Dr Slaa for presidency...Wananchi tunamchangia hela ya fomu

matumbo

JF-Expert Member
Jul 9, 2011
7,225
3,944
Wakuu mchakato wa urais umeiva ndani ya Chadema, msemaji wa chama zanzibar ndugu Salum Mwalimu katangaza jana kwenye press fomu zinaanza kuchukuliwa leo.

Sisi wananchi mamia wa Dar es Salaam tuliomsimika mzee wetu kuwa Chief wa Wazaramo wiki mbili zilizopita tumejitolea kumchangia Dr Slaa ambaye kwa sasa ni chief wetu pesa ya kuchukulia fomu ya kugombea urais ili apambane na wagombea watakaojitokeza ndani ya chama.

Kikubwa tunataka kufahamu toka makao makuu..Hizo fomu utaratibu wa kuzipata unatangazwa kwa wanachama rasmi lini? Maana tunasikia watu wameanza kuchukua fomu kabla atujatangaziwa utaratibu sisi wanachama.


Tuambiwe utaratibu ukoje tumchukulie fomu mzee wetu ambaye tumempa uchifu wa Dar es Salaam. Tunataka kuiona demokrasia ndani ya chama maana hiki ni chama cha demokrasia.

Hatutegemei kuona mchakato uliopelekea watu kuikimbia ccm baada ya kukatwa, huku uwe mbaya zaidi kwa kuvunja kanuni na taratibu za chama kwa kuwa na mchakato unaompa nafasi mtu mmoja kuchukua fomu..

Tunaomba na wagombea waliokimbia kuminywa kwa demokrasia upande wao huko walikotoka wakemee na ikibidi wasusie mchakato utaonyima wengine haki ya kugombea huku walipokuja.

Tumeishachanga pesa ya kutosha..Tunasubiri kutangaziwa mchakato tumuwezeshe Dr Slaa.

Dr Slaa for presidency..

Cc Tumaini Makene
 
Last edited by a moderator:
Atagombea kwa chama gani?
Mwenye Chama keshahamua mgombea wa CHADEMA ni Lowasa.
 
Back
Top Bottom