tusemeje.. wewe ndiye katibu mkuu wa ccm, na unakata kukaguliwa? Ulijuaje kama hawako tayari. CCM na CDM jitayarisheni Ufagio wa ZZK unakuja.
 
Hayo Mahesabu ya CHADEMA ni kuangaliwa vizuri sana, hela imekuwa ya kukopeshana, kuolea, kujengea nyumba binafsi, badala itumike kwenye malengo tarajiwa!

Zitto naibu WA Dr Slaa huyu hapa kishatoa ripoti.

Dah Ila nimeamini kuna sentinel humu ndani shida zinawatreat vibaya sana... mtu anadiriki kukitoa ufahamu... anaukalia ufahamu ilihali apate buku saba za lumumba hii Ni kidhalilisha nafsi husika. Pumbafu****:thumbup::thumbdown::thumbdown::thumbdown::thumbdown:
 
MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto, amemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, kuelezea sababu ya vyama vya siasa vinavyopokea ruzuku kutoka serikalini, kushindwa kukaguliwa mahesabu yao.

Zitto alisema kuwa viongozi wa vyama vya siasa watawajibika kukabiliana PAC, uso kwa uso wakiwemo katibu wakuu wa vyama vya siasa vinavyopokea ruzuku kutoka serikalini.

Kutokana na msimamo huo ambao unakubalika kisheria, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, anatarajiwa Kuwa miongoni mwa watakaohojiwa na kamati hiyo, inayoongozwa na Naibu wake, Zitto.

Wengine ni Katibu mkuu wa CCM Abrahaman Kinana, Julius Mtatiro CUF.
UPDATES
Zitto aitaka ofisi msajili wa vyama kusitisha ruzuku kwa vyama vyote vinavyopata ruzuku ya serekali

Mi natamani chama hypotenuse vifutiwe ruzuku. Naamini kuna vyama vitapata shida sana kwa mfano ccm naamini hakitaweza kusavaiv kwa kuwa wao kwao ruzuku Ilikuwa Ni ya disdain NA walikuwa wanaimissuse kuhongea kufanyia maovu ya kila aina. Ila kwa CDM wao naamini watatoboa NA watapeta wao si wanategemeaga nguvu ya umma? ? Nitafurahi sana
 
Good idea, fanya hivyo mh Zitto bila upendeleo, ukikuta madudu pasua jipu bila kuangalia ni nani na chama kipi
 
Mh. Zitto Kabwe amevitaka vyama vya siasa kupitia Makatibu wake wakuu kueleza kwa nini haufanyiki ukaguzi wa mahesabu na mkaguzi mkuu wa serikali ? Kikanuni kila panapopelekwa ruzuku ya serikali lazima ukaguzi ufanyike juu ya matumizi ya fedha hiyo.

Swali la kujiuliza; inamaana mkaguzi mkuu wa serikali ameshindwa kufanya ukaguzi ? mpaka Zitto aamuru iwe hivyo ? Yeye Zitto amesema makatibu karibu wote wa vyama wataitwa kujieleza mbele ya bunge kwa nini ukaguzi haufanyika. Ngoja tusubiri mwisho wake utakuwaje
 
Kama ukifanyika ukaguzi juu ya matumizi ya ruzuku tu bado ni kazi bure, kwan vyama haviendeshwi kwa kutegemea ruzuku tu.

Wakaguzi wanaoandaa hizi hesabu za vyama wanaangalia mapato na matumizi kwa ujumla wake na si hesabu za matumizi ya ruzuku tu kama sheria inavyotaka.

Sasa kukabiliana na udanganyifu unaoweza kujitokeza sheria ingevitaka vyama vionyeshe vyazo vyote vya mapato na vikaguliwe kwa kuzingatia mapato na matumizi hayo.

Kama sivyo basi dawa ni kufuta ruzuku kutoka serikalini kama chanzo cha mapato kwenye hivi vyama.

