Dr. Slaa kesho atasema nini?

Dr. Slaa kesho atasema nini?

Asiishie tu kuongelea ufisadi wa Lowassa, bali pia atuelezee ni nani Archtect wa uuzaji wa nyumba za serikali hadi kusababisha baadhi ya watendaji wakubwa serikalini wanakosa nyumba na kulala mahotelini kwa gharama za kodi wa WAPUMBAVU na MALOFA wa nchi hii.

Atakuwa ni yule jamaa aliyekuwa waziri mkuu kipindi hicho. jina lake nimelisahau, unaweza kunikumbusha mkuu?
 
Sisi wote ni wanafunzi na wahanga wa Dr. Slaa kifikra na kisiasa. Dr. Slaa umetufundisha watanzania wote kuwa CCM haifai na ndio chanzo cha ufisadi, ubadhilifu, wizi, matumizi mabaya na sera mbaya zisizotekelezaka na zilizosababisha maisha ya watanzania kuwa mabaya. Ukiwa na wenzako wa chadema kwa kutumia kampeni za sangara, M4C, redio na tv, ulitufundisha kuikataa CCM na tulikuelewa vizuri, tuliamini na tukafanya hivyo kwa moyo, kwa nguvu na kwa akili zetu zote. Wewe ndiye uliyesababisha taifa lote liichukie na kuikataa CCM kwa moyo na nguvu zote, watu wameshalielewa somo lako kuhusu ubaya wa CCM kwetu. Ulitufungua akili tuliokuwa hatujui siasa za chama cha CCM. Tulifanya hivyo kwakuamini kwamba wewe ni msomi mzuri na mtumishi wa Mungu husemi uongo na utakuwa umefanya utafiti mzuri kuhusu uhusiano uliyopo kati ya maisha ya watanzania na sera, utekelezaji wa sera na utawala wa CCM. Uliamsha hamasa na ari ya watanzania katika siasa na kufikiri juu ya maisha yao. Sasa tumeelimika sana kupitia wewe na wenzako wa chadema kuhusu ubaya wa CCM kwetu na kwa taifa, watu hawataki tena kusikia habari za CCM mitaani na maofisini. Ahsante sana baba!

Sasa wafuasi wako tumeanza kushikwa na butwaa kubwa kukuona wewe tena unakipigia debe CCM kiendelee kubakia madarakani!!!!@***&.com???. Hapa kuna mawili, ama wewe unataka kutugeuza sisi kichwa chini miguu juu, au wewe ndo umegeuka mwenyewe kichwa chini miguu juu. Tunajiuliza nini kimetokea kwa mwalimu wetu Dr. Slaa hadi kufanya hivi? Kama shida ni Lowassa kuhamia chadema basi hata wewe hukupaswa kuwa na uhalali wa kukilaumu CCM kwa ufisadi, ubadhilifu na huduma mbovu kwa wananchi, badala yake ulipaswa kuwalaumu viongozi waliotokana na CCM tu peke yake wasiofanya vizuri na sio chama chote cha CCM kuwa hakifai. Vinginevyo wewe ulikuwa katibu mkuu wa chadema hivyo ungeweza kuhakikisha kuwa rais (Lowassa) anayetokana na chama cha chadema angeongoza nchi kwa mujibu wa kanuni, taratibu na maadili ya chadema tu basi. Hivyo ukiwa kama katibu mkuu wa chadema hukuwa na sababu za msingi za kumuogopa Lowassa 'fisadi' kuhamia chadema au kugombea urais kupitia chadema maana chama chini ya katibu mkuu (wewe) kingemnyoosha na kumfanya kuongoza nchi kwa mujibu wa chadema. Kama hili limeshindikana kwako na kwa chadema kwanini ulitaka hili liwezekane kwa CCM? Ulikuwa unatudanganya kuhusu ubaya wa CCM? Ulipaswa kuwalaumu viongozi na watendaji wabaya wa CCM na sio chama cha CCM chote kama chama. Unapaswa kuwaomba samahani CCM hadharani kwa kukisema chama chao vibaya badala ya kumsema mwanachama/kiongozi wa CCM ambaye ni mwizi, mbadhilifu, fisadi, n.k, pili, uwaombe radhi watanzania kwa kuwapotosha kuhusu ubaya wa CCM kama chama.

