Dr Slaa atinga kwenye media za Kenya

Dr Slaa atinga kwenye media za Kenya

Ametoa hotuba kali ya kuponda nchi kutegemea misaada na akasema katika hotuba kuwa CHADEMA haioni misaada kama kitu cha maana.Cha ajabu kamalizia hotuba yake kwa kukiomba chuo cha Samford kitoe msada wa kuelimisha watanzania.Ni kujichanganya kwenda mbele!!

Karudie kusoma tena inaonekana hukuelewa vizuri
 
Tanzania ilipofia kuwa na raisi ambaye anadharauliwa na maraisi wa nchi jirani tena wengine ni wavuta bangi basi hiyo ni ishara ya wazi kuwa JK anaidhalilisha Ikulu ya Magogoni.

Mungu azidi kumjalia afya njema Dkt Slaa ili hatimaye watanzania wote wapate kunufaika na utumishi wake. Watanzania 2015 lazima kieleweke, hakuna kurudia makosa!
Kudharauliwa ni subjective na kwa maana hii sikuelewi unajenga hoja kwa dokezo lipi linalobeba uzito unaokufanya uone ni jambo la ajabu sana.

Mbona hata Marais wa nchi 'zilizoendelea' wanadharaulika ndani ya nchi zao achilia mbali nje ya nchi. Kitu gani kinakufanya uone kama kudharaulika ni jambo la ajabu sana.

Wengine walishawahi mpaka kupondewa viatu kwenye press conference.

By the way. Rais Kikwete haruhusiwi kikatiba kugombea tena, vile vile CHADEMA haijampitisha Dr. Slaa kuwa mgombea Urais, lakini kikubwa zaidi, mpaka sasa hatufahamu tutakuwa na mfumo gani wa serikaii tutakapoingia kwenye chaguzi kitaifa, otherwise unatupa ujumbe kuwa CHADEMA siyo chama cha demokrasia kama jina lake lisemavyo.
 
ametoa hotuba kali ya kuponda nchi kutegemea misaada na akasema katika hotuba kuwa chadema haioni misaada kama kitu cha maana.cha ajabu kamalizia hotuba yake kwa kukiomba chuo cha samford kitoe msada wa kuelimisha watanzania.ni kujichanganya kwenda mbele!!

mbona amesema toka mwanzo kuwa tanzania inahitaji misaada ya elimu, inahitaji tekinolojia ya kisasa wanachi wajifunze na si net, haujaelewa nini hatuhitaji samani tunahitaji ndoano ya kuvulia samaki ili tusiende kuomba tena, tatizo lako mkuu akiri yako imekaa kimagamba sana
 
Ni Mtazamo wangu tu wadau, nimefungua post hii kwa muwashawasha mkubwa lkn at the end nakutana na hiki1 comment:

  1. b36-rounded.png
    MAINAOctober 10, 2013 at 3:09 AM
    Tanzanians have a long way to go.....The have at first eradicate the slow culture especially in everything they do...But Still the corruption challenges Tanzania faces is not different as compared to many African countries including Kenya.Reply
Just a single comment only pamoja na uzuri wa hotuba ya muheshimiwa! nadhani mtoa mada next time tafakari juu ya kichwa cha habari ili kiendane na contents zilizomo ndani.

Umeanza kwa mbwembwe sana nanukuu ''Kama utani vile lakini ndio kweli.Ile speech aliyoitoa Dr Slaa sasa imeonekana kukubalika katika baadhi ya nchi za kiafrika.Kuanzia na jirani zetu wakenya ambao wao sasa wameanza kuijadili hotuba hiyo kwenye mitandao yao ya kijamii." huo wingi nilitegemea ungekuwepo kwenye comments. Anyway nimalizie Hotuba ilikuwa nzuri sana"
Mkuu usi-judge kwa kusoma comment za watu isome speech mwenyewe, mfano mgeni akisoma post za Simiyu Yetu atafikiri watanzania wote tuna akili za aina hiyo.
 
Last edited by a moderator:
Posted by Daniel Ominde at 2:39 AM mpaka sasa ni 3:19 PM, zaidi ya masaa 12 yamepita, ka comment kamoja tu. Nendeni mkajaze comments ionekane inajadiliwa kwa sana.

Hizo media "ZA" Kenya ziko wapi? si mngesema imebandikwa kwenye ka blog ka moja na ina comment moja tu mpaka sasa!

Hivi huwa mnaona sifa kujidanganya hata nafsi zenu?

