Dr. Slaa aongoza kwa 73% - CACT | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa aongoza kwa 73% - CACT

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by coby, Oct 9, 2010.

 1. coby

  coby JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2010
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 342
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nilikua nasikiliza taarifa asubuhi hii kutoka Radio Free Africa, nimeshtushwa na taarifa ya mtu aliyejitambulisha kua ni mkurugenzi wa taasisi inayojishughulisha na utafiti (CACT) kama wa REDET) akiipinga report ya REDET kwa kusema taasisi yao nayo inaendelea na utafiti huo kwa njia mbalimbali, sms, emails, kuhoji moja kwa moja, etc nchi nzima.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo hadi sasa Dr. Slaa anaongoza kwa 73%, JK 12% na Lipumba 9%. Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo anapinga kitendo cha REDET kuchagua baadhi ya mikoa na kuacha mikoa mingine especially kanda ya Ziwa ambako ndio kuna wapiga kura wengi na anapinga report yenye only 2600 samples.

  Siifahamu kampuni hii (CACT), wanaJF mwenye taarifa zaidi atuhabarishe
   
 2. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Bado hakujakucha subiri, hata maoni ya watu wengi kupitia itv walionyesha wasiwasi wa moja kwa moja kuhusu redet
   
 3. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,923
  Likes Received: 627
  Trophy Points: 280
  wewe hukuona jamaa wa REDET kuyatangaza alisema najua mtasema sana lakini habari ndio hiyo. huoni kama ile Tafiti imekaa kiumbea umbea!!
   
 4. p

  politiki JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2010
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Taarifa ya REDET inaweza kuwa sahihi kabisa inategemea umemwoji nani? cha msingi hapa ni sampling.
  ktk hawa watu 2600 ni lazima kuna wenye na wasio na vyama.

  Kwahiyo ktk ripoti yao ilibidi waonyeshe ktk waliowaoji ni wangapi wana ccm, wangapi wapinzani na la msingi wangapi kati ya hao 2600 hawana vyama. Hawa ni muhimu kwa maana ndio hasa wanaochagua Rais kwa maana watanzania wengi hawana vyama.

  Kwa Tanzania kama sample yako haina asilimia 30, aslimia 20 wapinzani na asimilia 50 ambao hawana
  vyama. Basi utafiti au survey yako nzima haina maana kwa maana it does not reflect reality.
   
 5. E

  EDOARDO Senior Member

  #5
  Oct 9, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hao REDET hawawezi kutoa taarifa sahihi. Lazima waipe moyo hiyo CCM. HAYO HAYAWEZI KUWA MATOKEO YA UTAFITI
   
 6. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Tutaona mengi
   
 7. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,552
  Trophy Points: 280
  Masahihisho ni kuwa taarifa ya REDET kamwe haiwezi kuwa ni sahihi kwa sababu malengo yake hayakuzingatiwa ambayo ni kupima joto la kisiasa nchi nzima wala siyo maeneo ambayo yanalenga kuupotosha umma wa watanzania.

  Tusitetee uozo nasi tukaoza. Tuukemee uozo ili usije ukarudia
   
 8. DICTATOR

  DICTATOR JF-Expert Member

  #8
  Oct 9, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  We still have a big challenge on professional ethics, njaa zinasumbua saana na hiyo ni kutokana na mtu kuwa trained ili awe tajiri kwa njia yeyote ile. Watu wengi wanasoma ili waibe na siyo kusoma ili wasaidie nchi kimaendeleo.

  Ndiyo maana taasisi kama REDET zinatumiwa na wanasiasa kufanyia kazi zao. Sehemu zenye kuelimisha umma zimeshakuwa za waanasiasa badala ya hawa wanasiasa kupata mawazo kutoka kwenye hizi taasisi sasa zimekuwa zikipata maelekezo kutoka kwa wasiasa mfano halisi ni kwa hawa REDET pamoja na kupoteza muda mwingi wakichimba/wakisoma darasaani ili kuleta tija katika taifa changa kama hili lakini badala yake wanasahau kuwa elimu yao ni nuru kwa taifa.

  Taasisi kama REDET ni kuanza nazo kuzivunja ili ziundwe zenye uhuru, kuaminika katika jamii na ufanisi wa hali ya juu. Tunahitaji kuamini tafiti toka kwa wataalamu ndiyo, lakini wa kwanza kutufanya tuamini ni hao wanaofanya hizo tafiti siyo kama sasa ambapo wanadhani watanzania bado wajinga kama 2005 au b4.
   
