Dr Slaa Atoa Tamko Juu ya Kutangaza Mali Zake!

WanaJF,

Katibu mkuu wa CHADEMA, Dr Slaa, ameandaa tamko maalumu kwa wapenzi wote wa CHADEMA na Watanzania kwa ujumla juu ya kuziweka mali zake hadharani!

Tukio hili la kijasiri ambalo limepangwa kufanywa na Dr Slaa litaenda sambamba na kuweka wazi mshahara wake anaopewa na CHADEMA pamoja na marupurupu mengine.

Katika kufikia hatua hiyo, Dr Slaa pamoja na wafuasi wake wanaamini wataweza kusambaratisha kasi ambayo ACT - Tanzania imekuja nayo.

Aidha, baadhi ya wadau wa mtaa wa Ufipa wamesema pamoja na Dr Slaa kuandaa tamko hili la kijasiri, bado wana mashaka juu ya usahihi wa orodha ya mali ambazo Dr Slaa ana miliki.

Je, wewe unadhani Dr Slaa, Mbowe, Sugu, Msigwa na makamanda wengine waandamizi wataweza kuziweka hadharani mali zao kama ambavyo mzalendo Zitto amethubutu kufanya?

Dada Hamida upo?
 
Eti kama mzalendo Zitto alivyofanya.Kwa akili yako ya kuzaliwa bila kuchanganya na za walimu waliokunoa darasani
UNASADIKI KUWA ZITTO ANAMILIKI 18 M?
Mshahara wa mbunge kwa mwezi nalipata kusoma humu ni around 11 M (nakaribisha kukosolewa)amekaa bungeni miaka 10.

Mimi nahisi watanzani tuna tatizo la uelewa au tunafanya makusudi. Ukirejea ile fomu imesema M 18 ni pesa taslimu alizokuwa nazo kipindi anajaza fomu kataja pia kiasi cha Tshs alizonazo bank, Euro pamoja na dola, na akaunti nyingine anayoimiliki pamoja na dada yake. Hata kama mtu anapata milioni 11 kwa mwezi kuna matumizi mengi tu anafanya ambayo huwezi ukayahesabu kama mali, yani unakuwa umetumia zimekwenda.
 
Haitawahi kutokea, habari za NURU NA UZIMA

zikaletwa na MJUMBE WA GIZA!

Haitatokea na wala usijisumbe kuzitilia maanani
 
Tangu lini umekuwa msemaji wa CHADEMA? Yasiyokuhusu mwachie Ngoswe.

WanaJF,

Katibu mkuu wa CHADEMA, Dr Slaa, ameandaa tamko maalumu kwa wapenzi wote wa CHADEMA na Watanzania kwa ujumla juu ya kuziweka mali zake hadharani!

Tukio hili la kijasiri ambalo limepangwa kufanywa na Dr Slaa litaenda sambamba na kuweka wazi mshahara wake anaopewa na CHADEMA pamoja na marupurupu mengine.

Katika kufikia hatua hiyo, Dr Slaa pamoja na wafuasi wake wanaamini wataweza kusambaratisha kasi ambayo ACT - Tanzania imekuja nayo.

Aidha, baadhi ya wadau wa mtaa wa Ufipa wamesema pamoja na Dr Slaa kuandaa tamko hili la kijasiri, bado wana mashaka juu ya usahihi wa orodha ya mali ambazo Dr Slaa ana miliki.

Je, wewe unadhani Dr Slaa, Mbowe, Sugu, Msigwa na makamanda wengine waandamizi wataweza kuziweka hadharani mali zao kama ambavyo mzalendo Zitto amethubutu kufanya?
 
Mbowe akitangaza mimi najihudhuru kuishi Duniani. Labda adanganye.
 
Sidhani kama Dr Slaa ana guts za kuanika mali zake. Hii nadhani inatokana na kujilimbikizia mali nyingi baada ya kuupata ukatibu mkuu wa CHADEMA!

jambo ambalo linanishangaza ni pale ambapo CHADEMA ilikuwa ikikemea matumizi mabaya yanayofanywa na serikali wakati huo huo na wao wanatumia pesa za walipa kodi wanazopata kwa njia ya ruzuku kununua Mashangingi kwa ajili ya viongozi waandamizi wa CHADEMA!

Sasa hapa najiuliza, huyu Dr Slaa akipata huo urais anaoutaka ataweza kubadili lolote linalofanywa sasa na serikali ya CCM? Au ni ujinga wa Watanzania kumuamini mtu bila ya kuwa na taarifa zake kiundani?
 
Upo sahihi kabisa,ukitumia akili ya asili bila ya kuchanganya ya mwalimu inawezekana sana ningekuwa na mawazo finyu na hafifu kama yako!

Labda nikusaidie kidogo tu kuondoa chengachenga za umbumbumbu. Unaposikia neno mali au "assets" ina maana kuwa kuna aidha mali zisizo hamishika, zinazo hamishika, hisa (untangible assets) na cash au pesa.

Kitu ambacho Zitto amefanya ni kutangaza mali zake pamoja na madeni.Kwa lugha ya kihasibu tunasema ametangaza 'assets' na 'liabilities'. Ambalo neno liability linajumuisha na madeni pia.

Hivyo basi, nakutaka wewe na watu wengine wa aina yako muelewe kuwa, neno mali halina maana ya cash pekee. Tena pia hata matajiri kama Mengi utakuwa pale alipo hata Million mia moja benki hana, Je utasema Mengi ni maskini? Watu wamewekeza kwenye hisa za makampuni, watu wanamiliki mahoteli, pesa ipo kwenye mizunguko ili ijizalishe zaidi.

Nadhani somo umelielewa.

Mbumbumbu unaweza kuwa wewe mkuu! Ukisoma alichotangaza zitto cash ni 18 M.asset ni nyumba mbili zenye thamani ya around milioni 223 gari 74 M,kiwanja na mashamba 24 M na madeni ya jumla ya jumla ya 174.6 M.
Sasa angilia analyisis yako ilivyo zero.Zito hana biashara hayo madeni ya 174.6 fedha alifanyia nini?.Ukifanya total ya asset alizomazo ni kama M miatatu na point.Ukichua mshahara wake wa miaka michache ulitosha kuwa na asset hizo,je mshahara wa miaka 10?alafu na hayo madeni ambayo ni nusu ya asset zote fedha hizo alipeleka wapi?
RUDI SHULE
 
Wakutakiwa kurudi shule ni wewe mkuu! Maana hata mimi ambae siipendi siasa niliweza kuisoma ile fomu ambayo Zitto amejaza na niliweza kuielewa. Kwa taarifa yako tu, baadhi ya assets zake ikiwemo nyumba na kiwanja huko Kigamboni alizipata kupitia pesa ya mkopo kutoka benki ya NBC na mkopo kutoka hazina.

Ushauri wangu: Badala ya kumwambia mleta mada aende shule, ni vyema urudi ukaisome ile fomu kwa utulivu ili uweze kujenga hoja zenye mashiko. Nje ya hapo, JF sio mahala pa watu wa kukurupuka tu, kwa tabia hiyo nenda kwa waweka viduku huko Facebook.
 
Sidhani Kama Slaa yuko too low kiasi cha kutaka kimbizana na mpuuzi wenu.

He is too old for that shit Kama huyo kima anafikiri CDM inaishi kwa kumfwata fwata yeye au kushindana naye amechemsha.

Mpe pole maana amepoteza dira kiasi cha kujisaliti hata nafsi yake kutoka kuwa mpinzani mpaka kuwa mpinzani Wa upinzani....

His hell is too near......

Sina cha kuongeza, umemaliza.
 
