dr.slaa amepoteza mvuto kabisa
Kinyume chake!!Dr.Slaa anazidi kuchuja kila siku.
chadema tuunde serikali yetu ya tanganyika bana,,ccm wanatuzingua sana
Hatuna haja na elton kama wewe hebu kaangalie tbccm mkulu wenu kapeleka bakuli kwa kameruni..
Dr Slaa anashukuru kwa muda, anasema ni muda muafaka kujadili jambo kama hili, anasema Katiba kwa tabia zake ni chombo cha kisiasa, kwa bahati mbaya watu wengi hawajui, watu wengi wanasema wanasiasa wameuteka mjadala wa katiba, naomba niweke sawa kwamba suala la katiba kimsingi ni suala la kisiasa, wengi watakumbuka kwamba mjadala wa katiba pamoja na jinsi nilivyolieleza mimi kwamba nilibeba kwenye ilani ya chadema 2010, lakini kumbuka kwamba suala la katiba liliombwa toka mwaka 1992, takriban miaka 20, wakati huo sikuwa mwanasiasa, hivyo huu mjadala haukuanza leo, kuna watu walikamatwa wakati ule kwasababu ya mfumo wa chama kimoja. Katiba kwa kawaida ni chombo kinachowaambia watawala kwamba sisi wananchi tunataka mtuongoze hivi, siyo watawala wawaambie wananchi tutawaongoza hivi.
Inapofika mahali kwamba waliopo ndani ya bunge wanajiona wapo juu ya wananchi, ni lazima wale walioanzisha mchakato sasa tuingilie, tumeona siku 42 bunge letu bado linajadili kanuni. Tuliishauri serikali maandalizi mahususi yafanyike, sasa kitendo cha kutumia siku 42 ni kiburi cha serikali kwa watanzania
Da kamchana vibaya JK na hotuba yake.
CCM kwa kuogopa serikali 3 wameamua kufanya kila aina ya propaganda! Viwanjani, wizara ya habari na michezo nao wamekuwa waandaa midahalo.
Rais wa mioyoni wa Watanzania.
Tuache ushabiki na watu tuache kujitoa ufahamu na tusiwe watumwa wa fikra lazima sasa kuna vitu kama mtu mzima na una akili zako timamu sio lazima ukae darasani ufundishwe juu ya huyu Dr.Slaa..huyu mzee ni Gifted jamani...huyu ni zaidi ya kiongozi....Hongera sana Dr.Slaa..huyu mtu hata kama akiongea masaa zaidi ya saba kamwe hutochoka kumsikiliza,kuna wakati hadi roho inauma why huyu mtu hakuwa Rais wa nchii hii!
Mleta pumba mashuhuri yuko uingereza kwa kipindi hiki.
CHADEMA WAMTELEKEZA MGOMBEA UBUNGE WAO CHALINZE
Zikiwa zimebakia siku zisizozidi sita wananchi wa Chalinze kupiga kura kuchagua mbunge wao, ni dhahiri kuwa Viongozi wa juu wa Chadema wamemtelekeza mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chadema jimboni humo Bw. Mathayo.
Mwananchi mmoja akilalamikia hili anasema, "..tulidhani Chadema ni Chama ya ukombozi, tukadhani maneno ya kuwa kinabagua na kutoa upendeleo kwa wachaga tu ni propaganda za CCM kumbe kweli bwana! Hivi huyu bwana angekuwa mchaga wasingeleta CHOPA hapa?,huku ni kumtelekeza Mathayo kisa sio mchaga!" Alilalamika kijana wa kimasai wa Chalinze mjini.
sema moyoni kwako. unamsifia mbulu mwenzako