Faiza, speech ya Dr. Slaa inapatikana pia hapo: Speech by Dr Slaa at The University of Samford, USA - wavuti.com

Tutaendelea kukupa updates kadiri speech ya Secretary General inavyozidi kusambaa around the globe. Vuta subira bibie.
 
Dr Slaa mungu akubariki sana, akupe maisha marefu yenye afya njema ili uje ulikomboe taifa letu tajiri linalotafunwa na kirusi cha kichina kwenye kila nyanja, huku vijiji wachina wanadiriki ku compete na wanakijiji kumiliki maeneo potential, nchi yetu tanzania inakua kama nchi ya familia ya kikwete, najaribu kujiuliza viongozi wa ccm hawaoni huu upuuzi unafanywa na rais kikwete? hawana hata uwezo wa kumkaripia??? mungu ailaani ccm na kiama chenu ni mwaka 2015
 
wewe ni mpuuzi kweli,
Kwaakili yako unafikiri Mods ndio wanaokwenda kutafuta habari?

Mimi soni ajabu yoyote kwa hotuba ya Dr. Slaa kutua kwenye mitandao ya Wakenya. Lakini nalaumu upendeleo wa wazi unaoonyeshwa na Mods humu. Mbona inasemekana hotuba ya "Mzee wa Mipasho" a.k.a Isha Mashauzi ilitua kwenye mitandao ya Waganga wa kienyeji wa Bwagamoyo, lakini hamkuiripoti humu! Je kule kwani haikuwa hadhi yake ile hotuba kutua? Si kila hotuba inatua kwenye sehemu yenye hadhi yake lakini?
 
Kudharauliwa ni subjective na kwa maana hii sikuelewi unajenga hoja kwa dokezo lipi linalobeba uzito unaokufanya uone ni jambo la ajabu sana.

Mbona hata Marais wa nchi 'zilizoendelea' wanadharaulika ndani ya nchi zao achilia mbali nje ya nchi. Kitu gani kinakufanya uone kama kudharaulika ni jambo la ajabu sana.

Wengine walishawahi mpaka kupondewa viatu kwenye press conference.

By the way. Rais Kikwete haruhusiwi kikatiba kugombea tena, vile vile CHADEMA haijampitisha Dr. Slaa kuwa mgombea Urais, lakini kikubwa zaidi, mpaka sasa hatufahamu tutakuwa na mfumo gani wa serikaii tutakapoingia kwenye chaguzi kitaifa, otherwise unatupa ujumbe kuwa CHADEMA siyo chama cha demokrasia kama jina lake lisemavyo.

Mkuu hapa sio mkutano wa Chama cha CHADEMA.Hii ni social media...ni watu wanatoa tu maoni yao...huwezi kuzuia maoni ya watu...Still huwezi kusema eti CHADEMA sio chama cha demokrasia kwa sababu washabiki wengi wanampendekeza dr slaa,tena kupitia social media ambayo sio kikao cha chama.

Otherwise.Hauhitaji darubini au hadubini kujua ni jinsi gani JK anadharaulika.....Refer kutengwa kwetu kwenye East Africa ni kwa sababu ya uongozi wake dhaifu,Kushindwa kujua kwa nn Tanzania ni maskini pia ni jambo ambalo hata mjinga atamdarau.........

Kudharaulika ni jambo la ajabu kwa sababu Baba ukidharauliwa na watoto nyumbani basi ujue una walakini katika uongozi wako...Kama wa nchi nyingine wandharaulika that does not justify JK kudharaulika...Two wrongs does not make a right.....Otherwise Tanzania itapaa tukimkabidhi huyu Visionary leader Dr Slaa jukumu la kutuongoza....TOGETHER WE CAN
 
Wapuuuzi,wajinga na wapumbavu ndio watakaopinga na kumis-interprete hotuba (it is neat speech) hii ya Dr.Slaa iliyojaa ukweli wenye mustakabali chanya wa Taifa letu la Tz.
 
Makubwa hayo, (sitaki msaada, nataka msaada!) babu kachanganyikiwa huyo.

cc Dr.W.Slaa

Acha ujinga wewe! Hataki msaada wa vyandarua; hataki msaada wa maboksi ya viatu; hataki msaada wa maziwa bali anataka msaada wa UJUZI (skills) ili resources zilizofurika kila mahali ziweze kutumika kuibadili Tanzania kuwa pepo ya kila mtanzania na sio ya mafisadi na vizazi vyao. Umemsoma?
 
