Dr Slaa akataa mjadala na Nape ITV badala na Kinana

Status
Not open for further replies.
Dr Slaa ni msomi,mtu makini na uwezo wake wa kuchambua mambo unajulikana na kila mtu,Naona kama mleta Post umetawaliwa na Mahaba juu ya Chama chako Cha CCM,Nape hana hadhi ya kuongea na Dr Slaa katika mijadala muhimu na aliondoka kwasababu aliona kama vile amevunjiwa heshima.Nape?Nape huyu huyu mlopokaji?Come on Guys be serious!Aonge na Dr Slaa?Dr Slaa alimtaka Katibu mwenziwe Bw Kinana na siyo kichwa kitupu Nape.No wonder he was gone disappointed.
 
Kweli CCM ni kituko, Dr Slaa azungumze na Nape? ITV waahirishe huo mjadala na Kinana akimaliza hivyo vikao vyake ngoma inogile.
 
Well done Dr Slaa, ni dharau kupewa nape. Huo udhuru wa Kinana umekuja dakika za mwisho ni uhuni tu, walijua hawezi kuongea na hana cha kuongea
 
Nape afanye mdahalo na DR. Slaa? hata hao ITV naona hawako serious!!
 
Kweli ccm wepesi wa kusahau..mumesahau jk alimkimbia dr. Slaa kwenye mdahalo wa urais?...munasahau nkuwa hata kinana kamkimbia dr.. Kisa eti yupo dodoma na anamtumia "mbwa wake" nape aje kuongea na dr..?

Acheni ushabiki wa kitoto..siungi mkono hoja dr slaa aongee na mbwa wakati wenye mbwa wanamkimbia na kumuogopa kiasi hicho...mpiga debe wa ccm hana hadhi ya kuongea na kiongozi wa ngazi ya juu ya cdm...nape level yake ni kina heche na wala sio hata zitto wala j.j. Mnyika.
 
Mwaliko wa kutoka ITV umeweka bayana kuwa ni wa viongozi waandamizi wa vyama vya siasa, lakini kama si sahihi kwa katibu mkuu kuwakilishwa na katibu wa halamashauri Kuu, ni nani alipaswa kulingana na protocol na kanuni za vyeo ndani ya Chama..?

Bahati mbaya vijana wengi wa CDM hawako makini wala hawaelewi nini maana ya chain of command, hawaelewi nani anawakilishwa na nani..? hawajui nafasi ya katibu mkuu wala maagizo yake..! Ni aibu kuwa na vijana wafuasi ambao hawajui hata nini wanakifuata..,hawajui muundo wala mtindo wa Chama chao.
 
Hata kama ingekuwa mimi nisingekubali kamchezo kakipumbavu kama hako. Nape? ... Makubaliano yalikuwa ni kuwakutanisha makatibu wakuu. Sasa kama ni shughuli nyingi kwani CHADEMA hawana shughuli nyingi? Mnataka Umma uelewe nini kutokana na hili tukio?...
Kinana pamoja na mapungufu yake ni mtu ambaye Dr Slaa angweza kukaa nae meza moja na kuongelea mambo yenye maslahi mapana kwa nchi yetu. Si huyu mwimba Taarabu asieleweka kwa kauli zake zenye kumponyoka kama ushuzi wa ngomani. Oh CDM ni ya Wachagga, Oh CDM ni ya Kidini? Oh Rais hatoki Kaskazini, Oh nilinukuliwa vibaya kwenye zoezi la kuvua Gamba!... Popo si ndege ...unamambo!!!

Wekeni tarehe na siku ambayo kinana atakuwepo ili tuone na kusikia sera za vyama hivi viwili ...otherwise mimi naichukulia kama ni strategy ya kumkimbia Dr Slaa na badala yake mkampeleka mwimbaji wa bendi ya Kibaokata...
 
nilishashauri kitambo umri kama wa slaa,lowasa siyo wakati wao tena katika siasa ambazo kwa kiasi kikubwa zinatawliwa na mawazo mapya ya vijana lakini kwa umri wa slaa hawezi tena kushindana na vijana.
 
Ni kweli kabisa. Kama 2010 chadema walipowakataza wagombea wao kushiriki midahalo ya TBC. Kubwa kuliko zote ni pale mgombea urais wa chadema alipogoma kushiriki mdahalo pale Kempinsky na badala yake akajitungia maswali akawapa waandishi makanjanja wamuulize pale Karimjee.

...umeua mbayaaa,sijui kama ataelewa unachomaanisha,maana nasikia ni mgonjwa huyu jamaaa....
 
