Dr Slaa Moshi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr Slaa Moshi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pdidy, Sep 23, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,415
  Likes Received: 5,687
  Trophy Points: 280
  • Ni ule wa serikali kuimaliza CHADEMA

  na Janet Josiah na Charles Ndagula, Moshi

  MGOMBEA urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ametangaza kunasa waraka wa siri ulioandikwa siku nne zilizopita, ambao pamoja na mambo mengine unawaagiza watendaji wakuu wa serikali kufanya kila wawezalo kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinashinda uchaguzi.

  Dk. Slaa mwanasiasa mwenye rekodi ya kunasa taarifa mbalimbali nyeti za serikali, alitangaza kuhusu kuuona waraka huo wakati akihutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza katika Manispaa ya Moshi.

  Akizungumzia suala hilo, Dk. Slaa alimtahadharisha mgombea wa urais wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuhakikisha anachukua hatua ya kuvidhibiti vyombo vyake vya usalama ili visimwage damu isiyo na hatia kwa sababu tu ya kutaka kushinda urais kwa gharama zozote zile.

  Dk. Slaa aliyekuwa akihutubia katika Uwanja wa Mashujaa mjini hapa, alisema dalili zimeanza kujitokeza katika mikoa mbalimbali aliyopita, ambako kumekuwapo na matukio ya watu kuonewa na viongozi wa serikali.

  Akifafanua, alisema waraka huo unaokwenda kwa vyombo vya usalama, wakiwemo wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa halmashauri za wilaya, unawataka wafanye lolote ili kuhakikisha CCM inashinda.

  "Ninao waraka ulioandikwa Septemba 19 (Jumapili iliyopita), mwaka huu na leo ni siku ya tatu, unakamilishwa na kusambazwa kwa viongozi hao kuwakumbusha kuwa lazima wahakikishe CCM inashinda, sikuupata hapa hapa, ila tayari umesambazwa nchi nzima," alisema Dk. Slaa.

  Dk. Slaa ambaye ni Katibu Mkuu wa chama hicho, kwa nafasi yake anatoa tamko hilo ili kumtahadharisha Rais Kikwete kuacha mara moja hujuma hiyo, na kuwa dalili zinaonyesha kwamba Watanzania wameamka na wanahitaji mabadiliko.

  Alisema pamoja na kupata hujuma hizo, chama chake kimejipanga vyema kukabiliana na mashambulizi ya CCM na serikali yake, kwa kuweka mfumo imara wa ulinzi kwa viongozi wao na wapiga kura wao.

  Alivitaka vyombo vya usalama kuacha kuhujumu msafara wake pamoja na watendaji wake, ambao wanatangulia katika vituo ambavyo anafanyia mikutano ya kampeni, kwa kuwa leo serikali ni ya CCM na kesho serikali itakuwa ya CHADEMA.

  Dk. Slaa alitoa kauli hiyo baada ya kupata taarifa za polisi kutaka kuwakamata vijana wa chama hicho, ambao wanapima viwanja vya kufanyia mikutano yao, ambavyo helikopta itaweza kutua kwa urahisi (GPS).

  Akizungumza na Tanzania Daima, mmoja wa vijana hao, Gwakisa Gwakisa, alikiri kutaka kukamatwa na polisi hao na kudai kuwa alipowaona alifungua mlango wa gari na kukimbia pamoja na wenzake wachache na kuacha gari la chama hicho, ambalo lilichukuliwa na polisi.

  Hata hivyo, Tanzania Daima ilipomuuliza Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) wa Kilimanjaro, Lucas Ng'hoboko, alikiri kuwa wanalishikilia gari la CHADEMA na kwamba wanamsaka mpima ramani ili wamkamate.

  "Bado tunamtafuta mpima ramani wa chama hicho ili baadaye tutoe taarifa kwenu nyinyi waandishi wa habari," alisema RPC Ng'hoboko.

  Akizungumzia tukio hilo, Dk. Slaa amewataka polisi kuwaacha Watanzania wanaotimiza mapenzi yao bila kuwabughudhi na kwamba kero hizo mwisho ni Oktoba 31.

  Akiwahutubia wananchi hao mara baada ya kutoa tamko la chama chake, Dk. Slaa aliwaomba wawachague wagombea wa chama chao ili waweze kufufua viwanda ambavyo vimekufa kutokana na sera mbovu za CCM.

