MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,565
- 836
Inaelekea Shein ni mkimya sana. Makamo wetu wa raisi huyu kwangu mimi ndiye ninayeona anayefaa kuongoza nchi 2015. Hayupo kwenye spotlight sana kama viongozi wengine wakuu. Katika viongozi tulionao mimi naona huyu mzee ni moja kati ya waliyo bora maana haendekezi siasa za jukwaani. Sijui kwa nini yeye hatajwi kati ya moja ya watu wanaoweza kumrithi JK, labda mwenyewe hautaki uraisi. Ukilinganisha na viongozi wengine wanao tajwa tajwa sasa mimi naona so far namsupport Shein for 2015.
Sababu zangu ni zifuatazo.
1.Hajaonyesha tamaa wala uchu wa madaraka.
2.Hana skendo yoyote kubwa anayo tajwa kuhusika.
3.Haelekei kuwa na makundi
4.Ni mpole na hapendi spotlight kitu ambacho kinaweza kuashiria he is all action and no talk.
5.Tetesi niliyo sikiaga ni kwamba 2005 Kikwete alikua na mgombea mwenza wake mwenyewe lakini baada ya majadiliano wakaona kwamba Shein ndiyo anafaa kuwa kwenye tiketi ya chama.
Sijui kama mwenyewe ana ndoto za 2015 lakini kwenye kundi la sasa yeye anaonekana kufaa kuliko wenzie. Wanaweza kutokea wengine wanaofaa kabla ya 2015 ila kwa sasa nimemuona huyu. Haya ni maoni yangu tu wakuu sijui nyie mna semaje.
Hivi kuna jambo gani ambaye amelifanya huyu mzee mpaka mkadhani anafaa kuchukua uongozi wa nchi? binafsi naona kama ni mtu ambaye ana kosa ushupavu wa kubeba mzigo mzito huu wa nchi masikini na iliyojaa ufisadi. Samahani lakini...mimi naona kama yupo yupo tu.....nielimisheni
nakupendekeza wewe naona unafaa zaidi
Heshima mbele mkuu. Makamu wa raisi kazi yake ni kumsaidia raisi. Kuna kazi ambazo raisi hawezi kuzifanya zote yeye atapewa na makamu wa raisi. Pia kuna wizara ambazo zipo chini yake. Wewe kwa nini unadhani anakosa ushupavu? Kwa sababu siyo muongeaji au haongei sana kwenye vyombo vya habari? Kumbuka ni makamo wa raisi na kuna mambo ambayo yana takiwa yashikiwe kidete na raisi mwenyewe kama hilo swala la ufisadi. Mimi jamaa naona ni all action and no talk siyo kama hawa wanasiasa wetu wengine ambao huongea sana lakini hauoni chochote.
Kwa nini asiingie mwakani?
Inaonekana wengi mnaona anafaa! jamani toeni elimu kwa wengine kama kweli ana mshiko....maana wengine tunamuona yupo yupo tu.Mkuu hii kama ni hoja mimi naunga mikono! Aingie mwakani kabsa.
Inaonekana wengi mnaona anafaa! jamani toeni elimu kwa wengine kama kweli ana mshiko....maana wengine tunamuona yupo yupo tu.
;;;;;;;;;;;;;;;.
Sababu zangu ni zifuatazo.
1.Hajaonyesha tamaa ;;;;;;;;;;;;;;;;;;;.
2.Hana skendo.......
3.Haelekei kuwa na makundi
4.Ni mpole .
5.Tetesi niliyo sikiaga ni kwamba 2005 Kikwete alikua na mgombea mwenza wake mwenyewe lakini baada ya majadiliano wakaona kwamba Shein ndiyo anafaa kuwa kwenye tiketi ya chama.
Haya ni maoni yangu tu wakuu sijui nyie mna semaje.
MWANAFALSAFA,
Mkuu, Hizo ndo sifa za Rais anaye faa Tanzania?
Mbona umerahisisha sana wadhifa huu?
Rais tunaye anayeifaa Tanzania ni yule mwenye mawazo ya kuibadilisha Tanzania kutoka katika uozo uliopo kuilekea katika maendeleo, na ambaye amejitokeza kuisemea Tanzania na serikali iliyoko madarakani.
Shein yuko katika serikali iliyoko madarakani, na anakubaliana nayo ndo maana bado yuko madarakani.
Shein is a good guy.
Anafaa kuongoza Tanzania......
PUMBA!!!!Mwinyi,Kikwete na Mkapa walifanya nini mpaka wakaweza kuchukua uongozi wa nchi.Fikiria kwanza kabla ya kuteremsha pumba zako hapa.Hivi kuna jambo gani ambaye amelifanya huyu mzee mpaka mkadhani anafaa kuchukua uongozi wa nchi? binafsi naona kama ni mtu ambaye ana kosa ushupavu wa kubeba mzigo mzito huu wa nchi masikini na iliyojaa ufisadi. Samahani lakini...mimi naona kama yupo yupo tu.....nielimisheni
Mkuu, sijui una maana gani haswa kusema Shein is a good guy...so, anafaa kuongoza Tanzania.
Nadhani Tanzania inahitaji Rais shupavu, mwenye vision, anayejua tatizo letu hasa ni nini, mwenye ushujaa wa kuchagua watu makini wa kumsaidia katika vita ya kuondoa umaskini na ufisadi na mwenye nguvu na uwezo wa kufanya maamuzi mazito wakati wowote bila kumuogopa mtu yeyote.
Shein, kwa mtazamo wangu, hana sifa hizo.
Hana mvuto na kama vile yupo yupo tu. Kwa uelewa wangu mdogo, naona tungekuwa fine tu hata kama cheo cha makamu wa rais kingefutwa. Sasa sijui ni kutokana na udhaifu wa mzee huyu au system iliyopo imemfanya mzee kufichwa
Watu wanaomfahamu wanajua kuwa ana mvuto ndio maana amefika pale alipo hivi sasa.
..hata ziara zake za mikoani viongozi wa huko wanamuogopa yeye kuliko wengine wote, heshima yake iko juu.