ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,279
- 7,681
Kamanda ZeM, nina imani watu wengi tunahisi amefika hapo alipo kwa sababu waheshimiwa walitaka mtu asiye na uwezo wa kuwa-challenge, mtu wa 'yes' 'yes' na mtu wasiyemuhofia kwa lolote....
Frankly, sioni huyu Dr. Chein akipewa nafasi ya kugombea urais whether 2010, 2015 au muda wowote ule!
SHEIN FOR PRESIDENT 2015.
Ana sifa zote za kuwa kiongozi kwa nchi masikini kama Tanzania.
Ok mkuu kwa hiyo unaona anayefaa yuko nje ya serikali mkuu? Na kama siyo Shein kwa sasa unaona nani mwenye muelekeo wa kufaa kumpokea JK? Kwa sasa mimi naona upinzani kuchukua ni ndoto labda yatokee mabadiliko ya ghafla na ya uhakika otherwise yoyote tutake ishia kumchagua atakuwa ndani ya serikali au CCM. Hapa tuna badilishana mawazo tu ndiyo niya ya thread.
Inaelekea Shein ni mkimya sana. Makamo wetu wa raisi huyu kwangu mimi ndiye ninayeona anayefaa kuongoza nchi 2015. Hayupo kwenye spotlight sana kama viongozi wengine wakuu. Katika viongozi tulionao mimi naona huyu mzee ni moja kati ya waliyo bora maana haendekezi siasa za jukwaani. Sijui kwa nini yeye hatajwi kati ya moja ya watu wanaoweza kumrithi JK, labda mwenyewe hautaki uraisi. Ukilinganisha na viongozi wengine wanao tajwa tajwa sasa mimi naona so far namsupport Shein for 2015.
Sababu zangu ni zifuatazo.
1.Hajaonyesha tamaa wala uchu wa madaraka.
2.Hana skendo yoyote kubwa anayo tajwa kuhusika.
3.Haelekei kuwa na makundi
4.Ni mpole na hapendi spotlight kitu ambacho kinaweza kuashiria he is all action and no talk.
5.Tetesi niliyo sikiaga ni kwamba 2005 Kikwete alikua na mgombea mwenza wake mwenyewe lakini baada ya majadiliano wakaona kwamba Shein ndiyo anafaa kuwa kwenye tiketi ya chama.
Sijui kama mwenyewe ana ndoto za 2015 lakini kwenye kundi la sasa yeye anaonekana kufaa kuliko wenzie. Wanaweza kutokea wengine wanaofaa kabla ya 2015 ila kwa sasa nimemuona huyu. Haya ni maoni yangu tu wakuu sijui nyie mna semaje.
Ukilinganisha na viongozi wengine wanao tajwa tajwa sasa mimi naona so far namsupport Shein for 2015.
asante mkuu. Lakini bado sijapata kitu cha kushika hapo. Kama yeye ndiye anayemsaidia rais, anatakiwa anakolegea rais yeye apakazie. Sawa jamaa sio muongeaje, hiyo siyo sifa ya kuwa rais. Ni kipi hasa ambacho mtu anaweza akasema shein alikisimamia kikaa vizuri? Huyu mzee ni kama sumaye, japo yy anaweza akawa sio fisadi lakini hana ile drive na determination ya ku-dare mambo kwa maslahi ya taifa. Huyu alikuwa picked na mzee mkapa kwa maslahi binafsi kama alivyofanya kwa sumaye.
Tatizo anaweza akawa kondoo kabisa mafisadi wakatamalaki...bado nahitaji kuelimishwa tafadhali.
Kwa nini asiingie mwakani?
Nakubaliana na wewe.Ile ndio NCHI yake. Ingawa sina uhakika kama WANAMAPINDUZI DAIMA wa UNGUJA watamkubalia.Usianze balaa lako - Shein ni 2010 kule Zanzibar.
Eee Mola tuepushe!!!!Mwakani ataingia Edward Lowasa.
SHEIN FOR PRESIDENT 2015.
Ana sifa zote za kuwa kiongozi kwa nchi masikini kama Tanzania.Bongo hatuhitaji kiongozi mwenye mvuto ,tunaitaji kiongozi serious hakuna kuchekacheka ni kazi tuu kwa kwenda mbele.Mambo ya mivuto tuwaachie akina Obama, nchi yao tajiri
Hao waliopita na mivuto yao wamefanya nini zaidi ya ufisadi tuu.
SHEIN FOR PRESIDENT- 2015
Lakini............. tunahitaji Rais ambaye ''''''''''''''''''''', haijalishi kama ''''''''''''''''' ni chizi, ,,,,,,,,,, lazima Rais ajaye awe na level fulani ya uchizi.''''''''''''''''''