Watanzania kwa jinsiwalivyopigika na kusagika wanahitaji inspiration,wanahitaji matumaini toka kwa kiongozi. Na kazi ya matumaini ilipaswa kufanywa na Kikwete ambaye kwa mujibu wa katiba anatuunganisha sisi sote CCM,CHADEMA na wasio vyama.Sasa Rais wetu anasema kuwa hajuwi umaskini wa Tanzania umesababishwa na nini na kuwa hajuwi hata huu udini unaosemwa unatoka wapi. Kwa hali hiyo ya fikra za Rais anaweza kutu-inspire kweli? Rais amejitoa katika nafasi hii na Dr. Slaa kaingia hapo na anasema lugha ya kuleta matumaini. Swali ni kwani Rais Kikwete amejitoa katika nafasi yake?