Dr Slaa Atoa Tamko Juu ya Kutangaza Mali Zake!

Dr Slaa Atoa Tamko Juu ya Kutangaza Mali Zake!

Hivi nyie chadema mbona wapuuzi? Kwani kiongoz mwadilifu kutangaza mali zake hadharan hilo linahitaj upinzan wa act na chadema??
 
Sidhani Kama Ni kweli, ila Kama Ni kweli, kiliachoandikwa Ni kweli Na kweli tupu, ntampuuza Dr Slaa, Na ntamwanini ZZK, sidhan Kama Dr anaweza kukopi Na kupesti, tena kwa lengo la kushindana Na ACT, I don't think that untill I see my and hear it. Watz wanajua kuwa huwezi kuwaaminisha kuwa wewe Ni mwema kwa kuandika umiliki wako wewe mwenyewe chumban kwako Na mkeo, then kesho ukausoma mwenyewe kwa chama chako, Na kushangiliwa Na wapambe wako, then ukasema nimeongeza kiwango cha iman kwa watz, sidhani. Nin maana ya Auditing,yaan taarifa inayokuhusu uiandae mwenyewe, uikague mwenyewe, uiwasilishe mwenyewe,then utegemee kuongeza kukubalika kwa kuwa taarifa hiyo itawaaminisha watz, huo nadhan Ni ukichaa, Ni uwendawazimu uliopitiliza, Kwan kuwa Na Mali chache ndo sifa ya kuwa rais? AMA kuwa Na Mali nyingi ndo kigezo cha kuwa mbunge? Mali Ni zako Na familia yako, Uzalendo wa kweli haupimwi kwa idadi ya umiliki alionao mtu. Unaniambia Nyumba zako ili iweje?? Napenda nione uwezo wako wa kuongoza, ujuzi wako juu ya mambo, maamzi yako Na shabaha ya maamzi hayo, mikakati yako katika utendaji, sera zako katika mambo ya msingi, uvunaji Na matumizi ya rasilimali za nchi, hivyo vina maana kwangu. Mapendekezo juu ya njia za kukabiliana Na changamoto za maisha, mchango wako katika utatuzi wa matatzo yetu, kiwango cha kodi Na matumizi take kwa manufaa ya nchi, uwajibikaji, nk sio kuimba ngonjera za huo ndo umilki wangu. Nonsense so Dr hawez kufanya ivo
 
Cdm wabaguz sana,ukanda ndo unawamaliza aisee,

Mkubali/msikubali dr. Slaa ndo aliyewafungua macho, watanzania waliowengi wakajua haki zao, ikumbuke Tz ya 1990s na baada ya mwaka 2000.
Kazi alofanya Dr. Slaa bungen miaka 2000 hadi 2010 ya kufichua ufisadi na kuibana serikali juu ya haki za wanyonge waweza kumfananisha na nani?
Ninachokiona kwa haraka ni kwamba hata ufanye harakati na ushujaa wa namna gani utasahaulika tuu! lkn kuwa na pesa tu utakumbukwa hata uwe dhambi litasahaulika
 
WanaJF,

Katibu mkuu wa CHADEMA, Dr Slaa, ameandaa tamko maalumu kwa wapenzi wote wa CHADEMA na Watanzania kwa ujumla juu ya kuziweka mali zake hadharani!

Tukio hili la kijasiri ambalo limepangwa kufanywa na Dr Slaa litaenda sambamba na kuweka wazi mshahara wake anaopewa na CHADEMA pamoja na marupurupu mengine.

Katika kufikia hatua hiyo, Dr Slaa pamoja na wafuasi wake wanaamini wataweza kusambaratisha kasi ambayo ACT - Tanzania imekuja nayo.

Aidha, baadhi ya wadau wa mtaa wa Ufipa wamesema pamoja na Dr Slaa kuandaa tamko hili la kijasiri, bado wana mashaka juu ya usahihi wa orodha ya mali ambazo Dr Slaa ana miliki.

Je, wewe unadhani Dr Slaa, Mbowe, Sugu, Msigwa na makamanda wengine waandamizi wataweza kuziweka hadharani mali zao kama ambavyo mzalendo Zitto amethubutu kufanya?

kuna ukweli wowote kuwa zzk anamiliki hizo tu?alikuwa wapi kutujuza hizo mali tangu kipindi chote alichojihusisha na siasa and why at this period?
Hizo ni siasa za kitoto.political maturity is needed.hatuhitaji sisi kujua mali zake ili kuudanganya umma kwamba yeye ni msafi.
Hulka yake inajidhihirisha wazi kwa wale wenye upeo wa kuelewa mambo hivyo haitupi shida kujua who is a puppet and a double standard
 
Kwa mtindo huu wa ACT na CHADEMA, upinzani hautachukua hii nchi kamwe. Daima naamini umoja ni nguvu, hao ACT na CHADEMA kama wangeungana na kusimamisha mgombea mmoja nahisi wangekuwa na nguvu zaidi.

Yaani CDM iungane na vibaraka was ccm? cdm IPO field inazidi kutoa dozi ya kujitambua huwezi ilinganisha na hilo genge LA wasaka tonge
 
Hivi nyie chadema mbona wapuuzi? Kwani kiongoz mwadilifu kutangaza mali zake hadharan hilo linahitaj upinzan wa act na chadema??

Kwanini Ujae Povu Wakati Habari Yenyewe Ni Ya Kutungwa Hii?
 
Eti kama mzalendo Zitto alivyofanya.Kwa akili yako ya kuzaliwa bila kuchanganya na za walimu waliokunoa darasani
UNASADIKI KUWA ZITTO ANAMILIKI 18 M?
Mshahara wa mbunge kwa mwezi nalipata kusoma humu ni around 11 M (nakaribisha kukosolewa)amekaa bungeni miaka 10.

Zitto ni mwizi mkubwa sana asidanganye watu hapa! Hivi lile hama ni sh.ngapi? Na zile millioni 500 ni za nani pale bank?
 
Unajua Zitto hana washauri vizuri, kiongozi wa Umma ndio anatakiwa atangaze mali zake kila mwaka. Sasa mimi sielewi kwani ACT ni nini? Mnajua msikurupuke kuandika vitu msivyo vijua, tena viongozi wote wa kuchaguliwa, na walioteuliwa wajathibitishwa na bunge. Sasa Zitto alipipewa uongozi huo wa ACT alithibitishwa na Bunge? Au amechaguliw na watanzania wote waliojiandikisha kwenye daftari la kupiga kura? Jamani msipotoshwe nyie wenye akili haba, leo hii mimi nitangaze mali zangu ba najaza fomu anayoitunza Mwigamba, jamani acheni kutupumbaza watanzania. Fomu za uhakiki wa mali zinapojazwa zinasimamiwa na tume ya maadili na kuhifaziwa huko kwa ajili ya kuziupdate kila mwaka, kama mali imeongezeka au imepungua, la mwisho namshukuru Mungu kwa kuwa Mtanzania maana nuru iko njiani.
 
Back
Top Bottom