Dr.Slaa live ITV akichambua hotuba ya Kikwete

Dr.Slaa live ITV akichambua hotuba ya Kikwete

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,648
Reaction score
164,807
Msikilize Dr.Slaa live ITV akiongelea sakata la Escrow na hotuba ya Kiwete.

Dr.Slaa, anamlaumu raisi Kikwete kwa kukosa uzalendo kwa jinsi anavyoshughulikia sakata hili la Escrow na kumlaumu kwa kuvunja katiba.

Dr.Slaa amlaumu Kikwete kwa double standard.Yaani kumuondoa Tibaijuka kazini na kumuweka kiporo Muhongo.Pia, amehoji utaratibu wa kumuweka mwanasiasa kiporo.

Dr.Slaa anasema Kikwete anapuuza bunge na kwamba hivi sasa ni serikali inayolisimamia bunge na si bunge linaisimamia serikali.

Dr.Slaa anasema Seth anastahili kuwa amekamatwa kwa kugushi nyaraka na pia kutolipa kodi na kwamba raisi anafumbia macho.

Dr.Slaa anasema singasinga huyu ana uhusiano na Ikulu kwa muda mrefu na ndio maana hachukuliwi hatua.

Pia,Dr.Slaa ameishaangaa polisi kupewa msaada wa fedha na singa singa.

Dr.Slaa pia anashangaa raisi kuwasiliana kwa email na mtuhumiwa mmoja na huku mtuhumiwa huyo akimwita raisi "dear".

Dr.Slaa anungana na maaskofu kutaka uwajibikaji wa watuhumiwa wa sakata hili na pia ameungana na wanaosema raisi anapaswa kujiuzulu(Deus Kibamba ni mmoja wa watu waliotoa kauli kuwa, kwa sakata hili,hata raisi anapaswa kuondoka madarakani-Tanzania Daima la leo).

Dr.Slaa amemalizia kwa kusema hawana chuki binafsi na Muhongo wa raisi.
 
Anaichambua hotuba ya rais

UP DATE;

Aeleza kuwa makosa ya Muhongo pamoja na mengine ambayo hayajawekwa wazi alisimamia masuala ambayo ambayo ni jinai.

Jinai kwa;
i. kughushi nyaraka
ii. kukwepa kodi

Aituhumu ikulu kuwa mhuusika mkuu katika sakata hili kupitia msimamizi mkuu wa ikulu Ngurumo

-Asema wakati bunge lindili Rugemalila alikuwa akimtumia e-mail Kikwete kwa kumwita Dear JK.
 
  • Thanks
Reactions: jme
Babu anajidai Eti kageuka Sumaku (magnet)ya kunasa mawasiliano. Kila mtu anajua kuwa unaweza kuanzisha Email mbili tofauti kwa kutumia majina unayotaka then ukarusha email ukaenda kutangaza umenasa mawasiliano.mfano fmbowe@yahoo.com na nyingine drslaa@Gmail.com then ukarusha any sms kutoka one account kwenda nyingine ukajitokeza kujifanya Sumaku ya kudaka mawasiliano.
 
Pole inakuuma wala hakuna mkombozi ambae hakuonekana kama kichaa lkn baadae ikajulikana kuwa n mkombozi
 
mna hangover mbona hamuandiki anachoongea?
 
ImageUploadedByJamiiForums1419568046.154901.jpg
Ni ITV na sio Star TV
 
Nimegundua slaa ni mtu makini sana! Anasema jk ingekuwa ni nchi nyingine angesha jiuzulu.
 
Back
Top Bottom