Dr Slaa aanza ziara Zanzibar

Dr Slaa aanza ziara Zanzibar

mkuu, hicho ulichoeleza ndo utofauti baina ya chama kama taasisi (ccm) na chama kama kichaka cha wahuni na waliochanganyikiwa (chadema)
mkuu kwani utaasisi wa ccm ni upi? Je ni ule wa kujifungia pale lumumba na kutengeneza watoa maoni feki? Au ni kule kukumbatia wauza unga na mafisadi?
 
Hongera dr slaa, usisahau kuwapa pole ndugu zetu wazanzibar kwa mpigania uhuru wa zanzibar kutimuliwa huko dodoma, waambie ccm bara wataendelea kuwaburuza wazanzibar mpaka wakome!
 
Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mhe. Tundu Lissu

Watembeleaji wa Zanzibar Daima hapa kuna jambo la kulijadili. Si lazima kukubaliana na kila anachokisema Mheshimiwa Tundu Lissu, lakini maoni haya ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (CHADEMA) tuyajadilini. Zanzibar Daima inayaona kuwa ni mlango mwengine uliofunguka kwa Zanzibar, ambao sio tu unatupa fursa ya kuijua nini CHADEMA inataka kwa nchi, bali pia wapi Wazanzibari wanapaswa kujipanga. Tujadiliane baada ya kusoma sehemu hii ya hotuba ya Mheshimiwa Lissu jana (14.11.2011) Bungeni, Dodoma.
Kwa mfano, Lissu analalamika kuwa: "Mamlaka ya Rais wa Zanzibar hayaishii tu kwenye uteuzi wa wajumbe na watendaji wa Tume, bali pia yanaingia hata katika uwasilishaji wa ripoti ya Tume. Kwa mujibu wa ibara 18(1) ya Muswada, mara baada ya kumaliza kazi yake, Tume itawasilisha ripoti yake kwa Rais na kwa Rais wa Zanzibar. Aidha, kwa mujibu wa ibara ya 18(2), mara baada ya kupokea ripoti hiyo, Rais, ‘baada ya kushauriana na kukubaliana' na Rais wa Zanzibar, "… atamuagiza Waziri kuwasilisha Muswada wa Katiba katika Bunge la Katiba." Kwa mapendekezo haya pia, Rais wa Zanzibar sio tu kwamba ana mamlaka karibu sawa na Rais wa Jamhuri ya Muungano bali pia ana kura ya turufu katika mchakato wa Katiba Mpya. Maana yake ni kwamba Rais wa Zanzibar asipopatiwa nakala ya ripoti ya Tume au asipokubaliana na Rais wa Muungano, basi Muswada wa Katiba hautawasilishwa kwenye Bunge la Katiba!"NAFASI YA ZANZIBAR
Mheshimiwa Spika,
Pengine mabadiliko makubwa yaliyofanywa katika Muswada ni mapendekezo yanayohusu nafasi ya Zanzibar katika mchakato wa Katiba Mpya. Itakumbukwa kwamba moja ya masuala yaliyozua tafrani kubwa katika mchakato wa kukusanya maoni juu ya Muswada wa Zamani hasa katika kituo cha Zanzibar ni kuwepo hisia kwamba nafasi ya Zanzibar ilikuwa imepuuzwa katika Muswada huo. Muswada sio tu kwamba umetekeleza matakwa yote ya ushirikishwaji wa Zanzibar, bali umekwenda mbali zaidi kwa kuifanya Zanzibar mwamuzi wa mustakbala wote wa kikatiba wa Tanzania. Hii imefanyika kwa njia mbili: kwanza, kwa kumfanya Rais wa Zanzibar kuwa mshirika sawa wa kikatiba wa Rais wa Jamhuri ya Muungano; na pili, kwa kuipa Zanzibar nafasi kubwa ya uwakilishi katika mchakato mzima wa Katiba Mpya."
NAFASI YA RAIS WA ZANZIBAR
Angalia ramani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Fikiria udogo wa Zanzibar ndani ya Tanganyika. Je, hili ni moja ya yanayowapa tabu akina Tundu Lissu?

Mheshimiwa Spika,
Muswada unapendekeza kwamba utekelezaji wa mamlaka yote ya Rais, Waziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano lazima ufanyike kwa ‘mashauriano na makubaliano' na Rais, Waziri au Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar. Kwa mfano, ibara ya 5 inayohusu kuundwa kwa Tume inamtaka Rais ‘kushauriana na kukubaliana' na Rais wa Zanzibar na kupata ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar. Vile vile, ibara ya 6(1) inayohusu uteuzi wa wajumbe wa Tume; ibara ya 8(1) na (2) inayohusu hadidu za rejea na kuongeza muda wa Tume; na ibara ya 13(2) inayohusu uteuzi wa Katibu wa Tume, zote zinataka kuwepo na makubaliano na Rais wa Zanzibar. Aidha, ibara ya 13(5) inayohusu uteuzi wa watendaji wengine wa Tume inalazimu makubaliano kati ya Waziri na Waziri mwenzake wa Zanzibar ambao nao ni wateuliwa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Zanzibar.
Mamlaka ya Rais wa Zanzibar hayaishii tu kwenye uteuzi wa wajumbe na watendaji wa Tume, bali pia yanaingia hata katika uwasilishaji wa ripoti ya Tume. Kwa mujibu wa ibara 18(1) ya Muswada, mara baada ya kumaliza kazi yake, Tume itawasilisha ripoti yake kwa Rais na kwa Rais wa Zanzibar. Aidha, kwa mujibu wa ibara ya 18(2), mara baada ya kupokea ripoti hiyo, Rais, ‘baada ya kushauriana na kukubaliana' na Rais wa Zanzibar, "… atamuagiza Waziri kuwasilisha Muswada wa Katiba katika Bunge la Katiba." Kwa mapendekezo haya pia, Rais wa Zanzibar sio tu kwamba ana mamlaka karibu sawa na Rais wa Jamhuri ya Muungano bali pia ana kura ya turufu katika mchakato wa Katiba Mpya. Maana yake ni kwamba Rais wa Zanzibar asipopatiwa nakala ya ripoti ya Tume au asipokubaliana na Rais wa Muungano, basi Muswada wa Katiba hautawasilishwa kwenye Bunge la Katiba!
Mheshimiwa Spika,
Mapendekezo haya yanaashiria kuwepo kwa mtazamo ambao chanzo chake ni Makubaliano ya Muungano kati ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika ya tarehe 25 Aprili 1964. Kwa mtazamo huo, Zanzibar ni nchi huru kama ilivyokuwa mwaka 1964 na kwa hiyo ni lazima sio tu ishirikishwe kwa usawa, bali pia lazima ikubaliane na mabadiliko yoyote ya kikatiba yanayopendekezwa na Muswada. Kama Profesa Palamagamba Kabudi wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alivyosema kwenye Semina ya Wabunge Juu ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba iliyofanyika tarehe 12 Novemba 2011: ‘Katika kuandika katiba mpya, wabia wa Muungano wanarudi kwa usawa.'
Hata hivyo, Mheshimiwa Spika, mtazamo huu sio sahihi. Kwanza kabisa, Zanzibar sio nchi huru tena kama ilivyokuwa mwaka 1964, kama ambavyo hakuna tena nchi inayoitwa Tanganyika wala serikali yake. Hii ni kwa sababu tangu kusainiwa kwa Hati za Muungano mwaka 1964, na kwa mujibu wa ibara ya 4(3) ya Katiba ya sasa, masuala yote yanayohusu Muungano kama vile Katiba ya Tanzania yamekasimiwa kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, ambayo pia imekasimiwa mamlaka juu ya masuala ya iliyokuwa Tanganyika. Masuala haya ya Muungano hayawezi kujadiliwa upya na kwa usawa kati ya nchi hizi mbili kwa vile moja kati ya nchi hizo haipo tena na iliyobaki imepoteza sehemu ya uhuru wake kutokana na Muungano huo! Hii ndio kusema hakuwezi tena kuwa na wabia wa Muungano bila kwanza kuirudisha Tanganyika kama nchi na bila kuirudisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar yenye uhuru na mamlaka kama iliyokuwa nayo kabla ya Muungano!
Pili, kuna dhana kwamba Rais wa Zanzibar hakushirikishwa katika mchakato wa maandalizi ya Muswada wa Zamani. Dhana hii vile vile ni potofu. Kwanza, Rais Ali Mohamed Shein mwenyewe ametamka wazi kwa waandishi wa habari kwamba alishiriki katika hatua zote za maamuzi kwenye Baraza la Mapinduzi. Pili, kwa mujibu wa ibara ya 54(1) ya Katiba ya sasa, Rais wa Zanzibar ni mmoja wa wajumbe wa Baraza la Mawaziri la Serikali ya Jamhuri ya Muungano na kwa hiyo ni mshiriki wa maamuzi yote ya Serikali hiyo. Kwa maana hiyo, maslahi ya Zanzibar yanawakilishwa ndani ya ‘chombo kikuu cha kumshauri Rais' katika Jamhuri ya Muungano. (ibara ya 54(3) Hii ni licha ya ukweli kwamba, kwa mlolongo wa madaraka uliopo katika ibara ya 54(2), Rais wa Zanzibar sio mmoja wa wajumbe wanaoweza kuongoza mikutano ya Baraza hilo.
Aidha, ndani ya Baraza la Mawaziri, Zanzibar inawakilishwa pia na Makamu wa Rais ambaye – kwa mujibu wa ibara ya 47(1) ya Katiba ya sasa – "… ndiye Msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya Muungano…." Kwa maana hiyo, mapendekezo ya Muswada yanayomfanya Rais wa Zanzibar kuwa sio tu mshiriki sawa lakini pia mwamuzi wa mustakbala wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano yanaenda kinyume sio tu na Katiba ya sasa bali pia na Hati za Muungano wenyewe. Kwa mapendekezo haya, endapo Rais wa Zanzibar hatakubaliana na uteuzi wowote wa wajumbe wa Tume au Katibu wake au watendaji wake wengine, anaweza kusimamisha mchakato mzima wa kikatiba hata kama unahusu masuala ya Tanzania Bara yasiyo ya Muungano!
UWAKILISHI WA ZANZIBAR
Bendera ya Zanzibar (kama inavyotakiwa kuwa). Haitoshi kuwaambia akina Tundu Lisu kwamba huu si mkoa wa Tanganyika?