Kama wewe ukishindwa kuyafanya haya yote mawili kwapamoja taifa hili litakuwa juu ya kichwa chako kwa kuliyumbisha na kutaka kulipasua vipande. CCM wanafunzi wako tunakuona kama mwalimu usiyekuwa na msimamo, uliyehongwa, mwenye ubinafsi wa kuwa rais kwa gharama yoyote, unayependa porojo, usiyependa maamuzi ya pamoja ndani ya chama, mpotoshaji, muongo, usiyejali wafuasi na familia yako, na usiyefaa kusikilizwa tena na watu wenye shida za maisha kama sisi. Hatujui kesho tena utasema nini, utakuwa wapi na nani. Kwaheri huwaminiki mzee!!!

Wewe hujaelewa. Sio Kwamba Dr Slaa anaipenda ccm no Ila yeye tatizo lake ni Lowasa kama ingewezekana mngemtoa Lowasa alafu mngempa Tundu lisu mngeona Dr Slaa akiwaunga mkono. Huwezi kufanya mabadiliko kwa kumtumia fisadi alafu ubaki na amani..... Kumbuka mafisadi wote waliobaki ccm wanasubiri mzee mnvi aapishwe waanze kugawana vya kugawana.
 
Kutoka kuitwa RAIS WA MIOYO YA WATANZANIA Mpaka kuitwa DR MIHOGO.Amma kweli ubinadamu kazi.
 
Sisi wote ni wanafunzi na wahanga wa Dr. Slaa kifikra na kisiasa. Dr. Slaa umetufundisha watanzania wote kuwa CCM haifai na ndio chanzo cha ufisadi, ubadhilifu, wizi, matumizi mabaya na sera mbaya zisizotekelezaka na zilizosababisha maisha ya watanzania kuwa mabaya. Ukiwa na wenzako wa chadema kwa kutumia kampeni za sangara, M4C, redio na tv, ulitufundisha kuikataa CCM na tulikuelewa vizuri, tuliamini na tukafanya hivyo kwa moyo, kwa nguvu na kwa akili zetu zote. Wewe ndiye uliyesababisha taifa lote liichukie na kuikataa CCM kwa moyo na nguvu zote, watu wameshalielewa somo lako kuhusu ubaya wa CCM kwetu. Ulitufungua akili tuliokuwa hatujui siasa za chama cha CCM. Tulifanya hivyo kwakuamini kwamba wewe ni msomi mzuri na mtumishi wa Mungu husemi uongo na utakuwa umefanya utafiti mzuri kuhusu uhusiano uliyopo kati ya maisha ya watanzania na sera, utekelezaji wa sera na utawala wa CCM. Uliamsha hamasa na ari ya watanzania katika siasa na kufikiri juu ya maisha yao. Sasa tumeelimika sana kupitia wewe na wenzako wa chadema kuhusu ubaya wa CCM kwetu na kwa taifa, watu hawataki tena kusikia habari za CCM mitaani na maofisini. Ahsante sana baba!

Sasa wafuasi wako tumeanza kushikwa na butwaa kubwa kukuona wewe tena unakipigia debe CCM kiendelee kubakia madarakani!!!!@***&.com???. Hapa kuna mawili, ama wewe unataka kutugeuza sisi kichwa chini miguu juu, au wewe ndo umegeuka mwenyewe kichwa chini miguu juu. Tunajiuliza nini kimetokea kwa mwalimu wetu Dr. Slaa hadi kufanya hivi? Kama shida ni Lowassa kuhamia chadema basi hata wewe hukupaswa kuwa na uhalali wa kukilaumu CCM kwa ufisadi, ubadhilifu na huduma mbovu kwa wananchi, badala yake ulipaswa kuwalaumu viongozi waliotokana na CCM tu peke yake wasiofanya vizuri na sio chama chote cha CCM kuwa hakifai. Vinginevyo wewe ulikuwa katibu mkuu wa chadema hivyo ungeweza kuhakikisha kuwa rais (Lowassa) anayetokana na chama cha chadema angeongoza nchi kwa mujibu wa kanuni, taratibu na maadili ya chadema tu basi. Hivyo ukiwa kama katibu mkuu wa chadema hukuwa na sababu za msingi za kumuogopa Lowassa 'fisadi' kuhamia chadema au kugombea urais kupitia chadema maana chama chini ya katibu mkuu (wewe) kingemnyoosha na kumfanya kuongoza nchi kwa mujibu wa chadema. Kama hili limeshindikana kwako na kwa chadema kwanini ulitaka hili liwezekane kwa CCM? Ulikuwa unatudanganya kuhusu ubaya wa CCM? Ulipaswa kuwalaumu viongozi na watendaji wabaya wa CCM na sio chama cha CCM chote kama chama. Unapaswa kuwaomba samahani CCM hadharani kwa kukisema chama chao vibaya badala ya kumsema mwanachama/kiongozi wa CCM ambaye ni mwizi, mbadhilifu, fisadi, n.k, pili, uwaombe radhi watanzania kwa kuwapotosha kuhusu ubaya wa CCM kama chama.

