Sisi wote ni wanafunzi na wahanga wa Dr. Slaa kifikra na kisiasa. Dr. Slaa umetufundisha watanzania wote kuwa CCM haifai na ndio chanzo cha ufisadi, ubadhilifu, wizi, matumizi mabaya na sera mbaya zisizotekelezaka na zilizosababisha maisha ya watanzania kuwa mabaya. Ukiwa na wenzako wa chadema kwa kutumia kampeni za sangara, M4C, redio na tv, ulitufundisha kuikataa CCM na tulikuelewa vizuri, tuliamini na tukafanya hivyo kwa moyo, kwa nguvu na kwa akili zetu zote. Wewe ndiye uliyesababisha taifa lote liichukie na kuikataa CCM kwa moyo na nguvu zote, watu wameshalielewa somo lako kuhusu ubaya wa CCM kwetu. Ulitufungua akili tuliokuwa hatujui siasa za chama cha CCM. Tulifanya hivyo kwakuamini kwamba wewe ni msomi mzuri na mtumishi wa Mungu husemi uongo na utakuwa umefanya utafiti mzuri kuhusu uhusiano uliyopo kati ya maisha ya watanzania na sera, utekelezaji wa sera na utawala wa CCM. Uliamsha hamasa na ari ya watanzania katika siasa na kufikiri juu ya maisha yao. Sasa tumeelimika sana kupitia wewe na wenzako wa chadema kuhusu ubaya wa CCM kwetu na kwa taifa, watu hawataki tena kusikia habari za CCM mitaani na maofisini. Ahsante sana baba!
Sasa wafuasi wako tumeanza kushikwa na butwaa kubwa kukuona wewe tena unakipigia debe CCM kiendelee kubakia madarakani!!!!@***&.com???. Hapa kuna mawili, ama wewe unataka kutugeuza sisi kichwa chini miguu juu, au wewe ndo umegeuka mwenyewe kichwa chini miguu juu. Tunajiuliza nini kimetokea kwa mwalimu wetu Dr. Slaa hadi kufanya hivi? Kama shida ni Lowassa kuhamia chadema basi hata wewe hukupaswa kuwa na uhalali wa kukilaumu CCM kwa ufisadi, ubadhilifu na huduma mbovu kwa wananchi, badala yake ulipaswa kuwalaumu viongozi waliotokana na CCM tu peke yake wasiofanya vizuri na sio chama chote cha CCM kuwa hakifai. Vinginevyo wewe ulikuwa katibu mkuu wa chadema hivyo ungeweza kuhakikisha kuwa rais (Lowassa) anayetokana na chama cha chadema angeongoza nchi kwa mujibu wa kanuni, taratibu na maadili ya chadema tu basi. Hivyo ukiwa kama katibu mkuu wa chadema hukuwa na sababu za msingi za kumuogopa Lowassa 'fisadi' kuhamia chadema au kugombea urais kupitia chadema maana chama chini ya katibu mkuu (wewe) kingemnyoosha na kumfanya kuongoza nchi kwa mujibu wa chadema. Kama hili limeshindikana kwako na kwa chadema kwanini ulitaka hili liwezekane kwa CCM? Ulikuwa unatudanganya kuhusu ubaya wa CCM? Ulipaswa kuwalaumu viongozi na watendaji wabaya wa CCM na sio chama cha CCM chote kama chama. Unapaswa kuwaomba samahani CCM hadharani kwa kukisema chama chao vibaya badala ya kumsema mwanachama/kiongozi wa CCM ambaye ni mwizi, mbadhilifu, fisadi, n.k, pili, uwaombe radhi watanzania kwa kuwapotosha kuhusu ubaya wa CCM kama chama.
Kama wewe ukishindwa kuyafanya haya yote mawili kwapamoja taifa hili litakuwa juu ya kichwa chako kwa kuliyumbisha na kutaka kulipasua vipande. CCM wanafunzi wako tunakuona kama mwalimu usiyekuwa na msimamo, uliyehongwa, mwenye ubinafsi wa kuwa rais kwa gharama yoyote, unayependa porojo, usiyependa maamuzi ya pamoja ndani ya chama, mpotoshaji, muongo, usiyejali wafuasi na familia yako, na usiyefaa kusikilizwa tena na watu wenye shida za maisha kama sisi. Hatujui kesho tena utasema nini, utakuwa wapi na nani. Kwaheri huwaminiki mzee!!!
Kwa mleta mada,
Sioni kama unatambua unachokilaumu ama kulalamika kuhusu Dr.Slaa.! Ni ajabu sana kwa "Vijana" wenye akili inayotakiwa kufanya kazi kwa umakini kuandika mambo uliyoandika bila kufikiria kwamba mnajaribu kupotosha watu.
