Elections 2010 Dr. Slaa aongoza kwa 73% - CACT

Kama Bana nae ni msomi basi vyuo vikuu vya tanzania is a bunch of commedians who called themselves professional.
 
Utafiti wa Redet wapingwa kila kona


Saturday, 09 October 2010 07:07
MATOKEO ya utafiti wa Redet yaliyoonyesha kuwa mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete anaongoza kwenye kura za maoni, yamepingwa vikali na wasomi, wanasiasa na wananchi ambao baadhi wameeleza kuwa "yamepikwa ili kuwavuruga wapiga kura".Hata CCM ambayo mgombea wake amepata alama nyingi, imeeleza kuwa matokeo hayo hayakutoa picha halisi ya maoni ya watu kwsa Kikwete, ikidai kuwa alistahili kuongoza kwa kura nyingi zaidi za maoni.
Redet ilitangaza matokeo ya utafiti wake juzi ikieleza kuwa Kikwete alipata asilimia 71.2 ya kura za maoni katika utafiti uliofanyika mwezi Septemba na kufuatiwa na mgombea wa Chadema, Willibrod Slaa aliyepata asilimia 12.3 wakati Prof Ibrahim Lipumba, ambaye katika chaguzi mbili zilizopita alikuwa akishika nafasi ya pili, alipata asilimia 10.1.
Huku kampeni za uchaguzi zikizidi kuwa kali katika siku 22 za mwisho, matokeo hayo ya utafiti yamepingwa na wadau wa demokrasia waliohojiwa na Mwananchi wakisema utafiti huo unapaswa kulaaniwa kwa kuwa ni mkakati maalumu wa taasisi hiyo 'kuifagilia' CCM na kuijengea mazingira ya ushindi katika uchaguzi ujao, huku wasomi wakihoji vigezo vilivyotumika kupata watu waliohojiwa.

Wasomi na wanazuoni

Muhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Ezavel Lwaitama alisema ripoti ya utafiti huo ina upungufu mwingi.
Alisema ripoti hiyo haijaeleza umri wa watu walioulizwa maswali na kwamba hata uchaguzi wa maeneo ambayo utafiti huo ulifanywa una walakini.
“Ukiangalia matokeo ya ju juu utapotea," alisema msomi huyo. "Kwanza inabidi ujiulize katika maeneo ambao utafiti ulifanyika kuna watu wangapi, uangalie jinsia, umri wa watu waliolizwa na pia hata swali lilikuwa linasemaje.
“Wangetuambia kama wamehoji watu wa miaka 40, 60 na kuendelea, hakuna mtu angeshitushwa na ripoti hii, lakini pia swali lilisema utamchagua mgombea wa chama gani, wangeuliza ni kiongozi wa aina gani utamchagua, tungekuwa tunazungumza mengine hapa.”
Lakini akaonya kuwa CCM inatakiwa ijifunze jambo kutokana na maeneo ambayo ripoti hiyo imebainisha kuwa chama hicho kimefanya vibaya na upinzani ukawa na nguvu.
“Kwa mfano angalia Dar es salaam, CCM inaongoza Temeke CCM, lakini Kinondoni ambako tunaamini kuwa kuna wasomi na watu walioerevuka Chadema ndio imeongoza. Kwa hiyo wakati mwingine mtafiti anaweza kukupa somo bila wewe kujua,” alieleza.
Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Tumaini, Dk Failres Ilomo aliuponda utafiti huo akieleza kuwa hana sababu ya kuuamini kwa kuwa taasisi yenyewe inawajibika serikalini.
“Sisi (Chuo cha Tumaini) tuliomba kufanya utafiti huo, lakini walitukatalia na badala yake kazi hiyo ikipewa taasisi ya Redet ambayo ni taasisi ya umma ambayo kimsingi imefanya kazi ya mkuu wao,” alisema Dk Ilomo.
"Hao waliofanya walichaguliwa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambacho kiko chini ya serikali, lakini hata kama chuo cha serikali kimepata kazi hiyo, kilitakiwa kiwashirikishe wadau wengine ambao hawako chini ya serikali.”

Msomi mwingine ambaye ni mwanafunzi wa Udaktari wa Falsafa (PHd) katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Gasper Mpehongwa alidai utafiti huo si sahihi kwa sababu Dk Bana ni mshauri wa masuala ya siasa wa Rais Kikwete.
“Ni mtu ambaye yuko jirani sana na Kikwete, hivyo hawezi kutoa matokeo ambayo ni tofauti na Kikwete,” alidai Mpehongwa.
Mhadhiri mwingine wa Tumaini, Ordination Mgongolwa alisema: “Mimi nilipopata ripoti hiyo jana nilifedheheka sana kwa sababu kwanza Redet ni taasisi ambayo haiko huru; lakini pia ripoti yake ina msukumo wa CCM.
"CCM inawasukuma watu katika kampeni zake kwa kutumia vitu wakati watu wanaojaa katika vyama pinzani wanavutiwa na sera, hivyo CCM imefanya mbinu ya kuwakatisha tamaa wapiga kura. It is something cooked(ni kitu kilichopikwa) kwa sababu wanalipwa na serikali."

