Huku kukiwa na shamrashamra na nderemo Iramba Magharibi kusubiri ujio wa kihistoria wa Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa siku ya Jumamosi tayari hujuma zimeanza dhidi ya ziara hiyo.
Dr Slaa anatarajiwa kuhutubia mkutano mkubwa sana wa hadhara jimboni Iramba Magharibi siku ya Jumamosi kwa lengo la kukusanya maoni ya wananchi katika mabaraza ya Katiba ya CHADEMA.
Taarifa kutoka Iramba zinasema katika hali ya kutapatapa kudhibiti watu wasihudhurie mkutano huo,mbunge wa jimbo hilo Mwigulu Nchemba amealika timu ya Simba ya Dar es Salaam kumenyana na timu ya Polisi Jamii ya hapo Iramba kwa mechi ya kirafiki.Mechi hiyo itafanyika eneo jirani na muda huo huo atakaohutubia Dr Slaa.
Katibu mkuu huyo anatarajiwa kuwasili jimboni humo akitumia helikopta na maelfu ya watu wamejiandaa kumlaki na kutoa maoni yao ya Katiba mpya.
Kuna uhamasishaji mkubwa wa CHADEMA unafanyika hapa kumsikiliza Katibu Mkuu huyo ambaye kwa sasa ni kipenzi kikubwa cha watanzania.