Kama wewe ukishindwa kuyafanya haya yote mawili kwapamoja taifa hili litakuwa juu ya kichwa chako kwa kuliyumbisha na kutaka kulipasua vipande. CCM wanafunzi wako tunakuona kama mwalimu usiyekuwa na msimamo, uliyehongwa, mwenye ubinafsi wa kuwa rais kwa gharama yoyote, unayependa porojo, usiyependa maamuzi ya pamoja ndani ya chama, mpotoshaji, muongo, usiyejali wafuasi na familia yako, na usiyefaa kusikilizwa tena na watu wenye shida za maisha kama sisi. Hatujui kesho tena utasema nini, utakuwa wapi na nani. Kwaheri huwaminiki mzee!!!

Tatizo hukumwelewa.
 
Kwa hoja zako, ni wazi kwamba hukumuelewa mwalimu wako Dr Slaa tangu awali. Pili, hata sasa humuelewi kabisa. Dr hata siku moja haamini katika kumpa fisadi ikulu

CCM ilikua mbovu kwa sababu ya Lowassa na mtandao wake. Chama kikajisafisha, kikamnyima fursa. Wasaliti wachache wachumia tumbo wakamuingiza cdm kwa mabavu na kumsaidia aende Ikulu. Ulitaka Dr Slaa akuambie na akutendee lipi zaidi ya kukataa hilo kwa vitendo?

Nafkiri umeelewa japo kidogo ewe mwanafunzi kichwa ngumu!
 
Mbaya zaidi aliowasema wamehamia upande wa pili yaani ukawa anahaki ya kuwasema na kwendda kuliko kutakatifu...cchama kimezika demokrasia jumlaaaa
 
Dr Slàa ameamua kulamba matapishi yake mwenyewe. Siku zote ameikandia Ccm kama ndio chanzo cha ufukara na umaskini wa watanzania. Lakini sasa anataka watanzania wairudishe ccm madarakani tena!!!

Ccm inarudi kwa nguvu, kwa kuwa ukawa ni walafi hawana misingi , wanahongeka sasa kama slaa wanasema kahongwa kutetea ccm, mbowe kahongwa kampokea lowasa. Hii ndio ukawa ya salum mwalim.
 
Watz sisi sijui tuna nini,ndugu mtoa mada unapomlaumu Dr kwa maneno yake umeegemea mahali ambapo hata wewe hujiulizi,we unadhani kwa upande wa pili inakuingiaje kilahisi lahisi mtu aliesemwa fisadi,jambazi,hafai,ashitakiwe na hawa hawa waliomkalibisha wakaenda mbali kuuaminisha uma kua hata ushahidi wa EL wanao.leo huo ushahidi wameupotezea na kauli za fisadi hawazisemi,badala yake wamekuja na neno jingine la MFUMO m'bovu wa ccm.jamani hata kama mtu hakwenda shule vzr hapa hadanganyiki,Dr Slaa yuko sawa wala hajatetea upande wowote,amepaponda chama tawala na ameponda alikotoka kumkalibisha mtu waliemhubili kwa ubaya!
 
Mie nina mtazamo tofauti kidogo kwani,kwani ameweza kusimamia maneno yake dhidi ya lowassa na kwamba tena waje wakae meza moja ni suala ambalo hakulitaka,kwa hilo nampongeza lakini kumhusisha yeye na ccm ni historia ya mbali sana,heko dr slaa
 
unaakili lkn hazikusaidii kufikiri unawezaje kumtenganisha liwasa na ccm au kwa vile saiv ni lowasa ni mgombea binafsi wa chadema. Slaa akimtuhumu lowasa ni sawa na kuituhumu ccm LOWASA NI FISADI KAMA MAFISAD WENGINE WALIOKO CCM

Sasa wewe unataka kusema ni nani anafa kwa mtazamo wako ni heri kumchagua fisadi mmoja aliyezungukwa na mfumo wa haki kuliko kumchagua msafi mmoja aliyezungukwa na mfumo wa kifisadi na mafisadi lukuki japo hata yeye akichunguzwa vizuri ni fisadi mwenzao
 