Vyama vya siasa
Katika hali isiyotarajiwa, utafiti huo pia umekosolewa na CCM ambayo imesema kuwa inaamini kuwa matokeo yake si sahihi kwa asilimia zote.
Meneja wa kampeni wa CCM, Abdulrahman Kinana alisema jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisi ndogo ya makao makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam kuwa utafiti huo una kasoro.
Hata hivyo, Kinana alikubaliana na utafiti huo katika kipengele kinachomwonyesha mgombea wa0 anaongoza, lakini akaeleza kuwa utafiti huo umeshindwa kueleza ukweli kwamba Kikwete atashinda zaidi ya asilimia 71.2.

“Hii ni tathmini ‘fair’ (nzuri), lakini si 100% correct (si sahihi kwa asilimia mia)," alisema Kinana.
Tutapata ushindi zaidi ya matokeo ya Redet. Kuna baadhi ya maeneo mimi sikubaliani nao. ‘I completely disagree’. Nyinyi mnaoripoti kila siku msubiri mtaona matokeo tutapata zaidi ya asilimia 90.”
Alitoa mfano wa maeneo ambayo alisema wazi kuwa hakubaliani na matokeo ya utafiti wa Redet ambayo aliyataja kuwa ni Kigoma Vijijini na Mvomero mkoani Morogoro ambako utafiti huo umeonyesha kuwa CCM imepata asilimia ndogo ya kura, lakini Kinana akasema chama hicho kitashinda kwa zaidi ya asilimia 90 katika maeneo hayo.

Alisema utafiti wa Redet ulifanywa kwa kuzingatia wilaya na si majimbo na kwamba upo uwezekano kwa waliohojiwa kutoka katika jimbo moja lenye mtazamo mmoja wa kisiasa na siyo majimbo yote katika wilaya.
Kuhusu kushuka kwa asilimia za ushindi wa mgombea wa CCM kulinganisha na utafiti wa taasisi hiyo wa mwezi Machi mwaka huu, Kinana alisema: “Nijibu hili la ‘kudrop, hii ni tathmini ‘fair’, lakini si ‘correct’ asilimia mia moja.”
Kwa kujiamini Kinana alisema mgombea wao wa urais atapata zaidi ya asilimia 80 ya kura na wabunge zaidi ya asilimia 76 na kuwaita wapinzani wasindikizaji, akieleza kuwa wagombea wake urais kwa ujumla wataambulia moja ya tatu ya kura za nafasi hiyo.

“Uchaguzi ni hesabu, ushindi ni hesabu, sisi tunajali hesabu... hii inatupa mwanga kuwa tutashinda," alijigamba.
Nayo CUF imesema haikubaliani na matokeo hayo ya Redet kwa kuwa inaamini kuwa ni mpango uliotumwa na CCM kufanya utafiti huo tena kwa maslahi binafsi.
Naibu katibu mkuu wa CUF- Bara, Joran Bashange alisema Redet inatumiwa na chama tawala tangu zamani hivyo kinachofanyika ni udanganyifu kwa wananchi.
“Huu mpango unatumiwa dhahiri na chama tawala kumfanyia mgombea wao kampeni ndio maana unaona wanampatia kura nyingi, lakini ikitokea kampuni nyingine inamuangusha," alisema.
Bashange alieleza baadhi ya mambo yanayofanya utafiti huo uonekana kuwa wa kupangwa ni pamoja na kutotoa mchanganuo wa idadi ya watu walioshiriki kutoa maoni zaidi ya kutaja asilimia zao tu.

"Maswali yanayoulizwa ni elekezi na hivyo majibu yake yalilingana na swali lilivyoulizwa," alisema.
Naye mgombea urais kwa tiketi ya APPT-Maendeleo, Peter Mziray aliuponda utafiti huo akisema haukufanywa kisayansi na umelenga kuibeba CCM.
“Kitaaluma, mimi ni mwanasayansi na utafiti uliofanywa na Redet naona kabisa haukufanywa kisayansi. Haiwezekani kura za Lipumba na Slaa zioane,” alisema.
“Mara kwa mara Redet wanapofanya utafiti wamekuwa wakiitaja CCM kuwa namba moja na sisi tunajua kwamba wanaibeba CCM,” alisema.
Alisema yeye amepita mikoa mingi kujinadi na kwamba anaelewa mwamko walionao wananchi kuhusu CCM na vyama vingine hivyo matokeo hayo kwa upande mwingine yanaweza kuwachanganya wananchi.
Alisema hata matokeo yanayoonyesha chama chake kupewa nafasi ndogo ya kushinda ni ya uongo kwa sababu yeye ametembea mikoa mingi na baadhi ya maeneo wananchi wana mwamko na chama chake.
Mwenyekiti huyo pia alitahadharisha kuwa kama taasisi hiyo itaendelea kuipendelea CCM, hawatavumilia watachukua hatua za kisheria.