Mimi nahisi watanzani tuna tatizo la uelewa au tunafanya makusudi. Ukirejea ile fomu imesema M 18 ni pesa taslimu alizokuwa nazo kipindi anajaza fomu kataja pia kiasi cha Tshs alizonazo bank, Euro pamoja na dola, na akaunti nyingine anayoimiliki pamoja na dada yake. Hata kama mtu anapata milioni 11 kwa mwezi kuna matumizi mengi tu anafanya ambayo huwezi ukayahesabu kama mali, yani unakuwa umetumia zimekwenda.

Soma hapo chini mwenzio nimemjibu
 
Kwenye kundi la watu wajinga sana hapa duniani usisahau kujiorodhesha. wewe ni mpumbavu kabisa.
 
Wakutakiwa kurudi shule ni wewe mkuu! Maana hata mimi ambae siipendi siasa niliweza kuisoma ile fomu ambayo Zitto amejaza na niliweza kuielewa. Kwa taarifa yako tu, baadhi ya assets zake ikiwemo nyumba na kiwanja huko Kigamboni alizipata kupitia pesa ya mkopo kutoka benki ya NBC na mkopo kutoka hazina.

Ushauri wangu: Badala ya kumwambia mleta mada aende shule, ni vyema urudi ukaisome ile fomu kwa utulivu ili uweze kujenga hoja zenye mashiko. Nje ya hapo, JF sio mahala pa watu wa kukurupuka tu, kwa tabia hiyo nenda kwa waweka viduku huko Facebook.

Ndio maana nikakuambia tumia akili! au rudi ukanoe akili.Mkopo au madeni aliyonayo yanafanya cover 50+parcent ya total asset alizoorodhesha.je mshahara wa 11 M kwa miaka 10 alikuwa anafanyia nini?
 
Sidhani kama Dr Slaa ana guts za kuanika mali zake. Hii nadhani inatokana na kujilimbikizia mali nyingi baada ya kuupata ukatibu mkuu wa CHADEMA!

jambo ambalo linanishangaza ni pale ambapo CHADEMA ilikuwa ikikemea matumizi mabaya yanayofanywa na serikali wakati huo huo na wao wanatumia pesa za walipa kodi wanazopata kwa njia ya ruzuku kununua Mashangingi kwa ajili ya viongozi waandamizi wa CHADEMA!

Sasa hapa najiuliza, huyu Dr Slaa akipata huo urais anaoutaka ataweza kubadili lolote linalofanywa sasa na serikali ya CCM? Au ni ujinga wa Watanzania kumuamini mtu bila ya kuwa na taarifa zake kiundani?

Naona Zitto anawasaidia CCM kuzima joto la ufisadi linalowakabili na kuelekeza attention CDM ili kufurahisha mabwana wake.

Bahati mbaya Sana jinsi mlivyo duni kiasi cha kupata akili ya kuchambia tu mnaingizwa kwenye migogoro binafsi ya huyo mpuuzi.

Ungekuwa na akili ungetumia muda huu kupigania maisha yako kuliko kuwa sehemu ya kupigania kilio cha mkosaji Zitto.
 
Last edited by a moderator:
shirika letu lina nafasi za kazi anatafutwa mtaalamu wa kuchoronga miamba (nafasi 6) , awe na uzoefu miaka 15, mshahara milioni 10, nyumba gari, atapewa. 2. Pia anatafutwa mpishi awe na uzoefu wa miaka 7 wa kupika migebuka, mshahara milioni 5, tafadhali sambaza matangazo haya hapo lumumba...tangazo hili limeletwa kwako kwa udhamini wa act-mwandiga kwa kushirikiana na mafisi (ccm) (na

Niko mtaa wa ufipa hapa. Tumelidiss tangazo lako.

Limekaa ki'shost zaid.
POLE SANA!
 
Mbowe akitangaza mimi najihudhuru kuishi Duniani. Labda adanganye.

Naona Zitto kaamua kufukazana na kimbunga....

Kwa asili ya uruhani alonayo anafikiri atawin....

Mkumbusheni Zitto ujumbe huu toka kwenye kitabu cha Mungu;

Mhubiri 12:14 ‘’Kwa maana MUNGU ataleta
hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri,
likiwa jema au likiwa baya.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom