Dr. Slaa aongea na wanafunzi katika Kongamano la wanavyuo

Dr. Slaa aongea na wanafunzi katika Kongamano la wanavyuo

Kurunzi

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
10,175
Reaction score
11,573
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, leo anatarajiwa kufungua kongamano la wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyoko Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili, Mwenyekiti wa Muungano wa Wanafunzi wa CHADEMA Vyuo Vikuu (CHASO) mkoani Dar es Salaam, Freddy Chacha alisema kongamano hilo litafanyika katika Ukumbi wa Msimbazi Center. Alisema katika kongamano hilo, vijana wanatarajiwa kuwaapisha viongozi wa shirikisho hilo kwa

Mkoa wa Dar es Salaam, kueleza mipango mipya kuelekea mwaka 2015, kutambulisha matawi na viongozi wake kwa viongozi wa kitaifa. Pia kuandikisha wanachama wapya na kutoa tamko lao dhidi ya vijana waliofanya usaliti, na kuanza kuichafua Chaso kwa kueneza harakati mbaya za CCM dhidi ya CHADEMA.

Mwenyekiti huyo alisema pamoja na Dk. Slaa, viongozi wengine wa chama hicho wanaotarajiwa kuwepo ni Mbunge wa Ubungo, John Mnyika; Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema; Mwenyekiti wa BAVICHAf Taifa, John Heche; Mhadhiri wa Chuo Kikuu na Mkuu wa Kitivo cha Elimu katika Chuo Kikuu kishiriki cha Chang’ombe, Dk. Kitila Mkumbo.

Mwenyekiti huyo alivitaja vyuo vitakavyoshiriki kuwa ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Taasisi ya Utawala wa Fedha (IFM), Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Chuo Kikuu cha Kampala (KIU),Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Teknolojia yaMadawa (IMTU), Chuo cha Ustawi wa Jamii,Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohane na Chuo Kikuu cha Muhimbili.

Tanzania Daima.
Muda wa kuanza Kongamano hilo nitawaupdate baadaye stay tuned.
 
Chama hiki nazidi kukipenda....ni kwenda mbele tuu!!!!!
Pigeni hatua makamanda, magamba wamepanic!!
 
Ni habari njema sana,tunaomba watakaokuwepo watupe live updates..
 
Nimepita maeneo ya Mabibo hostel nimeona tangazo la CHASO wanadai mkutano huo utafanyika DONBOSCO Morocco, ukweli ni upi?
 
Nipo Dar kikazi, nitajitahidi niwasili japo kusiki na kuona mwenyewe bila kusubiri kuambiwa. Big up CHADEMA.
 
Tupe muda kamanda na kama litarushwa hewani tujuze ni channel gani'CHADEMA MWENDO MDUNDO'
 
Chadema wameelekea kufiliska kisiasa kwa dhuluma za ccm hence kuwaunge mkono sana japo kwa maneno!
 
Nimepita maeneo ya Mabibo hostel nimeona tangazo la CHASO wanadai mkutano huo utafanyika DONBOSCO Morocco, ukweli ni upi?

Simple. Take the last update. Ni kama jeshini, take the last order.
 
Kila la heri makamanda, uzuri wa cdm wamewekeza kwa vijana na wasomi! Huu ni mwanzo mzuri kwa chama kinachojianda kushika dola.
 
Safi sana

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Nipo ndani ya ukumbi-msimbazi center ambapo Dr.Slaa ndo mgeni rasmi.... Fuatana nami!
 
Back
Top Bottom