Dr. Slaa kuzungumza na Vyombo vya Habari, Serena Hotel - Septemba 1, 2015

Status
Not open for further replies.
Aongee asiongee atajua mwenyewe

Haturudi nyuma sie

Umenisemea yote na zaidi Mimi kwa kule kuonyesha kujitenga nilisha muhukumu kama msaliti.na kumfunga nje ya fikira zangu.ataa hivi anaitisha press ni habari inayotia kichefuchefu kwangu
 
pole sana mkereketwa; naona una wakati mgumu sana leo

nina wakati MZURI au MGUMU? kwa miezi 5 mfululizo TANECCM wanakata umeme saa 12 asubuhi na kuwasha saa 5 usiku. siku CCM walipozindua kampeni nilikuwa na wakati mzuri kwa kuwa umeme haukukatwa. na leo umeme haujakatwa pia. hii ni FURAHA kuu kwangu kwa kuwa leo nitafanya shughuli zangu vizuri. siku UKAWA wanazindua kampeni nilipata hasara kwani umeme ulikatwa tangu asubuhi na kurejeshwa mara mkutano wa ufunguzi ulipoisha. umeona eeh?
 
Mzee wangu, kwa heshima nyingi ulizojijengea, huna sababu yoyote ya kurudi nyuma. Mungu akusaidie kuchagua fungu lililo njema. Sio wote tuliopenda wewe kuenguliwa ki hivyo. Lakini pamoja na kwamba hatukupenda yote yaliyotokea lakini bado tupo na wapiganaji wote wa CHADEMA na UKAWA. Tukiwa tunafahamu kuwa lengo letu ni moja ndani ya ukawa, bila kujalisha nani ni kiongozi wa kuongoza mabadiliko haya.

Tunakuomba urudi kwa moyo moja uungane nasi tuwe kitu kimoja ktk kipindi hiki. Uamuzi wowote wa kurudi kundini utafurahiwa hata na Malaika wa mbinguni.

Mimi ni mtu mdogo sana kukushauri lakini pia hakuna ushauri wa mtoto, ushauri ni ushauri. Naomba ubaki kuwa kiongozi wetu ndani ya chama. Wapinzani wetu wanafurahishwa na hiki kitendo cha kutenganishwa nawe na siku zote macho na masikio yao ni kuhusu lini tutavurugana. Naamini tutawasikiliza na utaungana na sisi wengine ambao bado tuna imani nawe lakini bado tunapambana kama askari wengine tukiwa na imani kuwa tutashinda.

Tunakuomba usijaribu kutoa maneno yoyote ya kutukatisha tamaa, utupe au utuongezee moyo wa kushinda vita hii.

Hakika leo ukikubali kuungana nasi, nitamsifu sana Mungu wetu kwa ushindi uliotukuka. Wewe ni baba na Kiongozi, ututazame kwa moyo wa huruma. Wewe ni nembo ya CHADEMA na huna budi kubaki nasi.

Nikusihi kwa msemo wangu niupendao sana na ndio mara zote unanifariji. Ni kwamba, ''Katika vita yoyote, ukiwa mstari wa mbele vitani usiangalie nyuma kuona ni maadui wangapi mmeua bali tuangalie mbele muda wote tuone tuna maadui wangapi ili tupate ushindi''.
 
Makanda nitakuwa nawajuzi masaa yaliyo baki Dr kuja kuwatibu!
Sasa yamebaki masaa manne tuu...!

Poleni makanda mtapona tuu japo dawa inauma!
Duuu kweli siasa ni unafiki mtupu,wewe ulikuwa ukimkandya Dr.W.P.SLAA kila uchao hapo JF,leo hii amegeuka kuwa malaika?. Ninavyomjua Dokta hawezi kuyumbishwa na wanafiki.
 