“Sasa hivi niko busy mikoani kwenye kampeni lakini nina haki kabisa ya kuwashtaki, na kama wataendelea hivyo hatutavumilia,” alisema Mziray.
Mwenyekiti NCCR-Mageuzi, James Mbatia jana alishindwa kuzungumzia matokeo ya utafiti huo kwa madai kuwa hajausoma, zaidi ya kuona habari katika magazeti.
Mbatia, ambaye anawania ubunge jimbo la Kawe, alisema: “Siwezi kusema lolote... ningeweza kuzungumza kama ningekuwa nimeupitia na kujua nini kilichomo. Nikiupitia ninaweza kusema lolote kwa kuwa nitakuwa nimeulinganisha na tafiti nyingine zilizowahi kutolewa na Redet,” alisema Mbatia.
Kaimu katibu mkuu wa Chadema, John Mnyika hakuwa tayari kuzungumza jambo lolote juu ya utafiti wa Redet kwa maelezo kuwa chama kitatoa tamko lake leo.

Hata hivyo, meneja wa kampeni wa Chadema, Profesa Mwesiga Baregu alisema taarifa hiyo ina udhaifu kadhaa.
“Bado naisoma ili tutoe taarifa kesho (leo), lakini jambo la msingi la kuangalia pale ni 'je nani kaulizwa maswali, utafiti umefanyika maeneo gani, swali lilikuwa linasemaje,” alisema Profesa Baregu.
“Inaelekea watafiti walipelekwa kwa wajumbe wa nyumba kumi wa CCM”.
Habari kutoka Tanga zinasema mgombea ubunge wa Jimbo la Korogwe Mjini kwa tiketi ya Chadema, Kalistus Shekibaha ameichachamalia taarifa ya utafiti huo akidai kuwa imepikwa ili kuwavuruga wapigakura.
Alisema utafiti huo haukubaliki na kuzitaka taasisi zinazoendesha tafiti kuwaachia wananchi waamue wenyewe viongozi wanaowafaa na si kuendesha kura za maoni ambazo zina lengo la kuwakatisha tamaa wagombea.

“Unapotoa taarifa za kitafiti, unatakiwa kutoa uchambuzi ambao utasababisha uheshimiwe na wananchi... lakini unapoonekana kubabaisha unasababisha wananchi kukosa imani na wewe,” alisema Shekibaha.
Mgombea huyo alisema, hata hivyo, kuwa kutokana na kuzifahamu njama hizo, wagombea kutoka vyama vya upinzani hawawezi kukata tamaa badala yake wataendelea kupiga kampeni ili kuwaachia wananchi kujua nani wa kuwafaa.
Wakati mgombea huo akieleza hayo, mwananchi mmoja jijini Dar es Salaam aliyejitambulisha kwa jina la Kilimba Fulgence alipiga simu Mwananchi na kusema kuwa kuna kila dalili kwamba utafiti huo umefanywa katika maeneo ambayo CCM ina mashabiki wengi.
Matokeo hayo ya Redet yamekuja katika kipindi ambacho kuna mzozo mkubwa baina ya taasisi nyingine inayofanya utafiti wa masuala ya kijamii, kisiasa na kiuchumi ya Synovate na Chadema ambayo inadai kuwa mgombea wake wa urais, Dk Willibrod Slaa aliongoza kwenye kura ya maoni iliyofanywa na taasisi hiyo.

Synovate imekana kufanya utafiti wa aina hiyo na kwamba hadi sasa imefanya utafiti kuhusu mwenendo wa vyombo vya habari katika kuripoti habari za uchaguzi mkuu, lakini Chadema imesema inao ushahidi kuwa taasisi hiyo iliendesha utafiti ulioonyesha kuwa Dk Slaa alipata asilimia 45 dhidi ya 40 za Kikwete.

Katika matokeo ya utafiti wa Redet, CCM inaonekana itapoteza wabunge wengi baada ya matokeo kuonyesha kuwa chama hicho tawala kitapata asilimia 66.7 za kura, ikiwa ni kuanguka kwa asilimia 4.5.

Kwa mujibu wa Redet, matokeo yangekuwa hivyo iwapo uchaguzi mkuu ungefanyika kati ya Septemba 20 hadi 28 mwaka huu.
Akitoa matokeo ya utafiti huo wa 17 uliofanyika katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na Visiwani katika kipindi hicho cha Septemba, Dk Bana alisema jana kuwa waliohojiwa walitakiwa kutoa maoni kuhusu uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani.

Alisema katika utafiti huo wahojiwa waliulizwa: "Mwezi Oktoba mwaka huu utafanyika uchaguzi mkuu.
Kama uchaguzi huo ungefanyika leo, je wewe ungemchagua mgombea wa chama gani?"
Alifafanua kuwa kutokana na swali hilo vyama vitatu vya CCM, CUF, Chadema vilipata alama nyingi kwa wagombea wake wa urais, wabunge na madiwani.

