nape sio size ya slaa. Mleta thread kwa nini hujaona kuwa aliekimbia mjadala ni kinana aliona ni bora hata asitokee kabisa!
Suala sio cheo cha mtu unayekutana nae.Hata ningekuwa mie Slaa ningetoka nduki
Nipangwe na Nape? Niongelee uchambuzi wa nini?
Mtu ambaye hawezi jutofautisha 'cheti cha sekendare' na 'cheti cha ualimu'?
Hili ni tusi kwa Slaa kumpanga mjadala na Nape wajadiliane.
kwa hiyo saiz hamjuti?Ndoi aliteuliwa kuwania urais huyo... hopeless kabisa. Watanzania tusipokuwa makin na wanaotaka kutuongoza tutajuta...
Ongea kama mtu mzima wewe! Hivi kwanini Dr. Slaa amwogope Nape halafu awe tayari kuongea na Kinana? Nape siyo size ya Dr. Slaa. Kumuweka Nape na Slaa ni kama kumshushia hadhi Dr. Slaa. Nape size yake ni Mnyika na si Dr. Slaa. Hata kwa Zitto tu Nape hana sifa za kukaa naye kwenye meza ya mjadala kwenye vyombo vya habari. Hata ningekuwa mimi ndiyo Dr. Slaa nisingekubali upuuzi kama huo. Hivi ukae kuongea na Nape utagain nini zaidi ya taarabu tu?Hahaahaha,
Dr ametoka nduki.
Chadema hawana ubavu wa kusimama na CCM.
Nape peke yake mnamuogopa je ingekuwa safu nzima ya CCM ingekuwaje?
slaa si saiz yake nape. Ningeitwa mimi k/mwenezi wa kata nipambane na nape
nilishashauri kitambo umri kama wa slaa,lowasa siyo wakati wao tena katika siasa ambazo kwa kiasi kikubwa zinatawliwa na mawazo mapya ya vijana lakini kwa umri wa slaa hawezi tena kushindana na vijana.
mnyika hana elimu ya kumwezesha kujadili mambo na nape. Form sx leaver huwezi kumkutanisha na mtu mwenye elimu ya degree
Dr Slaa ameshindwa kujadili hoja za kitaifa kisa anamuogopa Nape?
Sasa hii hali inaashiria nini kwa wana siasa tulionao?
Tuchukue mfano mdogo tu, mfano dr Slaa angeshinda katika uchaguzi mkuu wa 2010, je, asingeweza kususia baadhi ya watu au mambo ya msingi yanayo athiri taifa?
Hii hali ya kususa hawa CHADEMA itawaisha lini? Juzi tu mchungaji Msigwa amesusa kufanya majadiliano na kipindi cha jambo Tanzania kinachorushwa na TBC 1.
Sasa jamani dr Slaa na wewe unaisusia ITV? au nayo ni CCM?
Suala sio cheo cha mtu unayekutana nae.
Kama ingekuwa kufananisha vyeo basi Slaa hatakiwi hata awe anaingia hapa JF kwa sababu huwa anajibishana na wananchi wa kawaida tu hapa jukwaani.
Kama Dr Slaa ana nia ya kuelimisha umma na kunadi sera za chama chake aitakiwa atumie nafasi hii kuimaliza kabisa CCM kwani kama aonavyo yeye CCM wamewakilishwa na mtu ambaye sio saizi yake.
Kitendo cha Dr kukimbia sio cha kizalendo na kakiabisha chama chake hali ambayo imetufanya wengi tuzidi kuwaona chadema kuwa ni makanjanja tu kwenye ulingo wa siasa.
Kamanda haukimbii vita, kamanda unapambana kwenye vita kiume uwe mfano kwa makambanda wako kuwa wewe sio mwoga vitani na unaongoza mapambano kutoka mstari wa mbele.
Dr Slaa ni mwoga sana na ametuangusha wengi tunaomwona kiongozi
Nape VS Dr. Slaa mbona kama yanga na Bayern Munich sasa si kupotezeana muda tuu