 9. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #9
  Oct 9, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Kura ya Kwanza ya DR Slaa ni ya Kwangu so hawa sijui REDET sijui Synovate wataseeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeema weeee, lkn mwaka huu Rais wetu ni Dr. SLAA period!!!!!!!
   
 10. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #10
  Oct 9, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Taasisi ya REDET wanafanya majaribio kuona kama nchi inaweza kuingia katika vurugu za kisiasa.

  Taratibu. Tunaelekea huko. Bila shaka tutafika huko.
   
 11. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #11
  Oct 9, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Nimesikia pia asubuhi hii Redioni, Kilichonishangaza hakuna tv iliyoonyesha, wala gazeti lililoandika, SHUJAAA WA MWAKA!
   
 12. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #12
  Oct 9, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  MIMI ITAKUWA YA PILI, mpaka sasa anakura mbili hata kama hatajipigia.
   
 13. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #13
  Oct 9, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Shyt did they say this??? Yaani kama proffessional org. inaongea hivyo mbona safari ni ndeefu!
   
 14. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #14
  Oct 9, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Nafikiri tulisoma darasa moja
   
 15. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #15
  Oct 9, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Nadhani hii tafiti inayomptisha Dr. Slaa ndiyo ya kweli!!! tuamini hii mpaka baada ya uchaguzi!!!

  Mod itabidi uwe na kazi ya ziada kufuta threads zenye mauza uza baada ya uchaguzi natabiri waTanzania wata-tuprove wrong.

  Made in Tanzania:

  ---> Tanzania anayesikilizwa ni mwenye umbea na uzandiki sio mwenye kufanya tafti na kuwa na takwimu!!!
   
 16. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #16
  Oct 9, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Kura ya tatu JF kwa slaa Dr. ni yangu. Nawashukuru wanaCCM a.k.a REDET kumpa %12 kwa Slaa manake hata hao REDET/ccm 12% wamempigia Slaa hawamkubali mwanachama wao. Then 12%ccm+100%chadema+ kura za wasio na vyama=Mr.PRESIDENT SLAA. Hivi siku ya kuapishwa dr. Slaa ni lini nianze kuandaa nauli kuelekea dar. Mpaka sasa nimeweka sh.7,800/= nina imani ntapata 100,000/= maana kwa mara ya kwanza Rais msomi mzalendo anatinga ikulu.
   
 17. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #17
  Oct 9, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145

  Nakubaliana nawe ni kwa mara ya kwanza Tanzania kuongozwa na msomi baada ya JKN.
   
 18. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #18
  Oct 9, 2010
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hakuna anayetegemea wale waliopata asilimia ndogo katika utafiti huo wakae kimya!Imani yao na utafiti uliofanywa vinakuwa ni vitu visivyowiana.
  Kwa wale walipewa aslimia kubwa hiyo ni ishara ya ushindi kwao.Kama tafiti haziaminiki hakuna haja ya kupiga kelele kwa sababu mwisho wa yote ni sanduku la kura.
   
 19. bullet

  bullet JF-Expert Member

  #19
  Oct 9, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Hivi ni tafiti ngapi zimefanyika? Mbona REDET ndio imepewa uzito? Au kwa sababu CCM imeonyesha kushinda? Mbona opinion polls za magazeti mbali mbali ambazo zinaonyesha sura tofauti na REDET hazipewi uzito? Kumbuka wanaotoa maoni yao magazetini na mitandaoni wanasukumwa na nia zao kupiga kura si kama hao wa REDET wanaowafuta wale tu wanowahitaji. Mfano katika kipindi cha Tuongee Habari, leo asubuhi katika Star TV, mtu mmoja amepiga simu na kusema kuwa mtu wa kawaida kijijini ni vigumu kuulizwa anampenda rais gani akasema kinyume cha kumpendelea wa kutoka CCM ili asionekane mpinzani maana wanahisi kila mtu anayehoji ni Usalama wa taifa.
   
 20. u

  urasa JF-Expert Member

  #20
  Oct 9, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  lets prove them wrong kwa kuhamasishana kwenda kupiga kura hata kama kutakuwa na mvua siku nzima,maana huwezi jua kamati ya ushindi ya ccm imejiandaa vp kushirikiana na benchi la ufundi linaloongozwa na sheikh yahya hussein
   
Loading...