Kwa hoja zako, ni wazi kwamba hukumuelewa mwalimu wako Dr Slaa tangu awali. Pili, hata sasa humuelewi kabisa. Dr hata siku moja haamini katika kumpa fisadi ikulu

CCM ilikua mbovu kwa sababu ya Lowassa na mtandao wake. Chama kikajisafisha, kikamnyima fursa. Wasaliti wachache wachumia tumbo wakamuingiza cdm kwa mabavu na kumsaidia aende Ikulu. Ulitaka Dr Slaa akuambie na akutendee lipi zaidi ya kukataa hilo kwa vitendo?

Nafkiri umeelewa japo kidogo ewe mwanafunzi kichwa ngumu!

wewe ndo ambaye haoni vizuri na kama unaona unamuunga mkono wewee pia ni mchumia tumbo wa ccm
 
Slaa kwanza ni Mdini aliepitiliza, Pili amevuta kiasi kikubwa sana kutoka CCM na hili linathibitishwa na Josephine kuwa wamepata mtaji wa kuanzisha mahospitali na shule kibao ... Haihitaji akili ya ziada kujua kuwa Slaa alikuwa analindwa na system ya CCM ... TV zote zililipiwa na CCM .. akina Mwakyembe walikuwa wanampa sapoti tu .. Mzee sasa hivi ana mkwanja wa kutosha ..
...majuzi alisema nashindia mihogo na leo wanaanzisha mashule na hospitali????....amazing...kama ni kweli basi hata hayo mahospitali na mashule hawatayaweza....maana historia inamuhukumu slaa....hakuweza kushinda alichokisimamia.....fatilia historia yake....na sababu ni hizo hizo...kuasi mapito yake....
 
Watz sisi sijui tuna nini,ndugu mtoa mada unapomlaumu Dr kwa maneno yake umeegemea mahali ambapo hata wewe hujiulizi,we unadhani kwa upande wa pili inakuingiaje kilahisi lahisi mtu aliesemwa fisadi,jambazi,hafai,ashitakiwe na hawa hawa waliomkalibisha wakaenda mbali kuuaminisha uma kua hata ushahidi wa EL wanao.leo huo ushahidi wameupotezea na kauli za fisadi hawazisemi,badala yake wamekuja na neno jingine la MFUMO m'bovu wa ccm.jamani hata kama mtu hakwenda shule vzr hapa hadanganyiki,Dr Slaa yuko sawa wala hajatetea upande wowote,amepaponda chama tawala na ameponda alikotoka kumkalibisha mtu waliemhubili kwa ubaya!

kwa mtazamo wako mdogo naona umeamua kuishi bila raisi kuliko kubadili mfumo? kumbe kuna watanzania ambao bado hatuoni umuhimu wa nafasi ya Raisi heri kuishi tu. sisi hatuwezi tunangoa mfumo mbovu na kuweka mfumo wenye maana na tija kwa watanzania wote hata wewe ambae hautambui mfumo wa ukandamizaji ulioko kwa sasa
 
et analindwa na usalama wa taifa????!! tena serena hotel!!!!!
hivi hao usalama walishindwa nini kumlinda nyumbn kwake?????
 
kwa mtazamo wako mdogo naona umeamua kuishi bila raisi kuliko kubadili mfumo? kumbe kuna watanzania ambao bado hatuoni umuhimu wa nafasi ya Raisi heri kuishi tu. sisi hatuwezi tunangoa mfumo mbovu na kuweka mfumo wenye maana na tija kwa watanzania wote hata wewe ambae hautambui mfumo wa ukandamizaji ulioko kwa sasa

Endelea mbele na mtazamo wako mkubwa unaoufikilia,haya ndo maneno mnayoyatumia mnaishia kupata laana tu ya MUNGU,ungekua una mtazamo mpana usingekuja hata hapa ungesimama na kuzunguka inchini kuwaelimisha watz.hapa jf tuko thelusi tu ya Watanzania wote
 
Kweli huyu mzee ni mnafiki sana, kwanza kiongozi gani anayekubali kununuliwa? Hatutaki hata kumsikiliza hana maana. Kapoteza sifa na heshima ktk taifa hili. Akae kimya asipotoshe uma, hatufai
 