  "Ndugu zangu wana Moshi, ichagueni CHADEMA kwa kuwa CCM imeshindwa kuwaletea maendeleo, kwa kushindwa kufufua viwanda vyenu kama vile kiwanda cha ngozi, magunia, vyuma na viwanda vingine," alisema Dk. Slaa.

  Mapema akimnadi mgombea huyo, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, aliwataka Watanzania kuufanya mwaka huu kuwa wa maamuzi na si wa utani, kwa kuwachagua wagombea makini wa chama hicho.

  "Mwaka 2010 hatudanganyiki ndugu zangu wa Moshi…kwa kuwa tutaingia Ikulu na watu makini kama Dk. Slaa, kwa kuwa na nyie ni makini, hivyo mtatuchagua. "Kwa kuwa CCM ilitumia woga wenu Watanzania kuwatawala na kuwanyanyasa, lakini sasa Watanzania mmeondokana na woga…lakini imani kubwa ipo kwenu wana Moshi, kwa kuwa mmechangia mafanikio ya wana CHADEMA," alisema Mbowe.

  Mkutano huo ulitanguliwa na maandamano makubwa yaliyoanzia katika ofisi za wilaya za chama hicho zilizopo katika Kata ya Majengo na kupita katika barabara za Ghala na Mawenzi, maarufu kama Double Road, Florida hadi katika viwanja vya Mashujaa, huku waandamanaji wakisindikizwa na helikopta iliyokuwa ikiyahamasisha kwa saa nzima.
   
 2. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 1,992
  Likes Received: 1,045
  Trophy Points: 280
  Chadema uwekeni huo waraka kweye Front page ya magazeti ya kesho, ili kila Mtanzania na jamii yote ya Kimataifa iuone.

  Bila Wizi wa Kura this year CCM will be in the opposition side next year.
   
 3. LeopoldByongje

  LeopoldByongje JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2010
  Joined: Apr 28, 2008
  Messages: 373
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hii makala imekaa kishabiki mno. Kwa vile imetolewa na Gazeti linalomolikiwa na CHADEMA basi hii story ni mbinu za kisiasa. Yale yale ya Lamwai na Mrema !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
  Tuzungumze hoja na siyo majingu.
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,152
  Trophy Points: 280
  Aluta Continua
   
 5. M

  Mutu JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  yah jamaa wameaza,ARUSHA yule diwani wamempiga mpaka kazimia ,Mwema tuambiepolisi sehemu yausalama inakuwaje mtu anakaribia kufa?
  mkwere utaleta machafuko kwa uroho wako wa madaraka,mwaka huu upiti maana mpaka makada wa ccm wawakupi kuraingawa bado wanavaa kijani.
   
 6. M

  Mutu JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mgombea udiwani kwa tiketi ya CHADEMA kata ya Kati mjini Arusha Bwana Simba aumizwa vibaya kituo cha polisi wilaya ya Arusha.Bwana Simba alikamatwa na polisi kwa sababu ambazo bado sijazithibitisha.

  Bwana Simba alishambuliwa vibaya na watuhumiwa wenzake aliowakuta wamewekwa rumande katika kituo cha polisi hadi kuzimia na baadae kukimbizwa hospital ya mkoa wa Arusha [Mt meru Hospital] kwa matibabu.
   
 7. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #7
  Sep 23, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kasome MZALENDO na UHURU
   
 8. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #8
  Sep 23, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  ili mradi tu kilichoandikwa kilisemwa ..kuna ushabiki gani hapo..?

  anyway magazeti yapo mengi..! KASOME RAI NA UHURU UISHI KWA MATUMAINI
   
 9. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #9
  Sep 23, 2010
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Huwajui hawa jamaa vizuri , wakiuweka tu kwenye front page gazeti linafungiwa dakika hiyohiyo. Kutokana na nguvu alizopewa waziri wa habari kisheria. Na ukiwekwa kwenye tovuti yao itakuwa blocked. Hawa jamaa ni majasusi kamili mzee. The best way ni kuanzisha e-mail mpya anika ujumbe humo tuma kwenye e-mail address zooooooote za wtz.
   
 10. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #10
  Sep 23, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Unawezaje pata email au mobile number za waTz wote? tupe kaujuzi mzee nianze kuwatwangia
   
 11. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #11
  Sep 23, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Yaani mngejua mnavyonikera na hizo email zenu za chadema, wala msingenitumia. kwani hata kusoma huwa sisome achilia mbali kufoward, just simply i do delete. sio email wala simu (labda ninawazimu kama naweza tumia garama zangu kuwasaidia manyang'au

  halafu hata kama ni hujuma basi ni kwa vyama vyote visivyokuwa ccm, na si chadema tu. au huo waraka (kama upo lakini kwani zaweza kuwa porojo tu) umeandikwa chadema tu? Taburarasa reporting way.
   
