Dr Slaa aizika CCM Tunduma

Dr Slaa aizika CCM Tunduma

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa anaanza ziara rasmi ya kichama leo katika wilaya za Momba na Mbozi.Dr Slaa anaingia Tunduma akitokea Zambia alikokuwa takribani wiki moja kwa ziara ya kikazi.

Kiongozi huyo mwenye mvuto mkubwa wa kisiasa nchini leo atahutubia mkutano mkubwa wa hadhara mjini Tunduma katika viwanja vya shule ya msingi Tunduma.

Kesho Dr Slaa atahutubia mkutano mkubwa wa hadhara mjini Vwawa katika wilaya ya Mbozi.

Dr Slaa anatarajiwa kupokea maelfu ya wanachama wapya wengi wao wakitokea CCM. Pia Mwanasiasa huyo asiyeyumba atazindua matawi kadhaa ya CHADEMA na kufungua ofisi mpya za chama hicho.

Katika ziara hiyo Dr Slaa atafuatana na maafisa kadhaa wa makao makuu,maafisa wa Kanda ya nyanda za juu kusini na Mbunge wa Mbozi David Silinde.

Kwa wiki hii nzima hapa Tunduma kuna hekaheka kubwa ya wananchi wakiwa na hamu kubwa na ujio wa Dr Slaa. Pia Polisi wanahaha kupiga doria huku na huko wakijipanga kusimamia usalama wakati wa mapokezi yake kwani sikuzote mapokezi ya kiongozi huyo hapa Tunduma yanautikisa mkoa mzima. Dr Slaa anachukuliwa na wananchi wa hapa kama Mfalme wa Tunduma.

==============================
Up dates baadhi ya maneno ya Hotuba
==============================

============
Updates katika picha:
attachment.php

Watu huwa wanakuja wengi kumshangaa. Nikiwemo. Wengi wetu huwa hatuamini kama padre anaweza kuishi na kimada mpaka leo na pia huwa hatuamini kama huyu ni mwana siasa au mzee wa bonanza.
 
Nyie hakuna mnachopenda nchi hii hata makabisa hamuapendi maana ndo mnasema yamewafanya mkose kazi.. Wenzenu wanasoma nyie mko bize kuandik kukota kulia kwenda kushoto
Kigogo kwa nyuma, punguza jazba Mkuu... Upogo wa Udini umekujaa sana, unashindwa hata kuona maandishi vema. Adui wetu ni mmoja tu CCM. na ili tuing'oe tunahitaji michango ya waislam na wakristo kwa umoja wetu... sote tumepigika mbaya, Rasilimali zetu hazitunufaishi sis walengwa...
 
We muntu we Izina li wafumya kwi?
Utunjiyila izina. Nene ali Chilipamwao! we weni?
Nabadilisha Nene Chiliumupanga
 
Dr wa ukweli aliye mioyoni mwa watanzania,tuonyeshe njia nasi tutaifuata.
 
Back
Top Bottom