Dr slaa anaweza kuangushwa na ''wasomi'' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr slaa anaweza kuangushwa na ''wasomi''

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ntambaswala, Jul 24, 2010.

 1. N

  Ntambaswala JF-Expert Member

  #1
  Jul 24, 2010
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kikwazo kikubwa cha kuleta mabadiliko ya kweli nchi hii ni wasomi na wakaazi wa maeneo ya mjini. Nimesoma kwenye threads nyingi hapa, watu wengi wenye mashaka kuwa DR Slaa hatapita ni watu ambao wanatamani mabadiliko yatokee ila hawatambui kuwa wao ni sehemu ya kufanya hayo mabadiliko yatokee.

  Jana tulikuwa na wenzangu hapa Mzumbe University (Dar Campus) tunajadili kuhusu uchaguzi. Wengi wakawa wanasema watafurahi sana siku CCM ikiondoka madarakani. Lakini papo hapo wakawa wanasema Dr Slaa hataweza kuishinda maana CCM ni ''wezi'' wa kura hivyo haina haja ya kwenda kupiga kura maana upige kura usipige watashinda tu.

  Nilisikitika sana maana tuliokuwa tunajadili wengi walikuwa ni wanafunzi wa shahada za uzamili. Nikajiuliza hivi wasomi wa nchi hii wana matatizo gani, maana hii si mara ya kwanza kusikia maneno kama haya kutoka kwa wasomi wa nchi hii. Nilishaona mwaka 2000, 2005 na sasa 2010.

  Lakini cha ajabu mwezi wa tatu mwaka huu nilitembelea wilaya ya Newala kijiji kimoja kinaitwa Nkunya, nilikutana na wananchi wengi ambao kielimu naweza kusema sio wasomi- yaani ni darasa la saba kushuka chini, wao walikuwa wanasema kulingana na tabu wanazozipata akijitokeza mgombea yoyote wa upinzani ambaye ''anaeleweka'' wao watampigia kura na atashinda bila shida maana wamechoka na CCM. Maelezo kama haya nimeshayasikia mara nyingi sana huko vijijini kutoka kwa watu wasio wasomi.

  Sasa najiuliza kwanini wasiosoma wanaona upinzani unaweza kushinda lakini waliosoma wanaona tofauti?. Zamani kidogo kuna mwalimu mmoja mstaafu aliniambia tabia ya watanzania wasomi kuwa wapole, kuburuzwa, uoga wa kuthubutu na kutokuwa tayari kujitoa mhanga ni mpango kamili ulioratibitiwa katika aina ya elimu tunayopatiwa- yeye alisema Nyerere alitengeneza mfumo wa elimu ambao unatufanya tuwe hivyo. Sikukubaliana na mawazo yake kwa vile huyo mwalimu alikuwa hampendi kabisa Nyerere.

  Lakini sasa naanza kuamini watanzania ambao hawajasoma (wengi walioko vijijini) hawajalishwa sumu (indoctrinated) na elimu ya ''Nyerere'' ndo maana wanaona mageuzi yanawezekana lakini wasomi wanaona tofauti.

  Anyway, unahitajika utafiti kubaini kwanini wasomi wako pessmistic upinzani kushinda tofauti na watu wasio soma?
   
 2. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #2
  Jul 24, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,682
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  wasomi wenyewe wako wangapi? Dr. anaweza kukataa kura za wasomi na bado akashinda uchaguzi!! kampeni zielekezwe maeneo ya vijijini ambako kuna wapiga kura wengi. CCM huwa wanashnda kwa kura za vijijini haswa kwa wakulima, wafugaji na wavuvi. Hebu jiulize tana kwanini Kikwete kasema hataki kura za wafanyakazi???
   
 3. Kaduguda

  Kaduguda JF-Expert Member

  #3
  Jul 24, 2010
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 667
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 80
  Mkuu uyasemayo yapo tena kwa wasomi wengi wa kibongo. Hali ya kuthubutu ni adimu sana miongoni mwao. Wengi wao, hata nafasi walizo nazo, shule, mali a vitu walivyo navyo vimepatikana kiujanja ujanja tu. Hivyo kwanza wanaangalia kula zao, then yatokanayo kama wakithubutu.
   
