Wadau wa kutabiri mnadhani atawaahidi nini walimu huyu bingwa wa ahadi zisizotekelezeka?
Nimesoma gazetini kuwa Dr Slaa amesema kwamba JK amejialika kwenye mkutano wa kitaifa wa CHAMA CHA WAALIMU unaotarajiwa kufanyika Songea hapo kesho 3/10/2010.
Je kama ni kweli inapokelewaje hii?
Wadau wa kutabiri mnadhani atawaahidi nini walimu huyu bingwa wa ahadi zisizotekelezeka?
Mhh...ndo nini?:A S wink::A S wink:
1) atawaambia wamchague azidi kudumisha amani iliopo. hii ni ahadi pekee itayoweza kuwafanya walimu wamshangilie
2) atazidi kuboresha walimu kimaslahi
3)ataongeza nafasi za masomo kwa walimu wetu. kjambo ambalo kila mwalimu atalifurahia.
4) lkn pia atasema wasichague wapinzani kwani wanaweza kuleta fujo lkn hapa ataongeza kidogo. lkn jeshi letu limejipanga kukabliana na vurugu zozote zile
Nijuavyo mimi CWT wako makini sana katika mikakati yao, japokuwa katika maamuzi huwa wanatofautiana, lakini suala la kuwa tawi la ccm si sahihi sana!ataahidi kuwalipa madeni yao ya tangia 2006............after all hiyo CWT ni kama tawi la sisi em