Elections 2010 Dr. Slaa alazwa kwa matibabu

Ashangedere

Senior Member
Aug 9, 2010
119
31




Dr Slaa akiwa wodini

Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Dk. Willibrod Slaa, amelazwa katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili. Blogu hii ilizungumza na Dk Slaa hospitalini hapo, akasema alilazwa jana Jumatatu kwa ajili ya matibabu ya mkono wake uliovunjika mfupa wa juu ya kiwiko wiki moja iliyopita. Kwa maelezo yake, alishauriwa na daktari aliyemfunga 'mhogo' (POP) katika hospitali ya Bugando, Mwanza, kwamba alipaswa kurejea hospitali kwa uchunguzi mwanzoni mwa wiki hii. Alikwenda Muhimbili mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea urais kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, jana Jumanne.

Habari za kulazwa kwa Dk. Slaa zilipowafikia mashushushu wa CCM na marafiki wa mafisadi, zilipokelewa kwa hisia za kishabiki, hata baadhi yao wakadiriki kueneza uvumi kwamba Dk. Slaa yu mahututi. Mwenyewe alipozungumza na blogu hii kwa simu alisema: "Siko mahututi. Ni jambo la kawaida, nililazimika kurudi hospitali kwa ajili ya kufanyiwa matibabu ya ziada, ikiwa ni pamoja na kufungua POP."

Akiwa Muhimbili, Dk Slaa anaweza ama kufungwa POP jingine au kufanyiwa pia upasuaji mdogo ili kuwezesha mkono kupona haraka. Alisisitiza kwamba kulazwa kwake hakuathiri mchakato wa maandalizi ya kampeni zake; na kwamba alikuwa akifanya kazi kwenye kompyuta yake kama anavyoonekana kwenye picha hii, iliyopigwa na Joseph Senga leo Jumanne jioni katika wodi binafsi, F, hospitalini Muhimbili.


Hisani ya : mtwarakumekuchablogspot.com

 
Dr W Slaa:

Tunakuombea kwa Mungu upona haraka ili urudi ulingoni kurudisha matumaini ya wa-Tanzania yalipotea:
 
Mungu akuponye haraka uendelee na mapambano ya kuingia magogoni rasmi november 2010.
 
Tuendelee kumwombea RAIS WETU mtarajiwa. Anajaribu kulitumikia taifa katika wakati mgumu sana.

Nawaombeni sana wana JF wenye mapenzi mema wakati wa Mfungo tuliweke na hilo kwenye futari zetu. Kwa wale wasiojua tunawaomea nao wamtambue kuwa atakuwa mtetezi wao na wa watoto wao hapo baadae.

Mungu Mbariki Dr. Slaa
Mungu ibariki Tanzania,
Mungu Ibariki Africa.
 
Wengine watasema "Bwagamoyo si mchezo, kiScud ilikuwa kimuondoe mchungaji aliyeondolewa kundini, bahati yake kimemkuta bado anao upako"

But I would say probably it is the weight of the ensuing campaign on his mind.
 
Wengine watasema "Bwagamoyo si mchezo, kiScud ilikuwa kimuondoe mchungaji aliyeondolewa kundini, bahati yake kimemkuta bado anao upako"

But I would say probably it is the weight of the ensuing campaign on his mind.
Watu wenye akili za kupewa na mawazo mafupi yasiyozidi urefu wa pua zao utawajua tu.
 
Utakuta Dr alikuwa hapahapa JF. Pole sana dr. Kuvunjika kwa koleo ndiyo kwanza mwanzo wa uhunzi.

Tunakusubiri uje na ARI MPYA, NGUVU MPYA ya kikweli na uonyeshe ukweli wa maneno hayo UKOJE.

Pona haraka Sikonge tunakusubiri kama ulivyoahidi.
 
lakini hii picha ya Tanzania daima nimeipenda sana
chadema wamejiandaa kwa negative campaigns za ccm
 
I pray you get well soon and even if you happen to be the President of United Republic of Tanzania please continue getting medical services in Tanzania's hospitals and not abroad.
 
lakini hii picha ya Tanzania daima nimeipenda sana
chadema wamejiandaa kwa negative campaigns za ccm
una akili sana pamoja na ccm kutawala kwenye media lakini chadema wanazitumia hizo hizo media za ccm bila wao kujua, mfano mtu mfupi kwenye kundi la watu atafanya vituko vya ajabu ajabu ili ku draw attention ya watu kuwa na yeye yupo.
 
Back
Top Bottom