Dr.Slaa na Kinana sasa kuripoti kwa Zitto

Kurunzi

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
10,197
Reaction score
11,628
MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto, amemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, kuelezea sababu ya vyama vya siasa vinavyopokea ruzuku kutoka serikalini, kushindwa kukaguliwa mahesabu yao.

Zitto alisema kuwa viongozi wa vyama vya siasa watawajibika kukabiliana PAC, uso kwa uso wakiwemo katibu wakuu wa vyama vya siasa vinavyopokea ruzuku kutoka serikalini.

Kutokana na msimamo huo ambao unakubalika kisheria, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, anatarajiwa Kuwa miongoni mwa watakaohojiwa na kamati hiyo, inayoongozwa na Naibu wake, Zitto.

Wengine ni Katibu mkuu wa CCM Abrahaman Kinana, Julius Mtatiro CUF.
UPDATES
Zitto aitaka ofisi msajili wa vyama kusitisha ruzuku kwa vyama vyote vinavyopata ruzuku ya serekali
 
Hakuna tabu ila CCM hawako tayari kwa hili kwahiyo Zitto awe na Uhakika atakwamishwa tu! Lakini mwenye wajibu wa kuvikagua vyama vya siasa si msajili wa vyama na msajili ndo anakaguliwa na Mkaguzi mkuu wa serikali, maana Vyama vya siasa viko chini ya hiyo taasisi ya msajili wa vyama vya siasa!
 
zito naye anatapatapa tu wala hana kipya kamaliza kutaja mishara ya watu au anaendelea?
 
MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto, amemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, kuelezea sababu ya vyama vya siasa vinavyopokea ruzuku kutoka serikalini, kushindwa kukaguliwa mahesabu yao.

Zitto alisema kuwa viongozi wa vyama vya siasa watawajibika kukabiliana PAC, uso kwa uso wakiwemo katibu wakuu wa vyama vya siasa vinavyopokea ruzuku kutoka serikalini.

Kutokana na msimamo huo ambao unakubalika kisheria, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, anatarajiwa Kuwa miongoni mwa watakaohojiwa na kamati hiyo, inayoongozwa na Naibu wake, Zitto.

Wengine ni Katibu mkuu wa CCM Abrahaman Kinana, Julius Mtatiro CUF.

Kwa hiyo Katibu Mkuu wa CUF ni Julius Mtatiro?
 
Akague na mapato ya kinana kwenye ujangili wake, tufaham pato lake na matumizi
 
MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto, amemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, kuelezea sababu ya vyama vya siasa vinavyopokea ruzuku kutoka serikalini, kushindwa kukaguliwa mahesabu yao.

Zitto alisema kuwa viongozi wa vyama vya siasa watawajibika kukabiliana PAC, uso kwa uso wakiwemo katibu wakuu wa vyama vya siasa vinavyopokea ruzuku kutoka serikalini.

Kutokana na msimamo huo ambao unakubalika kisheria, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, anatarajiwa Kuwa miongoni mwa watakaohojiwa na kamati hiyo, inayoongozwa na Naibu wake, Zitto.

Wengine ni Katibu mkuu wa CCM Abrahaman Kinana, Julius Mtatiro CUF.

Why Julius Mtatiro CUF na sio Maalim Seif ???????
What is Zitto akajihoji mwenyewe kwa CHADEMA na CCM akamhoji Mwigulu ??????
Otherwise, Maalim Seif should be Responsible kama kuhojiwa wanahojiwa Makatibu Wakuu
 
Hayo Mahesabu ya CHADEMA ni kuangaliwa vizuri sana, hela imekuwa ya kukopeshana, kuolea, kujengea nyumba binafsi, badala itumike kwenye malengo tarajiwa!
 
MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto, amemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, kuelezea sababu ya vyama vya siasa vinavyopokea ruzuku kutoka serikalini, kushindwa kukaguliwa mahesabu yao.

