Dr.SLAA Hataukaribia ushindi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr.SLAA Hataukaribia ushindi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mwiba, Sep 8, 2010.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Huyu mgombea wa Chadema mheshimiwa Dr W.Slaa hatoweza kuukaribia ushindi kabisa na hapo alipo ni kuanguka kwake kisiasa au kwa lugha ingine tunasema ndio mwisho wake.

  Ukiangalia migongano ndani ya Chadema ambayo inawaka kama moto wa makumbi ameshindwa kuiweka sawa ,baada ya uchaguzi huu Chadema itakuwa na wakati mgumu sana ,inaweza kufa au kugawika na zaidi wanachama wake wakuu kwa kuwakusudia viongozi kuhama na kurejea CCM au kujiunga na vyama vingine kama tulivyoona.

  Wananchi wengi wameanza kupoteza imani baada ya Dr.Slaa kupita akimnadi mke mpya au tuseme mchumba mpya baada ya kueleza sera amekuwa akizungumzia mambo ya maisha yake binafsi ya kindoa kubwa zaidi kuwa sasa inasemekana ameeiba mke wa mtu au anatembea na mke wa mtu ,yaani hata ile mke akiishi nae hakuwa mke wa ndoa ni kuishi maisha ya kuhurumiana ,jambo ambalo wananchi wengi wameliona kuwa halifai kuwa nalo mtu ambae anaomba Uraisi na kutaka kuwa kiongozi katika nchi yenye watu masikini.

  Sasa Dr Slaa yumo katika mbio za kutaka kujisafisha badala ya mbio za kunadi sera ,amepoteza mvuto wa kisiasa na kuwa kivutio wa story za mapenzi na mipasho kwa wale wanaomuona amepoteza dira ,wengi ya wanaohudhuria mikutano huenda kusikiliza muendelezo wa story zake binafsi huku wakishangiria anapomsimamisha huyo mke mtarajiwa. Sielewi wapi tunaelekea.
   
 2. senator

  senator JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Just a minute wanakuja soon wale wakereketwa kumwaga utetezi wa anachokifanya Dr.
   
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  kwa hiyo atakayeshinda ni huyo Professor Lipumba? Your joking dude! Kwa taarifa yako labda mshirikiane na boss wenu sisi m kuchakachua kula sio rahisi huyo Lipumb..... ashinde. Bila shaka yeye atakuwa wa tatu nyuma ya sisi m
   
 4. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  MF,

  Huyu mwiba sio mwanacuf, ni mwana ccm anayepretend to be mpinzani. soma tena kwa makini utagundua kuwa ni bonge la mwanachama wa chama cha mafisadi
   
 5. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  wewe nawe kwa kupenda vilio hujaacha tu
   
 6. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mheshimiwa hata Lipumba hashindi kwa sababu ndumila kuwili ameshavuruga kila kitu,na kitu kimoja ambacho ninapenda muelewe kwa wale mnaoshabikia Chadema, wandugu Chadema hakuna kitu kiuongozi na kiutawala naweza kusema ni wabahatishaji tu ,hakuna kitu kabisa ,kama utahudhuria mikutano yao basi ni wao na mambo ya mafisadi epa,richmond kiwera na menginetele hakuna jipya ambalo litampa tamaa mwananchi wa kawaida ,vipi mwananchi muelewa anaweza kukubaliana nao ,Chadema hawana jipya na huwezi kabisa kulinganisha na CUF ,CUF wamejipanga na mwananchi anapowasikiliza basi anaguswa moja kwa moja na hoja zinavyozungumzwa.

  Chadema mnazungumzia watu binafsi na hamna ujumla wa kumjumuisha mwananchi ,hapa sizungumzii yale maandishi mliyoandika ,nasema mnapokuwa majukwaani mnashindwa kabisa kuzungumza ,labda niseme hamna wazungumzaji ukilinganisha na CUF .kubwa lenu ni kurudia yale yale ya mafisadi mambo ambayo unajulikana mwanzo wake lakinio mwisho wake haujulikani ,yaani mnakuwa kama cd iliyokwama.
   
 7. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #7
  Sep 8, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Licha ya CCM kukataa kukiri jambo ambalo ni kweli, CCM yenyewe imeutambua umakini wa Dk. Slaa, jambo ambalo limekifanya chama hiki kikongwe cha siasa kuingia kiwewe, badala ya kurekebisha mambo ambayo ni dhahiri kwamba yamekwenda mrama, badala yake, CCM inazidi kujichimbia kaburi miongoni mwa wananchi.