Nina furaha sana juu ya hii hotuba! Wale ambao nilikua nawaambia kwamba CHADEMA ndio mkombozi wetu wakawa wanasita nilipowapa hii kitu wamestaajabu sana kumbe na wao walishaipata kabla sijawapa na wanamatumaini na Chama hiki.
 
Hapa Ghana, nilimwonesha mmoja tu mwanzoni, mfanyakazi mwenzangu, baada ya kama dakika 10, wafanyakazi karibu wote 33, kila mmoja alikuwa na kopi ya hotuba hiyo, na kila mmoja akiomba digital copy ili aweze kuwatumia wenzake, na wengine wamesema wanawatumia viongozi wao wa serikali na wabunge. Kila mmoja ameifurahia, na kusema ndivyo viongozi wa Afrika wanavyotakiwa kufikiri na kutenda. Hotuba hiyo imekuwa ni gumzo.

Kuna yale maneno ya kwenye Biblia, 'Nabii hasifiki nyumbani', nimeamini. Wakati Watanzania walio wengi wameichukulia ni hotuba ya kawaida na baadhi kuibeza, wenzetu nchi nyingine wameipa uzito unaostahili. Ghana ipo juu sana kiuchumi na kidemokrasia ukilinganisha na Tanzania lakini kila aliyeisoma hotuba hiyo amestajabia uzito wa maneno yaliyopo ndani yake, na wengi wanasema kuwa huo ndiyo ulitakiwa kuwa msimamo na mwongozo wa utawala wa Africa.

Nakala: FaizaFoxy, Ritz, Simiyu Yetu, na Mabuku 7 wooote popote pale mlipo bila kulisahau li- stroke (Mungu apishe mbali. Liwamalize huko huko Lumumba)
 
Hotuba nimeisoma na kunisisimua. Hapa kuna kitu cha msingi. Lampuni kama African Barrick ambayo kimsingi ni kampuni ya Tanzania kwa maana baba yake ni Barrick Gold corporation na ina migodi 4 Tanzania. Kama bodi ya wakurugenzi inachota Tsh. Bilioni 76 kwa mwaka na zinaenda hukohuko Marekani na Canada. Kwa miaka 5 ni kiasi gani. Wakitunulia vyandarua kama msaada hii kweli haija tulia. Tulitakiwa kuwa na vission kama Mongolia na Botswana.
 
Makubwa hayo, (sitaki msaada, nataka msaada!) babu kachanganyikiwa huyo.

cc Dr.W.Slaa
Ukisoma kwa miwani ya magamba huwezi kuelewa...

Hebu vaa miwani huru uone ni vitu gani anavyotaka na asivyotaka kutoka kwao...

We need investors that will bring ..... a set of skills and creativity to turn our hardwood into high quality,
We need your partnership in fostering individual innovation within our people.
We need your technological know how.

We don't need your tax money; neither do we need your mosquito net donations, we need your skills.
We don't need shoe boxes, we need to know how to make our own shoes.
 
Dr Slaa mungu akubariki sana, akupe maisha marefu yenye afya njema ili uje ulikomboe taifa letu tajiri linalotafunwa na kirusi cha kichina kwenye kila nyanja, huku vijiji wachina wanadiriki ku compete na wanakijiji kumiliki maeneo potential, nchi yetu tanzania inakua kama nchi ya familia ya kikwete, najaribu kujiuliza viongozi wa ccm hawaoni huu upuuzi unafanywa na rais kikwete? hawana hata uwezo wa kumkaripia??? mungu ailaani ccm na kiama chenu ni mwaka 2015

NDUGU PUNGUZA MUNKARI,2015 FANYA IVI,,,,,:deadhorse:,,,,NA WEKA TIKI KWA,,,,,,,😛eace: ,,,,,
 
Mimi soni ajabu yoyote kwa hotuba ya Dr. Slaa kutua kwenye mitandao ya Wakenya. Lakini nalaumu upendeleo wa wazi unaoonyeshwa na Mods humu. Mbona inasemekana hotuba ya "Mzee wa Mipasho" a.k.a Isha Mashauzi ilitua kwenye mitandao ya Waganga wa kienyeji wa Bwagamoyo, lakini hamkuiripoti humu! Je kule kwani haikuwa hadhi yake ile hotuba kutua? Si kila hotuba inatua kwenye sehemu yenye hadhi yake lakini?

Duu, JF kuna mambo!?
 
Back
Top Bottom