Hata hivyo, Dk Bana alisema kiwango cha asilimia za kura kimepungua kwa mgombea wa CCM kulinganisha na utafiti uliofanywa na Redet mwezi Machi wakati matokeo yalipoonyesha kuwa asilimia 77.2 wangemchagua mgombea urais wa CCM na tofauti na asilimia 71.2 alizopata safari hii.
"Itakumbukwa kwamba matokeo ya utafiti wa Redet wa hapo Machi mwaka 2010 yalionyesha wengi wangemchagua mgombea urais wa CCM asilimia 77.2. Katika utafiti CCM bado inaongoza, hata hivyo kiwango cha asilimia kimepungua," alisema Dk Bana.
Dk Bana alisema utafiti huo wa Redet ulifanywa kwa kuwahoji watu 2,600 katika wilaya 52 na kwamba watu 1,849 ndio waliosema watamchagua mgombea wa CCM, 263 wa CUF na 319 mgombea wa Chadema.
Ikilinganisha na utafiti wake wa mwezi Machi mwaka huu, Redet ilisema kuwa katika kipindi cha miezi sita kilichopita, idadi ya watu ambao wangemchagua mgombea wa Chadema imeongezeka kwa asilimia nane (8) kutoka 4.2 za mwezi Machi hadi 12.3.

Redet ilitaja pia kuongezeka kwa asilimia 0.9 kwa kura za urais wa CUF, asilimia 02 kwa TLP na 0.1 kwa NCCR-Mageuzi huku ikitaja sababu kuwa ni kampeni za uchaguzi zinazoendelea.
Lakini, taasisi hiyo ilisema mgombea urais wa CCM anaongoza kwa kutajwa jina lake kama mtu ambaye wangependa awe rais wa Tanzania na asilimia 68.5 ya wahojiwa wote akifuatiwa na Dk Slaa wa Chadema aliye na asilimia 11.9 huku Profesa Lipumba wa CUF akiwa wa tatu kwa asilimia 9.3 ya wahojiwa.

Taasisi hiyo ya utafiti wa kitaalam ilisema kuwa katika kura za urais, CCM itapata kura kidogo zaidi katika Jimbo la Kigoma Vijijini ambako atapata asilimia 28 huku Jimbo la Nkasi akipata asilimia zote 100.
Kwa mujibu wa utafiti huo, kwa upande wa wabunge wa Jamhuri ya Muungano, pia asilimia ya watakaochagua mgombea wa CCM imepungua kwa asilimia 1.3, huku ikiongezeka kwa vyama vya upinzani, vikiongozwa na Chadema ambayo imeongezeka kwa asilimia 2.9, CUF 1.5, TLP na NCCR-Mageuzi asilimia 0.8 kila kimoja.

Habari hii imeandaliwa na Fidelis Butahe, Burhani Yakub, Tanga, Hussein Issa, Jackline Laizer, Nora Damian, Petro Tumaini, Fredy Azzah, Exuper Kachenje na Emmy Kihongole
 
Hizi kura za maoni zisikupe pressure, CCM wamezoea kuchakachua kila kitu. Lakini mwaka huu tumesema hatudanganyikiiiiii. REDET ni wakala wa chama tawala! Hapa maswali mengi yanajitokeza kuliko majibu. Ni vipi chombo cha kisomi namna hiyo kinakubali kununuliwa? Jibu: kulinda maswalihi binafsi. In this case some scholars have studied but they are not educated. Here is the origin (etymology) of the 'educate': educate
"bring up (children), train," from L. educatus, pp. of educare "bring up, rear, educate," which is related to educere "bring out, lead forth," from ex- "out" (see ex-) + ducere "to lead" (see duke). Meaning "provide schooling" is first attested 1580s. Tukichukua maana ya "bring out, lead forth", ni kusema kuwa kuelimika maana yake ni kuondoa ujinga au utumwa wa giza na kuingia katika mwanga wa uhuru. Sasa hawa wasomi wetu wa REDET tuwake wapi? EDUCATION FOR LIBERATION.
 
Nimekubali kuwa watu wanafuatilia vitu. Hayo ndiyo mambo kuliko kukaa pale Mlimani na kuanza kutengeneza tarakimu.
 
Unajua REDET walichokifanya wanajua wenyewe na ndo maana ata CCM sijawaona kushadadia ayo matokeo

Ni kweli mkuu CCM wenyewe wako kimya wala hawayashabikii hayo matokeo ya utafiti wa REDET maana dhamira zao zinawasuta. Inasemekana utafiti huo wa REDET uliwahusisha viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya shina hii ina maana kuwa hata viongozi wa CCM hawamtaki Kikwete.
 
Nimeona mambo mawili makubwa hapo
Mosi: kunatofauti kubwa kati ya tafiti za kisayansi zilizo endeshwa na wasomi na polls za media zinazo wezesha mtu kupiga kura hata mara 1000
Kenda:..................................

Hey, give me a break!!! wasomi wapi unaowasema?? UDSM kuna wasomi au waganga njaa? I would like to tell you Tanzania na hasa University of Dar es salaam hakuna msomi hata mmoja. Hawa unaowaita wewe wasomi ndiyo hawa wanaoishauri serikali kuhusiana na mambo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa, na hali ya Tanzania ndiyo hii unayoiona. Huwa wanashauri nini basi? Au usomi wao unaisaidiaje nchi? Ukitaka kujifunza zaidi kuhusu hao unaowaita wasomi, angalia ni nin wanafanya wakiingia kwenye siasa. Pumba tupu!! Utalinganisha vipi utendaji wa Ngeleja na Professor Magembe?

