Dr. Slaa kutogombea urais 2015 kupitia CHADEMA

Dr. Slaa kutogombea urais 2015 kupitia CHADEMA

Seif al Islam

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2011
Posts
2,156
Reaction score
640
Imefahamika sasa kuwa katibu mkuu wa Chadema Dr.Wilbroad Slaa hatogombea urais kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu wa 2015 tofauti na inavyodhaniwa na wanachama, wapenzi na wafuasi wa chadema.taarifa za kuaminka toka ndani ya uongozi wa juu wa Chadema makao makuu zinaeleza kuwa chama hicho kimejipanga "kunufaika" na mnyukano uliopo ndani ya ccm kuhusu mgombea urais huku kikijipanga "kumsajili" mmoja wa makada wa ccm atakaeonekana kuwa na nguvu katika kinyang'anyiro cha uteuzi wa mgombea urais kupitia CCM (bila kujali "taswira" yake mbele ya jamii) kama ilivyokuwa kwa Mrema na NCCR- Mageuzi katika uchaguzi wa 1995.

Kuibuka kwa taarifa hizi kumekuja wakati ambapo wanaotajwa kuusaka urais kupitia ccm wakijipanga na kuunda makundi ndani na nje ya ccm ili kujiimarisha kuelekea 2015.uwanja mwingine wa mapambano ya urais umekuwa bunge maalumu la katiba ambalo linadaiwa kuwa turufu pekee ya Samwel Sitta ambaye ametajwa kuwa mmoja wa walengwa wanaosubiriwa chadema iwapo watatemwa na ccm.wengine ni pamoja na edward lowassa na Fredrick Sumaye ambaye imeelezwa kuwa "havutii sana".Hii ni mara ya pili kwa Lowassa kuhusishwa na mipango ya kujiunga chadema hasa baada ya aliyekuwa kada wa ccm na mfuasi mkuu wa Lowassa huko Arusha Bw.James ole Millya kujiunga chadema.

Nawasilisha
 
Wewe ni msemaji wa CDM mkuu? CDM ina mfumo wa utoaji wa taarifa nyeti za ndani hapa JF!!! Ngoja tusubiri akina Tumaini Makene, Ben Saanane waje watupe taarifa kamili!!!! Sidhani kama ni kweli hii!!!
 
Haya una haki ya kutoa maoni yako hata kama ni uongo!
 
Asante kwa umbea au kutafuta taarifa.Kama unatafuta taarifa sidhani kama utafanikiwa kwa namna ulivyokuja.Kwa nn usifikiri kuwa Slaa hagombei,atagombea Lissu au prof Safari? Anyways,ngoja wadau waje wakujibu.
Karibu tena ndugu
 
Kawasilishe kwa wajinga wenzio wanaokataa maoni ya wananchi wanataka mahaba ya chama chao cha mafisadi na majangili wanaotaka serikali mbili.
 
Kwa hiyo chagadema inaikubali ccm na mapigo yake ndio mana inatamani makada wake wahamie huko
 
Chadema ipi hiyo anayohamia kada wa ccm kama hao uliowataja? Hii iliyofia kalenga?
 
Ndiyo maana Lowassa huwa haongelei CHADEMA mahala popote pale huwa anawaita hivi "hawa wenzetu" wala hakuwahi kuwatukana hasa huku Arusha anapofanya siasa yake wala CHADEMA huwa hawamnan'ngi sana kama wengine ila Wenje kule mwanza ndo ujaribu kurusha mabomu ya kisiasa kwake
 
Umeanza lini kuwa msemaji wa CHADEMA???
 
taarifa za kuaminka toka ndani ya uongozi wa juu wa Chadema makao makuu zinaeleza kuwa chama hicho kimejipanga “kunufaika” na mnyukano uliopo ndani ya ccm kuhusu mgombea urais huku kikijipanga “kumsajili” mmoja wa makada wa ccm atakaeonekana kuwa na nguvu katika kinyang’anyiro cha uteuzi wa mgombea urais kupitia CCM (bila kujali “taswira” yake mbele ya jamii) kama ilivyokuwa kwa Mrema na NCCR- Mageuzi katika uchaguzi wa 1995.

Alisema (Mbowe) kwamba chama hicho hakitasubiri wala kupokea waliokosa fursa za uteuzi katika vyama vingine, kikiwemo Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambao wanaokimbilia Chadema dakika za mwisho akisema kuwa uzoefu umeonyesha wengi wao wanaendelea kuwa mamluki.


Kama watakuwa wamepiga U-turn na kuwapokea hao "mamluki" basi kitakuwa ni chama ambacho hakina msimamo.
 
Imefahamika sasa kuwa katibu mkuu wa Chadema Dr.Wilbroad Slaa hatogombea urais kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu wa 2015 tofauti na inavyodhaniwa na wanachama, wapenzi na wafuasi wa chadema.taarifa za kuaminka toka ndani ya uongozi wa juu wa Chadema makao makuu zinaeleza kuwa chama hicho kimejipanga “kunufaika” na mnyukano uliopo ndani ya ccm kuhusu mgombea urais huku kikijipanga “kumsajili” mmoja wa makada wa ccm atakaeonekana kuwa na nguvu katika kinyang’anyiro cha uteuzi wa mgombea urais kupitia CCM (bila kujali “taswira” yake mbele ya jamii) kama ilivyokuwa kwa Mrema na NCCR- Mageuzi katika uchaguzi wa 1995.

Kuibuka kwa taarifa hizi kumekuja wakati ambapo wanaotajwa kuusaka urais kupitia ccm wakijipanga na kuunda makundi ndani na nje ya ccm ili kujiimarisha kuelekea 2015.uwanja mwingine wa mapambano ya urais umekuwa bunge maalumu la katiba ambalo linadaiwa kuwa turufu pekee ya Samwel Sitta ambaye ametajwa kuwa mmoja wa walengwa wanaosubiriwa chadema iwapo watatemwa na ccm.wengine ni pamoja na edward lowassa na Fredrick Sumaye ambaye imeelezwa kuwa “havutii sana”.Hii ni mara ya pili kwa Lowassa kuhusishwa na mipango ya kujiunga chadema hasa baada ya aliyekuwa kada wa ccm na mfuasi mkuu wa Lowassa huko Arusha Bw.James ole Millya kujiunga chadema.

Nawasilisha

Mie yangu macho!
 
Alisema (Mbowe) kwamba chama hicho hakitasubiri wala kupokea waliokosa fursa za uteuzi katika vyama vingine, kikiwemo Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambao wanaokimbilia Chadema dakika za mwisho akisema kuwa uzoefu umeonyesha wengi wao wanaendelea kuwa mamluki.


Kama watakuwa wamepiga U-turn na kuwapokea hao "mamluki" basi kitakuwa ni chama ambacho hakina msimamo.
upepo hubadilika - cha msingi ni kumpiga adui yako counter attack.
 
Alisema (Mbowe) kwamba chama hicho hakitasubiri wala kupokea waliokosa fursa za uteuzi katika vyama vingine, kikiwemo Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambao wanaokimbilia Chadema dakika za mwisho akisema kuwa uzoefu umeonyesha wengi wao wanaendelea kuwa mamluki.


Kama watakuwa wamepiga U-turn na kuwapokea hao "mamluki" basi kitakuwa ni chama ambacho hakina msimamo.
Usipoteze muda wako kuamini anachosema Mbowe,ebu rudi nyuma jikumbushe sakata la shangingi l seriakli (KUB) na sasa liko wapi.

 
habari za uhakika kutoka makao makuu zinasema mzee wa sumu ben saanane atapeperusha bendera ya chadema kwenye kiti cha urais mwakani
 
Maskini Josephine hizi si habari njema kwake hata kidogo.Mission failed
 
Back
Top Bottom