Nadhani aliyesepa si Dr Slaa bali ni Kinana hivi wapendwa mnaweza kumuandalia mdahalo Dr J.K na Mnyika? Hatuna mashaki na uwezo wa Mnyika vile vile hatuna mashaka na hoja zenu kwamba Nnauye anaweza lakini kukaa pamoja na Dr Slaa it was insubordination by design planned by organizers or CCM. Bahati mbaya sijui ni Slaa au CDM wamegundua mtego huo. Twendeni tukajipange upya turudi vingine "Janja yake Paka Panya kesha gundua hakuna mlo leo.
 
Dr Slaa ameshindwa kujadili hoja za kitaifa kisa anamuogopa Nape?

Sasa hii hali inaashiria nini kwa wana siasa tulionao?

Tuchukue mfano mdogo tu, mfano dr Slaa angeshinda katika uchaguzi mkuu wa 2010, je, asingeweza kususia baadhi ya watu au mambo ya msingi yanayo athiri taifa?

Hii hali ya kususa hawa CHADEMA itawaisha lini? Juzi tu mchungaji Msigwa amesusa kufanya majadiliano na kipindi cha jambo Tanzania kinachorushwa na TBC 1.

Sasa jamani dr Slaa na wewe unaisusia ITV? au nayo ni CCM?
 
nape;
acha kuzunguka mbuyu, kwani hata hili unalijua wazi kwamba hoja ni moja tu hapo, kwamba dr. Slaa siyo level yako. Dr. Slaa hawezi kuwa kwenye mjadala na wewe ili ujiongezee cv kwamba kuna siku uliwahi kuwa kwenye mjadala na dr. Slaa. Dr. Slaa alihudhuria kwasababu alijua wanakutana na katibu mkuu wa ccm na siyo wewe nape. Kinana baada ya kuona kwamba ana kashfa nyingi sana zinazokinzana na interest za nchi, akaamua kutafuta sababu.
Na wewe naüe, kwasababu huna kazi na huna hoja as a product ya thesis yako ya mzumbe ya masters, ukaona hii ni nafasi pekee ya kujiongezea umaarufu kwa kuropoka kwa kutafuta public sympathy kwamba dr. Slaa amekosa political tolerance!
Ni politoical tolerance ipi unaouongelea kwa dr. Slaa na hata viongozi wengine wa chadema ambao kila siku, wewe nape, ukiwa pamoja na kikundi chako maaarufu kama chama cha matusi dhidi ya chadema ukiwa na members wengine kama mtela, shonza, mwigulu , na wengineo, mmekuwa mkiwatukana na kuongea maneno machafu dhidi ya dr. Slaa na mara zote hujawahi kumsikia akikujibu kwa upuuzi wenu? Hii ni kwasababu anajua wewe una upeo mdogo sana katika mambo mbalimbali.

Nape,
kwa ufupi ni kwamba wewe hauko kwenye level sawa na dr.slaa ktk political arena.

kakaaaaaaa...kama unayo hiyoo niliyoi-bold in red tafadhali ibwage hapa tuzidi kujuwa ujinga uliomo deep inside that stupid boy....tafadhaliiiii.
 
Katoka baro? Duh babu anamhanya mjukuu wake ile mbaya, alijua kinana yupo ili kuendeleza siasa zake chafu dhidi ya Kinana.
 
Mwaliko wa kutoka ITV umeweka bayana kuwa ni wa viongozi waandamizi wa vyama vya siasa, lakini kama si sahihi kwa katibu mkuu kuwakilishwa na katibu wa halamashauri Kuu, ni nani alipaswa kulingana na protocol na kanuni za vyeo ndani ya Chama..?

Bahati mbaya vijana wengi wa CDM hawako makini wala hawaelewi nini maana ya chain of command, hawaelewi nani anawakilishwa na nani..? hawajui nafasi ya katibu mkuu wala maagizo yake..! Ni aibu kuwa na vijana wafuasi ambao hawajui hata nini wanakifuata..,hawajui muundo wala mtindo wa Chama chao.
Kama sikosei Nchemba ndo Naibu katibu Mkuu...Tayari alishakutanishwa na Zitto kama Naibu katibu mkuu wa CDM... Nape anatakiwa akutanishwe na Mnyika...Nadhani unakumbuka vizuri mdahalo wa Ndugai na Lisu ulivyokuwa wa upande mmoja....
 
Jamani aliekimbia mjadala hapa sio Dr.Slaa ni Kinana Nape sio saizi ya kuzungumza au kushiriki katika mdahalo na Nape hata na Myika.Kwa Dr slaa kushiriki katika mdahalo na Nape ni matusi n adharau kubwa kwanini ITV hawakumtaarifu kua Kinana kakimbia.
 
Nape sio size ya Slaa. Mleta thread kwa nini hujaona kuwa aliekimbia mjadala ni Kinana aliona ni bora hata asitokee kabisa!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom