Heshima Mbele,
Mhe. Dr. Slaa anahitajika kukamatwa na Vyombo vya sheria hasa baada ya kuwa na Nyaraka ambazo ni siri za Serikali alizozipata kutoka wizara ya Mambo ya Ndani.Tunatambua ni kosa kisheria kwa Mtanzania yeyote kuwa na nyaraka za siri za serikali.
Nchi hii inaongozwa kisheria,na tumekuwa tukipigania hili siku zote .Kwa mtazamamo wangu Naona kuna haja ya Dr. Slaa kuhojiwa hata kukamtwa kwa kumiliki nyaraka za serikali!
Binafsi, sioni hii kama 'nyara ya serikali kwani' kwa vile inasaidia kuondoa utata fulani katika issue ambayo ina walakini. Our concern siyo 'how he got it' bali 'why he has it' na kwa vile inasaidia kuleta 'solution' kwenye swala lenye walakini, kwangu mimi sioni kama Dr Slaa ana hatia yoyote kwa mantiki hii.