 12. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #12
  Sep 23, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Kule rumande hata mahabusi wanaingizwaga watu wa usalama kwa kazi maalumu, nadhani sasa CCM wana kila sababu ya kutumia mbinu za akiba kuwapoteza baadhi ya watu. Msihofu watanzania.

  atakayenyoosha mkono na kukudhuru ni mtanzania mwenzako ambaye anaimba ana mapenzi mema na nchi yake ilhali ni mapenzi mema kwa genge lake.
   
 13. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #13
  Sep 23, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  CHADEMA wekeni huu waraka hapa sisi tuusambaze, mwisho wataona aibu tu. Mambo bado JK...
   
 14. r

  rafiki2010 Member

  #14
  Sep 23, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizi zote ni harakati za kampein . CHADEMA si chama chenye mikakati zaidi ya kupiga makelele kwenye majukwaa kisha kusahau yaliyowapeleka ni jukwaani na kutangaza sera zao . kama iwapo chama kimeshindwa kujenga misingi imara kwa manufa ya chama chao kwani kuna sehemu hakuna hata ofisi ya chama ingawa ina pata rudhuku kutoka serikalini , je itawezakana vipi kufanikisha maendeleo ya taifa zima iwapo omeshindwa kumudu mafaniko ya chama , kwasababu inajionyesha dhahiri kwani hata chama chenye mipango madhubuti ya maendeleo hujipanga toka chini na si kukurupuka . kwa maana hiyo upinzani kwa CCM bado kwa wapinzani vyama vijipamge kwanza ili kutimiza adhima yao
   
 15. F

  Froida JF-Expert Member

  #15
  Sep 23, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  NI vizuri kuwa na ndoto za alinacha maishani wanasaikolojia huwa wanasema unaweza kujipa raha kwa kuamini yale ysiowezekanika kuwa yatawezekana endelea kusema wapinzani bado kwa CCM ngoja tarehe 31-0ctober,wapelekee salamu kwamba safari hii CCM lazima igalagazwe tuu hakuna namna nyingine
   
 16. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #16
  Sep 23, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,415
  Likes Received: 5,687
  Trophy Points: 280

  ataishi kwa matumaini gani wakati ashakata tamaa ya maisha na bado anaenda kupigia kura kikwete loh
   
 17. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #17
  Sep 23, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Hayo mawazo mgando yeayoweza kutolewa na mtu mwenye akili hasi tu! Wewe unajua CHADEMA inapokea Tsh Ngapi ya Ruzuku? Unajua ripoti ya matumizi ya chama? CHADEMA ni chama kinachoendeshwa kwa kujitolea, si chama cha mafisadi kama CCM chenye "uwezo" wa kumgharamia mpaka mke wa mgombea uraisi maakumi ya mamilioni kila siku! Wewe na CCM mlioongoza nchi hii toka uhuru ndy manaofahamu maendeleo yanapatikanaje-ndy sababu mmeifikisha hii nchi mahali ilipo! Mapato ya nchi hii ni makubwa sana Liziwani, kama msingekuwa mnayagawana nyie na wajomba zako! umewahi kujiuliza gharama inayotumika kumsafilisha mama yako kwa siku kwenda kwenye kampeni kama inaweza kujenga dispensary moja huko Mpandachawe?! Mmejaa roho za ubinafsi na urroho! Kama nchi hii imewashinda kwa miaka zaidi ya hamsini, leo ndy mtaiweza? Tunahitaji mabadiliko, WE NEED CHANGE!!
   
 18. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #18
  Sep 23, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Na sasa hv mtachungulia sana kwenye Forums, habari nyepesinyepesi zinaniambia kuwa hata shemeji salma amejiunga humu siku kadhaa zilizopita kwa username flani! NAKUAMBIENI WAZI KUWA, IMEKULA KWENU! watanzania wa leo hawaogofwi na nyau tena, fungeni virago kabla ya oktober, MTAFUNGWA.
   
 19. m

  muafaka Senior Member

  #19
  Sep 23, 2010
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kugombea urais!!, kunasa nyaraka!!, macho yangu mwaka huu. Nilidhani siasa ni kunadi sera !!
   
 20. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #20
  Sep 23, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  mwenye nao anipatie nitauweka hapa na kuutuma kwenye emails kibao nilizonazo kwenye database
   
Loading...