Mheshimiwa Spika,
Ushawishi mkubwa wa Zanzibar hauishii katika kura ya turufu aliyo nayo Rais wa Zanzibar pekee yake. Zanzibar ina ushawishi mkubwa vile vile kutokana na nafasi kubwa iliyo nayo katika vyombo vya maamuzi vinavyopendekezwa na Muswada. Kwa mfano, kwa mujibu wa ibara ya 6(2), "… muundo wa Tume utazingatia msingi wa kuwepo kwa uwakilishi ulio sawa kwa kila upande wa Jamhuri ya Muungano." Hii ina maana kwamba wajumbe wa Tume na Sekretarieti yake wanatakiwa wawe sawa kwa sawa kati ya Tanzania Bara na Zanzibar. Ikumbukwe kwamba Tume hii inatengeneza Katiba inayohusu masuala ya Muungano, ambayo ni haki kwa Zanzibar kushirikishwa kwa usawa kabisa, na vile vile masuala yasiyokuwa ya Muungano ya Tanzania Bara ambayo Zanzibar haina haki ya kushiriki.
BUNGE LA KATIBA
Mheshimiwa Spika,
Eneo la pili ambalo Zanzibar ina ushawishi mkubwa kutokana na uwakilishi wake ni katika Bunge la Katiba linalopendekezwa katika Sehemu ya Tano ya Muswada. Kwa mujibu wa ibara ya 20(2), wajumbe wa Bunge la Katiba watakuwa ni wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano; wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar; mawaziri wa katiba na sheria wa Jamhuri ya Muungano na wa Zanzibar; Wanasheria Wakuu wa Jamhuri ya Muungano na wa Zanzibar; na wajumbe mia moja kumi na sita wakaoteuliwa kutoka asasi zisizokuwa za kiserikali, asasi za kidini, vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, taasisi za elimu ya juu na makundi yenye mahitaji maalum katika jamii. Inaelekea kwamba, kwa mujibu wa ibara ya 20(4), wajumbe wasiokuwa wabunge ama wawakilishi nao pia watateuliwa na Rais licha ya kutoka nje ya mfumo wa kiserikali!
Mheshimiwa Spika,
Kwa mujibu wa ibara ya 66(1)(a) ya Katiba ya sasa ya Muungano, wajumbe wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ni pamoja na wabunge wa majimbo ya uchaguzi. Kwa composition ya sasa ya Bunge, kuna jumla ya majimbo ya uchaguzi 239 ambayo kati yao majimbo ya Zanzibar ni hamsini. Vile vile, kwa mujibu wa ibara ya 66(1)(c) ya Katiba, Baraza la Wawakilishi Zanzibar linawakilishwa na wabunge watano katika Bunge la Jamhuri ya Muungano. Aidha, kama inavyotakiwa na ibara ya 66(1)(b), kuna wabunge wanawake mia moja na mbili wanaojulikana kama ‘wabunge wa viti maalum.' Kwa mgawanyo wa sasa wa wabunge hawa, idadi ya wanaotoka Zanzibar ni ishirini na tano kwa vyama vyote vyenye uwakilishi bungeni. Na mwisho, kuna wabunge wasiozidi 10 wanaoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa ibara ya 66(1)(e). Hadi sasa, Rais ameshateua wabunge watatu ambao wote ni wa kutoka Zanzibar. Kwa hiyo, katika Bunge la sasa lenye wabunge 353, wabunge wanaowakilisha Zanzibar ni themanini na tatu au karibu 23.5% ya wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.
Kwa mujibu wa Sehemu ya Kwanza ya Sura ya Tano ya Katiba ya Zanzibar, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar ni pamoja na wawakilishi wa majimbo hamsini ya uchaguzi, wawakilishi kumi wa kuteuliwa na Rais wa Zanzibar na wawakilishi ishirini wa viti maalum na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kwa hiyo, jumla ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa sasa ni themanini na moja. Kwa maana nyingine ni kwamba endapo mapendekezo ya ibara ya 20(1)(b), (c) na (d) ya Muswada yatakubaliwa, idadi ya wajumbe wa Bunge la Katiba wanaotoka Zanzibar itaongezeka hadi kufikia mia moja sitini na nne kati ya wajumbe 545 wa Baraza hilo kwa mujibu wa ibara ya 20(2). Idadi hii ni sawa na 30% ya wajumbe wote wa Bunge la Katiba.
Idadi hiyo ya uwakilishi wa Zanzibar bado haitakidhi matakwa ya Muswada kwani ibara ya 20(3) inapendekeza kwamba "… idadi ya wajumbe wa Baraza la Katiba kutoka Tanzania Zanzibar … haitapungua theluthi moja ya wajumbe wote wa Bunge la Katiba"! Theluthi moja ya wajumbe wa Bunge la Katiba ni wajumbe 182. Kwa hiyo, ili kukidhi matakwa ya Muswada kuhusu uwakilishi wa Zanzibar, itabidi wajumbe 18 kati ya 116 waliotajwa na ibara ya 20(2)(e) watoke Zanzibar ili kufikisha idadi ya wajumbe 182 ambayo ndio theluthi moja ya wajumbe wote wa Bunge la Katiba.
Mheshimiwa Spika,
Kuna maeneo mengine ya Muswada ambayo pia yanazua maswali mengi juu ya nafasi ya Zanzibar katika mchakato wa Katiba Mpya. Kwa mfano, wakati ibara ya 21(1) inapendekeza kwamba Spika na Naibu Spika wa Bunge la Katiba wachaguliwe kutoka miongoni mwa wajumbe wa Bunge hilo, ibara ya 21(2) inapendekeza kwamba endapo Spika atatoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano basi Naibu wake lazima atoke upande mwingine. Sambamba na pendekezo hili, ibara ya 22(1) inapendekeza Makatibu wa sasa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar watakuwa ndio Katibu na Naibu Katibu wa Bunge la Katiba. Aidha, sawa na ibara ya 21(2), ibara ya 22(2) inapendekeza kwamba endapo Spika atatoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, basi Katibu wa Bunge la Katiba lazima atoke upande mwingine.
Mapendekezo haya yanaonyesha sio tu nafasi na ushawishi mkubwa wa Zanzibar katika mchakato wa Katiba Mpya, bali pia ni mwendelezo wa dhana potofu kwamba Zanzibar ni mshirika sawa wa Jamhuri ya Muungano. Hii inathibitishwa pia na pendekezo la ibara ya 24(3) ya Muswada inayotaka Katiba Mpya ikubaliwe na theluthi mbili ya wajumbe wa Bunge la Katiba wanaotoka Tanzania Bara na vile vile theluthi mbili ya wajumbe wanaotoka Zanzibar. Ni wazi, kwa hiyo, kwamba iwe ni kwa masuala ya Muungano yanayoihusu Zanzibar pia, au kwa masuala yasiyokuwa ya Muungano ya Tanzania Bara ambayo hayaihusu, Zanzibar itakuwa na kura ya turufu kwa mujibu wa mapendekezo ya Muswada huu.
Mheshimiwa Spika, Uwakilishi mkubwa wa Zanzibar katika Bunge la Jamhuri ya Muungano umetumika kihistoria kwa lengo la kuwatuliza Wazanzibari wakati Serikali ya Mwalimu Nyerere ilipokuwa inamomonyoa uhuru wa Zanzibar kwa kuongeza orodha ya Mambo ya Muungano kwenye Katiba ya Muungano. Katika kitabu chake Pan Africanism or Pragmatism? Lessons of Tanganyika – Zanzibar Union, Profesa Issa Shivji, mwanazuoni mashuhuri wa kikatiba na mwanafunzi wa historia ya Muungano huu amemnukuu aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar wakati wa utawala wa hayati Sheikh Abedi Amani Karume, Bw. Wolfgang Dourado akimnukuu Sheikh Karume juu ya nafasi ya Zanzibar katika Bunge la Jamhuri ya Muungano: "‘Msiwe na wasi wasi, sisi tuna haki ya kuwakilishwa katika Bunge lao lakini wao hawana haki ya kuwakilishwa katika Baraza letu la Mapinduzi'"!
Mheshimiwa Spika,
Sababu nyingine inatokana na kuongezeka kwa ushawishi na nafasi ya Zanzibar katika siasa za ndani ya CCM, hasa hasa katika zama hizi za vyama vingi na vita za makundi mbali mbali ndani ya chama hicho. Katika mazingira haya, mtu yeyote anayetaka kupitishwa kuwa mgombea urais kwa kupitia CCM anakuwa anahitaji kura za CCM Zanzibar ili kushinda katika kinyang'anyiro hicho. Kwa kauli ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere mwenyewe katika kitabu chake Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania, "sababu moja kubwa iliyofanya viongozi wetu wasitake kuwaudhi ‘Wazanzibari' … ni umuhimu wa kura za Zanzibar katika kumteua mwanachama wa CCM kuwa Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano. Kwa kiongozi yeyote anayeliona jambo hilo kuwa ni muhimu kupita mengine yote, kuwaudhi ‘Wazanzibari' ni dhambi ambayo haina budi iepukwe kwa kila njia." Kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, hofu hii ya kuwaudhi ‘Wazanzibari' ndio imepelekea kimya kikuu – ndani ya CCM na ndani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano – juu ya ukiukwaji mkubwa wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano uliofanywa na Sheria ya Mabadiliko ya Kumi ya Katiba ya Zanzibar, 2010.
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaamini kwamba upendeleo wa Zanzibar unaopendekezwa katika Muswada huu kuhusiana na uwakilishi katika Bunge la Katiba na katika vyombo vingine vya maamuzi juu ya mchakato wa Katiba Mpya sio wa haki na haukubaliki tena. Kwanza, ibara ya 64(2) ya Katiba ya sasa inaweka wazi kwamba Baraza la Wawakilishi Zanzibar lina mamlaka ya kutunga sheria katika Zanzibar '… juu ya mambo yote yasiyo mambo ya Muungano….' Hii pia ndio lugha ya ibara ya 78(1) ya Katiba ya Zanzibar kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka jana. ‘Katiba ya Tanzania' ni jambo la kwanza katika orodha ya Mambo ya Muungano iliyoko kwenye Nyongeza ya Kwanza ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano. Kwa Muswada Mpya kupendekeza kwamba Baraza la Wawakilishi Zanzibar liwe sehemu ya Bunge la Katiba ni kukiuka wazi wazi matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano na ya Katiba ya Zanzibar. Ni ajabu iliyoje kwamba wale wanaojifanya ni machampioni wa Muungano wanaweza kunyamazia ukiukaji huu wa Katiba!
Mheshimiwa Spika,
Thomas Paine, mwandishi maarufu wa Marekani ya wakati wa Mapinduzi ya mwaka 1776, aliwahi kuandika kijitabu alichokiita Common Sense juu ya uhalali wa Uingereza kutawala Bara la Amerika ya Kaskazini ambako alisema: '… [T]here is something very absurd in supposing a continent to be perpetually governed by an island [for] in no instance hath nature made the satellite larger than its primary planet…'! Yaani, ni ujinga kudhani kwamba bara linaweza kutawaliwa milele na kisiwa kwa sababu utaratibu wa asili haujawahi kufanya kitegemezi kuwa kikubwa kuliko sayari yake ya msingi. Hata kama ni kweli kwamba Tanganyika sio bara kama ilivyokuwa Marekani ya Kaskazini, bado tunakubaliana na Tom Paine kwamba ni ujinga kudhani kwamba Visiwa vya Zanzibar vitaendelea kuwa na maamuzi na ushawishi mkubwa katika masuala yasiyokuwa ya Muungano ya Tanganyika kwa sababu utaratibu wa asili haujawahi kufanya maslahi ya Visiwa hivyo kuwa bora zaidi ya maslahi ya Tanganyika!
Kwa maoni yetu, wakati umefika kwa Muungano kuwekwa kwenye msingi wa usawa na imara zaidi. Msingi huo unahitaji kurudishwa tena kwa Serikali ya Tanganyika ambayo ndio ilikuwa – pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar – mbia mkuu wa Muungano wa mwaka 1964. Kurudishwa huko kwa Tanganyika kutaiwezesha Zanzibar kujadiliana nayo kwa usawa juu ya masuala yote yanayohusu Muungano. Haya yote yanawezekana tu endapo Muungano huu utawekwa mbele ya wananchi ili waamue – kwa kura ya maoni – kama wanataka kuendelea nao au la; na kama wanataka kuendelea nao ni muundo gani wa Muungano wanaoutaka.
Mheshimiwa Spika, Mapendekezo ya kurudishwa kwa Tanganyika na Serikali yake sio mapya. Miaka ishirini iliyopita, Tume ya Rais ya Mfumo wa Chama Kimoja au Vyama Vingi vya Siasa (Tume ya Nyalali) ilipendekeza hivyo hivyo. Miaka saba baadae, Tume ya Kukusanya Maoni Juu ya Katiba, White Paper Na. 1 ya 1998 (Tume ya Kisanga) nayo ilipendekeza hivyo hivyo. Kuendelea kupuuza mapendekezo haya wakati Zanzibar inavunja Katiba ya sasa ya Muungano; kuendelea kukaa kimya kwa hofu ya kuwaudhi ‘Wazanzibari' wakati wao wanajitwalia uhuru wa kujiamulia mambo yao wenyewe huku wakiendelea kushiriki katika maamuzi ya mambo ya Tanganyika yasiyokuwa ya Muungano; kuendeleza kile alichokiita Mwalimu Nyerere falsafa ya ‘changu ni changu, chako ni chetu' katika mahusiano ya Zanzibar na Tanzania Bara, ni kutulazimisha tuipinge dhana nzima ya Muungano kati ya nchi zetu mbili kitu kinachoweza kupelekea kuvunjika kwa Muungano wenyewe. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni isingependa tufike huko lakini ndoa hii ya kulazimishana haiwezi ikadumu muda mrefu kwa taratibu za aina hii.
UDHOOFISHAJI WA UPINZANI
Mheshimiwa Spika,
Mapendekezo ya Muswada juu ya uwakilishi katika Bunge la Katiba yana athari nyingine kubwa katika majadiliano na maamuzi ndani ya Bunge la Katiba. Kwa mujibu wa uchambuzi uliofanywa na Profesa Issa G. Shivji kwa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, endapo mapendekezo ya ibara ya 20(2) ya Muswada yatapitishwa, CCM itakuwa na kati ya wajumbe 350 hadi 400 katika Bunge la Katiba ambalo lina wajumbe 545. Kwa upande mwingine Chama cha Wananchi (CUF) ambacho kina Wawakilishi 29 katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar kitakuwa na wajumbe 65 katika Bunge la Katiba. Kwa maana ya uwakilishi katika Bunge la Katiba, CUF itakuwa ndio chama cha pili kwa nguvu za kisiasa ndani ya Bunge hilo, licha ya kuwa na wabunge wawili tu wa kuchaguliwa kwa upande wa Tanzania Bara na licha ya kupata kura chache sana katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.
Na kama inavyojulikana, tangu Muafaka wa Kisiasa Zanzibar kati ya CCM na CUF wa mwaka 2010 na kuzaliwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, upinzani wa kisiasa Zanzibar umekufa na kwa upande wa Tanzania Bara, na hasa Bungeni na kwenye chaguzi ndogo kama ule wa Igunga, CUF imekuwa ikishirikiana na CCM kuipinga CHADEMA. Kwa mapendekezo haya, kambi ya CCM na CUF katika Bunge la Katiba inaweza kufika hata zaidi ya wajumbe 465 katika ya wajumbe 545 wa Bunge hilo! CHADEMA ambayo kwa sasa ndio chama kinachoongoza Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kutokana na matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2010, itabakia na Wabunge wake 48 na vyama vya kibunge vilivyobaki, yaani NCCR-Mageuzi, TLP na UDP vitabaki na jumla ya Wabunge sita. Kwa hiyo, CHADEMA itakuwa chama cha tatu kwa nguvu za kisiasa ndani ya Bunge la Katiba licha ya kuwa ni chama kikuu cha upinzani chenye nguvu na ushawishi mkubwa wa kisiasa nchini!
Kwa maana nyingine, iwe ni kwa makusudi au bila ya kujua au kwa kunuia, athari mojawapo kubwa ya mapendekezo ya Muswada kuhusu uwakilishi katika Bunge la Katiba itakuwa ni kuiongezea nguvu zaidi kambi ya CCM/CUF na kupunguza nguvu na ushawishi wa CHADEMA ambayo ndio chama pekee kinachobeba matarajio na matamanio ya Watanzania wengi wanaotaka mabadiliko ya kimsingi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii katika nchi yetu. Haihitaji kuwa na shahada ya uzamivu kujua kwamba Bunge la Katiba lenye uwakilishi wa aina hii litapitisha Katiba Mpya ambayo pengine itatofautiana na Katiba ya sasa kwa jina tu! Na wala haihitaji kisomo kikubwa kujua kwamba Bunge la Katiba la aina hii halitagusa ‘msingi mkuu' uliobaki wa Jamhuri ya Muungano, yaani Serikali mbili. Hapa pia ni wazi kuwa lengo halisi la mapendekezo haya ni kuhakikisha kwamba mchakato wa Katiba Mpya utazaa matunda yasiyokuwa tofauti sana na ya Katiba ya sasa!
‘UWAKILISHI' WA BUNGE LA KATIBA
Mheshimiwa Spika,
Sio Bunge hili tukufu la Jamhuri ya Muungano wala Baraza la Wawakilishi Zanzibar lenye mamlaka kikatiba na kisiasa ya kutunga Katiba Mpya ya Tanzania. Hii ni kwa sababu sisi wote tulioko humu ndani tulichaguliwa kwa mujibu wa Katiba ya sasa na mamlaka yetu yote yako ndani ya kona nne za Katiba hiyo. Kama ni kweli, kama anavyodai Profesa Kabudi, kwamba kitendo cha kutunga Katiba Mpya vile vile ni kitendo cha kuua Katiba ya Zamani, basi sisi Wabunge na Wawakilishi wa Zanzibar hatuna mamlaka ya kuiua Katiba ya sasa kwa sababu sisi wote tulikula kiapo cha kuilinda, kuihifandhi na kuitetea.
Pili, sisi sote ni Wabunge na Wawakilishi wa vyama vya siasa kwa sababu, kwa mujibu wa Katiba ya sasa sheria zote husika, tumechaguliwa kwa sifa kuu ya kuwa wanachama wa, na tuliopendekezwa na, vyama vya siasa. Kuligeuza Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuwa Bunge la Katiba ni sawa na kusema kwamba wasiokuwa wanachama wa vyama vya siasa hawana haki ya kushiriki katika kutunga Katiba Mpya kwa sababu ya kuwa na kilema cha kisheria kinachowakataza kuchaguliwa kuwa Wabunge na Wawakilishi! Ibara ya 20(4) ya Katiba ya sasa inatamka wazi kwamba "… ni marufuku kwa mtu yeyote kulazimishwa kujiunga na chama chochote…." Sio kosa, kwa hiyo, kwa mamilioni ya Watanzania ambao wameamua kwa hiari zao kutokuwa wanachama wa vyama vya siasa. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haikubaliani, na haiwezi kukubali, ubaguzi wa aina hii dhidi ya Watanzania walioamua kutumia haki zao za kikatiba ya kutokujiunga na chama chochote cha siasa. Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haitakubali Watanzania hao waadhibiwe kwa kunyimwa kushiriki katika Bunge la Katiba kwa sababu tu ya kutokuwa wanachama wa vyama vya siasa.
Tatu, wajumbe 116 wanaopendekezwa kuteuliwa kwenye Bunge la Katiba kwa mujibu wa ibara ya 20(2)(e) na (4) ya Muswada Mpya sio, na hawawezi kuwa, wawakilishi wa wananchi. Kwanza, hawajachaguliwa na mtu yeyote na wala taasisi zao kuwawakilisha katika Bunge la Katiba kwa sababu Muswada Mpya unapendekeza wateuliwe na Rais. Pili, Bunge la Katiba ni chombo cha uwakilishi wa moja kwa moja wa wananchi na kwa mila na desturi zinazokubalika na kutumika kimataifa, wajumbe wa Bunge la Katiba huchaguliwa moja kwa moja na wananchi bila ya kujali vyama vya siasa na huwa na kazi moja tu: kutunga Katiba Mpya. Kwa sababu zote hizi, Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza wajumbe wa Bunge la Katiba wachaguliwe moja kwa moja na wananchi na kusiwe na masharti yoyote kuhusu uanachama wa vyama vya siasa.
UHALALISHAJI WA KATIBA MPYA
Mheshimiwa Spika,
Muswada una mapendekezo ambayo yanaashiria kuachana na utaratibu wa kihistoria wa utungaji wa Katiba ambao umewaweka wananchi kando katika michakato wa kikatiba tangu miaka ya mwanzo ya uhuru. Kwa mujibu wa ibara ya 27(1), kutakuwa na kura ya maoni kwa lengo la kuihalalisha Katiba Mpya. Kwa mujibu wa ibara ya 30, watu wote walioandikishwa kuwa wapiga kura kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi ya Taifa na Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar, watakuwa na haki ya kupiga kura katika kura hiyo ya maoni. Aidha, kufuatana na ibara ya 32(2), matokeo ya kura ya maoni yataamuliwa kwa msingi wa kuungwa mkono kwa zaidi ya 50% ya kura zote zilizopigwa Tanzania Bara na kiasi hicho hicho kwa Zanzibar.
Mapendekezo ya ushirikishwaji wa wananchi katika kuipa Katiba uhai wa kisheria ni jambo la maana sana na linaonyesha kuwa tumeanza kuachana na urithi wa kikatiba wa kikoloni ulioanza na Katiba ya Uhuru ya mwaka 1961. Hata hivyo, mapendekezo haya yamejaa mitego na vichaka vingi vya hatari. Kwanza, ibara ya 27 inapendekeza kwamba kura ya maoni itaratibiwa na kusimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar. Tume hizi mbili – kwa mashauriano na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar – ndizo zitakazotengeneza swali litakaloulizwa kwenye kura ya maoni. (ibara ya 28(1) na (2) Aidha, kwa mujibu wa ibara ya 31, utaratibu utakaotumika katika kura ya maoni ni ule unaotumika katika chaguzi za kawaida katika nchi yetu, yaani Sheria ya Uchaguzi wa Taifa, Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura ya 292 na Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar.
 
Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mhe. Tundu Lissu Watembeleaji wa Zanzibar Daima hapa kuna jambo la kulijadili. Si lazima kukubaliana na kila anachokisema Mheshimiwa Tundu Lissu, lakini maoni haya ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (CHADEMA) tuyajadilini. Zanzibar Daima inayaona kuwa ni mlango mwengine uliofunguka kwa Zanzibar, ambao sio tu unatupa fursa ya kuijua nini CHADEMA inataka kwa nchi, bali pia wapi Wazanzibari wanapaswa kujipanga. Tujadiliane baada ya kusoma sehemu hii ya hotuba ya Mheshimiwa Lissu jana (14.11.2011) Bungeni, Dodoma. Kwa mfano, Lissu analalamika kuwa: “Mamlaka ya Rais wa Zanzibar hayaishii tu kwenye uteuzi wa wajumbe na watendaji wa Tume, bali pia yanaingia hata katika uwasilishaji wa ripoti ya Tume. Kwa mujibu wa ibara 18(1) ya Muswada, mara baada ya kumaliza kazi yake, Tume itawasilisha ripoti yake kwa Rais na kwa Rais wa Zanzibar. Aidha, kwa mujibu wa ibara ya 18(2), mara baada ya kupokea ripoti hiyo, Rais, ‘baada ya kushauriana na kukubaliana’ na Rais wa Zanzibar, “… atamuagiza Waziri kuwasilisha Muswada wa Katiba katika Bunge la Katiba.” Kwa mapendekezo haya pia, Rais wa Zanzibar sio tu kwamba ana mamlaka karibu sawa na Rais wa Jamhuri ya Muungano bali pia ana kura ya turufu katika mchakato wa Katiba Mpya. Maana yake ni kwamba Rais wa Zanzibar asipopatiwa nakala ya ripoti ya Tume au asipokubaliana na Rais wa Muungano, basi Muswada wa Katiba hautawasilishwa kwenye Bunge la Katiba!”NAFASI YA ZANZIBAR Mheshimiwa Spika, Pengine mabadiliko makubwa yaliyofanywa katika Muswada ni mapendekezo yanayohusu nafasi ya Zanzibar katika mchakato wa Katiba Mpya. Itakumbukwa kwamba moja ya masuala yaliyozua tafrani kubwa katika mchakato wa kukusanya maoni juu ya Muswada wa Zamani hasa katika kituo cha Zanzibar ni kuwepo hisia kwamba nafasi ya Zanzibar ilikuwa imepuuzwa katika Muswada huo. Muswada sio tu kwamba umetekeleza matakwa yote ya ushirikishwaji wa Zanzibar, bali umekwenda mbali zaidi kwa kuifanya Zanzibar mwamuzi wa mustakbala wote wa kikatiba wa Tanzania. Hii imefanyika kwa njia mbili: kwanza, kwa kumfanya Rais wa Zanzibar kuwa mshirika sawa wa kikatiba wa Rais wa Jamhuri ya Muungano; na pili, kwa kuipa Zanzibar nafasi kubwa ya uwakilishi katika mchakato mzima wa Katiba Mpya.” NAFASI YA RAIS WA ZANZIBAR Angalia ramani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Fikiria udogo wa Zanzibar ndani ya Tanganyika. Je, hili ni moja ya yanayowapa tabu akina Tundu Lissu? Mheshimiwa Spika, Muswada unapendekeza kwamba utekelezaji wa mamlaka yote ya Rais, Waziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano lazima ufanyike kwa ‘mashauriano na makubaliano’ na Rais, Waziri au Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar. Kwa mfano, ibara ya 5 inayohusu kuundwa kwa Tume inamtaka Rais ‘kushauriana na kukubaliana’ na Rais wa Zanzibar na kupata ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar. Vile vile, ibara ya 6(1) inayohusu uteuzi wa wajumbe wa Tume; ibara ya 8(1) na (2) inayohusu hadidu za rejea na kuongeza muda wa Tume; na ibara ya 13(2) inayohusu uteuzi wa Katibu wa Tume, zote zinataka kuwepo na makubaliano na Rais wa Zanzibar. Aidha, ibara ya 13(5) inayohusu uteuzi wa watendaji wengine wa Tume inalazimu makubaliano kati ya Waziri na Waziri mwenzake wa Zanzibar ambao nao ni wateuliwa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Zanzibar. Mamlaka ya Rais wa Zanzibar hayaishii tu kwenye uteuzi wa wajumbe na watendaji wa Tume, bali pia yanaingia hata katika uwasilishaji wa ripoti ya Tume. Kwa mujibu wa ibara 18(1) ya Muswada, mara baada ya kumaliza kazi yake, Tume itawasilisha ripoti yake kwa Rais na kwa Rais wa Zanzibar. Aidha, kwa mujibu wa ibara ya 18(2), mara baada ya kupokea ripoti hiyo, Rais, ‘baada ya kushauriana na kukubaliana’ na Rais wa Zanzibar, “… atamuagiza Waziri kuwasilisha Muswada wa Katiba katika Bunge la Katiba.” Kwa mapendekezo haya pia, Rais wa Zanzibar sio tu kwamba ana mamlaka karibu sawa na Rais wa Jamhuri ya Muungano bali pia ana kura ya turufu katika mchakato wa Katiba Mpya. Maana yake ni kwamba Rais wa Zanzibar asipopatiwa nakala ya ripoti ya Tume au asipokubaliana na Rais wa Muungano, basi Muswada wa Katiba hautawasilishwa kwenye Bunge la Katiba! Mheshimiwa Spika, Mapendekezo haya yanaashiria kuwepo kwa mtazamo ambao chanzo chake ni Makubaliano ya Muungano kati ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika ya tarehe 25 Aprili 1964. Kwa mtazamo huo, Zanzibar ni nchi huru kama ilivyokuwa mwaka 1964 na kwa hiyo ni lazima sio tu ishirikishwe kwa usawa, bali pia lazima ikubaliane na mabadiliko yoyote ya kikatiba yanayopendekezwa na Muswada. Kama Profesa Palamagamba Kabudi wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alivyosema kwenye Semina ya Wabunge Juu ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba iliyofanyika tarehe 12 Novemba 2011: ‘Katika kuandika katiba mpya, wabia wa Muungano wanarudi kwa usawa.’ Hata hivyo, Mheshimiwa Spika, mtazamo huu sio sahihi. Kwanza kabisa, Zanzibar sio nchi huru tena kama ilivyokuwa mwaka 1964, kama ambavyo hakuna tena nchi inayoitwa Tanganyika wala serikali yake. Hii ni kwa sababu tangu kusainiwa kwa Hati za Muungano mwaka 1964, na kwa mujibu wa ibara ya 4(3) ya Katiba ya sasa, masuala yote yanayohusu Muungano kama vile Katiba ya Tanzania yamekasimiwa kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, ambayo pia imekasimiwa mamlaka juu ya masuala ya iliyokuwa Tanganyika. Masuala haya ya Muungano hayawezi kujadiliwa upya na kwa usawa kati ya nchi hizi mbili kwa vile moja kati ya nchi hizo haipo tena na iliyobaki imepoteza sehemu ya uhuru wake kutokana na Muungano huo! Hii ndio kusema hakuwezi tena kuwa na wabia wa Muungano bila kwanza kuirudisha Tanganyika kama nchi na bila kuirudisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar yenye uhuru na mamlaka kama iliyokuwa nayo kabla ya Muungano! Pili, kuna dhana kwamba Rais wa Zanzibar hakushirikishwa katika mchakato wa maandalizi ya Muswada wa Zamani. Dhana hii vile vile ni potofu. Kwanza, Rais Ali Mohamed Shein mwenyewe ametamka wazi kwa waandishi wa habari kwamba alishiriki katika hatua zote za maamuzi kwenye Baraza la Mapinduzi. Pili, kwa mujibu wa ibara ya 54(1) ya Katiba ya sasa, Rais wa Zanzibar ni mmoja wa wajumbe wa Baraza la Mawaziri la Serikali ya Jamhuri ya Muungano na kwa hiyo ni mshiriki wa maamuzi yote ya Serikali hiyo. Kwa maana hiyo, maslahi ya Zanzibar yanawakilishwa ndani ya ‘chombo kikuu cha kumshauri Rais’ katika Jamhuri ya Muungano. (ibara ya 54(3) Hii ni licha ya ukweli kwamba, kwa mlolongo wa madaraka uliopo katika ibara ya 54(2), Rais wa Zanzibar sio mmoja wa wajumbe wanaoweza kuongoza mikutano ya Baraza hilo. Aidha, ndani ya Baraza la Mawaziri, Zanzibar inawakilishwa pia na Makamu wa Rais ambaye – kwa mujibu wa ibara ya 47(1) ya Katiba ya sasa – “… ndiye Msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya Muungano….” Kwa maana hiyo, mapendekezo ya Muswada yanayomfanya Rais wa Zanzibar kuwa sio tu mshiriki sawa lakini pia mwamuzi wa mustakbala wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano yanaenda kinyume sio tu na Katiba ya sasa bali pia na Hati za Muungano wenyewe. Kwa mapendekezo haya, endapo Rais wa Zanzibar hatakubaliana na uteuzi wowote wa wajumbe wa Tume au Katibu wake au watendaji wake wengine, anaweza kusimamisha mchakato mzima wa kikatiba hata kama unahusu masuala ya Tanzania Bara yasiyo ya Muungano! UWAKILISHI WA ZANZIBAR Bendera ya Zanzibar (kama inavyotakiwa kuwa). Haitoshi kuwaambia akina Tundu Lisu kwamba huu si mkoa wa Tanganyika? Mheshimiwa Spika, Ushawishi mkubwa wa Zanzibar hauishii katika kura ya turufu aliyo nayo Rais wa Zanzibar pekee yake. Zanzibar ina ushawishi mkubwa vile vile kutokana na nafasi kubwa iliyo nayo katika vyombo vya maamuzi vinavyopendekezwa na Muswada. Kwa mfano, kwa mujibu wa ibara ya 6(2), “… muundo wa Tume utazingatia msingi wa kuwepo kwa uwakilishi ulio sawa kwa kila upande wa Jamhuri ya Muungano.” Hii ina maana kwamba wajumbe wa Tume na Sekretarieti yake wanatakiwa wawe sawa kwa sawa kati ya Tanzania Bara na Zanzibar. Ikumbukwe kwamba Tume hii inatengeneza Katiba inayohusu masuala ya Muungano, ambayo ni haki kwa Zanzibar kushirikishwa kwa usawa kabisa, na vile vile masuala yasiyokuwa ya Muungano ya Tanzania Bara ambayo Zanzibar haina haki ya kushiriki. BUNGE LA KATIBA Mheshimiwa Spika, Eneo la pili ambalo Zanzibar ina ushawishi mkubwa kutokana na uwakilishi wake ni katika Bunge la Katiba linalopendekezwa katika Sehemu ya Tano ya Muswada. Kwa mujibu wa ibara ya 20(2), wajumbe wa Bunge la Katiba watakuwa ni wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano; wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar; mawaziri wa katiba na sheria wa Jamhuri ya Muungano na wa Zanzibar; Wanasheria Wakuu wa Jamhuri ya Muungano na wa Zanzibar; na wajumbe mia moja kumi na sita wakaoteuliwa kutoka asasi zisizokuwa za kiserikali, asasi za kidini, vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, taasisi za elimu ya juu na makundi yenye mahitaji maalum katika jamii. Inaelekea kwamba, kwa mujibu wa ibara ya 20(4), wajumbe wasiokuwa wabunge ama wawakilishi nao pia watateuliwa na Rais licha ya kutoka nje ya mfumo wa kiserikali! Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa ibara ya 66(1)(a) ya Katiba ya sasa ya Muungano, wajumbe wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ni pamoja na wabunge wa majimbo ya uchaguzi. Kwa composition ya sasa ya Bunge, kuna jumla ya majimbo ya uchaguzi 239 ambayo kati yao majimbo ya Zanzibar ni hamsini. Vile vile, kwa mujibu wa ibara ya 66(1)(c) ya Katiba, Baraza la Wawakilishi Zanzibar linawakilishwa na wabunge watano katika Bunge la Jamhuri ya Muungano. Aidha, kama inavyotakiwa na ibara ya 66(1)(b), kuna wabunge wanawake mia moja na mbili wanaojulikana kama ‘wabunge wa viti maalum.’ Kwa mgawanyo wa sasa wa wabunge hawa, idadi ya wanaotoka Zanzibar ni ishirini na tano kwa vyama vyote vyenye uwakilishi bungeni. Na mwisho, kuna wabunge wasiozidi 10 wanaoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa ibara ya 66(1)(e). Hadi sasa, Rais ameshateua wabunge watatu ambao wote ni wa kutoka Zanzibar. Kwa hiyo, katika Bunge la sasa lenye wabunge 353, wabunge wanaowakilisha Zanzibar ni themanini na tatu au karibu 23.5% ya wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano. Kwa mujibu wa Sehemu ya Kwanza ya Sura ya Tano ya Katiba ya Zanzibar, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar ni pamoja na wawakilishi wa majimbo hamsini ya uchaguzi, wawakilishi kumi wa kuteuliwa na Rais wa Zanzibar na wawakilishi ishirini wa viti maalum na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kwa hiyo, jumla ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa sasa ni themanini na moja. Kwa maana nyingine ni kwamba endapo mapendekezo ya ibara ya 20(1)(b), (c) na (d) ya Muswada yatakubaliwa, idadi ya wajumbe wa Bunge la Katiba wanaotoka Zanzibar itaongezeka hadi kufikia mia moja sitini na nne kati ya wajumbe 545 wa Baraza hilo kwa mujibu wa ibara ya 20(2). Idadi hii ni sawa na 30% ya wajumbe wote wa Bunge la Katiba. Idadi hiyo ya uwakilishi wa Zanzibar bado haitakidhi matakwa ya Muswada kwani ibara ya 20(3) inapendekeza kwamba “… idadi ya wajumbe wa Baraza la Katiba kutoka Tanzania Zanzibar … haitapungua theluthi moja ya wajumbe wote wa Bunge la Katiba”! Theluthi moja ya wajumbe wa Bunge la Katiba ni wajumbe 182. Kwa hiyo, ili kukidhi matakwa ya Muswada kuhusu uwakilishi wa Zanzibar, itabidi wajumbe 18 kati ya 116 waliotajwa na ibara ya 20(2)(e) watoke Zanzibar ili kufikisha idadi ya wajumbe 182 ambayo ndio theluthi moja ya wajumbe wote wa Bunge la Katiba. Mheshimiwa Spika, Kuna maeneo mengine ya Muswada ambayo pia yanazua maswali mengi juu ya nafasi ya Zanzibar katika mchakato wa Katiba Mpya. Kwa mfano, wakati ibara ya 21(1) inapendekeza kwamba Spika na Naibu Spika wa Bunge la Katiba wachaguliwe kutoka miongoni mwa wajumbe wa Bunge hilo, ibara ya 21(2) inapendekeza kwamba endapo Spika atatoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano basi Naibu wake lazima atoke upande mwingine. Sambamba na pendekezo hili, ibara ya 22(1) inapendekeza Makatibu wa sasa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar watakuwa ndio Katibu na Naibu Katibu wa Bunge la Katiba. Aidha, sawa na ibara ya 21(2), ibara ya 22(2) inapendekeza kwamba endapo Spika atatoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, basi Katibu wa Bunge la Katiba lazima atoke upande mwingine. Mapendekezo haya yanaonyesha sio tu nafasi na ushawishi mkubwa wa Zanzibar katika mchakato wa Katiba Mpya, bali pia ni mwendelezo wa dhana potofu kwamba Zanzibar ni mshirika sawa wa Jamhuri ya Muungano. Hii inathibitishwa pia na pendekezo la ibara ya 24(3) ya Muswada inayotaka Katiba Mpya ikubaliwe na theluthi mbili ya wajumbe wa Bunge la Katiba wanaotoka Tanzania Bara na vile vile theluthi mbili ya wajumbe wanaotoka Zanzibar. Ni wazi, kwa hiyo, kwamba iwe ni kwa masuala ya Muungano yanayoihusu Zanzibar pia, au kwa masuala yasiyokuwa ya Muungano ya Tanzania Bara ambayo