 4. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #4
  Jul 24, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  umenikumbusha mbali kaka ...............yaani 2000 nilikuwa form 6 while mimi nilienda kuandiksha nikiwa nimebeba cheti cha kuzaliwa (ushahidi wa kuwa nimetimiza umri since nilikuwa na umbo dogo), darasa zima nilikuwa peke yangu nilienda kupiga kura na nilichekwa vbaya sana...........ati ccm lazima itashinda japo kwa wizi kwa hiyo haina haja kupga kura
   
 5. w

  wa 16 Member

  #5
  Jul 24, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni kweli mkuu. umenena vema hakuna watu wanafiki kama wasomi wanchi hii, hata humu jf ilipotangazwa kuwa dr slaa ndo mgombea,
  kuna watu walikuwa wanampongeza then papo hapo wanasema haweze kushinda--

  watu wa vijijini wako siriazi sana na ndio maana wabunge wengi wa upinzani wanatokea huko vijijini na sio mjini kama dar ambako wanafiki wamejaa.

  kuna baadh ya watu huwa wanasubiri kufanyiwa mabadiliko na si kuwa sehemu ya mabadiliko.
   
 6. w

  wa 16 Member

  #6
  Jul 24, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  vipi ndugu ile kazi aliyokutuma bado hujaimaliza?
   
 7. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #7
  Jul 24, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  dhana ya kupga kura haijainga vizuri hasa maeneo ya mjni..............utakaaje mwanafunz wa sekondar umeshatimia umri usiende kupiga kura?
   
 8. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #8
  Jul 24, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Ntambaswala, asante kwa hii sredi yako. Umenena kilicho kweli kabisa. Wasomi - na mimi naongezea - na watu wengi wa mjini mwamko wao wa kuleta mabadiliko ni mdogo sana. Wengi wanasema wa kijijini ndo wenye shida. Si kweli. Kinyume chake ni sahihi. Watu wa mjini na wasomi ndiyo wanaoturudisha nyuma katika kuleta mabadiliko. Wanahitaji kubadilika kama kweli wanataka kuwe na mabadiliko.
   
 9. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #9
  Jul 24, 2010
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35

  1. Kwanza wewe ndugu, hivi uliweza wauliza hao wenzako wa Mzumbe kuwa ni kwanini wanataka kuitoa CCM madarakani? Usije ukawa umeenda pale ukaanza kuongelea upinzani nao wakakuunga mkono ukadhani kuwa kwa kukuunga mkono wanataka chama pinzani kiingie madarani! Ukiwa mpinzani wa kitu siyo lazima ukikatae chote, unaweza ukawa unapinga baadhi ya vitu. Kumweka mpinzani madarakani si kwamba atatekeleza yale unayotaka. No necessarily. This is true in Zambia, Kenya, Ghana na nchi chache zilizowahi fanya mabadiliko ya kweli Africa. Kwa kifupi, nikipinga CCM simaanishi kwamba wapinzani nawaunga mkono. I can make change within CCM. Na hii dhana ndiyo inawavuruga Watanzania wengi hata hawaelewi maana ya mabadiliko na lini kuyaanzisha.

  2. Hao watu wako uliwauliza kama wamejiandisha? Au hata kama wamejiandikisha wana hizo card za kupigia kura? Je walikwambia mikakati yao na Mpinzani wao mtarjiwa ya kuwawezesha kutoka hapo walipo kwenda juu? Uliuza kama watoto wao wamewapeleka shule au kuwinda? Pia uliwakumbusha kuhusu Elimu Dunia ilivyo tofauti na elimu ahera?
  Mimi nilienda kijiji kingine kiko Kilwa Kinaitwa Nyuni, kule katika majadiliano walisema wanataka mpinzani,, hasa CUF,,, kwa kuwa itawezesha wao kujiunga na OIC na pia kuwezesha sharia nchini!.

  3. Wasomi ni analytical. Kwanza unatakiwa mwenyewe ujiulize kama ume-fanya change kwako mwenyewe kabla ya kutafuta change nje. Afterall, change ni lazima? Kama ni lazima sawa. Lakini kam siyo lazima why go for it now and not later.

