Dr Slaa na Chadema sasa basi, inatosha! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr Slaa na Chadema sasa basi, inatosha!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Revolutionary, May 8, 2011.

 1. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hali ya nchi imekua tete sana siku hizi. Dr Slaa na Chadema wameifumuafumua CCM na serikali yake, wamebaki wanahaha kutwa kuchwa kumtafuta mchawi ni nani wakati wamejoroga wenyewe! CCM nako wanajikanyaga kanyaga tu kujivua gamba hakuwezekani kwani gamba linang'oka na ngozi! Ukiachilia unyoka wa CCM kubaki palepale, sijaona gamba hata moja lililovuliwa, wembe wa CCM ni ule ule UFISADI!

  Baada ya DR Slaa kuanza kufumua fumu fumu hadharani ufisadi wa CCM tangu alipokua bungeni na Chadema kuendeleza makali hayo kwa kasi na ari zaidi sasa uchafu wote wa serikali hadharani. Kila mwananchi anajua kila uchafu unaoendelea serikalini.

  Kwa miaka kadhaa wananchi tulikua tunafichwa UFISADI wa serikali ya CCM, vigogo walijimegea nchi kwa ari ya ajabu kabisa!

  Sasa wananchi tunaona na kuelewa Serikali yetu kwa namna inavyonuka hadi nasikia aibu! Rais baada ya kutajwa fisadi na ufisadi wake wa wazi nae anajikanyaga tu hana meno, hana guts za kumwadhibu yoyote kwa uchafu wake binafsi pia,magamba hayavuki basi tu! Kwa kujikomba komba kwa raia na watu anaishia kuwa msanii sanii na kutoa ahadi za kuclick, za uongo uongo hadi namuonea huruma huyu baba aliyewatoa wakwere kimasomaso, nchi inamshinda kwa kasi na ari ya Chadema ambayo imewashika na watanzania sasa inaivuruga vuruga serikali ya CCM hadi nahisi nchi inakwenda mrama sasa!

  Nawaomba Dr Slaa na Chadema kuwa jamani eeh waungwana inatosha tosha sasa, have mercy on our president, kasi yenu inafanya taifa halitawaliki kweli, chama cha magamba kushnei!
  Chadema naomba punguzeni spidi!
   
 2. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  aagh mkuu...umeanza vizuri lakini swala la kusema wapunguze kasi,nalipinga,kwa CCm 1 mistake 7 goals, huu moto ndo ushaanza hivyo na unaendelea,hadi kukipambazuka ...2015 hiyooo!! Bado pande za kusini Mtwara na Lindi hawajaenda!!watu wana hamu kweli ya mabadiliko kule ,sema basi tu hakuna muhamasishaji...!!
   
 3. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ni kweli dr Slaa kafichua ufisadi lakini nadhani siyo peke yake. Tofauti tu ni kwamba yeye alizua moto bungeni na kwenye mikutano ya hadhara. Ukisoma magazeti, ukinukuu thread nyingi hapa JF hasa za MM utakubali kwamba siyo dr Slaa peke yake. Wote wapewe sifa
   
 4. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33


  Mkuu nakubaliana nawe kabisa kwa yote; ila hapo kwenye nyekundu "sikubaliani nawe". Katika nchi za kiafrika ili tuendelee tunahitaji matumizi mazuri ya rasilimali za taifa. Na ili hili liwezekane, inabidi kukomesha ufisadi wa aina zote. Kukomesha ufisadi si jambo rahisi sana, ni mpaka wananchi waliowengi waamke (awareness) kujua namna viongozi wao wanavyowaibia na wawe na uwezo wa kujua namna ya kuwazuia wasiibe. Kwa msingi huo, elimu inayotolewa sasa na CDM inatakiwa iwafikie kila mtanzania hadi vijijini; na hapo ndo rasilimali za nchi hazitabakwa ki-urahisi na hivyo kutumika kwa maendeleo ya waliowengi-watanzania. Hivyo CDM ongezeni spidi kwenda hadi vijijini kuliko na watu wengi ambao hawajajua vema-na ambao hutumika kama mtaji wa watawala kuudanganya umma.
   
 5. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu kwa kweli hapo kusema wapunguze spidi ni kwamba namuonea tu huruma rais wetu! Sijawahi ona serikali iliyokosa mwelekeo kama hii!

  Halafu Chadema wana potential kubwa sana ukiacha hulo kusini ambako hawajaenda huku mjini tu kuna watu wangependa kuwa wanachama hata leo lakini ndo kama hivyo muihamasishaji hakuna!
   
 6. hKichaka

  hKichaka Senior Member

  #6
  May 8, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 199
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dr slaa ni mwanaume...........
   
 7. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Muhosni umejieleza vizuri sana, wote waliochokoza mijadala na kufichua ufisadi wapewe sifa, ujasiri wao umetukuka, haswa Dr Slaa!
   
 8. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Acha aisee Dr ni Dume la mbegu! Mtu mmoja kama CCM milioni moja!
   
 9. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nsimba hapo nimeongea kwa huruma tu! Hali ni mbaya! Ona hadi mbunge anarushiwa mawe aiseee!
  Mori wa Chadema sasa imewaingia wananchi! Najiuliza wakizidisha itakuaje! JK anaweza kurushiwa mawe pia! Si litakuwa balaa hilo!
   