Dr.Slaa alieleza kwa ufasaha na uwazi sababu za yeye kujitoa CDM na kukaa kimya kwanza,na hili lilitoa matokeo yafuatayo:
1-Minong'ono na habari zisizokuwa za ukweli kutoka kwa watu wasiyo makini na wadandiaji wa habari kwa kutumia uzushi.Tukianzia ndani ya UKAWA yenyewe kuuficha ukweli wa nini kilichotokea.Tuliambiwa na Mbowe ya kwamba Slaa yupo mapumzikoni na atarejea pale atakapomaliza likizo yake.Tukasikia na kusubiri.
2-Mitandao ya kijamii tukashuhudia habari nyingi zisizo rasmi kwamba Dr.Slaa atahudhuria ufunguzi wa kampeni za CCM jangwani...nazo zikawa hazikuzaa matunda.Ziliandikwa na zikasemwa taarifa nyingi na hata nyingine za kutengeneza ionekane ya kwamba mzee huyu kaziandika.Lakini yote haya yalizushwa tu.
Kuna msemo "Silence means a lot.."Kwa hivyo ukimya wake huu uliibua mengi kutoka kwa wadau wa habari na matukio.
Sasa ukaja wakati akaamua kuachana na ukimya ule baada ya kuona kuna upotoshaji mwingi ambao nitauita uchokozi kwa Dr. Slaa atasema nini.Akaitisha mkutano wa wanahabari na wengi tukawa na shauku ya kujua mengi kutoka kwake ili kuondoa minong'ono iliyozagaa katika jamii yetu.
Kiukweli alijieleza kwa ufasaha na mpangilio mzuri tu hata kwa mtu aliyekunywa Whisky angemuelewa.
Hoja zile zilizungumzia ukweli wa mambo yalivyotokea na yalikuwa mambo ya msingi ikiwa ni pamoja na ushahidi wa nakala mbalimbali alizozionyesha pale.Nilitarajia wahusika waliotajwa katika mkutano ule na wao kujitokeza kujibu hoja zile ili sisi wanajamii tusikilize na kuweka kwenye mizani vichwani mwetu kupima na kutambua ukweli wake.
Cha ajabu kabisa tukashuhudia kelele za stand ya mabasi!!!!Kila mmoja ananadi biashara yake itoke!
Si CHADEMA,Lowassa,Prof.Safari waliyojitokeza kujibu tuhuma zile kifasaha.Ama UKAWA ambayo mpaka sasa hatumjui ni nani msemaji mkuu. Ni James Mbatia,"Askofu" Gwajima,Gazeti la Mawio au ni nani ili pawepo na mawasiliano rasmi kati yetu.
Kituko kingine,ni kwa "Askofu"Gwajima alipoamua kujitokeza na kuitisha mkutano wa waandishi wa habari na kusema yake.Hapa tukawa na shauku ya kujuwa mambo ya msingi kutoka kwa Askofu huyo.Badala ya kujibu tuhuma zile tukajikuta tukisimuliwa mambo BINAFSI kati ya Dr.Slaa na mwenzi wake Josephine!!!
Kimsingi watuhumiwa wa saga hili hawana muda wa kujibu lolote wanaona bora liende.Huu ndio ukweli wenyewe.
Kwa nchi za wenzetu jambo kama hili halichukuliwi kimzaha.Litatakiwa lipatiwe majibu yatokanayo na shutuma.Na umma unatakiwa uridhike na majibu yale.
Sasa tunahitaji mabadiliko ya aina gani kama anayepita kuomba kura,yeye na timu yake hawana hata msemaji rasmi?
Wanataka kushika dola na ya Mungu mengi.Katika masuala ya kiutawala kuna mipangilio na taratibu rasmi kwa ajili ya kiitwacho REFERENCE.
Leo hii ukimtuhumu Rais wa Tanzania kwamba ni mlevi,tuhuma hii haitajibiwa na Mchungaji Christopher Mtikila.Itajibiwa na Salva Rweyemamu wa Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu.Hili lipo wazi.
Ukiituhumu wizara,suala lile litajibiwa na katibu mkuu wa wizara husika au mtu maalumu ambaye ni msemaji kisheria.
Kwa hivyo nahitimisha hivi:
Maelezo ya Dr. Slaa na tuhuma zilizomo bado hatujapata majibu na badala yake zinaning'inia na kila mmoja anajibu anavyoona ni sawa kwa akili yake.MILUZI MINGI INAMPOTEZA MBWA.
Kiujumla suala hili lipo sawa kabisa na shughuli za sokoni.Dr.Slaa katoa hoja.....majibu ya hoja ni WORK DONE=ZERO!
Wasalaam.