  4.Kama ukitaka mabadiliko, yafanye wewe mwenyewe. Usiangalie wasomi au wana kijiji Nkunya. Afterall kura unapiga peke yako hakuna mtu unakuwa naye.
   
 10. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #10
  Jul 24, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Yaani umesema kweli tupu i second you, hilo tatizo lipo hata humu JF tunao wengi na ndio wanaotumika kukatisha tamaa wengine ambao wako tayari kuona mabadiliko yakitokea.
   
 11. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #11
  Jul 24, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,240
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  wasomi wetu wengi wao wamesomea chieti na si kuelimika ndo maana wako hivyo!!
   
 12. P

  Paul S.S Verified User

  #12
  Jul 24, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  mkuu unachosema kinaweza kuwa na mantiki sana lakini umejaribu kukaa ukatafakari ni kwa nini wasomi wanakuwa hivyo?.kwa hali ya kawaida tunategemea wasomi watakuwa ni watu wenye upeo mkubwa wa kufikiri, kuamua, nk,

  Au pengine wametathmini kwa kina na kuona pengine wapinzani hawana jipya, wamekosa mbadala, hivyo wanaona bora jini akujuaye...........

  unajua wakati mwingine wapinzani wanaongea sana mambo ya maana hasa katika kutoa kasoro, lakini linapokuja swala labda chaguzi zao kwakweli wanatia mashaka,wengine wamegeuza vyama mali zao ubabe ubabe tu. wakati mwingine havina sana sura ya kitaifa,

  hivyo kuna mambo mengi pia yakutafakari kabla ya kuamua, swala lakuwa CCM sio dhambi wala makosa, mimi naamini wasomi sio kama wanawaangusha kuleta mabadiliko, inawezekana ukatumia ukabwelwa kuwapata watu wa kijijini pengine kutokana na kutokujua kwao, na ukashindwa kuwashawishi wasomi kirahisi rahisi. hoja sio kuchagua upinzani tu je wapinzani nao wamefanya nini kuwashawishi wasomi.

  kuna mambo mengi yametokea wale tuliodhani wapinzani kumbe hamna kitu wamearudi CCM huwezi kuamini kama ndio yeye alikuwa upinzani.lazima tujue kuwa wapinzani ni binadamu kama wengine, tena wengine walikuwa hukohuko CCM TENA vigogo

  utitiri wa vyama nao nitatizo lingine tupinzani unagawana sana kura dhidi ya CCM, wenzetu walioendelea vyama labda viwili tu, kikiboronga hiki unakipa hiki, sasa hapa tabu tupu utasikiliza kampeni wagombea kumi na kunahitajika kufanyika kitu cha ziada kwa upinzani ili kuingoa CCM, umoja wa vyama ni jambo muhimu .

  Kenya waliweza lakini kwa mfumo huu wetu ndio maana watu wanasema Dr Slaa hatashinda, pamoja na wizi wa kura unaosemwa bado pia upinzani haujafanya juhudi za makusudu kuitoa CCM, kukaa kwenye majukwaa na kukosoa peke yake haitoshi,kwa nchi kama zetu minadhani tuige mfano wa kenya
   
 13. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #13
  Jul 24, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Tanzania wasomi ni wachache wengi ni watu waliomaliza vidato kwaajili ya vyeti ndio maana hata ajira zetu ni za vyeti. Kwa hiyo unapozungumzia wasomi naomba uwe makini. tungekuwa na wasomi tusingekuwa mikataba ya akina chifu bushiri na mangungo mpaka karne hii ya sayansi nateknolojia.bungeni wamejaa na vyeti vya kufoji benki kuu usiseme.

  Spika anasema vyeti havihusiki na ubunge.ubunge unataka mtu anaejua kusoma na kuandika tu.. kufoji ni kosa la jinai.kwahiyo ccm wanataka kutuambia trafiki wakisimamisha gari kwa ajili ya ukaguzi wakikuta gunia la bangi waliache kwa sababu halihusiki na ukaguzi wa gari?

  Kifupi tz hakuna wasomi.kama kuna anayejua msomi hata mmoja anitajie.
   