 10. d

  daniel.nickson Member

  #10
  May 8, 2011
  Joined: Apr 30, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wote yani watanzania kwa ujumla wake sasa tumekubali kwamba chadema inakubalika. na hasa baada ya chadema kufahamu udhaifu wao ulikua wapi.
  tunajua kwamba baadhi ya weakness ilikua.
  1. migogoro iliyosababisha (mfano) kigoma ambayo kwa upande wangu ilikuwa ndiyo ngome ya upinzani kupoteza majimbo manne kwa nccr ambapo leo hiki chama kingekuwa marehemu.
  2.kutokuwekeza vijijini.
  asilimia karibia tisini ya majimbo na kata zote yako vijijini lakini hadi uchaguzi wa mwaka jana ni maeneo machache sana ya vijijini yalikua yamefikiwa na hii weakness ccm waliitumia vizuri.

  maoni yangu.
  1.ni vizuri chadema wakawekeza sasa kuanzia kwenye matawi kwa mbinu yoyote ile itakayonekana inafaa.
  2.wasielekeze nguvu tuu kwenye yale maeneo wanayofiri kwamba wanakubalika bali ni wakati wa kufika kwenye yale maeneo ambayo hayafikiki na kufungua matawi.
  na mwisho kabisa alama za nyakati zinaonyesha kwamba 2015 ikulu ni ya cdm, wanataka kuniambia kwamba wataingia ikulu bila ya kuwa na wabunge na madiwani kutoka mtwara na lindi?, ninaomba kufahamishwa ratiba ya huko.
   
 11. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #11
  May 8, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,960
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  hata Bob Marley hakuanzisha reggae, ila ndiyo LEGEND
   
 12. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  lakini hali haitakuwa nzuri kwa CDM kupiga kimya ila kwa serikali kuwajibika. JK bado anao muda na uwezo mkubwa wa kuwanyamazisha CDM na Dr. Slaa kwa kuyashughulikia yale ambayo yanawafanya cdm wazunguke na kuyadai, baadhi ya hayo mambo ni kama:-
  Kuboresha hali za wafanyakazi kwa kupunguza kodi na kupandisha kima cha chini cha mishahara, kupunguza ugumu wa maisha kwa kupunguza kodi nyingi ktk bidhaa muhimu kama mafuta.
  Kupunguza matumizi ya anasa ya serikali ikiwa pamoja na mishahara mikbwa na marupurupu ya viongozi kama wabunge kuwepo na uwiano kati ya mishahara na kiwango cha elimu na unyeti wa kazi yenyewe.
  Kuheshimu na kufata utawala wa sheria watu wahukumiwe ktk muda muafaka maamuzi ya siasa yasibind maamuzi ya mahakama.
  Kusimamia maadili ya viongozi kwa ukaribu na athubutu kuwaadhibu na kuwafikisha mahakamani wtuhumiwa wakuu wa ufisadi ikibidi kuwafunga hata kama ni marafiki zake.
  Kupitia upya mikataba yoote ya rasilimali za taifa na iandikwe kwa manufaa ya wananchi, pamoja na transparency ktk uendeshaji wa nchi, kupunguza ukubwa wa serikali.
  Hayo ni baadhi tu ila kuna mambo mengi mengi ambayo CDM na watz wengi yanawaboa akiweza kubadilisha mbona cdm watacease coz watakuwa hawana la kuishtaki ccm kwa wananchi otherwise this movement is unstopable yaani hata Cdm na Dr wakinyamaza kwa hali ya sasa hata mawe yatapiga kelele
   
 13. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #13
  May 8, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Dawa katika mazingira kama haya si kwa Chadema kupunguza mwendo, isipokuwa wale walioshindwa waachie ngazi ili Chadema wandeshe nchi inavyotakiwa
   
 14. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #14
  May 8, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Aisee umenifurahisha hapo mwishooo uliposema "this movement is unstopable yaani hata Cdm na Dr wakinyamaza kwa hali ya sasa hata mawe yatapiga kelele"
   
 15. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #15
  May 8, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Yani pamoja na matatizo yote tuliyonayo chini ya uongozi wa magamba bila kusahau potential wanayoionyesha CDM bado watu wanahitaji kuhamasishwa???Kweli waTanzania wameridhika......
   
 16. G

  Giddy Mangi JF-Expert Member

  #16
  May 8, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 833
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Peoples Power hakika kurudi Nyuma ni Dhambi kubwa hakika ndugu zangu
   
 17. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #17
  May 8, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Nimekubaliana na wewe ila kwenye kupunguza kasi sijaafiki kabisa,Chadema mwendo mdundo 120 ileile.
   
 18. O

  Omr JF-Expert Member

  #18
  May 8, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Slaa amefanya nini zaidi ya kuimba wimbo wa UFISADI? Imebaki atoe wimbo wa Taarab aupe jina FISADI. Alete mambo mapya sio kukalia tatizo moja kila siku. Kila kipanda kwenye jukwaa anatoa list ya watu. Tunataka kusikia chama chake kina fanya nini bungeni? Uchaguzi umepita sasa wabunge wake wafanye kazi yao bungeni, na hii tabia ya kidemu ya kususa waache.
   
 19. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #19
  May 8, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
   
 20. O

  Omr JF-Expert Member

  #20
  May 8, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tunajua wazi kuwa ukisema ukweli juu ya ubovu wa Slaa basi unaitwa mnafiki. Endeleeni kumtukuza na siku akiwaharia ndio mtajua kwamba yeye ni mwanasiasa na wala sio malaika kama mnavyo amini..
   
Loading...