  Ukweli ni kwamba wananchi wengi sana wameamka, na wametamka wazi wazi (mimi nikishuhudia) kwamba HAWATAIPA KURA CCM mwaka huu. Juzi nilikuwa Moshi Mjini, nikashuhudia akinamama - wajasiriamali, ukipenda kuwaita - wakijadiliana hadharani, tena kwa hoja nzito, kwamba wamechoka kuwaona viongozi wa CCM wakineemeka, mwaka hadi mwaka, wakati wao hali yao kiuchumi inazidi kuwa mbaya, tena wakipandishiwa ushuru kwenye masoko kila siku, sasa wanayakimbia masoko hayo. Wameamua kutafuta maeneo yasiyo rasmi kufanya biashara zao kwa kuwa ushuru wanaotozwa kwenye masoko ni mkubwa kuliko kipato chao.

  CCM wametambua tishio kubwa dhidi yao kutoka kwa Dk. Slaa na wabunge wengi wa CHADEMA. Huu ndio msingi wa kesi isiyo na kichwa wala miguu, ya kwenda kudai fidia kwa Dk. Slaa, wakimchukua mamluki Mahimbo, ambaye anadaiwa kulipwa fedha nyingi kwa ajili ya KUJIABISHA hadharani. Hivi mwanaume anayejiheshimu anaweza kweli kutamka hadharani kwamba NIMEPORWA MKE na fulani? Ingekuwa mimi ningekaa kimya kuliko kujidhalilisha; UTU wa MTU haununuliwi, hata kwa shilingi bilioni moja!

  Mahimbo anadai kuporwa mke. Hivi inawezekana mwanamke - tena mrembo, mwenye akili timamu kama Josephine - akakubali "kuporwa" kutoka kwa mumeme Mahimbo? Inaingia akilini kweli hii?

  CCM wamekosea step. Badala ya wananchi kumchukia, sasa wanampenda zaidi. JK anajidhalilisha, kwani wananchi hawamwelewi. Wana-CCM wengi tu wamekiri - tena wengi wakiwa viongozi waandamizi - kwamba kesi ya madai dhidi ya Slaa ina msingi wa kisiasa, kwamba ni lengo la kumharibia.

  Mimi nilidhani kuna mtu ambaye aliwaambia wananchi WASIICHAGUE CCM. Waliamua hata kabla Slaa hajatangazwa kugombea urais, na alipotangazwa rasmi, kwa wengi wa maskini hawa imekuwa ni majibu ya ndoto zao. Sikujua kwamba kila kona nchini, Kaskazini hadi Kusini, Mashariki hadi Magharibi, ni wimbo mmoja tu unaoimbwa - CHADEMA! Hata vyama vingine vya siasa havitajwi kwa mapenzi. Tembea mtaani kwako, wasalimie kwa alama ya vidole viwili - nembo ya CHADEMA - uone ni mikono mingapi itarudi kwako.

  Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alisema: Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM.

  Viongozi wa CCM hawakumwelewa. Walidhani kwamba kutatokea baadhi ya watu, ndani ya CCM, wakajitokeza na kuleta upinzani. La hasha! Wapinzani wa kweli ndani ya CCM ni WANACHAMA WAKE, ambao sasa wamechoshwa na kila aina ya uonevu, majungu, vitimbi na ufisadi ndani ya CCM. Ile kauli ya "CCM ina wenyewe na wenyewe ndio sisi" ni mojawapo ya vitendo vya ufisadi ambavyo wana-CCM wamechoshwa navyo. Nenda kwenye Jimbo la Uchaguzi, Masasi, uone jinsi mgombea wa CCM, Mariam Kasembe, anavyohenyeshwa kwenye kampeni. Rudi hapa Kawe, uone jinsi Angela Kizigha anavyozomewa, tena na wana-CCM, wanaompa alama ya vidole viwili kila anapojaribu kwenda kuhutubia.

  Mwanzo wa mwisho wa utawala wa CCM umefika. Kila kadri CCM wanavyozidi kumchafua Dk. Slaa na wagombea wengine wa CHADEMA, ndivyo wanavyozidi kumfagilia yeye pamoja na CHADEMA. Walivyoharibu (EPA, Richmond, Meremeta, Deep Green, n.k.), labda hawakufikiria kwamba wangekuja kulipa siku moja, tena wangekuja kulipa kwa KUONDOLEWA madarakani. Vyama vya upinzani havina kazi kubwa ya kujinadi, kwani tayari CCM imeshawafanyia kampeni miaka mingi iliyopita. Wananchi waliipa CCM mtihani wao wa mwisho, walipomchagua Kikwete kwa kura nyingi (Lina uhakika hili?), lakini AMEFELI mtihani huo!

  Kadri CCM wanavyochafua - na kweli wamejichafulia, kuanzia kwenye kura za maoni ndani ya CCM - ndivyo wanachama wao wanavyochukia, na wameapa kupiga kura ya kisasi. Watanzania wengine wamesema HAWAYAONI hayo maisha bora waliyoahidiwa, na wanashangaa ari zaidi ni ya nini wakati kuna mafisadi ambao bado hawajahukumiwa; kasi zaidi ni ya nini wakati hata nusu ya ahadi za uchaguzi za 2005 hazijatekelezwa; na nguvu zaidi ni ya nini wakati umaskini umekithiri na unazidi kuwaangamiza vijana wanaoteketea kwa kukimbilia mijini (wengi wao wakipigwa, kuchomwa moto na kupoteza maisha yao, kwa kujihusisha na ubakaji), huku vijiji vikibakia na wazee, watoto na wanawake!

  Ushindi ni dhahiri kwa Slaa na CHADEMA, kwa kuwa ufisadi umevuka mipaka. Wananchi wameona jinsi CCM wanavyotumbua pesa kwenye kampeni. Wamesema kama ni hongo watapokea, lakini kwa upande wa kura, CCM isahau kurejeshwa madarakani. Asilimia themanini (80%) ya viti vya ubunge vitakwenda upinzani, huku asilimia tisini (90%) ya viti vya udiwani vitakwenda upinzani. Slaa atashinda kwa asilimia sitini (60%), na hii ni kwa kuwa bado kuna 'wajinga' wanaopumbazwa, kwamba Kikwete bado ni "mtu wa watu"!

  -> Mwana wa Haki

  2010 HATUDANGANYIKI. CCM mnajidanganya!
   
 8. senator

  senator JF-Expert Member

  #8
  Sep 8, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Eti wanadai JF haswa huku kwenye politics ni kwa wanachadema..ndo mana kwa kauli ya huyo Mwiba nikamwambia asubiri waje wanachama.Sina kilio chochote hapo...
   
 9. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #9
  Sep 8, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  CCM kwa vilaza? SIDANGANYIKI
   
 10. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #10
  Sep 8, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  hOJA YA WATU BINAFSI MLIIANZA NYINYI. KUMBE KWELI NYANI HAONI KUNDULE
   
 11. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #11
  Sep 8, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  kina nani hao wasio na majina?
  ni vilio tu na kutojiamini, taja majina ya hao wenye madai (kama yapo)
   
 12. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #12
  Sep 8, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  mafisadi wa ccm kwa unafiki wanaongoza
   
 13. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #13
  Sep 8, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  MWANAHAKI unaonekana ni mgeni wa siasa za Tanzania ,ushindi wa CCM hautegemei kupigiwa kura ,hilo kwanza napenda ulifahamu kabisa na uliweke kama akiba pindipo matokeo hayatakufurahisha kwani unaweza kupata maradhi ya ghafla.

  Ningependa pia ufahamu kuwa wananchi wengi sana bado wanaimani na CCM kwani wanafaidika nayo kama ulivyomti ,shina matawi na majani ndivyo hivyo majani ni hao wananchi ambao huna la kuwambia ,watakuja kwenye mikutano yako wataishambulia CCM lakini yote hayo kura yao bado wataipeleka CCM na kukuwacha wewe ukiwa na kubaki na kilemba cha ukoka kwamba ni chama kinachopendwa sana na chenye muamsho na mvuto.

  Kwa kukukatisha tu usijipe tamaa ya ushindi hata kidogo na si wewe bali na wengine wote wale wenyetatizo kama lako kuwa CHADEMA itaibuka mshindi ,maana kama ni hilo basi CUF ingelishinda huko tutokako pigo ililolipata haikupata mbunge hata mmoja na si kuwa wananchi hawakuichagaua au hawakuwachagua wabunge kwa tiketi ya CUF waliwachagua tena sehemu nyingi tu CUF ilishinda ,bali kumbuka CCM haishindi kwa kutegemea kura na hapo ndipo mtakapopigwa na chini.
   
 14. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #14
  Sep 8, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Mwiba waweza jiridhisha na nafsi yako tu. LAkini hakuna marefu yaso na ncha:glasses-nerdy:
   
 15. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #15
  Sep 8, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145

  Bora umesema mwenyewe kwamba ushindi wa CCM hautegemei kura... kumbe ni kweli ushindi wa CCM UNATEGEMEA WIZI WA KURA?! Duh!

  Kiongozi anayeshinda kwenye uchaguzi ulio huru na wa kidemokrasia anashinda kwa wingi wa kura. Kama CCM haitegemei kushinda kwa kura, basi, inategemea kushinda kwa wizi, jambo ambalo SIO DEMOKRASIA.

  CCM itaendelea kushinda kwa njia ya wizi wa kura? Sidhani kama mwaka huu tutaruhusu hali hii. Tumejipanga kikamilifu.