 14. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #14
  Jul 24, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe. Ndani ya CCM fanya kama marehemu Sokoine na Kolimba halafu utaona matokeo yake, sijui utayaona?
   
 15. Mgeninani

  Mgeninani Senior Member

  #15
  Jul 24, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vitu vinavvyowakwaza wapinzani ni mfumo mzima na tabia ya CCM kugeuza hii ni nchi yao peke yao, tume huru ya uchaguzi na mgombea binafsi ni risasi zinazoweza kuing'oa CCM na wanalijua hilo ndo maana wanafanya Delaying tactics.

  Dkt Slaa ashinde au asishinde inatosha kutuma ujumbe kwa JK kwamba atumikie wananchi wake kwa dhati sio kuendeleza umangimeza wa CCM.
   
 16. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #16
  Jul 24, 2010
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wasomi wa Tanzania ni tatizo kubwa...tena kadiri mtu anavyosoma kwenda juu elimu haimsaidii...ha ha ha...hatari sana.Yaani PHD za Tanzania,wale wanaitwa madaktari ndo ovyo kabisa.Nafikiri kadili watu wanavyoendelea na makamuzi ya shule ndo wanakosa ile independent thinking...fikra zao zote zinaelekea kwenye vitabu tu...plus wanajiona ni class nyingine tofauti...pumbaf!
   
 17. m

  mpangwa1 JF-Expert Member

  #17
  Jul 24, 2010
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 279
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  wasomi wengi wa tanzania ni waoga wa mabadiliko wamekarili tu mfumo unawangozi ndiyo sahihi, utasikia utafuti wa REDET utakavyompamba kikwete,
   
 18. Mujuni2

  Mujuni2 Senior Member

  #18
  Jul 24, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 142
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kabla ya kuandika hayo yote, inabidi tukubaliane a universal definition ya "msomi" maana usije ukawa unahesabu msafara wa mamba, ujue na kenge wamo! unaposema wasomi una maana gani? baada ya uhuru tafsiri ya msomi, ilianzia darasa la 12, kwa sasa mambo ni tofauti.Tuweke sawa kabla hatujachangia.
   
 19. N

  NguchiroTheElde Member

  #19
  Jul 24, 2010
  Joined: Jun 13, 2010
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo siyo IDADI ya wasomi bali ni ule mtezamo wao HASI (negative outlook) ulioanzishwa kufundishwa Chuo Kikuu cha DSM miaka ya 60 na 70, hasa baada ya kumwondoa Dr Chagula na kuwaweka Mabwana Msekwa na Kaduma in charge. Uongozi wa Chuo Kikuu cha DSM wakati huo ulitafuta maprofesa wenye mtezamo HASI kutoka kokote duniani, wengi wakiwa ni wanachama wa vyama vya kikomunisti nchini kwao au wafuasi wa Trotsky kutoka nchi za magharibi. Hawa wakaja ku-HASI fikra na hivyo akili za wasomi nchini na mfumo huo ukahakikisha kuwa huo mtezamo hasi unakuwa endelevu (sustainable) kwa kuchagua maprofesa wa kesho kwa kigezo cha jinsi walivyoelewa na kuukumbatia mtezamo hasi.

  Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu tumekuwa na viongozi ambao wamelelewa kikamilifu chini ya mtezamo na elimu ya mfumo hasi, na kwa kuwa mfumo huu ndiyo bado unafundishwa, siyo UDSM tu bali katika vyuo vingi, ikiwa ni pamoja na vyuo vikuu na vyuo vya ualimu, akili za wasomi wengi hazitaweza kuchangia maendeleo CHANYA (positive development) ya nchi yetu bali zitakuwa zinapinga bidii za kuirudisha nchi kwenye mtezamo chanya. Tofauti na hilo zitakuwa zinashangaashangaa tu.
   
 20. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #20
  Jul 24, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hivi Unawezaje kujiita Msomi kama Hujui umuhimu wa KURA yako katika kuleta Mabadiliko? Hivi Jitu Zima linasema kwamba halitapiga kura just Because CCM wataiba halafu kwa Argument hiyo Linajiita SOMI! Huu Ni Ujinga ambao bado unawasumbuwa Ma Elite wengi
   
Loading...