Dr Slaa aijibu serikali kuhusu maandamano

Dr Slaa aijibu serikali kuhusu maandamano

watu wakichoka wataingia barabarani tu, hakuna wa kututisha, mie nimeshaichoka siku nyingi, naendelea kusubiri idadi kubwa ya wadanganyika nao wachoke tuingie mtaani bila shaka.
 
Serikali imekosa hoja kwa kukimbilia kutunga sheria. Hivi kwanini wameshindwa kutekeleza mahitaji ya wananchi badala ayke wanataka kuwanyamazisha wananchi kwa mkono wa sheria za kikoloni?? Kamwe sisi wananchi hatutakubali sheria hiyo ipitishwe. Nguvu ya umma itazuia hilo. Werema akipewa Nchi anaweza kuwa kama Hitler
 
PENYE NIA NDIPO NJIA ILIPO. SASA KAMA LA UKWELI NI MABADILIKO LITAKUWA KWANI ITAKUWA NDIYO WAKATI WAKE. CCM KULAZIMISHA MAMBO WAKUBALIKE NI SAWA NA KULAZIMISHWA UWE MKE AU MUME BILA KUPENDA.......We are all Tanzanian.. Let us fight for Peace and Development.
 
Hamjaiskia sheria ya maandamano yaMUSSEVEN????sasa huku inaonekana wamemtumia WE'REMA,wangeongea wenye mamlaka wangezodolewa,na werema anakubali kutumiwa kama hakusoma sheria,ingawa anasema kuna watu hawapendi maandamano,,,,,,mbona hata mimi sipendi misafara mirefu ya viongoz????issue ni kuvumiliana,maana ndio demokrasia hiyooo
 
If the government is sick of demonstrations, then it has to act responsibly to stubborn puzzles facing the normal citizens.

Hapo umenena kweli, yani hawa viongozi wetu bwana.

sasa Werema yeye haoni kuwa watanzania ni wasomi siku hizi na wanazitambua alama za nyakati nadhani warema anashida kidogo alipo chaguliwa alijisifu sana kuwa atakuwa makini sana ila kadri siku zinakwenda anakuwa bogus 100% na uanasheria wake hajui kusoma alama za nyakati kweli au ni utumwa tena?

Hizi njaa na kutokuwa wazalendo jamani kutawaponza! Mfano tu ajaribu kuangalia Arab World ikoje sasa, hali yao ya hewa kwa hao viongozi! Wewe badala ya kudeal na issue za raia na ku simplify way of living nae anataka kukandamiza wenzio wanaenda mbele wewe unalazimishia ati kuna watu wengine hawataki maandamano unataka kuchukua mfano wa Libya?

Kwa taarifa yenu Aljazeer walipata siri ya Libya ni kuwa Tripoli pia kuna watu hawamtaki Gaddafi ni watu wanajipendekeza kwa kuwa anawapa pesa watu walihojiwa wakiwa wameficha nyuso zao ukimpinga Gaddafi wanakuua, Ndio hayo Werema anataka ku implement
 
Well said Dr. wa Kweli!!!!!!!!!!!!!! Hatutakubali sauti ya Mungu ambayo ndiyo yetu watanzania kunyamazishwa na kibaraka kama Werema. The worst AG Tanzania had ever since independence. Hivi huyu Werema kama anapenda siasa si aachie ngazi? Hatutakubali ujinga wako Werema. Peoples Poweeeeeeeeeeeeer! Aluta Continua!!!!! Nchi si yako wewe Kibaraka Werema!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Wana jf, kila mmoja afanye utafiti wake mdogo kuhusu matatizo yanayowakabili wtz. Binafsi nimefanya kautafiti wa nishati nimejiridhisha pasipo shaka kwamba wtz waishio mijini hadi vijijini wako ktk giza totoro. Wa mjini mgao wa umeme njoo ars ujionee mwenyewe, wa vijijini mafuta taa hayanunuliki nenda vijijini ujionee mwenyewe.

Haya mambo ndo yashughulikiwe na sio maandamano tena ya amani. Wale mnaoweza waambieni serikali wajishughulishe na mtzo sio ushenzi ushenzi
 
Serikali isiyo na upeo ndiyo udhania kuwa kwa kutumia sheria kali na dola (polisi na jeshi) basi serikali hiyo inaweza kukaa madarakani bila wasiwasi. Lakini hiyo imepitwa na wakati na mfano halisi ni kinachotokea katika nchi za kiarabu.

Hivi huyu AG anadhani wananchi wa Tunisia, Misri, Libya, Syria, Yemen etc walikuwa wanaruhusiwa kuandamana kwa mujibu wa sheria? Kama jibu ni siyo basi ajue yeye analiandalia taifa letu machafuko. Kwasababu si uwepo wa sheria legelege kwa waandamanaji unaowafanya wananchi waingie mitaani kudai haki zao. La asha!

Narudia; Kama sheria hiyo itapitishwa basi inaandaa machafuko nchini mwetu. Utulivu na amani uletwa na utawala bora na usimamizi wa haki na si nguvu ya Polisi au Jeshi.

Jifunzeni kwa wenzenu la sivyo JK ataishia kuwa kama rais Saad wa Syria!
 
the government missed the point long ago!
 
hivi ninyi magwanda hamna njia nyingine ya kufanya siasa mpaka maandamano au mnataka watu wafe ndio mwende ikulu kwa kukanyaga damu za watu, kama mlivyofanya Arusha.
Linda ugali wako coz najua upo kwa payroll ya magamba...lakin chama chenu kinasambaratika na hzo ajira hamtazipata tena...
 
Hili linadhihirisha jinsi siasa yaweza kupofua watu. Sikutegemea mtu kama jaji kutotambua kuwa tatizo si maandamano...... tatizo ni mambo yanayopelekea kuwepo kwa hayo maandamano.

Unaweza tumia nguvu na mali zote ulizo nazo kudhibiti nguvu ya umma bila mafanikio. Nguvu ya umma udhibitika kwa kutimiza matarajio ya umma na si kwa kutunga sheria.
 
Back
Top Bottom