Dr. Slaa Akamatwe, ahojiwe na ikiwezekana achukuliwe hatua

Mzee mbona ile picha ya handsome boy umeiondoa? Ingekuwepo ile picha na mawazo yako uliyoyatoa ungewakaba sana watu hapa we ujui tu. Hata hivyo siyo mbaya sana tumeanza kuona matunda ya masters yako, Dr Slaa si ni mwajiriwa wa mambo ya ndani lazima akamatwe.

Ha ha ha sheria haiwezi kutumika kulinda group fulani na kukandamiza wengine. Sijaona matunda ya masters unayoisifia sijui ndio ya Gembe ulie mquote hapo juu, sasa kama with masterrs somebody still sees things like a fish which has one experience of being in water then the masters has no use. I bet with masters he could be able to see things like an amphibious creature that has due experience both being in water and dry land.
 
Kama nakumbuka vizuri na hii hesabu ni sahihi:
EPA bilion 133
Matumizi mabaya ya madaraka b 11
BoT b 221
Richmond b 154
na zingine ...
Jumla ni kama billion 700

Na hizi zote zimeliwa kwa njia ya siri.

Hii inanifanya nishindwe kuelewa kama huu umaskini tulionao ni wa kiukweli au ni siri.

Kama tunazo fedha au mali yenye thamani kama hii, umaskini unatokana na nini?

Hawa wakulu wanatumia pazia la siri kutuficha ukweli juu ya hali ya nchi.

Mtu kama una akili nzuri ukiletewa nyaraka kabla hujaanza kutamba nayo lazima utakuwa umeielewa na unajua content yake na madhara yake.

Si dhani mtu kama Dr Slaa (PhD) ni mtu wa kukurupuka kama Dr. K... (Honor).

Tzingatie Usiri na maslahi ya taifa.
 
HTML:
[QUOTE
Si dhani mtu kama Dr Slaa (PhD) ni mtu wa kukurupuka kama Dr. K... (Honor) [/QUOTE]


Nimeipenda sana hii, Hii Dr K!!! K can mean anything, Kingunge, Karamavi, Kuhani....Ku..
 


Jiulize kama Barua hiyo ingekuwa inahusu mambo ya kijeshi na nia ya serikali ingekuwaje? Kuna tatizo sehemu na hapa ndipo pahala pa kupata suluhisho lenyewe. Mie nimeanza kuogopa kwa kweli, kama watu wanaweza kupata Barua kutoka kwa Waziri kwenda kwa waziri Mkuu? kuna tatizo hapa


Mkuu Gembe.

Huwezi amini, wazalendo ndani ya ofisi za Umma wapo makini kutenganisha ni nyaraka ipi ni kwa maslahi ya taifa hasa na ni ipi ni ya maslahi binafsi lakini yenye kofia ya " Siri za Serikali"

Wazalendo hawa wanalijua hilo "... mambo ya kijeshi" hata Dr. Slaa yuko makini na hayo.

Unafikiri siku zote, nyaraka kama hizo si zimetulia mafahili hayo hayo zilipo za ufisadi? , nani keshazigusa???

Watumishi wamechoshwa na ufisadi unaokomba raslimali za nchi wakati vipato vya vi duni.
 
- Mkulu Gembe, heshima mbele sana, tatizo ni kwamba utafukua mengi sana kwa mfano hii barua ya Masha kwa waziri mkuu, ninajua kuwa imelikishwa kwa makusudi na hao hao tuliowakabidhi dhamana ya kulinda sheria zetu,

- Again huwezi kuwa na maelezo ya kutosha kuhusu ni wapi magazeti ya Mengi yanapata habari nyeti nyingi za uporaji mali wa Mkapa na zingine mbali mbali, sasa tumefikia mpaka mawaziri kurekodiwa kwenye vikao muhimu vya serikali, sasa uta-draw wapi the fine line ya kamata kamata na siri za serikali?

Serikali yetu ya sasa sio siri ina matatizo makubwa sana na utunzaji wa nyaraka za serikali, infact sio vibaya kuiita ni Banana Republic, maana mimi sijawahi kuona mambo ya ajabu kama ya hii serikali, I mean haina siri tena kuna wanazozivujisha wenyewe na ambazo hawana control nazo kabisa,

Sasa ukimkamata Dr. Slaaa then utaishia kuikamata serikali nzima, ndio maaan hawawezi hilo, na besides DR. Slaaa analisaidia taifa zima na hizi nyaraka, na hata sometimes serikali yenyewe, sasa unaona ni kwa nini hii ni Banana Republic?