hayaihusu, Zanzibar itakuwa na kura ya turufu kwa mujibu wa mapendekezo ya Muswada huu. Mheshimiwa Spika, Uwakilishi mkubwa wa Zanzibar katika Bunge la Jamhuri ya Muungano umetumika kihistoria kwa lengo la kuwatuliza Wazanzibari wakati Serikali ya Mwalimu Nyerere ilipokuwa inamomonyoa uhuru wa Zanzibar kwa kuongeza orodha ya Mambo ya Muungano kwenye Katiba ya Muungano. Katika kitabu chake Pan Africanism or Pragmatism? Lessons of Tanganyika – Zanzibar Union, Profesa Issa Shivji, mwanazuoni mashuhuri wa kikatiba na mwanafunzi wa historia ya Muungano huu amemnukuu aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar wakati wa utawala wa hayati Sheikh Abedi Amani Karume, Bw. Wolfgang Dourado akimnukuu Sheikh Karume juu ya nafasi ya Zanzibar katika Bunge la Jamhuri ya Muungano: “‘Msiwe na wasi wasi, sisi tuna haki ya kuwakilishwa katika Bunge lao lakini wao hawana haki ya kuwakilishwa katika Baraza letu la Mapinduzi’”! Mheshimiwa Spika, Sababu nyingine inatokana na kuongezeka kwa ushawishi na nafasi ya Zanzibar katika siasa za ndani ya CCM, hasa hasa katika zama hizi za vyama vingi na vita za makundi mbali mbali ndani ya chama hicho. Katika mazingira haya, mtu yeyote anayetaka kupitishwa kuwa mgombea urais kwa kupitia CCM anakuwa anahitaji kura za CCM Zanzibar ili kushinda katika kinyang’anyiro hicho. Kwa kauli ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere mwenyewe katika kitabu chake Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania, “sababu moja kubwa iliyofanya viongozi wetu wasitake kuwaudhi ‘Wazanzibari’ … ni umuhimu wa kura za Zanzibar katika kumteua mwanachama wa CCM kuwa Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano. Kwa kiongozi yeyote anayeliona jambo hilo kuwa ni muhimu kupita mengine yote, kuwaudhi ‘Wazanzibari’ ni dhambi ambayo haina budi iepukwe kwa kila njia.” Kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, hofu hii ya kuwaudhi ‘Wazanzibari’ ndio imepelekea kimya kikuu – ndani ya CCM na ndani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano – juu ya ukiukwaji mkubwa wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano uliofanywa na Sheria ya Mabadiliko ya Kumi ya Katiba ya Zanzibar, 2010. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaamini kwamba upendeleo wa Zanzibar unaopendekezwa katika Muswada huu kuhusiana na uwakilishi katika Bunge la Katiba na katika vyombo vingine vya maamuzi juu ya mchakato wa Katiba Mpya sio wa haki na haukubaliki tena. Kwanza, ibara ya 64(2) ya Katiba ya sasa inaweka wazi kwamba Baraza la Wawakilishi Zanzibar lina mamlaka ya kutunga sheria katika Zanzibar ‘… juu ya mambo yote yasiyo mambo ya Muungano….’ Hii pia ndio lugha ya ibara ya 78(1) ya Katiba ya Zanzibar kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka jana. ‘Katiba ya Tanzania’ ni jambo la kwanza katika orodha ya Mambo ya Muungano iliyoko kwenye Nyongeza ya Kwanza ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano. Kwa Muswada Mpya kupendekeza kwamba Baraza la Wawakilishi Zanzibar liwe sehemu ya Bunge la Katiba ni kukiuka wazi wazi matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano na ya Katiba ya Zanzibar. Ni ajabu iliyoje kwamba wale wanaojifanya ni machampioni wa Muungano wanaweza kunyamazia ukiukaji huu wa Katiba! Mheshimiwa Spika, Thomas Paine, mwandishi maarufu wa Marekani ya wakati wa Mapinduzi ya mwaka 1776, aliwahi kuandika kijitabu alichokiita Common Sense juu ya uhalali wa Uingereza kutawala Bara la Amerika ya Kaskazini ambako alisema: ‘… [T]here is something very absurd in supposing a continent to be perpetually governed by an island [for] in no instance hath nature made the satellite larger than its primary planet…’! Yaani, ni ujinga kudhani kwamba bara linaweza kutawaliwa milele na kisiwa kwa sababu utaratibu wa asili haujawahi kufanya kitegemezi kuwa kikubwa kuliko sayari yake ya msingi. Hata kama ni kweli kwamba Tanganyika sio bara kama ilivyokuwa Marekani ya Kaskazini, bado tunakubaliana na Tom Paine kwamba ni ujinga kudhani kwamba Visiwa vya Zanzibar vitaendelea kuwa na maamuzi na ushawishi mkubwa katika masuala yasiyokuwa ya Muungano ya Tanganyika kwa sababu utaratibu wa asili haujawahi kufanya maslahi ya Visiwa hivyo kuwa bora zaidi ya maslahi ya Tanganyika! Kwa maoni yetu, wakati umefika kwa Muungano kuwekwa kwenye msingi wa usawa na imara zaidi. Msingi huo unahitaji kurudishwa tena kwa Serikali ya Tanganyika ambayo ndio ilikuwa – pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar – mbia mkuu wa Muungano wa mwaka 1964. Kurudishwa huko kwa Tanganyika kutaiwezesha Zanzibar kujadiliana nayo kwa usawa juu ya masuala yote yanayohusu Muungano. Haya yote yanawezekana tu endapo Muungano huu utawekwa mbele ya wananchi ili waamue – kwa kura ya maoni – kama wanataka kuendelea nao au la; na kama wanataka kuendelea nao ni muundo gani wa Muungano wanaoutaka. Mheshimiwa Spika, Mapendekezo ya kurudishwa kwa Tanganyika na Serikali yake sio mapya. Miaka ishirini iliyopita, Tume ya Rais ya Mfumo wa Chama Kimoja au Vyama Vingi vya Siasa (Tume ya Nyalali) ilipendekeza hivyo hivyo. Miaka saba baadae, Tume ya Kukusanya Maoni Juu ya Katiba, White Paper Na. 1 ya 1998 (Tume ya Kisanga) nayo ilipendekeza hivyo hivyo. Kuendelea kupuuza mapendekezo haya wakati Zanzibar inavunja Katiba ya sasa ya Muungano; kuendelea kukaa kimya kwa hofu ya kuwaudhi ‘Wazanzibari’ wakati wao wanajitwalia uhuru wa kujiamulia mambo yao wenyewe huku wakiendelea kushiriki katika maamuzi ya mambo ya Tanganyika yasiyokuwa ya Muungano; kuendeleza kile alichokiita Mwalimu Nyerere falsafa ya ‘changu ni changu, chako ni chetu’ katika mahusiano ya Zanzibar na Tanzania Bara, ni kutulazimisha tuipinge dhana nzima ya Muungano kati ya nchi zetu mbili kitu kinachoweza kupelekea kuvunjika kwa Muungano wenyewe. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni isingependa tufike huko lakini ndoa hii ya kulazimishana haiwezi ikadumu muda mrefu kwa taratibu za aina hii. UDHOOFISHAJI WA UPINZANI Mheshimiwa Spika, Mapendekezo ya Muswada juu ya uwakilishi katika Bunge la Katiba yana athari nyingine kubwa katika majadiliano na maamuzi ndani ya Bunge la Katiba. Kwa mujibu wa uchambuzi uliofanywa na Profesa Issa G. Shivji kwa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, endapo mapendekezo ya ibara ya 20(2) ya Muswada yatapitishwa, CCM itakuwa na kati ya wajumbe 350 hadi 400 katika Bunge la Katiba ambalo lina wajumbe 545. Kwa upande mwingine Chama cha Wananchi (CUF) ambacho kina Wawakilishi 29 katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar kitakuwa na wajumbe 65 katika Bunge la Katiba. Kwa maana ya uwakilishi katika Bunge la Katiba, CUF itakuwa ndio chama cha pili kwa nguvu za kisiasa ndani ya Bunge hilo, licha ya kuwa na wabunge wawili tu wa kuchaguliwa kwa upande wa Tanzania Bara na licha ya kupata kura chache sana katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana. Na kama inavyojulikana, tangu Muafaka wa Kisiasa Zanzibar kati ya CCM na CUF wa mwaka 2010 na kuzaliwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, upinzani wa kisiasa Zanzibar umekufa na kwa upande wa Tanzania Bara, na hasa Bungeni na kwenye chaguzi ndogo kama ule wa Igunga, CUF imekuwa ikishirikiana na CCM kuipinga CHADEMA. Kwa mapendekezo haya, kambi ya CCM na CUF katika Bunge la Katiba inaweza kufika hata zaidi ya wajumbe 465 katika ya wajumbe 545 wa Bunge hilo! CHADEMA ambayo kwa sasa ndio chama kinachoongoza Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kutokana na matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2010, itabakia na Wabunge wake 48 na vyama vya kibunge vilivyobaki, yaani NCCR-Mageuzi, TLP na UDP vitabaki na jumla ya Wabunge sita. Kwa hiyo, CHADEMA itakuwa chama cha tatu kwa nguvu za kisiasa ndani ya Bunge la Katiba licha ya kuwa ni chama kikuu cha upinzani chenye nguvu na ushawishi mkubwa wa kisiasa nchini! Kwa maana nyingine, iwe ni kwa makusudi au bila ya kujua au kwa kunuia, athari mojawapo kubwa ya mapendekezo ya Muswada kuhusu uwakilishi katika Bunge la Katiba itakuwa ni kuiongezea nguvu zaidi kambi ya CCM/CUF na kupunguza nguvu na ushawishi wa CHADEMA ambayo ndio chama pekee kinachobeba matarajio na matamanio ya Watanzania wengi wanaotaka mabadiliko ya kimsingi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii katika nchi yetu. Haihitaji kuwa na shahada ya uzamivu kujua kwamba Bunge la Katiba lenye uwakilishi wa aina hii litapitisha Katiba Mpya ambayo pengine itatofautiana na Katiba ya sasa kwa jina tu! Na wala haihitaji kisomo kikubwa kujua kwamba Bunge la Katiba la aina hii halitagusa ‘msingi mkuu’ uliobaki wa Jamhuri ya Muungano, yaani Serikali mbili. Hapa pia ni wazi kuwa lengo halisi la mapendekezo haya ni kuhakikisha kwamba mchakato wa Katiba Mpya utazaa matunda yasiyokuwa tofauti sana na ya Katiba ya sasa! ‘UWAKILISHI’ WA BUNGE LA KATIBA Mheshimiwa Spika, Sio Bunge hili tukufu la Jamhuri ya Muungano wala Baraza la Wawakilishi Zanzibar lenye mamlaka kikatiba na kisiasa ya kutunga Katiba Mpya ya Tanzania. Hii ni kwa sababu sisi wote tulioko humu ndani tulichaguliwa kwa mujibu wa Katiba ya sasa na mamlaka yetu yote yako ndani ya kona nne za Katiba hiyo. Kama ni kweli, kama anavyodai Profesa Kabudi, kwamba kitendo cha kutunga Katiba Mpya vile vile ni kitendo cha kuua Katiba ya Zamani, basi sisi Wabunge na Wawakilishi wa Zanzibar hatuna mamlaka ya kuiua Katiba ya sasa kwa sababu sisi wote tulikula kiapo cha kuilinda, kuihifandhi na kuitetea. Pili, sisi sote ni Wabunge na Wawakilishi wa vyama vya siasa kwa sababu, kwa mujibu wa Katiba ya sasa sheria zote husika, tumechaguliwa kwa sifa kuu ya kuwa wanachama wa, na tuliopendekezwa na, vyama vya siasa. Kuligeuza Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuwa Bunge la Katiba ni sawa na kusema kwamba wasiokuwa wanachama wa vyama vya siasa hawana haki ya kushiriki katika kutunga Katiba Mpya kwa sababu ya kuwa na kilema cha kisheria kinachowakataza kuchaguliwa kuwa Wabunge na Wawakilishi! Ibara ya 20(4) ya Katiba ya sasa inatamka wazi kwamba “… ni marufuku kwa mtu yeyote kulazimishwa kujiunga na chama chochote….” Sio kosa, kwa hiyo, kwa mamilioni ya Watanzania ambao wameamua kwa hiari zao kutokuwa wanachama wa vyama vya siasa. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haikubaliani, na haiwezi kukubali, ubaguzi wa aina hii dhidi ya Watanzania walioamua kutumia haki zao za kikatiba ya kutokujiunga na chama chochote cha siasa. Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haitakubali Watanzania hao waadhibiwe kwa kunyimwa kushiriki katika Bunge la Katiba kwa sababu tu ya kutokuwa wanachama wa vyama vya siasa. Tatu, wajumbe 116 wanaopendekezwa kuteuliwa kwenye Bunge la Katiba kwa mujibu wa ibara ya 20(2)(e) na (4) ya Muswada Mpya sio, na hawawezi kuwa, wawakilishi wa wananchi. Kwanza, hawajachaguliwa na mtu yeyote na wala taasisi zao kuwawakilisha katika Bunge la Katiba kwa sababu Muswada Mpya unapendekeza wateuliwe na Rais. Pili, Bunge la Katiba ni chombo cha uwakilishi wa moja kwa moja wa wananchi na kwa mila na desturi zinazokubalika na kutumika kimataifa, wajumbe wa Bunge la Katiba huchaguliwa moja kwa moja na wananchi bila ya kujali vyama vya siasa na huwa na kazi moja tu: kutunga Katiba Mpya. Kwa sababu zote hizi, Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza wajumbe wa Bunge la Katiba wachaguliwe moja kwa moja na wananchi na kusiwe na masharti yoyote kuhusu uanachama wa vyama vya siasa. UHALALISHAJI WA KATIBA MPYA Mheshimiwa Spika, Muswada una mapendekezo ambayo yanaashiria kuachana na utaratibu wa kihistoria wa utungaji wa Katiba ambao umewaweka wananchi kando katika michakato wa kikatiba tangu miaka ya mwanzo ya uhuru. Kwa mujibu wa ibara ya 27(1), kutakuwa na kura ya maoni kwa lengo la kuihalalisha Katiba Mpya. Kwa mujibu wa ibara ya 30, watu wote walioandikishwa kuwa wapiga kura kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi ya Taifa na Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar, watakuwa na haki ya kupiga kura katika kura hiyo ya maoni. Aidha, kufuatana na ibara ya 32(2), matokeo ya kura ya maoni yataamuliwa kwa msingi wa kuungwa mkono kwa zaidi ya 50% ya kura zote zilizopigwa Tanzania Bara na kiasi hicho hicho kwa Zanzibar. Mapendekezo ya ushirikishwaji wa wananchi katika kuipa Katiba uhai wa kisheria ni jambo la maana sana na linaonyesha kuwa tumeanza kuachana na urithi wa kikatiba wa kikoloni ulioanza na Katiba ya Uhuru ya mwaka 1961. Hata hivyo, mapendekezo haya yamejaa mitego na vichaka vingi vya hatari. Kwanza, ibara ya 27 inapendekeza kwamba kura ya maoni itaratibiwa na kusimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar. Tume hizi mbili – kwa mashauriano na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar – ndizo zitakazotengeneza swali litakaloulizwa kwenye kura ya maoni. (ibara ya 28(1) na (2) Aidha, kwa mujibu wa ibara ya 31, utaratibu utakaotumika katika kura ya maoni ni ule unaotumika katika chaguzi za kawaida katika nchi yetu, yaani Sheria ya Uchaguzi wa Taifa, Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura ya 292 na Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar.
 
