Mwana Mpotevu
Platinum Member
- Sep 7, 2011
- 3,295
- 2,500
Taarifa nilizozipata hivi punde ni kwamba waziri Mansoor Himid (CCM) ambaye alikuwa waziri asiyekuwa na wizara maalum, ametimuliwa uwaziri na Rais wa Zanzibar Dr Shein.
Kisa cha kutimuliwa ni kutokana na msimamo wake wa kutaka muuungano wa mkataba jambo ambalo ni kinyume na sera za CCM za serikali mbili.
Nitawapeni taarifa zaidi
Kama wazenj wamechoka na neema toka bara si muwaache wende zao? Nadhani Shein analijua hili. Hataki hawa wanaopiga kelele baadaye wamsumbue wakilia lia baada ya kupata kitu tofauti na walivyodanganywa baada ya muungano kuvunjika. Watu wengine hata hawafikirii vizuri. Hivi zenj bado haioni inavyobebwa kwa kipande cha ardhi kisicholingana na hata wilaya ya kibaha kupewa hadhi ya nchi?

Ataingia uamsho kwa nguvu zaidi huku akijipalia makaa..kazi ipo vuguvugu si dogo ati Shein ajipange sana kwa mapambano maana adui yake hawezi kumjua kwa sasa wako wengi chini kwa chini
Shein kampiku mr. Dhaifu. Mfano hai wa maamuzi magumu.
Wakati huo huo.....
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete anaanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku nne katika Taifa la Kifalme la Oman, ikiwa ni ziara ya kwanza ya Kiserikali kufanywa na Rais wa Tanzania katika nchi hiyo.
Rais Kikwete na ujumbe wake ameondoka mjini Dar es Salaam asubuhi ya leo, Jumatatu, Oktoba 15, 2012, kwenda Oman kuanza ziara hiyo inayofanyika kwa mwaliko wa Kiongozi wa Ufalme wa Oman, Mfalme Qaboos bin Said, ambaye atakuwa mwenyeji wake kwa siku zote nne.
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Muscat, Rais Kikwete anatarajiwa kulakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Mheshimiwa Yousef bin Abdullah bin Alawi ambaye ataandamana naye hadi Jumba la Muscat Gate ambako Rais atapokelewa na Mfalme Qaboos. Kutoka hapo wataandamana hadi Kasri ya Kifalme ya Al Alam ambako atapokelewa rasmi kwa heshima zote za Kiserikali.
Shughuli kubwa ya jioni ya leo ya Mheshimiwa Rais itakuwa ni kufanya mazungumzo rasmi ya Kiserikali kati ya Serikali za Tanzania na Ufalme wa Oman na pia kuhudhuria dhifa rasmi ambayo Mfalme Qaboos atamwandalia mgeni wake kwenye Kasri ya Al Alam.
Kesho, Jumanne, Oktoba 16, 2012, Rais Kikwete atatembelea Jumba la Makumbusho la Majeshi ya Ulinzi ya Oman, atafungua Mkutano wa Wafanyabiashara wa Tanzania na Oman, atashuhudia utiaji saini makubaliano ya mikataba miwili kati ya nchi hizo mbili, ukiwamo ule wa kuundwa kwa Baraza la Biashara la Tanzania na Oman na ule wa Kuendeleza na Kulinda Uwekezaji katika nchi hizo mbili.
Jioni, Rais Kikwete atatunukiwa nishani ya juu kabisa ambayo Ufalme wa Oman hutoa kwa viongozi wa nchi za nje ya First Order Medal kwenye Chakula Maalum cha Usiku kitakachoandaliwa na Mfalme Qaboos kwa heshima ya Rais Kikwete.

I hope it is true kwani mkala yangu ya mwishi ilimtaja Shein kuwa Anawaendekeza. Wakitaka muungano wa mkataba watoker ccm na cuf kwanza halafu waanze harakati za kudai uhuru. Lazima afuatie mwanasheria mkuu wa Zanzibar naye.