...Nakubaliana nawe. Cha ajabu ni kwamba mwakani hii hii Banana Goverment itarudi kwenye utawala kwa ushindi wa kishindo courtesy ya sisi wapiga kura na hivyo sisi wenyewe kushiriki kujirudisha tena kwenye kuwa Banana Republic! A sad, sad case indeed!
 
Last edited:
HTML:
[QUOTE
Si dhani mtu kama Dr Slaa (PhD) ni mtu wa kukurupuka kama Dr. K... (Honor) [/QUOTE]


Nimeipenda sana hii, Hii Dr K!!! K can mean anything, Kingunge, Karamavi, Kuhani....Ku..

Huyu atakuwa labda Karamagi wengine wanapenda kumwita Kanywamaji au nimekosea.
Duh umeniacha hoi hahahaha:D
 
Hiyo yawezekana alipewa mtu apeleke sehemu na hiyo siri sana msisitizo wa hali ya juu.Asivujishe

Afisa akiandika memo na kusema "Mhe. zile zawadi ulizoagiza zimeshaingizwa kwenye mfuko wako. Kiasi kingine tumeshampatia Katibu x,y na yeye zimepitia UK" halafu akaweka "Siri Sana" je ni haki kuvujisha kitu kama hicho?

Sheria zipo lakini sheria za kidhalimu hazipaswi kutiiwa. Hatusemi "utawala wa sheria" kwa maana ya kukubali kila kitu kinachoitwa sheria; sheria ina nguvu pale sheria hiyo ni halali, inazingatia misingi ya haki, inaheshimu katiba na pia inahakikisha haki za raia na za binadamu. Sheria iliyoko kinyume cha hapo, ni sheria ambayo haipaswi kutiiwa.
 
Gembe,
Mie nilikuwa najiuliza na kulaumu kwa nini Dr. Slaa hakuitwa "Man of the year 2008" kwa sababu mambo aliyofanya hakuna Mtanzania anayeishi duniani amewahi kuwa na hizo guts. Governmen Classified information becomes equivalent to "toiletpapers" if they are full of filthy and lies; and they shud not be termed Gov Classified. Dr. Slaa has shown us how most of us with and without masters and PHDs like you Gembe can do; this is our own country it is Dr. Slaa's country and Gembes country, and we have equal rights to any information as long as we do not break laws.

I remind you again all those guys who were named below the shade of Mwembe Yanga threatened him but now they are the ones who are in. And for your information, as long as Mkapa is living he must test the wrath, and all those guys who thought they can betray the poor people through the so called "Government Classified information" be prepared, we are after you!
 
Hoja ni nzuri ila ni "unpopular" kama alivosema (SUSUVIRI) nafkili tuichambue kisheria zaidi kuliko emotions zitutawale! Kuna kesi iliwahi kutokea miaka ya nyuma ilimuhusu Mwandishi Adam Mwaibabile "Mwana" alihukumiwa jela mwaka mmoja kwa kukutwa na hizo wanazoita "siri za serikali" badae akakata rufaa kwa msaada wa waandishi wenzie akashinda. Labda mwenye kujua vigezo gani vilitumika kwa huyu bwana kushinda kesi basi atatuweka kwenye nafasi nzuri sana kwenye mjadala huu!
 
Dr Slaa akamatwe! akamatwe!
Apigwe mpaka macho atokwe
Asiachwe ikibidi shingo akatwe,
Hukumu hii tunataka iletwe.

Aah! Nashtuka na kukumbuka,
Jambo moja mtumbuka,
Ishu ilipobumburuka
Watu waliumbuka.

Ndiyo! Iliyowahusu mawaziri,
Katika soo alikuwapo Naazir
4 katakiwa kuutema uwaziri,
Hata yule richman kutoka Monduli.

Naazir akaumbuka kabakia na ubunge,
Haya ikamfika kama liyepigwa kwa mlonge,,
Baadaye yakaibuka huko huko ndani ya Bunge,
Nazir wa TICCS ajitetee kwa Bunge.

Katika kuthibitisha, TICCS ipo kihalali,
Kara kachaplisha, hadi mtaa wa Luthuli,
Doc kakamatishwa, ni ya baraza la mawaziri,
Bungeni akaiwasilisha, ikaonekana kafanya vizuri.