Ili kila chama kibuni vyanzo vyake halali vya mapato
 
Dhumuni ya ukaguzi wa CAG ni kuhakikisha kodi ya wananchi haiendi hovyo. Vyanzo vyao vingine haviwahusu wananchi wote, vinawahusu walio changia. Vyama viwajibike kwa wachangiaji.
Ila hizi hela za ruzuku wanakatwa watanzania wote, hata wale ambao sio wanachama wa chama hicho. Ni hesabu za serikali. Na ndio maana zinakaguliwa na CAG na PAC kama ilivyo kwa matumizi yote ya serikali.
But I agree with you on one point: kuna vyama ambavyo vitaonekana visafi kwa kutumia ruzuku ipaswavyo, huku kukiwa na uwezekano wa ufisadi mkubwa kuendelea katika hesabu ya income zingine. Hapa ndipo wanachama wanatakiwa kuweka ushabiki pembeni na kuwawajibisha viongozi wao.
 
Hahahahaha safi sana Zitto Kabwe.....

Dr. Slaa atakomaje maana safari zake za kutalii nje hazina supporting documents pia alitumia hela za chama kumchumbia Bi. Josephine Mushumbusi......

Hii issue ya ukaguzi itawa cost CHADEMA Big Tym!!!!!!!!!!!!!!!!1111

Go Go Go Zitto Kabwe
 
Kuna vyama ambavyo hata sheria ya uchaguzi inayoagiza wagombea wao waonyeshe gharama walizotumia kwenye kampeni inakua issue kweli kweli.
 
Hahahahaha safi sana Zitto Kabwe.....

Dr. Slaa atakomaje maana safari zake za kutalii nje hazina supporting documents pia alitumia hela za chama kumchumbia Bi. Josephine Mushumbusi......

Hii issue ya ukaguzi itawa cost CHADEMA Big Tym!!!!!!!!!!!!!!!!1111

Go Go Go Zitto Kabwe

You are in for a rude shock!
 
Hatuna namna yoyote ya kuvinyima ruzuku hiyo maana mfumo tulionao sasa unaruhusu vyama vingi,sasa vyama vingi n pamoja na hivyo vyama vidogovidogo.

Ni kweli lakini ni vyema kama mfumo huu ukaangaliwa upya kwa maslahi ya Taifa. Manake vyama vingine vimeanzishwa na kusajiliwa vikiwa na lengo la kujipatia ruzuku na kuzitafuna kama ilivyo kwa baadhi ya NGO's.
 
ila mimtu miongo humu,taratibu hazimruhusu Zitto kumhoji Dr.Slaa coz ana interest na chama

Tatizo ni kua itakua vigumu kupata mtu ambae hana chama. Kumbuka Dkt Slaa hahojiwi na Zitto anahojiwa na taasisi. interesting point thought
 
Kuagiza kusitisha ruzuku,sidhani kama ni sahihi.Agizo hili la kamati ya zitto kama litatekelezwa,litaviathiri vyama vya upinzani zaidi,kwani havina vyanzo vingine vya mapato.

On the contrary nadhani vyama vya siasa vya upenzani vimebuni njia mbadala ya kufanikiwa bila kutumia hela za umma. Wanahamasisha wanachama kwa hoja na matendo, sio tshirt na keps. Leo wanapata zaidi toka vyanzo binafsi kuliko hizo za ruziku.
 
Mi natamani chama hypotenuse vifutiwe ruzuku. Naamini kuna vyama vitapata shida sana kwa mfano ccm naamini hakitaweza kusavaiv kwa kuwa wao kwao ruzuku Ilikuwa Ni ya disdain NA walikuwa wanaimissuse kuhongea kufanyia maovu ya kila aina. Ila kwa CDM wao naamini watatoboa NA watapeta wao si wanategemeaga nguvu ya umma? ? Nitafurahi sana

Hiyo staili ya kutembeza bakuri ccm walishaiachaga kitambo sana, hicho chama kina pesa acha kabisa, wana miradi mikubwa ya kibiashara.
 
Hiyo staili ya kutembeza bakuri ccm walishaiachaga kitambo sana, hicho chama kina pesa acha kabisa, wana miradi mikubwa ya kibiashara.

wangekuwa na miradi wasingeiba hela za EPA,MEREMETA etc
 
Back
Top Bottom