Last edited by a moderator:
DEMOKRASIA IFATWE TU
KAMA AKIAMUA KUBWAGA MANYANGA KISIASA,BAAS
KAMA AKIAMUA KUBAKI CHADEMA,IT IS OK
KAMA AKIAMUA KUJIUNGA NA CHAMA CHOCHOTE,nayo ni RUKSA na hiyo NDO DEMOKRASIA real
TANZANIA YANGU
MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
aiseee shikamooo tanzania hii karata ya leo chadema wanaweza cheka au kulia, same same na CCM
 
dr slaa leo anarejea rasmi kazini...magamba mjiandae kupokea dozi kali kutoka kwa kamanda dr w.p slaa.
 
dr slaa leo anarejea rasmi kazini...magamba mjiandae kupokea dozi kali kutoka kwa kamanda dr w.p slaa.

Dr Slaa hawezi kurudi katika kundi linalopotea la chadema na hakika leo mzee Slaa atatoa dira ya Tanzania tuitakayo chini ya Jemedari Magufuli
 
basi hapo CCM ndo wanaona watalamba karata dume........ Forget that aisee..... Dr Slaa ataongea katika maelezo ambayo yatazidi kuididimiza CCM.... hawez saliti chama....
 
mzee wangu, kwa heshima nyingi ulizojijengea, huna sababu yoyote ya kurudi nyuma. Mungu akusaidie kuchagua fungu lililo njema. Sio wote tuliopenda wewe kuenguliwa ki hivyo. Lakini pamoja na kwamba hatukupenda yote yaliyotokea lakini bado tupo na wapiganaji wote wa chadema na ukawa. Tukiwa tunafahamu kuwa lengo letu ni moja ndani ya ukawa, bila kujalisha nani ni kiongozi wa kuongoza mabadiliko haya.

Tunakuomba urudi kwa moyo moja uungane nasi tuwe kitu kimoja ktk kipindi hiki. Uamuzi wowote wa kurudi kundini utafurahiwa hata na malaika wa mbinguni.

Mimi ni mtu mdogo sana kukushauri lakini pia hakuna ushauri wa mtoto, ushauri ni ushauri. Naomba ubaki kuwa kiongozi wetu ndani ya chama. Wapinzani wetu wanafurahishwa na hiki kitendo cha kutenganishwa nawe na siku zote macho na masikio yao ni kuhusu lini tutavurugana. Naamini tutawasikiliza na utaungana na sisi wengine ambao bado tuna imani nawe lakini bado tunapambana kama askari wengine tukiwa na imani kuwa tutashinda.

Tunakuomba usijaribu kutoa maneno yoyote ya kutukatisha tamaa, utupe au utuongezee moyo wa kushinda vita hii.

Hakika leo ukikubali kuungana nasi, nitamsifu sana mungu wetu kwa ushindi uliotukuka. Wewe ni baba na kiongozi, ututazame kwa moyo wa huruma. Wewe ni nembo ya chadema na huna budi kubaki nasi.

Nikusihi kwa msemo wangu niupendao sana na ndio mara zote unanifariji. Ni kwamba, ''katika vita yoyote, ukiwa mstari wa mbele vitani usiangalie nyuma kuona ni maadui wangapi mmeua bali tuangalie mbele muda wote tuone tuna maadui wangapi ili tupate ushindi''.

mlichomfanyia slaa ni wema? Au unafikiri ye hana moyo au ana moyo wa chuma? Siku zoote hapa memsahau leo; mko na fisadi lenu; leo hii kwakuwa anasema anataka kuongea na vyombo vya habari ndo mnajifanya kumuona wa maana! Acheni unafiki bwana
 
Yule Mzee ana misimamo ya hatari, hakukubaliana na ujio wa Lowasa Chadema, nategemena the best he could do ni kustaafu siasa.

Harudi kokote kule...
 
Tulia wewe mwana Chadema msulubiwe leo dhambi yenu ya usaliti acha kumchezea Dr Slaa
Mzee wangu, kwa heshima nyingi ulizojijengea, huna sababu yoyote ya kurudi nyuma. Mungu akusaidie kuchagua fungu lililo njema. Sio wote tuliopenda wewe kuenguliwa ki hivyo. Lakini pamoja na kwamba hatukupenda yote yaliyotokea lakini bado tupo na wapiganaji wote wa CHADEMA na UKAWA. Tukiwa tunafahamu kuwa lengo letu ni moja ndani ya ukawa, bila kujalisha nani ni kiongozi wa kuongoza mabadiliko haya.