Taifa liko njia panda, linahitaji kuwa na rais haraka iwezekavyo. Kama CCM haifai na Lowassa hafai kwa mujibu wa Dr. Slaa na wenzake, atuambie watanzania sasa ni nani anafaa ili tumpe kura zetu? hawezi kutuambia CCM inafuga mafisadi na Lowassa hafai bila kusema categorically nani anafaa sasa kuchaguliwa wa kutoka chama gani. Huu ndio ubaya uliokithiri wa Dr. Slaa kwa taifa, analichanganya taifa yeye pamoja na Mushumbusi kwa faida binafsi. Mtu kama huyu lazima adhibitiwe na kupuuzwa kwa nguvu zetu zote maana hafai hata kidogo, hafai kwa CCM, UKAWA wala kwa taifa. Anasababisha taifa likose muelekeo kwa uchu wake wa madaraka na fedha. Yeye kashatembea nchi nzima akiambia watu kuwa CCM haifai kabisaaaaa, ni wezi, mafisadi na wana sera zisizotekelezeka hadi akadai CCM waliiba kura zake 2010 na akashindwa kumtambua rais JK kama mshindi halali. Leo mtu huyuhuyu kwa muda mfupi huuhuu anasema Lowassa hafai huku akijua kuwa Lowassa anawakilisha vyama vinavyounda UKAWA vyenye wafuasi wengi sana pia kama ilivyo kwa CCM. Anawaweka wananchi na taifa njia panda, tusimchekee huyu mtu mroho, anaweza kusababisha maafa makubwa mwaka huu 2015. Anagonganisha CCM na UKAWA zenye wafuasi wengi sana katika taifa hili kwasasa, nini malengo yake ya muda mfupi, kati na muda mrefu? Yeye ndiye aliyesababisha wananchi wengi hasa vijana hawaipendi CCM, na sasa anasababisha wanachama wa CCM wawachukie wafuasi wa ukawa na lowassa wao, kwanini taifa limuache awe huru mtu kama huyu?

Mkilala mkiamka mnamuwaza Dr acha awape tiba maana ndo kazi yake na mtajuta kumfaham..... Akili yako ikiwa imetawaliwa na mihemko huwezi muelewa Dr milele ila uki relax hutajutia kumsikiliza tena na tena.... Dr hajamchagulia mtu rais alichofanya ni kummulika Lowasa na UFISADI wake wa RICHMOND na uroho wa kutaka madaraka kwa nguvu zote pia Magufuri na suala la nyumba (japo ni rumours tu)..... Sasa ni juu yako kutumia akili yako kuangalia nani anafaa kuliko mwenzie... Na hili liko wazi Dr Magufuri ndo mtu msafi hivyo naomba tumpe kura zetu ili tuendelee mbele kama taifa
 
Lowassa ni wa kuogopwa kama ukoma, ni fisadi mzoefu wa tangu enzi za mwalimu, mwaka 1992 wakati ni mkuu wa kitengo cha maafa ofisi ya waziri mkuu alilamba pesa yote waliyokuwa wakicgangia watu kwa ajili ya mafuriko yaliyotokea Lindi na Mtwara na kuwaaca watu wa Lindi na Mtwara wakikosa pa kujihifadhi. Alipokuwa waziri wa ardhi, alijitwaalia maeneo mengi ikiwa ni pamoja na ku-revoke hati za watu kwa kisingizio kwamba eneo linatakiwa kwa matumizi ya serikali, (Amglikana walishakumbwa na kadhia hii): Hii ya richmond kimekuwa kama kibwagizo tu verse ziko nyingi sana.
Mbaya zaidi ni fisadi anayeogopwa na serikali zote zilizowahi kuundwa na ccm hivyo umpe Kura au usimpe akiamua kuendelea na ufisadi wake hakuna wa kumzuia.

Mtanzania mpe Kura yako Lowasa tuone kama atajifisadi mwenyewe
 
Endelea mbele na mtazamo wako mkubwa unaoufikilia,haya ndo maneno mnayoyatumia mnaishia kupata laana tu ya MUNGU,ungekua una mtazamo mpana usingekuja hata hapa ungesimama na kuzunguka inchini kuwaelimisha watz.hapa jf tuko thelusi tu ya Watanzania wote

Chachu ya maendeleo inaanza na mmoja kumbe heri mimi mwenye theluthi ya watanzania ambao waliobaki tutasaidiana na wengine walioipokea taarifa hii na kuiona ina maana kwetu
 
Back
Top Bottom