Swali ninalojiuliza, ipi ndiyo SIRI KUU,
Ya masha aliyoandika, kwenda kwa waziri mkuu?
Au ya BARAZA‘liyokubaliana akiwamo Waziri Mkuu?

Gembe! Tafakari hili; Nazir akiwa mbunge kuchukua SIRI ya Ikulu na Slaa akiwa mbunge kuletewa siri ya wizara lipi ni kosa la mtu kushitakiwa kuwa anamiliki nyaraka za serikali?
 
Mnyamahodzo

Mkuu nimependa sana hizo beti tatu za juu....uko makini ujumbe umeufikisha kwa Gembe kishairi, Bravo
 
HIZO SIO SIRI ZA SERIKALI BALI NI UWOZO WA SERIKALI, INABIDI TUMSHUKURU SANA fATHER sLAA KWA KWELI ALIYOYAFANYA SIO MADOGO, SASA MLOLONGO UTAKUA HUU WA KWANZA KUSTAKIWA ATAKUWA SLAA WAPILI MAFISADI KWA SABABU NDIO WENYE HIZO SIRI ZA SERIKALI, WA TATU SPIKA WA BUNGE KWA KUKUBALI SIRI ZA SERIKALI ISOMWE BUNGENI, WA NNE WABUNGE WOTE WALIOBUNGENI KWA SABABU WOTE WALIZIJADILI SIRI ZA SERIKALI NA MWISHO BWANA JK ANAPANDA KIZIMBANI KWA SABABU YEYE NDIO MKUU WA NCHI YENYE HIZO SIRI
HAYO YOTE YALISHAONEKANA NA NDIO MAANA dR SLAA APANDISHWI KOKOTE
 
There is no such thing as " nyaraka za siri" when it come to my tax money, it's my money
i am a taxpayer. NI HELA YETU NDIYO itatumika. it is my money too, they need to understand and respect that.
 
Kisheria kukutwa na nyaraka za siri za serikali ni kosa linalostahili adhabu, naunga mkono hoja ya dr kukamatwa lakini nahitaji kueleimishwa kuhusu SIRI

Najua hapa kuna wataalam wa kada zote na nitasaidiwa
 
Hivi wangemsubilisha nini Dr Slaa siku zote hizi kama wangejua ana kesi ya kujibu? Wanajua sana kwamba wakithubutu kumgusa itakula kwao!

Ila mzee wangu Slaa nakupongeza sana na Mungu akutie nguvu, Kazi unayo ifanya hakika ni ya utume. Naamini nabii hafi mpaka akamilishe jukumu lililo mleta, Mungu wetu atakulinda mpaka ukamilishe utume huu wa ukombozi wa Mtanzania toka mikononi mwa MAFISADI.
 
Gembe unaweza kuwa right kabisa. Lakini tunapata taAbu na wewe kitu kimoja, utawala wa sheria unaozungumzia ww ni wa upande mmoja. Sheria inapaswa kukata kuwili so AANZWE MASHA KUKAMATWA KWA KUVUNJA SHERIA KUINGILIA MCHAKATO WA ZABUNI NA KUTUMIA GHARAMA/KODI KWENDA KWENYE MAJADILIANO MACHAFU YASIYOFUATA SHERIA NA HAO WAZABUNI WATARAJIWA HUKO GENEVA.
 
Slaa hawezi kukamatwa kwa sababu inawezekana kabisa kuwa pandikizi au mamluki,na anatumika kuwakandamizia wengine kwa kupenyezewa huo uwoza wa serikali na kuambiwa go ahead hatoki mtu ,yaani inawezekana kabisa akawa anatumika na CCM . suali ni wanamtandao wepi wanaomtumia Slaa kuwamaliza wengine wanaoonekana wapo mstari wa mbele katika kukoromea.

Sasa nikija kwa Slaa nahisi anakosea kuzisubmit hizi Nyaraka zinazoitwa za siri na anazifanyia mapema au haraka,alichotakiwa kufanya iwe ni last momentum pale ambapo atakuwa ameshairaiz issue na kufikia stage ya kutakiwa alete uthibitisho, yaani kwa ufupi asiwaeleze watu kuwa nina nyaraka bali aeleze kuwa nina ushahidi wa kutosha kuwa mtu au watu fulani walifanya kitendo kinyume za taratibu ,yaani iwe ni ushahidi wa mwisho kabisa ukipatikana mhusika anaingia hatiani moja kwa moja.
 
Back
Top Bottom