Dr. Slaa kutogombea urais 2015 kupitia CHADEMA

Dr. Slaa kutogombea urais 2015 kupitia CHADEMA

Asante kwa umbea au kutafuta taarifa.Kama unatafuta taarifa sidhani kama utafanikiwa kwa namna ulivyokuja.Kwa nn usifikiri kuwa Slaa hagombei,atagombea Lissu au prof Safari? Anyways,ngoja wadau waje wakujibu.
Karibu tena ndugu
Jambo leo wako kAZINI
 
Huu mtego utawachanganya sana kamati kuu ya CCM, maana wakimtosa mtu mwenye nguvu ndani ya chama chao kwa sababu tu za ki-fitna- basi sisi wazanaki huwa tuna kamsemo kanasema "mali ganyanja"
 
Chadema ipi hiyo anayohamia kada wa ccm kama hao uliowataja? Hii iliyofia kalenga?

hivi na wewe kweli unajivunia ushindi wa kalenga na chaguzi nyingine za hapa TANZANIA,huwa unaamini kweli CCM inashinda kihalali!?au ndo yaleyale ya ushindi ni ushindi tu hata kama ni goli la mkono au offsaidi.
 
Imefahamika sasa kuwa katibu mkuu wa Chadema Dr.Wilbroad Slaa hatogombea urais kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu wa 2015 tofauti na inavyodhaniwa na wanachama, wapenzi na wafuasi wa chadema.taarifa za kuaminka toka ndani ya uongozi wa juu wa Chadema makao makuu zinaeleza kuwa chama hicho kimejipanga “kunufaika” na mnyukano uliopo ndani ya ccm kuhusu mgombea urais huku kikijipanga “kumsajili” mmoja wa makada wa ccm atakaeonekana kuwa na nguvu katika kinyang’anyiro cha uteuzi wa mgombea urais kupitia CCM (bila kujali “taswira” yake mbele ya jamii) kama ilivyokuwa kwa Mrema na NCCR- Mageuzi katika uchaguzi wa 1995.

Kuibuka kwa taarifa hizi kumekuja wakati ambapo wanaotajwa kuusaka urais kupitia ccm wakijipanga na kuunda makundi ndani na nje ya ccm ili kujiimarisha kuelekea 2015.uwanja mwingine wa mapambano ya urais umekuwa bunge maalumu la katiba ambalo linadaiwa kuwa turufu pekee ya Samwel Sitta ambaye ametajwa kuwa mmoja wa walengwa wanaosubiriwa chadema iwapo watatemwa na ccm.wengine ni pamoja na edward lowassa na Fredrick Sumaye ambaye imeelezwa kuwa “havutii sana”.Hii ni mara ya pili kwa Lowassa kuhusishwa na mipango ya kujiunga chadema hasa baada ya aliyekuwa kada wa ccm na mfuasi mkuu wa Lowassa huko Arusha Bw.James ole Millya kujiunga chadema.

Nawasilisha
CHADEMA hakina mpango na mafisadi zaidi ya kuwashughulikia na sio kuwakumbatia, hizo porojo zako ndio zinazokuweka mjini nenda Lumumba ukachukue 7000 zako
 
Binafsi ninaunga mkono Dr. Silaa kuachana na ndoto za Urais, regardless kama hii habari ni kweli ama si kweli.
 
By the way, wether agombee au asigombee, HAWEZI LETA ANY SEQUEL, HE IS LESS MOMENTOUS
 
Dr akiacha hiyo nafasi,Josephine si wake tena,mushumbus ndoto zake kuwa mke wa Rais,ata Wa wangwasuma
 
Back
Top Bottom