Nguvu ya Hoja
JF-Expert Member
- Oct 10, 2012
- 276
- 125
Kabla sijafafanua mahali wanapokutana waheshimiwa wengi kwa wakati mmoja,naomba nitoe historia fupi iliyonifikisha mahali wanapokutana wanasiasa na watu maarufu kwa pamoja.
Ni hivi, bosi wangu alifiwa na shemeji yake huko kijiji cha Rubale wilaya ya Bukoba na ikabidi tusafiri kwenda msibani,baada ya shughuli ya msiba tulielelkea kijijini kwa bosi Ibwera,kwa vile alikuwa anashughulikia kuingiza umeme kwenye nyumba yake mpya,tulikaa pale mimi na wenzangu kwa takribani siku 6, na tukiwa hapo Ibwera ndipo nikajua mambo mengi sana kuhusu wanasiasa wetu na watu mashuhuri kama ifuatavyo:
Hapa ndipo nyumbani kwa mhe. Twaha Tasilima wa CUF na mbunge wa Afrika Mashariki,nyumbani kwa Wilifred Lwakatare wa Chadema,nyumbani kwa Josephine Mushumbusi mke wa Dk. Slaa,nyumbani kwa prof. Ruhangisa wa Escrow,nyumbani kwa ndg. Khalid Kangezi mlinzi wa zamani wa Dk. Slaa,kwa mzee mwenzake Lowassa, mzee Lenson ambapo watoto wao wameoana,hapa ni nyumbani kwa DK.Medard Mutungi muasisi wa Chadema na Baba yake msajili wa vyama vya siasa Tanzania.
Pia hapa ndipo ilipo familia ya kizungu ya mama Kinje mke wa mzee Kingunge,hapa ndipo alipoolea balozi Khamis Kagasheki(japo inadaiwa mkewe waliachana).Hayo ni maeneo niliyofikishwa mimi mwenyewe kwa kuonyeshwa kuwa hapa ni kwa fulani na pale ni kwa fulani.
Katika kutafutwa kuungwa mkono na watu wa eneo hili pia mbunge wao wa sasa ndg Rweikiza amenunua nyumba hapo na sasa naye anajiita mtu wa Ibwera ila nimeambiwa kuwa yeye sio wa pale.
Kwa kweli nimeshangazwa sana na umaarufu wa kisiasa wa eneo hili,na Dk Slaa ni maarufu sana kwani nasikia kuna kipindi alikuja likizo huku akatembelea watu wengi majumbani mwao hata nyumbani kwa diwani wa CCM alikula pale chakula,pia Lowassa naye amefika kwa mzee mwenzake mara kadhaa.
Hapa ndipo wanapokutana wanasiasa hawa,wengine ni kwao wengine ukweni na wengine kwa wazee wenzao,ni umbali kama km 40 hivi kutoka mjini Bukoba.