Dr Slaa aizika CCM Tunduma

Dr Slaa aizika CCM Tunduma

Greenwhich

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
1,337
Reaction score
968
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa anaanza ziara rasmi ya kichama leo katika wilaya za Momba na Mbozi.Dr Slaa anaingia Tunduma akitokea Zambia alikokuwa takribani wiki moja kwa ziara ya kikazi.

Kiongozi huyo mwenye mvuto mkubwa wa kisiasa nchini leo atahutubia mkutano mkubwa wa hadhara mjini Tunduma katika viwanja vya shule ya msingi Tunduma.

Kesho Dr Slaa atahutubia mkutano mkubwa wa hadhara mjini Vwawa katika wilaya ya Mbozi.

Dr Slaa anatarajiwa kupokea maelfu ya wanachama wapya wengi wao wakitokea CCM. Pia Mwanasiasa huyo asiyeyumba atazindua matawi kadhaa ya CHADEMA na kufungua ofisi mpya za chama hicho.

Katika ziara hiyo Dr Slaa atafuatana na maafisa kadhaa wa makao makuu,maafisa wa Kanda ya nyanda za juu kusini na Mbunge wa Mbozi David Silinde.

Kwa wiki hii nzima hapa Tunduma kuna hekaheka kubwa ya wananchi wakiwa na hamu kubwa na ujio wa Dr Slaa. Pia Polisi wanahaha kupiga doria huku na huko wakijipanga kusimamia usalama wakati wa mapokezi yake kwani sikuzote mapokezi ya kiongozi huyo hapa Tunduma yanautikisa mkoa mzima. Dr Slaa anachukuliwa na wananchi wa hapa kama Mfalme wa Tunduma.

==============================
Up dates baadhi ya maneno ya Hotuba
==============================
Utambulisho unaendelea viongozi mbalimbali wanatambulishwa saizi.!!!
======
Mama Josepheni anasema yeye hana tamaa ya kwenda ikulu ya majambazi. Ndugu zangu Dr. Slaa haitaji kwenda ikulu anaelimu ya kutosha kuishi popote.
Naomba mniombee nimtunze Dr. Wenu vizuri ili tuweze kuiondoa ccm madarakani.!!!

=========

Chadema ilichukua Kura zote tatu hapa tunduma. Diwani,mbunge na Rais. Anatoa mhitasari wa maendeleo yaliyofanywa na chadema Tunduma. Jimbo la mbozi ndio lenye madarasa mengi zaidi mkoa wa mbeya kupitia chadema.

Silinde....
Kulinga na uhaba wa maji mdogo wa Tunduma, nilitoa milioni 35 kwa ajili ya visima na visima vimechimbwa.

==========

Tanzania sio. Ya wakristo wala sio waislamu..... Sitamung'unya maneno Le....... Udini umeletwa na viongozi wenye tamaa ya madaraka.

=========
Dr.Slaa
Nimekuja kwenu kuleta matumaini mapya. Kwanini watanzania ni maskini ccm imeshindwa kutupa jibu ndani ya miaka 50. Maji ni siasa,barabara ni siasa, afya ni siasa.... Siasa imetawala kila kitu ndio maana hata ugumu wa maisha unasavavishwa na siasa...

Jukumu la kwanza la shekhe na Askofu ni kukemea uonevu dhidi ya wananchi.

Dr. slaa: sioni haja kuilinda mikutano yangu wakati raslimali za taifa zinaibiwa kila siku. Nataka kumwambia kikwete ameshindwa kuongoza nchi. Sababu raslimali zetu zinaibiwa kila siku na yeye yupo tu hachukui hatua..

Dr.Slaa...
Akichambua vifungu vya sheria kuhusu kazi ya mwanasiasa. Anaelezea kazi ya mwanasiasa ni kuikosoa na kuierekebisha serikali dhidi ya makosa kwa nchi.!!!

Dr.Slaa...
Siasa safi ziliondoka na mwalimu Nyerere sio saizi..... Watanzania wamefanywa maskini, umaskini wetu sio mpango wa Mungu ni sera mbovu za ccm. Ari zaidi, kasi zaidi, inamfanya mtanzania awe maskini zaidi.!!!!

Dr.Slaa...
Chadema inaandaa makamanda 36000 kwa ajili ya kusambaza majimbo yote Tanzania. Kuanzia sasa tunataka tuwe na mabalozi wa chadema kila mtaa. Mtu akiambiwa taja balozi wako utaje wa chadema na sio ccm tena.!!!!

Dr.Slaa...
Tuliaidi kwamba uwezo wa kubadilisha nchi tunao. Kwa raslimali zetu hata SA hawatufikii... Adui wa ccm sio chadema...
Boresheni maisha ya mtanzania muone kama mtasemwa.!!

Dr.Slaa...
Usalama wa Taifa ni weupe kama karatasi. Mipango yao yote inaishia mikononi mwa chadema...

Dr.Slaa
Kikwete ndio mdini namba moja Tanzania. Kwa kuuanzisha kuulea na kuundeleza kwa maslai yake na hatimae taifa limepasuka mikononi kwake.!!

Dr.Slaa....
Kikwete ndi mchechezi mkubwa wa udini. Simsemi kikwete sababu ya imani yake. Nimefanya kazi na mwinyi kwa muda mrefu hakujawai kutokea udhaifu kama wa kikwete.

Dr.Slaa...
Anamaliza sasa kwa kuwaomba wenye nia nzuri na nchi hii wajitolee kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya ustawi wa chadema Tunduma.