mkuu, hicho ulichoeleza ndo utofauti baina ya chama kama taasisi (ccm) na chama kama kichaka cha wahuni na waliochanganyikiwa (chadema)

Hizo Siasa zenu Ndio mlitaka kuzipeleka kwenye Jumuia ya Afrika Mashariki wakaamua kuwatenga.Kweli CCM ni Janga,Tushirikiane kuitokomeza.
 
Zanzibar na Dr Slaa wapi na wapi?, mbona muda mrefu tu Dr Slaa ameshakataliwa Zanzibar?, nani amemdanganya kuwa Wazanzibar wapo tayari kutoa maoni kwa Dr Slaa?
 
Zanzibar na Dr Slaa wapi na wapi?, mbona muda mrefu tu Dr Slaa ameshakataliwa Zanzibar?, nani amemdanganya kuwa Wazanzibar wapo tayari kutoa maoni kwa Dr Slaa?

Iwapo slaa atapigania maslahi ya zanzbr na kuungana katika harakati za kurejesha mamlaka kamili ya zanzbr na tanganyika basi waznzbr tupo pamoja nae kinyume na hapo aishie huko huko kaskazini.
 
Zanzibar na Dr Slaa wapi na wapi?, mbona muda mrefu tu Dr Slaa ameshakataliwa Zanzibar?, nani amemdanganya kuwa Wazanzibar wapo tayari kutoa maoni kwa Dr Slaa?

ziara ya Slaa zanzibar yatetemesha Lumumba ! Kwi! Kwi! Kwi! Kwi!
 
Hizo Siasa zenu Ndio mlitaka kuzipeleka kwenye Jumuia ya Afrika Mashariki wakaamua kuwatenga.Kweli CCM ni Janga,Tushirikiane kuitokomeza.

Usihofu mkuu farudume , mikakati ya mwanzo kabisa ya cdm baada ya kuikomboa nchi hii ni kuirejesha hadhi yake ndani ya jumuiya ya east africa .
 
mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, mhe. Tundu lissu watembeleaji wa zanzibar daima hapa kuna jambo la kulijadili. Si lazima kukubaliana na kila anachokisema mheshimiwa tundu lissu, lakini maoni haya ya kambi rasmi ya upinzani bungeni (chadema) tuyajadilini. Zanzibar daima inayaona kuwa ni mlango mwengine uliofunguka kwa zanzibar, ambao sio tu unatupa fursa ya kuijua nini chadema inataka kwa nchi, bali pia wapi wazanzibari wanapaswa kujipanga. Tujadiliane baada ya kusoma sehemu hii ya hotuba ya mheshimiwa lissu jana (14.11.2011) bungeni, dodoma. Kwa mfano, lissu analalamika kuwa: "mamlaka ya rais wa zanzibar hayaishii tu kwenye uteuzi wa wajumbe na watendaji wa tume, bali pia yanaingia hata katika uwasilishaji wa ripoti ya tume. Kwa mujibu wa ibara 18(1) ya muswada, mara baada ya kumaliza kazi yake, tume itawasilisha ripoti yake kwa rais na kwa rais wa zanzibar. Aidha, kwa mujibu wa ibara ya 18(2), mara baada ya kupokea ripoti hiyo, rais, ‘baada ya kushauriana na kukubaliana' na rais wa zanzibar, "… atamuagiza waziri kuwasilisha muswada wa katiba katika bunge la katiba." kwa mapendekezo haya pia, rais wa zanzibar sio tu kwamba ana mamlaka karibu sawa na rais wa jamhuri ya muungano bali pia ana kura ya turufu katika mchakato wa katiba mpya. Maana yake ni kwamba rais wa zanzibar asipopatiwa nakala ya ripoti ya tume au asipokubaliana na rais wa muungano, basi muswada wa katiba hautawasilishwa kwenye bunge la katiba!"nafasi ya zanzibar mheshimiwa spika, pengine mabadiliko makubwa yaliyofanywa katika muswada ni mapendekezo yanayohusu nafasi ya zanzibar katika mchakato wa katiba mpya. Itakumbukwa kwamba moja ya masuala yaliyozua tafrani kubwa katika mchakato wa kukusanya maoni juu ya muswada wa zamani hasa katika kituo cha zanzibar ni kuwepo hisia kwamba nafasi ya zanzibar ilikuwa imepuuzwa katika muswada huo. Muswada sio tu kwamba umetekeleza matakwa yote ya ushirikishwaji wa zanzibar, bali umekwenda mbali zaidi kwa kuifanya zanzibar mwamuzi wa mustakbala wote wa kikatiba wa tanzania. Hii imefanyika kwa njia mbili: Kwanza, kwa kumfanya rais wa zanzibar kuwa mshirika sawa wa kikatiba wa rais wa jamhuri ya muungano; na pili, kwa kuipa zanzibar nafasi kubwa ya uwakilishi katika mchakato mzima wa katiba mpya." nafasi ya rais wa zanzibar angalia ramani ya jamhuri ya muungano wa tanzania. Fikiria udogo wa zanzibar ndani ya tanganyika. Je, hili ni moja ya yanayowapa tabu akina tundu lissu? Mheshimiwa spika, muswada unapendekeza kwamba utekelezaji wa mamlaka yote ya rais, waziri na mwanasheria mkuu wa serikali ya jamhuri ya muungano lazima ufanyike kwa ‘mashauriano na makubaliano' na rais, waziri au mwanasheria mkuu wa zanzibar. Kwa mfano, ibara ya 5 inayohusu kuundwa kwa tume inamtaka rais ‘kushauriana na kukubaliana' na rais wa zanzibar na kupata ushauri wa mwanasheria mkuu wa serikali ya jamhuri ya muungano na mwanasheria mkuu wa zanzibar. Vile vile, ibara ya 6(1) inayohusu uteuzi wa wajumbe wa tume; ibara ya 8(1) na (2) inayohusu hadidu za rejea na kuongeza muda wa tume; na ibara ya 13(2) inayohusu uteuzi wa katibu wa tume, zote zinataka kuwepo na makubaliano na rais wa zanzibar. Aidha, ibara ya 13(5) inayohusu uteuzi wa watendaji wengine wa tume inalazimu makubaliano kati ya waziri na waziri mwenzake wa zanzibar ambao nao ni wateuliwa wa rais wa jamhuri ya muungano na rais wa zanzibar. Mamlaka ya rais wa zanzibar hayaishii tu kwenye uteuzi wa wajumbe na watendaji wa tume, bali pia yanaingia hata katika uwasilishaji wa ripoti ya tume. Kwa mujibu wa ibara 18(1) ya muswada, mara baada ya kumaliza kazi yake, tume itawasilisha ripoti yake kwa rais na kwa rais wa zanzibar. Aidha, kwa mujibu wa ibara ya 18(2), mara baada ya kupokea ripoti hiyo, rais, ‘baada ya kushauriana na kukubaliana' na rais wa zanzibar, "… atamuagiza waziri kuwasilisha muswada wa katiba katika bunge la katiba." kwa mapendekezo haya pia, rais wa zanzibar sio tu kwamba ana mamlaka karibu sawa na rais wa jamhuri ya muungano bali pia ana kura ya turufu katika mchakato wa katiba mpya. Maana yake ni kwamba rais wa zanzibar asipopatiwa nakala ya ripoti ya tume au asipokubaliana na rais wa muungano, basi muswada wa katiba hautawasilishwa kwenye bunge la katiba! Mheshimiwa spika, mapendekezo haya yanaashiria kuwepo kwa mtazamo ambao chanzo chake ni makubaliano ya muungano kati ya jamhuri ya watu wa zanzibar na jamhuri ya tanganyika ya tarehe 25 aprili 1964. Kwa mtazamo huo, zanzibar ni nchi huru kama ilivyokuwa mwaka 1964 na kwa hiyo ni lazima sio tu ishirikishwe kwa usawa, bali pia lazima ikubaliane na mabadiliko yoyote ya kikatiba yanayopendekezwa na muswada. Kama profesa palamagamba kabudi wa kitivo cha sheria cha chuo kikuu cha dar es salaam alivyosema kwenye semina ya wabunge juu ya muswada wa sheria ya marekebisho ya katiba iliyofanyika tarehe 12 novemba 2011: ‘katika kuandika katiba mpya, wabia wa muungano wanarudi kwa usawa.' hata hivyo, mheshimiwa spika, mtazamo huu sio sahihi. Kwanza kabisa, zanzibar sio nchi huru tena kama ilivyokuwa mwaka 1964, kama ambavyo hakuna tena nchi inayoitwa tanganyika wala serikali yake. Hii ni kwa sababu tangu kusainiwa kwa hati za muungano mwaka 1964, na kwa mujibu wa ibara ya 4(3) ya katiba ya sasa, masuala yote yanayohusu muungano kama vile katiba ya tanzania yamekasimiwa kwa serikali ya jamhuri ya muungano, ambayo pia imekasimiwa mamlaka juu ya masuala ya iliyokuwa tanganyika. Masuala haya ya muungano hayawezi kujadiliwa upya na kwa usawa kati ya nchi hizi mbili kwa vile moja kati ya nchi hizo haipo tena na iliyobaki imepoteza sehemu ya uhuru wake kutokana na muungano huo! Hii ndio kusema hakuwezi tena kuwa na wabia wa muungano bila kwanza kuirudisha tanganyika kama nchi na bila kuirudisha jamhuri ya watu wa zanzibar yenye uhuru na mamlaka kama iliyokuwa nayo kabla ya muungano! Pili, kuna dhana kwamba rais wa zanzibar hakushirikishwa katika mchakato wa maandalizi ya muswada wa zamani. Dhana hii vile vile ni potofu. Kwanza, rais ali mohamed shein mwenyewe ametamka wazi kwa waandishi wa habari kwamba alishiriki katika hatua zote za maamuzi kwenye baraza la mapinduzi. Pili, kwa mujibu wa ibara ya 54(1) ya katiba ya sasa, rais wa zanzibar ni mmoja wa wajumbe wa baraza la mawaziri la serikali ya jamhuri ya muungano na kwa hiyo ni mshiriki wa maamuzi yote ya serikali hiyo. Kwa maana hiyo, maslahi ya zanzibar yanawakilishwa ndani ya ‘chombo kikuu cha kumshauri rais' katika jamhuri ya muungano. (ibara ya 54(3) hii ni licha ya ukweli kwamba, kwa mlolongo wa madaraka uliopo katika ibara ya 54(2), rais wa zanzibar sio mmoja wa wajumbe wanaoweza kuongoza mikutano ya baraza hilo. Aidha, ndani ya baraza la mawaziri, zanzibar inawakilishwa pia na makamu wa rais ambaye – kwa mujibu wa ibara ya 47(1) ya katiba ya sasa – "… ndiye msaidizi mkuu wa rais kuhusu mambo yote ya jamhuri ya muungano…." kwa maana hiyo, mapendekezo ya muswada yanayomfanya rais wa zanzibar kuwa sio tu mshiriki sawa lakini pia mwamuzi wa mustakbala wa katiba ya jamhuri ya muungano yanaenda kinyume sio tu na katiba ya sasa bali pia na hati za muungano wenyewe. Kwa mapendekezo haya, endapo rais wa zanzibar hatakubaliana na uteuzi wowote wa wajumbe wa tume au katibu wake au watendaji wake wengine, anaweza kusimamisha mchakato mzima wa kikatiba hata kama unahusu masuala ya tanzania bara yasiyo ya muungano! uwakilishi wa zanzibar bendera ya zanzibar (kama inavyotakiwa kuwa). Haitoshi kuwaambia akina tundu lisu kwamba huu si mkoa wa tanganyika? Mheshimiwa spika, ushawishi mkubwa wa zanzibar hauishii katika kura ya turufu aliyo nayo rais wa zanzibar pekee yake. Zanzibar ina ushawishi mkubwa vile vile kutokana na nafasi kubwa iliyo nayo katika vyombo vya maamuzi vinavyopendekezwa na muswada. Kwa mfano, kwa mujibu wa ibara ya 6(2), "… muundo wa tume utazingatia msingi wa kuwepo kwa uwakilishi ulio sawa kwa kila upande wa jamhuri ya muungano." hii ina maana kwamba wajumbe wa tume na sekretarieti yake wanatakiwa wawe sawa kwa sawa kati ya tanzania bara na zanzibar. Ikumbukwe kwamba tume hii inatengeneza katiba inayohusu masuala ya muungano, ambayo ni haki kwa zanzibar kushirikishwa kwa usawa kabisa, na vile vile masuala yasiyokuwa ya muungano ya tanzania bara ambayo zanzibar haina haki ya kushiriki. bunge la katiba mheshimiwa spika, eneo la pili ambalo zanzibar ina ushawishi mkubwa kutokana na uwakilishi wake ni katika bunge la katiba linalopendekezwa katika sehemu ya tano ya muswada. Kwa mujibu wa ibara ya 20(2), wajumbe wa bunge la katiba watakuwa ni wabunge wote wa bunge la jamhuri ya muungano; wajumbe wote wa baraza la wawakilishi zanzibar; mawaziri wa katiba na sheria wa jamhuri ya muungano na wa zanzibar; wanasheria wakuu wa jamhuri ya muungano na wa zanzibar; na wajumbe mia moja kumi na sita wakaoteuliwa kutoka asasi zisizokuwa za kiserikali, asasi za kidini, vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, taasisi za elimu ya juu na makundi yenye mahitaji maalum katika jamii. Inaelekea kwamba, kwa mujibu wa ibara ya 20(4), wajumbe wasiokuwa wabunge ama wawakilishi nao pia watateuliwa na rais licha ya kutoka nje ya mfumo wa kiserikali! Mheshimiwa spika, kwa mujibu wa ibara ya 66(1)(a) ya katiba ya sasa ya muungano, wajumbe wa bunge la jamhuri ya muungano ni pamoja na wabunge wa majimbo ya uchaguzi. Kwa composition ya sasa ya bunge, kuna jumla ya majimbo ya uchaguzi 239 ambayo kati yao majimbo ya zanzibar ni hamsini. Vile vile, kwa mujibu wa ibara ya 66(1)(c) ya katiba, baraza la wawakilishi zanzibar linawakilishwa na wabunge watano katika bunge la jamhuri ya muungano. Aidha, kama inavyotakiwa na ibara ya 66(1)(b), kuna wabunge wanawake mia moja na mbili wanaojulikana kama ‘wabunge wa viti maalum.' kwa mgawanyo wa sasa wa wabunge hawa, idadi ya wanaotoka zanzibar ni ishirini na tano kwa vyama vyote vyenye uwakilishi bungeni. Na mwisho, kuna wabunge wasiozidi 10 wanaoteuliwa na rais wa jamhuri ya muungano kwa mujibu wa ibara ya 66(1)(e). Hadi sasa, rais ameshateua wabunge watatu ambao wote ni wa kutoka zanzibar. Kwa hiyo, katika bunge la sasa lenye wabunge 353, wabunge wanaowakilisha zanzibar ni themanini na tatu au karibu 23.5% ya wabunge wote wa bunge la jamhuri ya muungano. Kwa mujibu wa sehemu ya kwanza ya sura ya tano ya katiba ya zanzibar, wajumbe wa baraza la wawakilishi zanzibar ni pamoja na wawakilishi wa majimbo hamsini ya uchaguzi, wawakilishi kumi wa kuteuliwa na rais wa zanzibar na wawakilishi ishirini wa viti maalum na mwanasheria mkuu wa serikali ya mapinduzi ya zanzibar. Kwa hiyo, jumla ya wajumbe wa baraza la wawakilishi kwa sasa ni themanini na moja. Kwa maana nyingine ni kwamba endapo mapendekezo ya ibara ya 20(1)(b), (c) na (d) ya muswada yatakubaliwa, idadi ya wajumbe wa bunge la katiba wanaotoka zanzibar itaongezeka hadi kufikia mia moja sitini na nne kati ya wajumbe 545 wa baraza hilo kwa mujibu wa ibara ya 20(2). Idadi hii ni sawa na 30% ya wajumbe wote wa bunge la katiba. Idadi hiyo ya uwakilishi wa zanzibar bado haitakidhi matakwa ya muswada kwani ibara ya 20(3) inapendekeza kwamba "… idadi ya wajumbe wa baraza la katiba kutoka tanzania zanzibar … haitapungua theluthi moja ya wajumbe wote wa bunge la katiba"! Theluthi moja ya wajumbe wa bunge la katiba ni wajumbe 182. Kwa hiyo, ili kukidhi matakwa ya muswada kuhusu uwakilishi wa zanzibar, itabidi wajumbe 18 kati ya 116 waliotajwa na ibara ya 20(2)(e) watoke zanzibar ili kufikisha idadi ya wajumbe 182 ambayo ndio theluthi moja ya wajumbe wote wa bunge la katiba. Mheshimiwa spika, kuna maeneo mengine ya muswada ambayo pia yanazua maswali mengi juu ya nafasi ya zanzibar katika mchakato wa katiba mpya. Kwa mfano, wakati ibara ya 21(1) inapendekeza kwamba spika na naibu spika wa bunge la katiba wachaguliwe kutoka miongoni mwa wajumbe wa bunge hilo, ibara ya 21(2) inapendekeza kwamba endapo spika atatoka upande mmoja wa jamhuri ya muungano basi naibu wake lazima atoke upande mwingine. Sambamba na pendekezo hili, ibara ya 22(1) inapendekeza makatibu wa sasa wa bunge la jamhuri ya muungano na wa baraza la wawakilishi zanzibar watakuwa ndio katibu na naibu katibu wa bunge la katiba. Aidha, sawa na ibara ya 21(2), ibara ya 22(2) inapendekeza kwamba endapo spika atatoka upande mmoja wa jamhuri ya muungano, basi katibu wa bunge la katiba lazima atoke upande mwingine. Mapendekezo haya yanaonyesha sio tu nafasi na ushawishi mkubwa wa zanzibar katika mchakato wa katiba mpya, bali pia ni mwendelezo wa dhana potofu kwamba zanzibar ni mshirika sawa wa jamhuri ya muungano. Hii inathibitishwa pia na pendekezo la ibara ya 24(3) ya muswada inayotaka katiba mpya ikubaliwe na theluthi mbili ya wajumbe wa bunge la katiba wanaotoka tanzania bara na vile vile theluthi mbili ya wajumbe wanaotoka zanzibar. Ni wazi, kwa hiyo, kwamba iwe ni kwa masuala ya muungano yanayoihusu zanzibar pia, au kwa masuala yasiyokuwa ya muungano ya tanzania bara ambayo hayaihusu, zanzibar itakuwa na kura ya turufu kwa mujibu wa mapendekezo ya muswada huu. Mheshimiwa spika, uwakilishi mkubwa wa zanzibar katika bunge la jamhuri ya muungano umetumika kihistoria kwa lengo la kuwatuliza wazanzibari wakati serikali ya mwalimu nyerere ilipokuwa inamomonyoa uhuru wa zanzibar kwa kuongeza orodha ya mambo ya muungano kwenye katiba ya muungano. Katika kitabu chake pan africanism or pragmatism? Lessons of tanganyika – zanzibar union, profesa issa shivji, mwanazuoni mashuhuri wa kikatiba na mwanafunzi wa historia ya muungano huu amemnukuu aliyekuwa mwanasheria mkuu wa zanzibar wakati wa utawala wa hayati sheikh abedi amani karume, bw. Wolfgang dourado akimnukuu sheikh karume juu ya nafasi ya zanzibar katika bunge la jamhuri ya muungano: "‘msiwe na wasi wasi, sisi tuna haki ya kuwakilishwa katika bunge lao lakini wao hawana haki ya kuwakilishwa katika baraza letu la mapinduzi'"! Mheshimiwa spika, sababu nyingine inatokana na kuongezeka kwa ushawishi na nafasi ya zanzibar katika siasa za ndani ya ccm, hasa hasa katika zama hizi za vyama vingi na vita za makundi mbali mbali ndani ya chama hicho. Katika mazingira haya, mtu yeyote anayetaka kupitishwa kuwa mgombea urais kwa kupitia ccm anakuwa anahitaji kura za ccm zanzibar ili kushinda katika kinyang'anyiro hicho. Kwa kauli ya baba wa taifa, mwalimu nyerere mwenyewe katika kitabu chake uongozi wetu na hatima ya tanzania, "sababu moja kubwa iliyofanya viongozi wetu wasitake kuwaudhi ‘wazanzibari' … ni umuhimu wa kura za zanzibar katika kumteua mwanachama wa ccm kuwa mgombea wa urais wa jamhuri ya muungano. Kwa kiongozi yeyote anayeliona jambo hilo kuwa ni muhimu kupita mengine yote, kuwaudhi ‘wazanzibari' ni dhambi ambayo haina budi iepukwe kwa kila njia." kwa maoni ya kambi rasmi ya upinzani bungeni, hofu hii ya kuwaudhi ‘wazanzibari' ndio imepelekea kimya kikuu – ndani ya ccm na ndani ya serikali ya jamhuri ya muungano – juu ya ukiukwaji mkubwa wa katiba ya jamhuri ya muungano uliofanywa na sheria ya mabadiliko ya kumi ya katiba ya zanzibar, 2010. Kambi rasmi ya upinzani bungeni inaamini kwamba upendeleo wa zanzibar unaopendekezwa katika muswada huu kuhusiana na uwakilishi katika bunge la katiba na katika vyombo vingine vya maamuzi juu ya mchakato wa katiba mpya sio wa haki na haukubaliki tena. Kwanza, ibara ya 64(2) ya katiba ya sasa inaweka wazi kwamba baraza la wawakilishi zanzibar lina mamlaka ya kutunga sheria katika zanzibar '… juu ya mambo yote yasiyo mambo ya muungano….' hii pia ndio lugha ya ibara ya 78(1) ya katiba ya zanzibar kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka jana. ‘katiba ya tanzania' ni jambo la kwanza katika orodha ya mambo ya muungano iliyoko kwenye nyongeza ya kwanza ya katiba ya jamhuri ya muungano. Kwa muswada mpya kupendekeza kwamba baraza la wawakilishi zanzibar liwe sehemu ya bunge la katiba ni kukiuka wazi wazi matakwa ya katiba ya jamhuri ya muungano na ya katiba ya zanzibar. Ni ajabu iliyoje kwamba wale wanaojifanya ni machampioni wa muungano wanaweza kunyamazia ukiukaji huu wa katiba! Mheshimiwa spika, thomas paine, mwandishi maarufu wa marekani ya wakati wa mapinduzi ya mwaka 1776, aliwahi kuandika kijitabu alichokiita common sense juu ya uhalali wa uingereza kutawala bara la amerika ya kaskazini ambako alisema: '… [t]here is something very absurd in supposing a continent to be perpetually governed by an island [for] in no instance hath nature made the satellite larger than its primary planet…'! Yaani, ni ujinga kudhani kwamba bara linaweza kutawaliwa milele na kisiwa kwa sababu utaratibu wa asili haujawahi kufanya kitegemezi kuwa kikubwa kuliko sayari yake ya msingi. Hata kama ni kweli kwamba tanganyika sio bara kama ilivyokuwa marekani ya kaskazini, bado tunakubaliana na tom paine kwamba ni ujinga kudhani kwamba visiwa vya zanzibar vitaendelea kuwa na maamuzi na ushawishi mkubwa katika masuala yasiyokuwa ya muungano ya tanganyika kwa sababu utaratibu wa asili haujawahi kufanya maslahi ya visiwa hivyo kuwa bora zaidi ya maslahi ya tanganyika! Kwa maoni yetu, wakati umefika kwa muungano kuwekwa kwenye msingi wa usawa na imara zaidi. Msingi huo unahitaji kurudishwa tena kwa serikali ya tanganyika ambayo ndio ilikuwa – pamoja na serikali ya mapinduzi ya zanzibar – mbia mkuu wa muungano wa mwaka 1964. Kurudishwa huko kwa tanganyika kutaiwezesha zanzibar kujadiliana nayo kwa usawa juu ya masuala yote yanayohusu muungano. Haya yote yanawezekana tu endapo muungano huu utawekwa mbele ya wananchi ili waamue – kwa kura ya maoni – kama wanataka kuendelea nao au la; na kama wanataka kuendelea nao ni muundo gani wa muungano wanaoutaka. Mheshimiwa spika, mapendekezo ya kurudishwa kwa tanganyika na serikali yake sio mapya. Miaka ishirini iliyopita, tume ya rais ya mfumo wa chama kimoja au vyama vingi vya siasa (tume ya nyalali) ilipendekeza hivyo hivyo. Miaka saba baadae, tume ya kukusanya maoni juu ya katiba, white paper na. 1 ya 1998 (tume ya kisanga) nayo ilipendekeza hivyo hivyo. Kuendelea kupuuza mapendekezo haya wakati zanzibar inavunja katiba ya sasa ya muungano; kuendelea kukaa kimya kwa hofu ya kuwaudhi ‘wazanzibari' wakati wao wanajitwalia uhuru wa kujiamulia mambo yao wenyewe huku wakiendelea kushiriki katika maamuzi ya mambo ya tanganyika yasiyokuwa ya muungano; kuendeleza kile alichokiita mwalimu nyerere falsafa ya ‘changu ni changu, chako ni chetu' katika mahusiano ya zanzibar na tanzania bara, ni kutulazimisha tuipinge dhana nzima ya muungano kati ya nchi zetu mbili kitu kinachoweza kupelekea kuvunjika kwa muungano wenyewe. Kambi rasmi ya upinzani bungeni isingependa tufike huko lakini ndoa hii ya kulazimishana haiwezi ikadumu muda mrefu kwa taratibu za aina hii. udhoofishaji wa upinzani mheshimiwa spika, mapendekezo ya muswada juu ya uwakilishi katika bunge la katiba yana athari nyingine kubwa katika majadiliano na maamuzi ndani ya bunge la katiba. Kwa mujibu wa uchambuzi uliofanywa na profesa issa g. Shivji kwa kamati ya katiba, sheria na utawala, endapo mapendekezo ya ibara ya 20(2) ya muswada yatapitishwa, ccm itakuwa na kati ya wajumbe 350 hadi 400 katika bunge la katiba ambalo lina wajumbe 545. Kwa upande mwingine chama cha wananchi (cuf) ambacho kina wawakilishi 29 katika baraza la wawakilishi zanzibar kitakuwa na wajumbe 65 katika bunge la katiba. Kwa maana ya uwakilishi katika bunge la katiba, cuf itakuwa ndio chama cha pili kwa nguvu za kisiasa ndani ya bunge hilo, licha ya kuwa na wabunge wawili tu wa kuchaguliwa kwa upande wa tanzania bara na licha ya kupata kura chache sana katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana. Na kama inavyojulikana, tangu muafaka wa kisiasa zanzibar kati ya ccm na cuf wa mwaka 2010 na kuzaliwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa, upinzani wa kisiasa zanzibar umekufa na kwa upande wa tanzania bara, na hasa bungeni na kwenye chaguzi ndogo kama ule wa igunga, cuf imekuwa ikishirikiana na ccm kuipinga chadema. Kwa mapendekezo haya, kambi ya ccm na cuf katika bunge la katiba inaweza kufika hata zaidi ya wajumbe 465 katika ya wajumbe 545 wa bunge hilo! Chadema ambayo kwa sasa ndio chama kinachoongoza kambi rasmi ya upinzani bungeni kutokana na matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2010, itabakia na wabunge wake 48 na vyama vya kibunge vilivyobaki, yaani nccr-mageuzi, tlp na udp vitabaki na jumla ya wabunge sita. Kwa hiyo, chadema itakuwa chama cha tatu kwa nguvu za kisiasa ndani ya bunge la katiba licha ya kuwa ni chama kikuu cha upinzani chenye nguvu na ushawishi mkubwa wa kisiasa nchini! Kwa maana nyingine, iwe ni kwa makusudi au bila ya kujua au kwa kunuia, athari mojawapo kubwa ya mapendekezo ya muswada kuhusu uwakilishi katika bunge la katiba itakuwa ni kuiongezea nguvu zaidi kambi ya ccm/cuf na kupunguza nguvu na ushawishi wa chadema ambayo ndio chama pekee kinachobeba matarajio na matamanio ya watanzania wengi wanaotaka mabadiliko ya kimsingi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii katika nchi yetu. Haihitaji kuwa na shahada ya uzamivu kujua kwamba bunge la katiba lenye uwakilishi wa aina hii litapitisha katiba mpya ambayo pengine itatofautiana na katiba ya sasa kwa jina tu! Na wala haihitaji kisomo kikubwa kujua kwamba bunge la katiba la aina hii halitagusa ‘msingi mkuu' uliobaki wa jamhuri ya muungano, yaani serikali mbili. Hapa pia ni wazi kuwa lengo halisi la mapendekezo haya ni kuhakikisha kwamba mchakato wa katiba mpya utazaa matunda yasiyokuwa tofauti sana na ya katiba ya sasa! ‘uwakilishi' wa bunge la katiba mheshimiwa spika, sio bunge hili tukufu la jamhuri ya muungano wala baraza la wawakilishi zanzibar lenye mamlaka kikatiba na kisiasa ya kutunga katiba mpya ya tanzania. Hii ni kwa sababu sisi wote tulioko humu ndani tulichaguliwa kwa mujibu wa katiba ya sasa na mamlaka yetu yote yako ndani ya kona nne za katiba hiyo. Kama ni kweli, kama anavyodai profesa kabudi, kwamba kitendo cha kutunga katiba mpya vile vile ni kitendo cha kuua katiba ya zamani, basi sisi wabunge na wawakilishi wa zanzibar hatuna mamlaka ya kuiua katiba ya sasa kwa sababu sisi wote tulikula kiapo cha kuilinda, kuihifandhi na kuitetea. Pili, sisi sote ni wabunge na wawakilishi wa vyama vya siasa kwa sababu, kwa mujibu wa katiba ya sasa sheria zote husika, tumechaguliwa kwa sifa kuu ya kuwa wanachama wa, na tuliopendekezwa na, vyama vya siasa. Kuligeuza bunge la jamhuri ya muungano na baraza la wawakilishi zanzibar kuwa bunge la katiba ni sawa na kusema kwamba wasiokuwa wanachama wa vyama vya siasa hawana haki ya kushiriki katika kutunga katiba mpya kwa sababu ya kuwa na kilema cha kisheria kinachowakataza kuchaguliwa kuwa wabunge na wawakilishi! Ibara ya 20(4) ya katiba ya sasa inatamka wazi kwamba "… ni marufuku kwa mtu yeyote kulazimishwa kujiunga na chama chochote…." sio kosa, kwa hiyo, kwa mamilioni ya watanzania ambao wameamua kwa hiari zao kutokuwa wanachama wa vyama vya siasa. Kambi rasmi ya upinzani bungeni haikubaliani, na haiwezi kukubali, ubaguzi wa aina hii dhidi ya watanzania walioamua kutumia haki zao za kikatiba ya kutokujiunga na chama chochote cha siasa. Aidha, kambi rasmi ya upinzani bungeni haitakubali watanzania hao waadhibiwe kwa kunyimwa kushiriki katika bunge la katiba kwa sababu tu ya kutokuwa wanachama wa vyama vya siasa. Tatu, wajumbe 116 wanaopendekezwa kuteuliwa kwenye bunge la katiba kwa mujibu wa ibara ya 20(2)(e) na (4) ya muswada mpya sio, na hawawezi kuwa, wawakilishi wa wananchi. Kwanza, hawajachaguliwa na mtu yeyote na wala taasisi zao kuwawakilisha katika bunge la katiba kwa sababu muswada mpya unapendekeza wateuliwe na rais. Pili, bunge la katiba ni chombo cha uwakilishi wa moja kwa moja wa wananchi na kwa mila na desturi zinazokubalika na kutumika kimataifa, wajumbe wa bunge la katiba huchaguliwa moja kwa moja na wananchi bila ya kujali vyama vya siasa na huwa na kazi moja tu: Kutunga katiba mpya. Kwa sababu zote hizi, mheshimiwa spika, kambi rasmi ya upinzani bungeni inapendekeza wajumbe wa bunge la katiba wachaguliwe moja kwa moja na wananchi na kusiwe na masharti yoyote kuhusu uanachama wa vyama vya siasa. uhalalishaji wa katiba mpya mheshimiwa spika, muswada una mapendekezo ambayo yanaashiria kuachana na utaratibu wa kihistoria wa utungaji wa katiba ambao umewaweka wananchi kando katika michakato wa kikatiba tangu miaka ya mwanzo ya uhuru. Kwa mujibu wa ibara ya 27(1), kutakuwa na kura ya maoni kwa lengo la kuihalalisha katiba mpya. Kwa mujibu wa ibara ya 30, watu wote walioandikishwa kuwa wapiga kura kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi ya taifa na sheria ya uchaguzi ya zanzibar, watakuwa na haki ya kupiga kura katika kura hiyo ya maoni. Aidha, kufuatana na ibara ya 32(2), matokeo ya kura ya maoni yataamuliwa kwa msingi wa kuungwa mkono kwa zaidi ya 50% ya kura zote zilizopigwa tanzania bara na kiasi hicho hicho kwa zanzibar. Mapendekezo ya ushirikishwaji wa wananchi katika kuipa katiba uhai wa kisheria ni jambo la maana sana na linaonyesha kuwa tumeanza kuachana na urithi wa kikatiba wa kikoloni ulioanza na katiba ya uhuru ya mwaka 1961. Hata hivyo, mapendekezo haya yamejaa mitego na vichaka vingi vya hatari. Kwanza, ibara ya 27 inapendekeza kwamba kura ya maoni itaratibiwa na kusimamiwa na tume ya taifa ya uchaguzi kwa kushirikiana na tume ya uchaguzi ya zanzibar. Tume hizi mbili – kwa mashauriano na mwanasheria mkuu wa serikali ya jamhuri ya muungano na mwanasheria mkuu wa zanzibar – ndizo zitakazotengeneza swali litakaloulizwa kwenye kura ya maoni. (ibara ya 28(1) na (2) aidha, kwa mujibu wa ibara ya 31, utaratibu utakaotumika katika kura ya maoni ni ule unaotumika katika chaguzi za kawaida katika nchi yetu, yaani sheria ya uchaguzi wa taifa, sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa, sura ya 292 na sheria ya uchaguzi ya zanzibar.
hi risala utaisoma mwenyewe kwani haina mantiki ni kiporo.
 
Chadema wana mawazo mazuri sana ya kuirejeshea zanzibar mamlaka kamili, wazanzibar kama wanaipenda nchi yao sharti waunge mkono jitihada zinaendeshwa na chama hiki, vinginevyo....
 
wanamplekea wakati tume imeshasema hawapokei. ulaji tu wa pesa za wananchi
mkuu, nimepita kwenye
chadema blog nikakuta post yao kuwa watapeleka maoni yao kwa lori kwa
vile ni mengi. baada ya kutafakari sana nikagundua kuwa chadema hawana
wachambuzi kama walivyofanya ccm. pia chadema wamehangaika na idadi
badala ya kuangalia vipengele vya rasimu ya katiba
 
mkuu, hicho ulichoeleza ndo utofauti baina ya chama kama taasisi (ccm) na chama kama kichaka cha wahuni na waliochanganyikiwa (chadema)

Je, umewahi kuona picha ya Julius K Nyerere akiwa na sare za chama chenu? Jiulize kwa nini?
 
Lizabon sijui kama akili yako iko sawa labda imejaa matope jaribu kuandika kama mtu walau uliyeliona hata lile saba au ulikula ziro kuanzia la kwanza hadi hapo ulipo.

Halafu kwa utumbo unaoandikwa na watu wa design yake wameonekana wamerusha post nyingi JF. Kuliko kuwa na post za watu kama hawa ni bora usiandike hata moja.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Dr. Alas karibu Zanzibar na tafadhali wasikilize Wa-Zanzibari kilio chao
 
Back
Top Bottom