Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,173
Watendaji wengi ambao kwa nyadhifa zao huteuliwa na rahisi sasa hivi ni tumbo moto wakihofia ujio wa utawala mpya wa Dr. Slaa.
Utafiti wangu umebaini ya kuwa wengi wao wanayafurahia mabadiliko hayo hususani watumishi wa ngazi za kati ambao wanawaona wakubwa zao wengi wao hawana sifa na ni mzigo kwa taifa.
Lakini hao wakubwa ndiyo wameshika mpini na wanaweza kutumia nafasi zao kwa hali na mali katika kulinda ulaji wao hapo serikalini katika kuchakachua matokeo ya kura.
Mwaka 1995, Augustine Mrema kosa alilolifanya ni kuwatishia wakubwa serikalini ajira zao badala ya kuwatoa wasiwasi ya kuwa watendaji wazuri serikali mpya ijayo itawajali na kuheshimu mikataba yao.
Kutokana na vitisho na jazba za Mrema, vibosile hawa walitumia nafasi zao kuchakachua matokeo na historia iliyofuata sote tunaifahamu.
Ushauri kwa Dr. Slaa, kwenye mikutano yake awaondolee wasiwasi haswa watendaji wazuri serikalini ili nao wapate uhakika wa ajira zao na hivyo kumsaidia kwa hali na mali.
Serikalini watendaji wengi wazuri wana manung'uniko sugu juu ya utawala dhalimu wa JK kwa sababu ajira na kupanda vyeo hakuzingatii sifa ila kufahamiana na wanachohitaji na kutarajia kwa Dr. Slaa ni kuhakikishiwa tu kuwa sera za ajira serikalini na kwenye taasisi zote za umma zitaheshimu kanuni za utumishi na wala siyo vinginevyoooooooooooo