Tunakuomba urudi kwa moyo moja uungane nasi tuwe kitu kimoja ktk kipindi hiki. Uamuzi wowote wa kurudi kundini utafurahiwa hata na Malaika wa mbinguni.

Mimi ni mtu mdogo sana kukushauri lakini pia hakuna ushauri wa mtoto, ushauri ni ushauri. Naomba ubaki kuwa kiongozi wetu ndani ya chama. Wapinzani wetu wanafurahishwa na hiki kitendo cha kutenganishwa nawe na siku zote macho na masikio yao ni kuhusu lini tutavurugana. Naamini tutawasikiliza na utaungana na sisi wengine ambao bado tuna imani nawe lakini bado tunapambana kama askari wengine tukiwa na imani kuwa tutashinda.

Tunakuomba usijaribu kutoa maneno yoyote ya kutukatisha tamaa, utupe au utuongezee moyo wa kushinda vita hii.

Hakika leo ukikubali kuungana nasi, nitamsifu sana Mungu wetu kwa ushindi uliotukuka. Wewe ni baba na Kiongozi, ututazame kwa moyo wa huruma. Wewe ni nembo ya CHADEMA na huna budi kubaki nasi.

Nikusihi kwa msemo wangu niupendao sana na ndio mara zote unanifariji. Ni kwamba, ''Katika vita yoyote, ukiwa mstari wa mbele vitani usiangalie nyuma kuona ni maadui wangapi mmeua bali tuangalie mbele muda wote tuone tuna maadui wangapi ili tupate ushindi''.
 
WATANZANIA TUMPUUZE DR SLAA.
By Fandre

Dhambi ya UNAFIKI, USALITI na TAMAA ya Madaraka inaendelea kumtesa Dr Slaa.Ikumbukwe, Aliwasaliti wakatoriki aliokua akiwaongoza, aliisaliti ndoa yake na mkewe Rose Kamili.

Ikumbukwe mwaka 2010, Mh Mbowe kwa ajili ya mapenzi yake mema kwa Taifa na moyo wa uzalendo aliona ni heri kukaa pembeni na kumpisha Dr Slaa agombee Urais kwa tiketi ya CHADEMA. Jambo hili litakumbukwa daima kwakua Mh Mbowe aliweka mbali mapenzi yake binafsi na kulijali taifa ili kuleta mabadiliko.

Safari ya Mabadiliko ni safari ya KUJIKANA NAFSI yako, ndio maana hata katika kitabu cha Biblia kuna mahali mtu mmoja alimwuliza Yesu.."nifanyeje nipate kuurithi Ufalme wa Mbinguni?" ndipo Yesu akamjibu akamwambia KAUZE MALI ZAKO ZOTE KISHA UNIFATE. Hapa tunajifunza Safari ya Mabadiliko yeyote inaendana na kuikana nafsi yako, kuua mapenzi na tamaa zako binafsi na kuwa tayari kuweka maamuzi ya wengi ambao wana nia na malengo ya Mabadiliko kuwa ndio msingi ili mabadiliko yatokee.

Tabia ya kususa, kudengua au kutaka kuonekana wewe ni bora sana mbele ya kila Mtanzania wakati huwezi kuikana nafsi yako kwa ajili ya MABADILIKO ni jambo la kijinga ambalo linachukiza sana.

Laana ya MABADILIKO itawapata wote watakaokubali kurubuniwa na CCM ili kuharibu umoja wenye nguvu wa UKAWA ambao ndio njia sahihi ya kuiondoa CCM Madarakani mwaka huu.

Dr Slaa, usiyarudie matapishi yako wala kuidharau kazi nzuri uliyoianza kuijenga kwa miaka mingi ukiwa pamoja na makamanda wenzako. Mlijiaminisha kwetu na Tuliwaamini kuwa mnaweza kuleta mabadiliko nchini.

