Ndugu wana Jamavi, Sina shaka habari za Iramba zimetawala sana jamvi jioni hii. Hata hivyo, sakata hili limechukua sura mpya baada ya vijana 11 wa Chama Cha Mapinduzi wilayani hapa kuja na malalamiko mazito ya kudaiwa kurudisha fedha walizopewa kwa nyakati tofauti ili kuhamasisha ushiriki kwenye mechi ya Simba leo jioni. Vijana hao wamewasilisha maelezo yao kwa mwenyekiti wa CCM wilaya, maelezo ambayo amepatiwa pia kiongozi mmoja wa CHADEMA hapa Kiomboi, na wanajiandaa pia kuyatoa kwenye media. Akizungumza mmojawapo kati ya vijana hao anayejulikana kwa jina la Laurent Kiula amesema; "Tuliitwa siku ya jumanne na aliekuwa mgombea wa Mkutano mkuu wa taifa bwana Daudi Amosi Madelu aliekuwa pamoja na aliewahi kuwa mwenyekiti wa Urughu, Simon Tyosela. Katika kikao hicho, Madelu alitupa kazi ya kuhamasisha mtaa hadi mtaa watu wahudhurie mechi ya Simba jumamosi (leo) badala ya mkutano wa wapinzani wetu CHADEMA na akatuahidi angetupa fedha ya kulifanikisha hilo. Alituomba tuwe 10, lakini baadae alituongezea dada mmoja kutoka Arusha tukawa 11. Siku ya Alhamisi, Madelu alituomba tukutane J.L.C Club iliyo nyuma ya ofic za CCM wilaya na akatuomba feedback. Tulimpa strategies zetu na akatutambulisha kwa dada huyo kutoka Arusha aitwae Scholastika, ambae ndie angekuwa master planner wetu. Alitupa Laki 3 kwa ajili ya mafuta, mabango na T'shirt, ingawa tulimwambia zisingetosha, na Tyosela alituongezea elfu 80. Madelu aliahidi kutupa zingine Ijumaa saa 4 asubuhi pamoja na posho zetu. Jioni ya Ijumaa, Tyosela alituomba tumpelekee T'shirt kadhaa kama ziko tayari, lakini tulimwambia kuwa tumecancel wazo la T'shirt kwa kuwa muda ulikuwa umeisha. Jumamosi asubuhi Madelu alituita Kisiriri Guest haraka. Tukiwa tunaendelea kujadiliana, alipigiwa simu na Mbunge ambae alimpa taarifa kuwa CHADEMA wanaanza mkutano sa kumi, hivyo tujipange vizuri na hapo ndipo tukajua kua mbunge ana taarifa. Cha ajabu, majira ya saa sita mchana, tulisikia matangazo kuwa mkutano wa CHADEMA unaanza saa 7 mchana!! Tulipompigia Mbunge, hakuwa anapatikana na ya Madelu hakuwa anapokea. Ilipofika saa 7, watu wengi walianza kufurika uwanjani kwenye mkutano wa CDM. Kilichonishangaza, mida ya saa 12 jioni tumeitwa na Tyosela na Madelu wakitutuhumu kuwa tulikuwa tunawasiliana na Kitila Mkumbo na viongozi wa BAVICHA Mkoa na wa wilaya ya Singida mjini na kuwavujishia mpango huu huku wakiwa hawana kithibitisho chochote. Cha ajabu zaidi, tumepewa muda hadi kesho turudishe fedha zote kwao la sivyo tutavuliwa uanachama. Yule dada aliekuwa anatusimamia (Skola) ameshaondoka tangu sa'9 alasiri kuelekea Arusha. Huku ni kuoneana, kosa letu ni Lipi"? Anamaliza Laurent ambae anasema alipewa jukumu la kuhamasisha watu wa kata yake ya Bomani. Source: Laurent Kiula Katibu-UVCCM BOMANI-KIOMBOI