Zitto alisema kuwa viongozi wa vyama vya siasa watawajibika kukabiliana PAC, uso kwa uso wakiwemo katibu wakuu wa vyama vya siasa vinavyopokea ruzuku kutoka serikalini.

Kutokana na msimamo huo ambao unakubalika kisheria, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, anatarajiwa Kuwa miongoni mwa watakaohojiwa na kamati hiyo, inayoongozwa na Naibu wake, Zitto.

Wengine ni Katibu mkuu wa CCM Abrahaman Kinana, Julius Mtatiro CUF.

Ni kweli ni vema wakakaguliwa. Na is a spirit of kuwajibika. Ila naamini kuna mawili, kuna wale ambao matumizi yao na mapato yao yamekuwa hayaeleweki. Sidhani kama watalipokea vizuri hilo. Otherwise sidhani kama kuna mwenye ubavu wa kusema "sh.......zilitumika kusimamia black ops za chama...."! On the other hand itakapofikia kwenye CDM kukaguliwa nitapenda kusikia mh. Zito anadeclare "conflict of interrest" na anakaa pembeni. Ni sehemu ya kuwa muadilifu kutokana na uwajibikaji sahihi!
 
Hayo Mahesabu ya CHADEMA ni kuangaliwa vizuri sana, hela imekuwa ya kukopeshana, kuolea, kujengea nyumba binafsi, badala itumike kwenye malengo tarajiwa!
teh teh mkuu mbavu zangu mie, kama ccm hela zao hutumika kununulia kanga na tshirt, pia zingine hutumika kwa kuwahonga wagombea wa upinzani ili wajiondoe kwenye kinyang'anyiro badala ya kuwalipa watumishi wa chama mpaka ngazi za chini!
 
Hapa tayari Zitto anajua ninikinafanyika ndani ya chadema,na hasa zile ziara za nje ya nchi mara kwa mara!
 
akague na hesabu za vijana wa lumumba tujue kwa mwaka wametengewa sh ngapi kwa ajili ya kupost upuuzi kwenye mitandao ya kijamii
 
Hapa tayari Zitto anajua ninikinafanyika ndani ya chadema,na hasa zile ziara za nje ya nchi mara kwa mara!

Huyu dogo Mjanja sana, kusema kote huko aliilenga CHADEMA maana anafahamu kinachoendelea pale!...
 
Waendeshwe kwa mfumo wa reimbursement on quarterly basis, mtu anapewa pesa akatumie kutokana na maombi kwa mujibu wa sheria kwa miezi mitatu na hatapokea zinazofuata mpaka mpaka amekabidhi docs (retirement) na hakuna kutazama kunyazi la mtu. Utaona kama kuna mtu atabaki katika vyama lakini kuwahoji makatibu wakuu hakuna jipya ni mbinu zile zile kutatua matatizo yaleyale.

Hizi zingine ni fursa wanasiasa wametengeneza wenyewe kwa manufaa yao, angalia hata hao wanaoenda kuhoji makatibu hawana weledi wa finance. Manake hizo kamati awepo mtu aliepita katika accounting firm kufanya kazi ya ukaguzi na wawe na vitabu vya invoice na receipt. Chama kikizingua wanapewa invoice warudishe pesa za walipa kodi wakimbwela anakwenda mtu lupango na kunadi mali za chama, ala! USAID wanamfumo mzuri sana katika hili.
 
Hayo Mahesabu ya CHADEMA ni kuangaliwa vizuri sana, hela imekuwa ya kukopeshana, kuolea, kujengea nyumba binafsi, badala itumike kwenye malengo tarajiwa!
Kichekesho.., hivi kati ya ccm na cdm nani anahofu ya ukaguzi?
 
Hapa zitto kanikosha sana kwakuwa anajua chama chake kinaufisadi mkubwa sana unaofanywa na slaa . Dr kazi kwako mngojee naibu wako atakapokuweka chini na kukuhoji. Pia itamsaidia zito kujua pesa za ruzuku ziingiazo katika chama chake zinatumikaje kwakuwa yeye katengwa kama sio mwanachadema vile.
 
Back
Top Bottom