Tunafahamu fika ya kuwa CCM inajua ya kwamba imeshapoteza na mwaka huu ndio kiama chake hivyo inafanya kila njia kuhakikisha inaharibu umoja wa UKAWA kwa kuwahonga na kuwanunua baadhi ya waasisi wa UKAWA ili kuvunja vuguvugu hili la mabadiliko nchini.

TUMPUUZE DR SLAA
Watanzania wenzangu, wapenda Mabadiliko na wananchi wote tuliochoka na mateso, dhiki na umasikini tuliovikwa na CCM kwa muda wote tangu uhuru wa nchi hii leo tumuonyeshe Dr Slaa kuwa umoja wetu hautavunjwa na maneno machache yasitoka moyoni mwa Slaa ila yanayoshinikizwa na nguvu ya pesa toka CCM.

Kama akina Mh Mbowe walijikana na kuacha wenzao wenye mashiko wagombee kwa sababu ya Uzalendo, inashindikanaje kwa Dr Slaa?

Tujiulize maswali..."Je, huyu ndio Dr Slaa yule tunayemfahamu?"

Dr Slaa aliyevunjwa mkono, Dr Slaa ambaye mke wake alipigwa na serikali ya CCM, Dr Slaa ambaye aliwashawishi watanzania kuunga mkono harakati za mabadiliko kwa miaka mingi na hata wengi kufa na kuwa walemavu wa maisha yao yote?

Leo akiyapa kisogo mambo yote hayo na kuamua kuwaunga mkono watu waliomtesa kwa miaka mingi na waliowaua makamanda wenzake wengi tutajifunza nini kama Taifa?

Maamuzi yeyote ya Dr Slaa kuiunga mkono CCM ni maamuzi ya kibinafsi, kikatili, kijambazi, kinafiki na maamuzi ya kijinga ambayo laana ya mabadiliko haitaiacha nyumba yake miaka yote.

Tutasema ukweli Daima, Dr Slaa asingeweza kuleta mapinduzi haya makubwa katika siasa za Tanzania kwani alishachuja katika siasa za Ushawishi na Kupendwa(Charismatic) na kila mtu kama ilivyo kwa Mh. Lowassa.

Safari ya Mabadiliko haitasimama mpaka tutakapokua tumeridhika na serikali tutakaitaka, serikali yenye uwezo wa kuwafanya watanzania wakanufaika na rasilimali zao.

Mabadiliko haya hatazuiwa na Dr Slaa, Prof Lipumba wala shetani au jini yeyote kwa maana hata Mungu mwenyewe ameyaona mateso ya watanzania kwa muda mrefu sasa.

Mwisho namaliza na kusema, Safari hii ngumu ya Mabadiliko itasalitiwa na wengi ila mwisho watakosa mahali pa kujificha na aibu hii kwani Watanzania tutashinda vita hii na kuiweka serikali mpya yenye kuwajali wananchi.

Tumpuuze Dr Slaa leo na tumdharau kwa maamuzi yeyote mabaya atakayoyafanya kinyume na mabadiliko wanayoyahitaji watanzania. Tulimpuuza Lipumba sasa ni zamu ya kumpuuza huyu mwingine.

#Tanzania Mpya Inakuja
#Safari ya Mabadiliko
#Chagua Lowassa
#Chagua UKAWA
 
The best way ni kuzunguka nchi nzima kumnadi Dr Magufuli na kuwaambia Watanzania mabaya ya lowasa na wanachadema waliosaliti harakati za chadema kwenda Ikulu chini ya Dr slaa
Yule Mzee ana misimamo ya hatari, hakukubaliana na ujio wa Lowasa Chadema, nategemena the best he could do ni kustaafu siasa.

Harudi kokote kule...
 
mlichomfanyia slaa ni wema? Au unafikiri ye hana moyo au ana moyo wa chuma? Siku zoote hapa memsahau leo; mko na fisadi lenu; leo hii kwakuwa anasema anataka kuongea na vyombo vya habari ndo mnajifanya kumuona wa maana! Acheni unafiki bwana

mbona na yeye alikuwepo na kukubali lowassa akaribishwe cdm!!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom