Dr Slaa azushiwa kifo

Status
Not open for further replies.

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,096
2,000
Katika hali inayoonekana Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa anatikisa anga la siasa za Tanzania jana wabaya wake wamemzushia kifo.

Katika SMS zilizokuwa zinasambazwa kwa watu mbalimbali ilidaiwa Dr Slaa amepata ajali ya gari na kufariki dunia.

Hali hiyo ilisababisha hofu kubwa kwa watu mbalimbali na kwa muda mfupi simu zilikuwa zikipigwa kila kona huku Taifa likiwa na tahuruki kubwa kwa muda mfupi.

Akizungumza na Nipashe Dr Slaa alisema yeye ni mzima wa afya bali kinachofanywa ni mchezo mchafu.Dr Slaa alisema maadui wa CHADEMA wanaweweseka na wanadhani wakizusha hivyo wanamtakia mabaya.Kiongozi huyo shupavu aliongeza kuwa kumzushia kifo ni kumuombea mema ambapo siku zake za kuishi zinaongezeka.

Source: Nipashe Jumapili.
 
kelao

JF-Expert Member
Sep 24, 2012
6,941
2,000
Tatizo la magamba kuishiwa sera ndo wanatapatapa kwa kila njia,lakini wakumbuke alilolipanga MUNGU binadamu hawezi kulibadili.
 
  • Thanks
Reactions: Ame

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
37,629
2,000
Ukiona hivyo, ujue kuna mpango unaandaliwa na wanajaribu kusoma reaction ya watanzania endapo watatekeleza huo mpango wao.
 
Nicholas

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
25,289
2,000
wanajiandaa tena mdhuru kwa ajali?Ndio wanaanza bipu wananchi?hata wakifanya hivyo nchi haitakalika, na huyo mamluki wao naye hatopata.
 
MNAMBOWA

JF-Expert Member
Oct 17, 2011
2,024
1,500
Alianza yeye kumzushia mkuu wa mkoa wa shy wakati wa uchaguzi kuwa amefariki kwake leo anaona uchungu?
 
RC.

JF-Expert Member
May 24, 2012
444
0
Katika hali inayoonekana Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa anatikisa anga la siasa za Tanzania jana wabaya wake wamemzushia kifo.

Katika SMS zilizokuwa zinasambazwa kwa watu mbalimbali ilidaiwa Dr Slaa amepata ajali ya gari na kufariki dunia.

Hali hiyo ilisababisha hofu kubwa kwa watu mbalimbali na kwa muda mfupi simu zilikuwa zikipigwa kila kona huku Taifa likiwa na tahuruki kubwa kwa muda mfupi.

Akizungumza na Nipashe Dr Slaa alisema yeye ni mzima wa afya bali kinachofanywa ni mchezo mchafu.Dr Slaa alisema maadui wa CHADEMA wanaweweseka na wanadhani wakizusha hivyo wanamtakia mabaya.Kiongozi huyo shupavu aliongeza kuwa kumzushia kifo ni kumuombea mema ambapo siku zake za kuishi zinaongezeka.

Source: Nipashe Jumapili.
POLE SANA DR.ila naomba uwe makini kwani yawezekana ndio plan zao!tunaomba jambo hilo lifuatiliwe ikibidi mtu huyo aliyetuma ujumbe huo akamatwe na kuswekwa ndani,kwani upuuzi kama huo utaendelea na kuua watanzania wenye pressure!
 
Domy

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
4,698
1,195
Wanakusafishia njia baba usishtuke tuko nyuma yako na Mwenyezi MUNGU akulinde maisha yako yote.hatutegemei uchawi kama wao, Tulianza na MUNGU tutamaliza na MUNGU.
 
  • Thanks
Reactions: Ame

mmwaisoba

JF-Expert Member
May 20, 2012
434
0
Huko ni kujitafutia Umaarufu. Hicho kifo kakibuni Slaa mwenyewe baada ya kuona anguko la kasi la propaganda za CHADEMA na MTIKISIKO WA MKUTANO WA KINANA ARUSHA. KWA HILI BABU SLAA APUMZIKE TU WANAMDANGANYA. HANA MVUTO UONGO WAKE UMESHAELEWEKA KWA WATANZANIA NA KUDAI ANATAKA KUUWAWA AU KUDAI AMEKUFA NI SEHEMU YA POROJO AMBAZO SI MPYA KWA WATANZANIA. NO BODY HAS TIME AND SPACE FOR SUCH HHHHHHHAAAAAAAAAAAAA
 
STIDE

JF-Expert Member
Sep 1, 2011
997
195
Thubutuuu!!!!

Ccm tuachieni nchi yetu kwa amani, hii mizengwe yenu ya kipumbavu haitowasaidia!! Sana sana tutawaingizia vijiti ndo iwe heshima kwenu!!!
 
Domy

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
4,698
1,195
Huko ni kujitafutia Umaarufu. Hicho kifo kakibuni Slaa mwenyewe baada ya kuona anguko la kasi la propaganda za CHADEMA na MTIKISIKO WA MKUTANO WA KINANA ARUSHA. KWA HILI BABU SLAA APUMZIKE TU WANAMDANGANYA. HANA MVUTO UONGO WAKE UMESHAELEWEKA KWA WATANZANIA NA KUDAI ANATAKA KUUWAWA AU KUDAI AMEKUFA NI SEHEMU YA POROJO AMBAZO SI MPYA KWA WATANZANIA. NO BODY HAS TIME AND SPACE FOR SUCH HHHHHHHAAAAAAAAAAAAA
Mbona mwenyekiti wa magamba aliwahi kuzushiwa kwamba ana UKIMWI mpaka akaanzisha kampeni ya kupima kwa hiari! Na yeye akaenda kupima.Je ilikuwa ni kutafuta umaarufu?
 
Status
Not open for further replies.
Top Bottom