My friend, ondoa kabisa habari ya wasomi uchwara hawa wanaotafuta kupata chochote kutoka CCM. Jiulize ni kwa vipi utafiti wa Synovate ulizuiwa usitangazwe halafu wa REDET ukashadadiwa hivyo? Hapa hakuna kitu kabisa, REDET ni toilet paper ya CCM.
 
nina babu yangu kimazichana hata kutumia internet hawezi, asilimia kubwa ya watanzania si watumiaji wa internet basi hizo on-line hatafika hata robo ya watanzania.. subiri majibu october 31st .. hapa nasubiri slaa akitafuta sababu za kushindwa kwake
 
Dr Slaa yes we can! :llama:
Huyu ni mtanzania wa pili baada ya Nyerere kuchukia ufisadi kwa vitendo. Ni mtanzania wa pili kuchukia umaskini wa watanzania kwa vitendo. Ni Dr. Slaa aliyesimama na kutaja majina ya wala rushwa na mafisadi. Akataka wale wanaopinga wampeleke mahakamani. Hakuna aliyethubutu kujitokeza kumpeleka mahakamani.


Ni Dr. Slaa aliyesimama bungeni kuomba posho za wabunge kupunguzwa kuzielekeza zaidi kwa watanzania maskini. Ni Dr Slaa aliyesimama bila woga kunyosha vidole kwa matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa amekuwa mtanzania baada ya Nyerere kutoa hoja za nguvu zinazomlenga kumkomboa mtanzania maskini. Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi? Ajira milioni moja ziko wapi? Hebu mwenye mbavu za kujibu swali hili ajibu bila unafiki!


Ni Dr Slaa anayeweza kudhibiti matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa anayeweza kuwapa elimu ya bure watoto wetu pale mlimani. Achana na longolongo za CCM kuwatoza ushuru watoto. Waulizeni majukwaani wao Nyerere aliwatoza ada? Kama si kutaka watanzania waendelee kuwa mambumbumbu ni nini? kama si kutaka watanzania tuendelee kuwa watumwa ni nini?


Ni Dr Slaa anayeongelea mfumko wa bei -nani hajajua dola leo hii ni sawa na tsh 1500. Uchumi unadidimia kwa kasi. Ahadi nyingine za uongo lukuki zinatolewa tena, wakati zile tulizoahidiwa mwaka 2005, hata moja haijatekelezwa. Watanzania walio wengi na hasa wa vijijini, wamelala usingizi. Wanafumbuliwa macho, lakini wamesinzia bado! Wanatabasamu, wanachekelea na kuridhika na vitisheti vya kijani na vikofia za njano. Wamekwishazoea shida kiasi kwamba wanadhani ni sehemu ya maisha yao. Ee mwenyezi Mungu, tunusuru na hili balaa..


Ni Dr.Slaa anaweza kuzuia wizi wa matrilion ya pesa kutoka migodi yetu ya Buzwagi, Geita, Bulyankulu, Buhemba, Nyamongo, Tulawaka, Nzega na Tanzanite. CCM wameshindwa kwa sababu ni washirka wakubwa na wameruhusu wizi huo. Ni Dr Slaa anaeweza kuwalipa wafanyakazi zaidi ya shilingi 350.000 achana na longolongo za CCM ambayo imeshindwa kusimamia maliasili ambazo zingeliwapa wafanyakazi kima cha chini kinachokidhi mahitaji yao. :llama:


Ni Dr. Slaa ambaye amepanga kubadili katiba ili Rais afuate matakwa ya walio mwajiri ambao ni wananchi. Waulize CCM hata kama mtu kaiba anapewa mda arudishe pesa. Hivi inaingia akilini kweli? Utawala wa sheria uko wapi?


CCM hawawezi hayo? Eti wanataka ushahidi. Nani kawambia rushwa tule wawili harafu tutoe vielelezo? Tunaiona rushwa kwa matokeo yake. Matengenezo ya barabara ya bilion 200, baada ya siku mbili imeharibika. Kwanini usimfukuze waziri na katibu wake wa wizara kwanza? CCM hawawezi! eti wanataka vielelezo!


Ni Dr Slaa anayeweza kufanya hayo. Nani anabisha! Si tumeona alivyowataja mafisadi wote! hapo akiwa ni mbunge tu! Je akiwa rais si watakimbia nchi? Jamani nawambia tumpe miaka mitano tu awakurupushe muone moto utakavyowaka.. Tutapata dawa, tutapata shule za bure, tutapata madawati. Jamani hivi kweli karne ya leo watoto wanasoma wamekalia mawe? We must be serious!


Nani asiye jua madaktari wetu wengi bingwa wapo botswana kwa sababu ya maisha duni Tanzania na hivi kwenda kutafuta maisha bora wakati hapa kwetu wananchi maskini wanakufa bila madawa? Nani asiyejua matatizo ya umeme, maji, makazi, maradhi, yanavyotutesa? Nani asiyejua wakulima wetu wasivyokuwa na masoko ya mazao yao? Nani asiejua asilimia 85 ya watanzania wanatumia vibatari au makoroboi kama mwanga? nani asiejua tunavyonyonywa na hawa wakoloni waliokuja kuchukua kila kitu?