  HATUDANGANYIKI! Mnajishaua na kujishebedua, hampati kitu, hata mkiiba kura zote, bado MTASHINDWA TU!
   
 16. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #16
  Sep 8, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Yapo mengi yasio na ncha moja wapo ni hilo ,halafu wacheni jazba ,nionavyo wengi wenu hamujawahi kuona mikutano ya kile kinachozungumzwa na Chadema ,au hata kama mmeona hamuelewi na mnashindwa kukipanga kile kinachozungumzwa ,just mkitajwa mambo ya mafisadi ndio mshafika na hicho ndio chama, Slaa anasema ndani ya siku 100 ataleta mabadiliko ,maana atajiuzulu na kufanywa uchaguzi mwengine.

  Chadema ni wababaishaji na ukitaka kujua kwanza zile uniform makoti haijulikani kama ni wanajeshi au mgambo ,kusema kweli zile nguvu za kuishinda CCM hamnazo kabisa ,sehemu ambazo mnakubalika zinahesabika tena ni chache sana , halafu mimi sina tabia ya kushindana sana kwa jambo lenye uhakika nalo ,moja ni hili la kushindwa kwa Chadema ,100% Chadema haishindi na itashindwa vibaya sana ,sasa hapa huwa sihitajii kuzozana sana kwani wale nizungumnza nao hawaelewi ni kwa namna gani ushindi unapatikana.
   
 17. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #17
  Sep 8, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hamruhusu hili wewe na nani ? Aloo wacheni kujipa moyo ,wacheni kujidanganya wacheni umimi ,kushindwa kwenu hakuna mbadala na hakuna hata moja mtakalolifanya ili mshinde ,hilo halipo ,kwa hali yeyote ile CCM itaibuka mshindi tena ushindi mnono ,ikiwa wataiba kura au hawaibi hilo sio lenu ni lao ,how ,when and why wao ndio wanaojua ,kwenu ni kufuata mkondo tu wa upigaji kura na kusubiri matokeo. tuone msiruhusu ushindi wao ,tuone ,hapa watu hawatishani maana kila ukitisha ndio unawatisha na wenzako.
   
 18. RAJ PATEL JR

  RAJ PATEL JR JF-Expert Member

  #18
  Sep 8, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  The husband whose wife was messing around with Mr Slaa has the right to defend his marriage. Vote JK.
  Vote CCM for the better life, transparency and equality for all Tanzanians regardless of national origin, religious back ground or race.
  Chadema and CUF are anti-business, anti-foreign investment, and full of fear mongerers and xenophopic.
  Give CCM another 5 years to take care the unfinished business.
  Let's build Tanzania together! Tanzania is for all
  Vote CCM
   
 19. m

  mozze Senior Member

  #19
  Sep 8, 2010
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 185
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unajua Kura ni siri, na kila mtu anapiga mwenyewe. Hivyo kuna uwezekano kabisa CCM ikashindwa. Bado kuna mwezi na zaidi hadi kufikia 31 Oct, hiki ni kipindi kirefu sana na hali inaweza kubadilika sana. CCM wamewahi kushambulia, hivyo wapinzani wakifanikiwa kuyatuliza hayo mashambulizi ni dhahiri kuwa CCM itakosa hoja, na Hoja za wapinzani zitakuwa na nguvu sana!
  Ni ukweli usiopingika, hata wazazi na babu zetu waliokuwepo wakati wa uhuru watakuwa wameshachoka siasa za uongo na ahadi zisizotimilika. Kashfa zilizoibuliwa na Chadema na Ufujaji wa mali zimewakera watu wengi, ISIPOKUWA WALE WALIOFAIDIKA KAMA WATOTO NA WATU WA KARIBU WA MAFISADI. Hivyo CCM kujidanganya kuwa bado ina wapenzi itakuwa imekosea. Kutakuwa na Kupiga kura za kulipa kisasi mwaka huu, wananchi wameelimishwa na vyama vya upinzani vimewafikia wananchi wengi. Waraka uliotolewa na vyombo vya dini kama makanisa na Misikiti pia vimefungua macho watu na ndio mana unaona mikutano yote ya Kampeni inafutia watu, sio tu ya CCM.
  CCM inaonekana imekuwa chama cha watu wachache ambao wapo juu ya sheria na hicho ndio kitakachoipeleka kaburini, masikini hawatakipa kura.
  KUIBA KURA SIO MWAKA HUU! Watu wamefunguka sana! CCM itaweza kupindisha matokeo kama kutakuwa na tofauti ndogo, lakini kwa ushindi wa 70% and above hakuna jinsi ya kuweza kupindisha, unless wakitaka kuleta Machafuko!
   
 20. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #20
  Sep 8, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,491
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  sidanganyii kwa kofia za yanga
   
Loading...