Dr. Slaa: CHADEMA ni chama kinachoamini mfumo wa KIBEPARI

ZeMarcopolo

Platinum Member
Joined
May 11, 2008
Posts
14,279
Reaction score
7,690
Dr. Slaa ni mwanasiasa MLAGHAI.

Wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 Dr. Slaa alizunguka baadhi ya sehemu za Tanzania (hakufanya kampeni nchi nzima) na kuwalaghai watu kuwa iwapo watampigia kura basi atashusha bei ya cement mpaka shilingi elfu tano kwa mfuko mmoja. Wapo vijana wasiofikiri kwa kina waliolaghaika na kushabikia ahadi hiyo ya kilaghai, lakini watanzania wengi walikuwa werevu na kutambua ulaghai wa Dr. Slaa na hivyo hawakumpigia kura. Matokeo yake Dr. Slaa alishindwa vibaya katika uchaguzi huo na kushindwa kupata hata asilimia 29 ya kura!

Leo bila aibu Dr. Slaa ametoa taarifa hadharani kuwa Chadema ni chama kinachoamini mfumo wa KIBEPARI. Katika taarifa yake hiyo amefafanua kuwa Chadema inaamini kwenye Market Economy ambapo bei ya kitu huamuliwa na nguvu za demand and supply. Kwa lugha nyepesi ni kwamba taarifa aliyotoa leo Dr. Slaa ni kuwa yeye na chama chake cha Chadema wanaamini kuwa kupanga bei ya cement iwe sh. elfu tano SIO SAHIHI.

Huu ni ulaghai wa hali ya juu. Katika sehemu alizozunguka, Dr. Slaa aliwalaghai watu wazima na machifu wa jamii mbalimbali juu ya bei ya cement. Katika jamii za kiafrika inaaminika kuwa kumlaghai chifu ni kuikosea heshima jamii yote anayoiongoza. Kwa hiyo Dr. Slaa amedhihirisha uchu wa madaraka uliopitiliza kiwango mpaka anazivunjia heshima jamii za watanzania.

Kistaarabu, baada ya Dr. Slaa leo kukiri kuwa alivyokuwa anatangaza kushusha bei ya cement alikuwa anadanganya, basi anawajibika kuomba radhi. Kuomba radhi ni jambo la kiungwana, hata hivyo Dr. Slaa anafahamika kwa tabia yake ya kutokuomba radhi kwa makosa mbalimbali anayofanya. Katika historia, Dr. Slaa ndio mgombea Urais wa kwanza aliyewahi kutamka hadharani kuwa ana mpango wa kuanzisha vurugu ili nchi isitawalike. Hata hivyo hakuomba radhi kwa kauli yake hiyo chafu mpaka leo!

Hata pale alipotoa siri za ofisi yake hadharani kwa lengo la kumdhalilisha mwanasiasa mwenzake, pia hakuomba radhi!

Katika historia ya siasa za Tanzania Dr. Slaa hajawahi kuomba radhi hata siku moja. Hii ni kumaanisha kuwa anajiona kuwa yuko perfect.

Kuomba radhi ni hatua ya awali ya uwajibikaji. Kiongozi asiyekuwa na utashi wa kuomba radhi kwa makosa yake yaliyo bayana, hawezi hata kujiwajibisha kwa kujiuzuru. Hii si dalili nzuri kwa upande wa Dr. Slaa. Mtu wa namna hii hafai kuaminiwa katika majukumu yenye mamlaka kubwa. Watu wenye macho wameshaona hilo...

Kijana wa leo usikubali kuwa victim wa siasa za kilaghai...
 
Leo ZeMarcopolo utapata comment nyingi sana.Huna vitu vya kujenga mwanachama mwenzangu wa CCM hadi umshambulie mtu binafsi? Kwani Dr.Slaa alikuwa haitangazi Ilani ya CHADEMA? Ndugu yangu,yetu yanatushinda ndio tutayaweza ya wenzetu? Tafakari
 
Last edited by a moderator:
Huna akili, hujafikiri kabla ya kuandika, mbona hujawauliza EWURA ni sababu zipi wanapanga bei za mafuta na nauri? Mbona hata sasa tuko kwenye mfumo huo japo ccm inadai ina ujamaa? Nenda shule usomeusitegemee ujinga wako huo...
 
Huna akili, hujafikiri kabla ya kuandika, mbona hujawauliza EWURA ni sababu zipi wanapanga bei za mafuta na nauri? Mbona hata sasa tuko kwenye mfumo huo japo ccm inadai ina ujamaa? Nenda shule usome usitegemee ujinga wako huo...
 
Ngoja tusubiri tuone magamba watakavo changia huu Uzi usio na maana!
 
Mkuu inaonekana hujui unachokiongea na umekurupuka sana. Yawezekana kukawa na mfumo wa kibepari na bei ya cement ikawa 5000 Tsh, kuna techniques nyingi za kuregulate bei ya bidhaa katika soko. Ushawahi jiuliza kwa nini pamoja na viwanda vya saruji kupata malighafi zote za kutengenezea saruji toka ndani ya nchi lakini bado inaonekana saruji inayotengenezwa nchini inauzwa bei ghali kuliko saruji inayotoka nje ya nchi licha ya saruji ya nje kuongezeka cost ya usafiri per unit item toka huko itokapo mpaka inaingia nchini ..? Ukijijibu hili swali kwa usahihi naamini utakuwa ushaelewa Dr slaa alikuwa anamaanisha nini 2010.
 
ZeMarcopolo,

Literacy rate ya Tanzania inaweza kuwa imeshuka sana lakini wapo watanzania wengi tu bado wanajua kusoma. Ilani za vyama including CHADEMA na CCM ziko kwenye election manifesto zao, kwa miaka kadhaa sasa. Hivyo huna haja ya kuunga-unga story. Tulia, kamata party manifesto, soma.

Rai, hebu jamani watanzania sasa tujitahidi kuinua viwango vya mijadala hapa jamvini.
 
Leo ZeMarcopolo utapata comment nyingi sana.Huna vitu vya kujenga mwanachama mwenzangu wa CCM hadi umshambulie mtu binafsi? Kwani Dr.Slaa alikuwa haitangazi Ilani ya CHADEMA? Ndugu yangu,yetu yanatushinda ndio tutayaweza ya wenzetu? Tafakari

Mzee Tupa Tupa wa Lumumba,

Hii thread sio shambulio binafsi. Ni changanuo la sera za kilaghai.

Nchi yetu ina majanga mengi. Janga mojawapo ni siasa za kilaghai ambapo mwanasiasa anasema chochote kile ilimradi tu achaguliwe. Siasa za namna hii huchelewesha maendeleo.

Huu ni mfano HALISI wa siasa za kilaghai.
 
Dr. Slaa ni mwanasiasa MLAGHAI.

Wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 Dr. Slaa alizunguka baadhi ya sehemu za Tanzania (hakufanya kampeni nchi nzima) na kuwalaghai watu kuwa iwapo watampigia kura basi atashusha bei ya cement mpaka shilingi elfu tano kwa mfuko mmoja. Wapo vijana wasiofikiri kwa kina waliolaghaika na kushabikia ahadi hiyo ya kilaghai, lakini watanzania wengi walikuwa werevu na kutambua ulaghai wa Dr. Slaa na hivyo hawakumpigia kura. Matokeo yake Dr. Slaa alishindwa vibaya katika uchaguzi huo na kushindwa kupata hata asilimia 29 ya kura!

Leo bila aibu Dr. Slaa ametoa taarifa hadharani kuwa Chadema ni chama kinachoamini mfumo wa KIBEPARI. Katika taarifa yake hiyo amefafanua kuwa Chadema inaamini kwenye Market Economy ambapo bei ya kitu huamuliwa na nguvu za demand and supply. Kwa lugha nyepesi ni kwamba taarifa aliyotoa leo Dr. Slaa ni kuwa yeye na chama chake cha Chadema wanaamini kuwa kupanga bei ya cement iwe sh. elfu tano SIO SAHIHI.

Huu ni ulaghai wa hali ya juu. Katika sehemu alizozunguka, Dr. Slaa aliwalaghai watu wazima na machifu wa jamii mbalimbali juu ya bei ya cement. Katika jamii za kiafrika inaaminika kuwa kumlaghai chifu ni kuikosea heshima jamii yote anayoiongoza. Kwa hiyo Dr. Slaa amedhihirisha uchu wa madaraka uliopitiliza kiwango mpaka anazivunjia heshima jamii za watanzania.

Kistaarabu, baada ya Dr. Slaa leo kukiri kuwa alivyokuwa anatangaza kushusha bei ya cement alikuwa anadanganya, basi anawajibika kuomba radhi. Kuomba radhi ni jambo la kiungwana, hata hivyo Dr. Slaa anafahamika kwa tabia yake ya kutokuomba radhi kwa makosa mbalimbali anayofanya. Katika historia, Dr. Slaa ndio mgombea Urais wa kwanza aliyewahi kutamka hadharani kuwa ana mpango wa kuanzisha vurugu ili nchi isitawalike. Hata hivyo hakuomba radhi kwa kauli yake hiyo chafu mpaka leo!

Hata pale alipotoa siri za ofisi yake hadharani kwa lengo la kumdhalilisha mwanasiasa mwenzake, pia hakuomba radhi!

Katika historia ya siasa za Tanzania Dr. Slaa hajawahi kuomba radhi hata siku moja. Hii ni kumaanisha kuwa anajiona kuwa yuko perfect.

Kuomba radhi ni hatua ya awali ya uwajibikaji. Kiongozi asiyekuwa na utashi wa kuomba radhi kwa makosa yake yaliyo bayana, hawezi hata kujiwajibisha kwa kujiuzuru. Hii si dalili nzuri kwa upande wa Dr. Slaa. Mtu wa namna hii hafai kuaminiwa katika majukumu yenye mamlaka kubwa. Watu wenye macho wameshaona hilo...

Kijana wa leo usikubali kuwa victim wa siasa za kilaghai...
Wakati nasoma post hii nilipokuta neno uongo na kuomba radhi nikapa jibu.
Jibu kikwete alituaidi maisha bora kwa kila mtz je yako wapi? Na amefanya nini
 
ZeMarcopolo,

Literacy rate ya Tanzania inaweza kuwa imeshuka sana lakini wapo watanzania wengi tu bado wanajua kusoma. Ilani za vyama including CHADEMA na CCM ziko kwenye election manifesto zao, kwa miaka kadhaa sasa. Hivyo huna haja ya kuunga-unga story. Tulia, kamata party manifesto, soma.

Rai, hebu jamani watanzania sasa tujitahidi kuinua viwango vya mijadala hapa jamvini.

FJM, je unataka kusema kuwa Slaa hajasema kuwa bei ya cement ataishusha mpaka shilingi elfu 5? This is too soon kuanza kubadilisha badilisha lugha. Zipo video zimerekodiwa wakati Slaa anaahidi kushusha bei ya cement. Akibisha tutazileta video tatu katika maeneo matatu tofauti aliyorekodiwa akisema hivyo.
 
Kutokwenda shule na kuvamia siasa ndiyo taabu yake, huelewi kabisa uchumi na masoko na mtililiko wake katika dunia hii. Bado unadhani tanzania inafuata siasa ya ujamaa.
 
Thread haizungumzii uchumi wa Tanzania. Inazungumzia siasa za kilaghai za kuahidi kushusha bei ya cement mpaka shilingi elfu 5, halafu miaka mitatu baadae mtu huyohuyo anasema anaamini bei inapaswa kuwa determined na forces of demand and supply.
 
Nyie mamluki na wala vya kutupiwa na ccm,hamna haya hata kidogo kwani mnawadharau watanzania kwa kushabikia na kujaribu kufuta aibu za ccm,kwa kuleta uzi zisizo na miguu wala kichwa.Mlaaniwe na mwenyezi mungu wote kwa kuwauwa TEMBO,KUTOROSHA TWIGA,KUIBA KODI ZA WANANCHI,EPA,RICHMOND,MEREMETA,KUUZA MKOA WA MTWARA KWA WACHINA,SHAME ON YOU CCM,MUUNGU AWALAANI
 
Hahahahahahaha

Mkuu, umenikumbusha Slaa kila siku hadhithi yake ni EPA tu. Hana jipya zaidi ya story za EPA ndio maana ameamua kutunga ulaghai wa kushusha bei ya cement.
 
Wakati nasoma post hii nilipokuta neno uongo na kuomba radhi nikapa jibu.
Jibu kikwete alituaidi maisha bora kwa kila mtz je yako wapi? Na amefanya nini

Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania MWENYE BIDII.

Huwezi kukaa kibarazani unapiga story kuanzia asubuhi mpaka jioni halafu utegemee maisha bora yakufuate.

Nyinyi ndio watu mnaolalamika kuwa Mengi ana vitalu vingi, lakini ukiulizwa wewe umeomba vingapi unajibu hujawahi kuomba! Sasa kama hujawahi kuomba kwanini unakasirika Mengi akiwa navyo vingi?
 
Nazidi kuamini kuwa sisi watanzania tuna matatizo, na zaidi ya hapo naamini zaidi kuwa kuna bbadhi yetu hawafikirii kabisa. Mfano ni huyu mleta uzi.
Asanteni wadau kwaa kumpa majibu murua, kama ana akili ataelewa.
 
Dr. Slaa ni mwanasiasa MLAGHAI.

Wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 Dr. Slaa alizunguka baadhi ya sehemu za Tanzania (hakufanya kampeni nchi nzima) na kuwalaghai watu kuwa iwapo watampigia kura basi atashusha bei ya cement mpaka shilingi elfu tano kwa mfuko mmoja. Wapo vijana wasiofikiri kwa kina waliolaghaika na kushabikia ahadi hiyo ya kilaghai, lakini watanzania wengi walikuwa werevu na kutambua ulaghai wa Dr. Slaa na hivyo hawakumpigia kura. Matokeo yake Dr. Slaa alishindwa vibaya katika uchaguzi huo na kushindwa kupata hata asilimia 29 ya kura!

Leo bila aibu Dr. Slaa ametoa taarifa hadharani kuwa Chadema ni chama kinachoamini mfumo wa KIBEPARI. Katika taarifa yake hiyo amefafanua kuwa Chadema inaamini kwenye Market Economy ambapo bei ya kitu huamuliwa na nguvu za demand and supply. Kwa lugha nyepesi ni kwamba taarifa aliyotoa leo Dr. Slaa ni kuwa yeye na chama chake cha Chadema wanaamini kuwa kupanga bei ya cement iwe sh. elfu tano SIO SAHIHI.

Huu ni ulaghai wa hali ya juu. Katika sehemu alizozunguka, Dr. Slaa aliwalaghai watu wazima na machifu wa jamii mbalimbali juu ya bei ya cement. Katika jamii za kiafrika inaaminika kuwa kumlaghai chifu ni kuikosea heshima jamii yote anayoiongoza. Kwa hiyo Dr. Slaa amedhihirisha uchu wa madaraka uliopitiliza kiwango mpaka anazivunjia heshima jamii za watanzania.

Kistaarabu, baada ya Dr. Slaa leo kukiri kuwa alivyokuwa anatangaza kushusha bei ya cement alikuwa anadanganya, basi anawajibika kuomba radhi. Kuomba radhi ni jambo la kiungwana, hata hivyo Dr. Slaa anafahamika kwa tabia yake ya kutokuomba radhi kwa makosa mbalimbali anayofanya. Katika historia, Dr. Slaa ndio mgombea Urais wa kwanza aliyewahi kutamka hadharani kuwa ana mpango wa kuanzisha vurugu ili nchi isitawalike. Hata hivyo hakuomba radhi kwa kauli yake hiyo chafu mpaka leo!

Hata pale alipotoa siri za ofisi yake hadharani kwa lengo la kumdhalilisha mwanasiasa mwenzake, pia hakuomba radhi!

Katika historia ya siasa za Tanzania Dr. Slaa hajawahi kuomba radhi hata siku moja. Hii ni kumaanisha kuwa anajiona kuwa yuko perfect.

Kuomba radhi ni hatua ya awali ya uwajibikaji. Kiongozi asiyekuwa na utashi wa kuomba radhi kwa makosa yake yaliyo bayana, hawezi hata kujiwajibisha kwa kujiuzuru. Hii si dalili nzuri kwa upande wa Dr. Slaa. Mtu wa namna hii hafai kuaminiwa katika majukumu yenye mamlaka kubwa. Watu wenye macho wameshaona hilo...

Kijana wa leo usikubali kuwa victim wa siasa za kilaghai...

hii rubbish inakuwa reduced to this:Kwa vile kila alichosema alipanga na kukisimamia na bado ni kweli.Ulishawahi msahuri JK hilo..?Haya mauaji nchini....?
 
Back
Top Bottom