Jamani wafanyakazi, wakulima, na wanafunzi, kwa nini mnalala usingizi? Kwa nini mnapiga miayo ya njaa wakati maghala yetu yamejaa nafaka? Ni akili gani hii? Nchi yetu inazo raslimali za kututosha, lakini wanaozifaidi ni vibaka wachache. Mtalala hadi lini?


Ni Dr Slaa mzalendo wa kweli, na sio kwa ajili ya sifa, anaweza kutuvusha tulipo. Nchi hii ni maskini na umaskini wenyewe ni wa kujitakia. Tanzania ni tajiri tuna kila kitu - mito, maziwa, national parks, migodi, mazao ya misitu, na kila aina ya utajiri. Lakini kila leo rais kuwaabudu wazungu na bakuli la kuombaomba! Naona huruma na umaskini wa kifikra wa watanzania. Ee Mungu utuhurumie! :llama:


Hivi kuna mtu hajui mapolisi wanalala kwenye vibanda vya mabati? Hivi kuna ambao hawajui mapolisi watendaji wanalipwa laki moja? Wamekosa nini hawa? Ni ajabu! pamoja na laki yao moja utakuta bado wanatumika kuwanyanyasa watetezi wao. Hata maaskari amkeni hiyo laki moja yenu haina tija hadi mrubuniwe kuwanyanyasa wapinzani ambao kimsingi wanawatetea ninyi! Hivi maaskari mnayo macho ya kuona? Jamani tuache woga inawezekana! Mbona Kenya wameweza? Mbona malawi wameweza?Mbona zimbabwe wameweza? Mbona Ghana wameweza? Kufanya mabadiliko sahihi, inawezakana na nafasi ni hii tuitumie.


Tumtume Dr Slaa atukurupushie wezi wote na atuwekee katiba sawa. Huo ndio msingi wa yote. Ni Dr. Slaa asiyeogopa kuwepo na mgombea binafsi. CCM hili hawaliwezi. Wamelipinga hadi mahakamani. Wanataka wao tu ndio waendelee kututawala na kutunyonya.

Jamani 2010 hakuna kudanganyika! enough is enough. Acheni kudanganyika. Wakati ndio huu. Watanzania msipoamua sasa, mtamlaumu nani tena? Nawatamani watu wa kule Mara -hakuna kura inaibiwa. Zote zinasimamiwa. Tukibadilika inawezekana, tena ni rahisi.


Peleka ujumbe huu kwa marafiki, ndugu, jamaa, babu na bibi yako kule kijiji ambako wanadhani bado Nyerere ndiye rais wa nchi hii. Waambie Nyerere alikwishakufa na nchi imeishatekwa nyara na vibaka. Peleka ujumbe huu haraka kwa simu kama ipo, au kwa njia ya posta, mradi tu wale jamaa waliochoka kuishi wasiikwapue barua wakidhani ni hela..

:llama: :preggers:
 
:smow: :llama::smow::moony:
Dr Slaa yes we can!
Huyu ni mtanzania wa pili baada ya Nyerere kuchukia ufisadi kwa vitendo. Ni mtanzania wa pili kuchukia umaskini wa watanzania kwa vitendo. Ni Dr. Slaa aliyesimama na kutaja majina ya wala rushwa na mafisadi. Akataka wale wanaopinga wampeleke mahakamani. Hakuna aliyethubutu kujitokeza kumpeleka mahakamani.


Ni Dr. Slaa aliyesimama bungeni kuomba posho za wabunge kupunguzwa kuzielekeza zaidi kwa watanzania maskini. Ni Dr Slaa aliyesimama bila woga kunyosha vidole kwa matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa amekuwa mtanzania baada ya Nyerere kutoa hoja za nguvu zinazomlenga kumkomboa mtanzania maskini. Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi? Ajira milioni moja ziko wapi? Hebu mwenye mbavu za kujibu swali hili ajibu bila unafiki!


Ni Dr Slaa anayeweza kudhibiti matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa anayeweza kuwapa elimu ya bure watoto wetu pale mlimani. Achana na longolongo za CCM kuwatoza ushuru watoto. Waulizeni majukwaani wao Nyerere aliwatoza ada? Kama si kutaka watanzania waendelee kuwa mambumbumbu ni nini? kama si kutaka watanzania tuendelee kuwa watumwa ni nini? :llama::A S 112::moony:


Ni Dr Slaa anayeongelea mfumko wa bei -nani hajajua dola leo hii ni sawa na tsh 1500. Uchumi unadidimia kwa kasi. Ahadi nyingine za uongo lukuki zinatolewa tena, wakati zile tulizoahidiwa mwaka 2005, hata moja haijatekelezwa. Watanzania walio wengi na hasa wa vijijini, wamelala usingizi. Wanafumbuliwa macho, lakini wamesinzia bado! Wanatabasamu, wanachekelea na kuridhika na vitisheti vya kijani na vikofia za njano. Wamekwishazoea shida kiasi kwamba wanadhani ni sehemu ya maisha yao. Ee mwenyezi Mungu, tunusuru na hili balaa..


