Mbokaleo,
Huwa nawashangaa kutoa kauli hizi za jumble jumla, unayasema hayo ukimwakilisha nani? Umewakuta wapi hao unaowawekea maneno mdomoni?
Nimefika Chakechake. Nimefanya mkutano wa ndani wa Takriban watu 300, tena wakiwemo wa CUF. Hizi ni kauli hatari sana Watanzania ni lazima kuepukana na watu wa aina hii wanaojenga chuki miongoni mwa jamii. Inawezekana kwa upeo wake mdogo haelewi madhara. Watanzania kwa miaka 50 wamechanganyika sana. Wanashirikiana misiba na sherehe, watoto wanasoma shule mmoja na wanakaa dawati mmoja. Ni mtu asiyefikiri madhara yag kaulinyake tu anaweza kutamka maneno haya. Ni mmomonyoko mkubwa na wa kutisha wa maadili na ustaarabu wa ki Tanzania.
Nimepokelewa Chakechake kwa furaha na vifijo tangia uwanja wa ndege wa Chakechake, sikuona ubaguzni wowote. Nimekutana uwanjani na Baba yangu. Mhe. Salim Ahmed Salim na kusalimiana naye kwa upendo mkubwa. Wapemba wengi, kwa maana hiyo waislamu wengi tu baada ya mkutano wameomba kupiga picha namimi na hizo picha watabaki nano Kama kumbukumbu zao na watakuwa nazi ndani ya nyumba zao, tumekula chakula pamoja, nimechumiwa "Mabungo" na kutengenezewa juice, himeletewa " halua". Sasa ndugu yangu unamwakilisha nani? Au unafikiri watagnzania ni mazezeta! Maneno yako ni matusi si kwangu, Mimi nimeyazoea lakini kwa wazanzibari na Watanzania. Fikiria, tafakari, chunguza dhamira yako, chuki yako binafsi usipende kuwapandikizia wengine. Madhara yatakapotokea, hakuna atakayebaki hata wewe mwenyewe, ndugu zako na watoto wako! Nawashukuru sana wananchi waliojitokeza kwa hiari Yao, bila kubebwa, kulipwa posho Bali walijua kutimiza wajibu wao.
QUOTE=mbokaleo;7207139]Mwambieni huyo slaa!
Mfumo kristo aupeleke huko bara!
Huku visiwani hawataki kabisa!
Halafu wana hasira sana na waparokia! Bora arudi tu akahubiri huko arusha!
[/QUOTE]
[MENTION=50976]Dr. W. Slaa. Maneno yako ni matamu sana kama ya wana siasa wengi hapa nchini!
Lkn wanasema waswahili" maneno matupu bila vitendo yamekufa"
Leo hii tumeyashuhudia matukio ya killa namna yanayohusu kuwahujumu waislamu hapa nchini! Ccm imekuwa ikishirikiana na hao wanaojiita wawakilishi wa waislamu kukandamiza zaidi waislamu na haki zao! Na yoote hayo mnayaona wazi! Lkn hakuna anae yaongelea hayo, sababu?? Mtasema hayawahusu!
Mfano, Suala la waislamu kutaka kadhi mkuu Tanzania, japo kuwa ni suala ambalo haliwahusu wala kuwaingilia wasio kuwa waislamu, limepingwa vikali na viongozi mbali mbali nchini!
Tena baadhi yao kwa kukosa haya wala aibu, wanakwenda kuliongelea hili suala ndani ya makanisa (refer to Mary Nagu speech)!
Juzi juzi hapa yametokea matukio ya waislamu kupigwa risasi na askari wa chama tawala! Hatukuona cha maana chochote kutoka kwenye chama chako au wanachama wako au kwako wewe binafsi kulikemea hili suala,!!
it was just a minimum or almost nothing from your side!!
Why?! Au kwa sababu 90% ya wasio kuwa waislamu kusema kuwa shehe ponda ni gaidi??
Au humesahau ile kauli ya wahenga inayosema" ukitaka kuwa mbaya basi dai chako"? Na ndicho shehe ponda alichokuwa anadai! Na haki yake kama mwananchi na muislamu!!
Lakini on the other hand, tukio ovu likitokea kwa kiongozi au muumini wa KANISA! Nyie ndio mnakuwa wa kwanza kwenye vyombo vya habari kukemea vikali na kutoa maonyo mbalimbali!
Mkuki kwa nguruwe kwa binaadamu mchungu!"
Kwa muumini yyt duniani suala la imani yake kiini cha maisha yake!
Kusema kwenu kuwa waislamu ni wenzenu! Mnakula nao. Mkafurahi nao n.k halafu mkakaa kimya kwenye key issues km hizi.lkn inapokuja tokea issue ya wasio waislamu!! Tunakuoneni ktk killa chombo cha habari!! ni kutuletea yale ya nyerere!
Mnawapaka waislamu mafuta kwa mgongo wa chupa!
Watu wamechoka na maneno bila vitendo! Na ni wajibu wako wewe km kiongozi wa chama cha siasa kuonyesha wazi wananchi wote kuwa wewe ni kiongozi wa vitendo na sio domokrasi peke yake.
Na mimi sina nia ya kuleta chuki km unavyodai bali kusema ukweli ni kipengele cha sheria ktk imani yangu!!
Na kama kuna muislamu anapingana na hoja zangu hapo juu! Naomba anikosoe hapa.
Mungu ibariki nchi yangu Tanzania.