Maana chadema ni ya wananchi.!!!!
============
Updates katika picha:
attachment.php
 

Attachments

  • zzzz.jpg
    zzzz.jpg
    48.5 KB · Views: 848
  • zxzxzx.jpg
    zxzxzx.jpg
    38.6 KB · Views: 7,014
  • zaza.jpg
    zaza.jpg
    36.3 KB · Views: 2,466
Nawatakia kila la kheri kwenye mkutano wa leo na itakayofuata,picha muhimu.
 
Tahadhari, mwe waangalifu na vijana wa UVCCM wanaweza valishwa magwanda wakaleta vurugu ikaonekana ni CHADEMA, na hapohapo zikafanyika vurugu mlengwa akiwa Dr. Slaa, kwani huyu jamaa magamba ni kama wanamuombea mabaya siku zote, kwahiyo chukueni tahadhari zote.
 
Kila la heri, ila amani iwe mbele hasa kipindi hiki .
 
Ukombozi lazima uje!! Dr. ongoza gari letu katika njia sahihi. CCM fainali uzeeni 2015
 
Chadema mnapenda habari nzuri nzuri kuhusu nyie.duh!

Ni haki yao Mkuu; sidhani kama kuna binadamu yeyote mwenye akili timamu anayependa habari mbaya. By the way, hivi tukiwa-rank, ni Katibu Mkuu yupi anashika nafasi ipi kwa uongozi mahiri ndani ya vyama vyao?

1. Col. Abdulrahmani Kinana (CCM)
2. Maalim Seif Sharif Hamad (CUF)
3. Sam Ruhuza (NCCR-Mageuzi)
4. W. P. Slaa (Chadema)
5. General Secretary Emeritus Nnape Nnauye (CCJ/CCK)
6. xxx (UPDP)
7. xxx (UMD)
8. xxx (Tadea)
9. xxx (NRA)
10. xxx (TLP)
11. xxx (ADC)
12. xxx (UDP)

Hebu tupe maoni yako hapo.
 
Ni haki yao Mkuu; sidhani kama kuna binadamu yeyote mwenye akili timamu anayependa habari mbaya. By the way, hivi tukiwa-rank, ni Katibu Mkuu yupi anashika nafasi ipi kwa uongozi mahiri ndani ya vyama vyao?

1. Col. Abdulrahmani Kinana (CCM)
2. Maalim Seif Sharif Hamad (CUF)
3. Sam Ruhuza (NCCR-Mageuzi)
4. W. P. Slaa (Chadema)
5. General Secretary Emeritus Nnape Nnauye (CCJ/CCK)
6. xxx (UPDP)
7. xxx (UMD)
8. xxx (Tadea)
9. xxx (NRA)
10. xxx (TLP)
11. xxx (ADC)
12. xxx (UDP)

Hebu tupe maoni yako hapo.

Acha kuharibu sred ya mwenzio Kwa Kuanzisha nyingine.. Vilevile huwezi kumchanganya Slaa Na Kundi la Madudedude tia heshma mkuu..

Slaa ni Mtu mwenye heshima zake Ndani Na NJE ya uzio Wa mipaka ya Nchi yetu. Wewe dudus Mtu akikuchanganya Na mavi utafurahi..? Acha ivo bana
 
Last edited by a moderator:
Ni haki yao Mkuu; sidhani kama kuna binadamu yeyote mwenye akili timamu anayependa habari mbaya. By the way, hivi tukiwa-rank, ni Katibu Mkuu yupi anashika nafasi ipi kwa uongozi mahiri ndani ya vyama vyao?

1. Col. Abdulrahmani Kinana (CCM)
2. Maalim Seif Sharif Hamad (CUF)
3. Sam Ruhuza (NCCR-Mageuzi)
4. W. P. Slaa (Chadema)
5. General Secretary Emeritus Nnape Nnauye (CCJ/CCK)
6. xxx (UPDP)
7. xxx (UMD)
8. xxx (Tadea)
9. xxx (NRA)
10. xxx (TLP)
11. xxx (ADC)
12. xxx (UDP)

Hebu tupe maoni yako hapo.

Ndugu yangu dudus hapa umeua kabisa..
 
Last edited by a moderator:
Kila lakheli dr slaa wewe ndio mkombozi wetu hata wanaokuchukia ipo siku watakupenda tu.
katibu mkuu wa chadema dr wilbroad slaa anaanza ziara rasmi ya kichama leo katika wilaya za momba na mbozi.

Kiongozi huyo mwenye mvuto mkubwa wa kisiasa nchini leo atahutubia mkutano mkubwa wa hadhara mjini tunduma katika viwanja vya shule ya msingi tunduma.

Kesho dr slaa atahutubia mkutano mkubwa wa hadhara mjini vwawa katika wilaya ya mbozi.

Dr slaa anatarajiwa kupokea maelfu ya wanachama wapya wengi wao wakitokea ccm. Pia mwanasiasa huyo asiyeyumba atazindua matawi kadhaa ya chadema na kufungua ofisi mpya za chama hicho.

Katika ziara hiyo dr slaa atafuatana na maafisa kadhaa wa makao makuu,maafisa wa kanda ya nyanda za juu kusini na mbunge wa mbozi david silinde.

Kwa wiki hii nzima hapa tunduma kuna hekaheka kubwa ya wananchi wakiwa na hamu kubwa na ujio wa dr slaa. Pia polisi wanahaha kupiga doria huku na huko wakijipanga kusimamia usalama wakati wa mapokezi yake kwani sikuzote mapokezi ya kiongozi huyo hapa tunduma yanautikisa mkoa mzima. Dr slaa anachukuliwa na wananchi wa hapa kama mfalme wa tunduma.
 
Back
Top Bottom