Ni Dr.Slaa anaweza kuzuia wizi wa matrilion ya pesa kutoka migodi yetu ya Buzwagi, Geita, Bulyankulu, Buhemba, Nyamongo, Tulawaka, Nzega na Tanzanite. CCM wameshindwa kwa sababu ni washirka wakubwa na wameruhusu wizi huo. Ni Dr Slaa anaeweza kuwalipa wafanyakazi zaidi ya shilingi 350.000 achana na longolongo za CCM ambayo imeshindwa kusimamia maliasili ambazo zingeliwapa wafanyakazi kima cha chini kinachokidhi mahitaji yao.


Ni Dr. Slaa ambaye amepanga kubadili katiba ili Rais afuate matakwa ya walio mwajiri ambao ni wananchi. Waulize CCM hata kama mtu kaiba anapewa mda arudishe pesa. Hivi inaingia akilini kweli? Utawala wa sheria uko wapi? :hand::llama::preggers::smow:


CCM hawawezi hayo? Eti wanataka ushahidi. Nani kawambia rushwa tule wawili harafu tutoe vielelezo? Tunaiona rushwa kwa matokeo yake. Matengenezo ya barabara ya bilion 200, baada ya siku mbili imeharibika. Kwanini usimfukuze waziri na katibu wake wa wizara kwanza? CCM hawawezi! eti wanataka vielelezo!


Ni Dr Slaa anayeweza kufanya hayo. Nani anabisha! Si tumeona alivyowataja mafisadi wote! hapo akiwa ni mbunge tu! Je akiwa rais si watakimbia nchi? Jamani nawambia tumpe miaka mitano tu awakurupushe muone moto utakavyowaka.. Tutapata dawa, tutapata shule za bure, tutapata madawati. Jamani hivi kweli karne ya leo watoto wanasoma wamekalia mawe? We must be serious!


Nani asiye jua madaktari wetu wengi bingwa wapo botswana kwa sababu ya maisha duni Tanzania na hivi kwenda kutafuta maisha bora wakati hapa kwetu wananchi maskini wanakufa bila madawa? Nani asiyejua matatizo ya umeme, maji, makazi, maradhi, yanavyotutesa? Nani asiyejua wakulima wetu wasivyokuwa na masoko ya mazao yao? Nani asiejua asilimia 85 ya watanzania wanatumia vibatari au makoroboi kama mwanga? nani asiejua tunavyonyonywa na hawa wakoloni waliokuja kuchukua kila kitu? :llama::tonguez::moony:


Jamani wafanyakazi, wakulima, na wanafunzi, kwa nini mnalala usingizi? Kwa nini mnapiga miayo ya njaa wakati maghala yetu yamejaa nafaka? Ni akili gani hii? Nchi yetu inazo raslimali za kututosha, lakini wanaozifaidi ni vibaka wachache. Mtalala hadi lini?


Ni Dr Slaa mzalendo wa kweli, na sio kwa ajili ya sifa, anaweza kutuvusha tulipo. Nchi hii ni maskini na umaskini wenyewe ni wa kujitakia. Tanzania ni tajiri tuna kila kitu - mito, maziwa, national parks, migodi, mazao ya misitu, na kila aina ya utajiri. Lakini kila leo rais kuwaabudu wazungu na bakuli la kuombaomba! Naona huruma na umaskini wa kifikra wa watanzania. Ee Mungu utuhurumie!


Hivi kuna mtu hajui mapolisi wanalala kwenye vibanda vya mabati? Hivi kuna ambao hawajui mapolisi watendaji wanalipwa laki moja? Wamekosa nini hawa? Ni ajabu! pamoja na laki yao moja utakuta bado wanatumika kuwanyanyasa watetezi wao. Hata maaskari amkeni hiyo laki moja yenu haina tija hadi mrubuniwe kuwanyanyasa wapinzani ambao kimsingi wanawatetea ninyi! Hivi maaskari mnayo macho ya kuona? Jamani tuache woga inawezekana! Mbona Kenya wameweza? Mbona malawi wameweza?Mbona zimbabwe wameweza? Mbona Ghana wameweza? Kufanya mabadiliko sahihi, inawezakana na nafasi ni hii tuitumie. :llama::smow::preggers:


Tumtume Dr Slaa atukurupushie wezi wote na atuwekee katiba sawa. Huo ndio msingi wa yote. Ni Dr. Slaa asiyeogopa kuwepo na mgombea binafsi. CCM hili hawaliwezi. Wamelipinga hadi mahakamani. Wanataka wao tu ndio waendelee kututawala na kutunyonya.

Jamani 2010 hakuna kudanganyika! enough is enough. Acheni kudanganyika. Wakati ndio huu. Watanzania msipoamua sasa, mtamlaumu nani tena? Nawatamani watu wa kule Mara -hakuna kura inaibiwa. Zote zinasimamiwa. Tukibadilika inawezekana, tena ni rahisi.


Peleka ujumbe huu kwa marafiki, ndugu, jamaa, babu na bibi yako kule kijiji ambako wanadhani bado Nyerere ndiye rais wa nchi hii. Waambie Nyerere alikwishakufa na nchi imeishatekwa nyara na vibaka. Peleka ujumbe huu haraka kwa simu kama ipo, au kwa njia ya posta, mradi tu wale jamaa waliochoka kuishi wasiikwapue barua wakidhani ni hela..
:llama::decision::smow:
 
Nilikua nasikiliza taarifa asubuhi hii kutoka Radio Free Africa, nimeshtushwa na taarifa ya mtu aliyejitambulisha kua ni mkurugenzi wa taasisi inayojishughulisha na utafiti (CACT) kama wa REDET) akiipinga report ya REDET kwa kusema taasisi yao nayo inaendelea na utafiti huo kwa njia mbalimbali, sms, emails, kuhoji moja kwa moja, etc nchi nzima.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo hadi sasa Dr. Slaa anaongoza kwa 73%, JK 12% na Lipumba 9%. Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo anapinga kitendo cha REDET kuchagua baadhi ya mikoa na kuacha mikoa mingine especially kanda ya Ziwa ambako ndio kuna wapiga kura wengi na anapinga report yenye only 2600 samples.

Siifahamu kampuni hii (CACT), wanaJF mwenye taarifa zaidi atuhabarishe

StarTV pia walionesha kwenye taarifa ya habari ya saa2 usiku jana. Waliwahoji jamaa na kuwaonesha mahojiano hayo.
 
nina babu yangu kimazichana hata kutumia internet hawezi, asilimia kubwa ya watanzania si watumiaji wa internet basi hizo on-line hatafika hata robo ya watanzania.. subiri majibu october 31st .. hapa nasubiri slaa akitafuta sababu za kushindwa kwake

Umezaliwa wapi? pwani? maana vijiji vingi watu wamebadilika;
 
Ni kweli mkuu CCM wenyewe wako kimya wala hawayashabikii hayo matokeo ya utafiti wa REDET maana dhamira zao zinawasuta. Inasemekana utafiti huo wa REDET uliwahusisha viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya shina hii ina maana kuwa hata viongozi wa CCM hawamtaki Kikwete.
I know ur joking

paulss, kumbuka watakopiga kura trh 31Oktoba ni hao unaowaita si wasomi kwani ndiyo walio wengi na nafasi waliyoipata kueleza msimamo wao ni kwenye hizo media unazozidharau.
Mkuu nadhani hapa hatutofautiana kukubaliana kwetu,
nilikuwa namaanisha kuwa hao wasio wasomi na walio wengi hawana access ya kuvote ktk media polls,hivyo matokeo ya polls hizo hayana uwakilishi wao hivyo hayana credibility yoyote


Hey, give me a break!!! wasomi wapi unaowasema?? UDSM kuna wasomi au waganga njaa? I would like to tellyou Tanzania na hasa University of Dar es salaam hakuna msomi hata mmoja . Hawa unaowaita wewe wasomi ndiyo hawa wanaoishauri serikali kuhusiana na mambo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa, na hali ya Tanzania ndiyo hii unayoiona. Huwa wanashauri nini basi? Au usomi wao unaisaidiaje nchi? Ukitaka kujifunza zaidi kuhusu hao unaowaita wasomi, angalia ni nin wanafanya wakiingia kwenye siasa. Pumba tupu!! Utalinganisha vipi utendaji wa Ngeleja na Professor Magembe?

My friend, ondoa kabisa habari ya wasomi uchwara hawa wanaotafuta kupata chochote kutoka CCM. Jiulize ni kwa vipi utafiti wa Synovate ulizuiwa usitangazwe halafu wa REDET ukashadadiwa hivyo? Hapa hakuna kitu kabisa, REDET ni toilet paper ya CCM.
Lukolo kwanini mnapenda kugeneralise, leo kwasababu tu REDET ina wasomi wa UDSM na wametoa matokeo usiyoyapenda wewe basi nchi hii haina wasomi, hivi hao wasomi wa CHADEMA wamesoma wapi? unauliza ya Ngeleja na Magembe, vipi ya Beregu na zitto? usitake niamini ndio maana mmesimamisha mwenza wa Slaa STD seven
Mkuu ntakuelewa mantiki yako kama utadai REDET kama wao wamevurunda lakini kuhoji usomi wa UDSM hapo utakuwa nje ya mstari

nina babu yangu kimazichana hata kutumia internet hawezi, asilimia kubwa ya watanzania si watumiaji wa internet basi hizo on-line hatafika hata robo ya watanzania.. subiri majibu october 31st .. hapa nasubiri slaa akitafuta sababu za kushindwa kwake
Mkuu nakubaliana na wewe kabisa nina hakika ni asilimia kama 1,5 ndio wana access na net
Kila chaguzi mambo huwa hivi hivi na mwisho wa siku tafiti za REDET ndizo hutoa taswira inayo oana na matokeo ya mwisho
 
Back
Top Bottom