Dr Shein amtimua kazi Waziri Himid! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr Shein amtimua kazi Waziri Himid!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana Mpotevu, Oct 15, 2012.

 1. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #1
  Oct 15, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Taarifa nilizozipata hivi punde ni kwamba waziri Mansoor Himid (CCM) ambaye alikuwa waziri asiyekuwa na wizara maalum, ametimuliwa uwaziri na Rais wa Zanzibar Dr Shein.

  Kisa cha kutimuliwa ni kutokana na msimamo wake wa kutaka muuungano wa mkataba jambo ambalo ni kinyume na sera za CCM za serikali mbili.

  Nitawapeni taarifa zaidi

  Updates:

  Ni kweli.

  Shein afanya mabadiliko katika Baraza la Mapinduzi

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt Ali Mohammed Shein amefanya mabadiliko katika Baraza la Mapinduzi. Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Abdulhamid Yahya Mzee imesema katika mabadiliko hayo, Rais Dkt Shein amemteua Shawana Bukheti Hassan kuwa mjumbe wa Baraza la Mapinduzi.

  Rais Dkt Shein amefuta uteuzi wa mjumbe wa Baraza la Mapinduzi, Mansoor Yussuf Himid.

  Katika uteuzi mwengine Dkt Shein amewateua Mtumwa Kheir Mbarak kuwa Naibu Waziri wa Kilimo na Maliasili na Mohammed Said Mohamed kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi. Katika hatua nyengine, Rais Dkt Shein amefanya mabadiliko ya baadhi ya Makatibu Wakuu katika Wizara za Miundombinu na Mawasiliano, Wizara ya Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati.

  Dkt. Juma Malik Akili ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano akichukua nafasi ya Dkt. Vuai Idd Lila atapangiwa kazi nyengine. Ali Khalil Mirza ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati.
  Kabla ya uteuzi huo, Mirza alikuwa Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar,aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Mwalimu Ali Mwalimu atapangiwa kazi nyengine.

  Taarifa ya Ikulu imesema pia Rais Dkt Shein amemteua Tahir M. Abdulla kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano,aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Msanif Haji Mussa atapangiwa kazi nyengine.
  Uteuzi mwengine ni Mustafa Aboud Jumbe ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo alikuwa Tahir M Abdulla ambaye amehamishiwa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano.

  Rais Dkt Shein ameteua CDR Julius Nalim Maziku kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kapteni Juma Abdulla Juma ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar hivi karibuni.

  Uteuzi mwengine ni Juma Ameir Hafidh ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais(Fedha,Uchumi na Mipango ya Maendeleo) ambaye amechukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Abdi Khamis Faki aliyeteuliwa kuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar.

  Aidha, aliyepata kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar, Saleh Ramadhan Ferouz ameteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar ambaye anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Ali Khalil Mirza aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Makaazi,Maji na Nishati.

  Pia Rais Dk Shein amemteua Mussa Haji Ali kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu uchumi Zanzibar. Uteuzi huo wote unaanza Oktoba 15 mwaka 2012.

  Thanks EMT for this


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Muungano wa mkataba mara ngapi?

  Hata muungano wa sasa ni wa mkataba, mkataba ni katiba na articles za muungano.

  Semeni katika mkataba mnataka nini?
   
 3. s

  sambamba Senior Member

  #3
  Oct 15, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  zanzibar juuuuuuuuuuuuuuuu!
   
 4. Gogo la choo

  Gogo la choo JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 8, 2012
  Messages: 714
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Naona mait inamuuguza mgojwa..wavunje hilo liimungano lao..cc tunafanya ya kwetu tu..!!
   
 5. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kama wazenj wamechoka na neema toka bara si muwaache wende zao? Nadhani Shein analijua hili. Hataki hawa wanaopiga kelele baadaye wamsumbue wakilia lia baada ya kupata kitu tofauti na walivyodanganywa baada ya muungano kuvunjika. Watu wengine hata hawafikirii vizuri. Hivi zenj bado haioni inavyobebwa kwa kipande cha ardhi kisicholingana na hata wilaya ya kibaha kupewa hadhi ya nchi?
   
 6. m

  malaka JF-Expert Member

  #6
  Oct 15, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Heheh. CCM bana. Inakimbia kivuli chake. Ila poa tu liwalo na liwe style.
   
 7. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #7
  Oct 15, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,312
  Likes Received: 5,599
  Trophy Points: 280
  Ataingia uamsho kwa nguvu zaidi huku akijipalia makaa..kazi ipo vuguvugu si dogo ati Shein ajipange sana kwa mapambano maana adui yake hawezi kumjua kwa sasa wako wengi chini kwa chini
   
 8. K

  KITEKSORO Senior Member

  #8
  Oct 15, 2012
  Joined: Sep 25, 2012
  Messages: 156
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Hata hivyo hakuwa na wizara maalumu so he was just a political prostitute!
   
 9. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #9
  Oct 15, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Na huyu waziri ni ndugu wa damu na Shadya Karume
   
 10. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #10
  Oct 15, 2012
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Kupewa hazi ya nchi na nani?

  Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
   
 11. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #11
  Oct 15, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Jussa naye ni mpiga debe mkuu wa hili, dawa yake huenda inachemmka maana la CCM ndio la CUF
   
 12. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #12
  Oct 15, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Shein kampiku mr. Dhaifu. Mfano hai wa maamuzi magumu.
   
 13. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #13
  Oct 15, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Naona hapo ndiyo wameshawasha moto, itabidi watimuliwe wengi kama ndiyo hivyo sasa.
   
 14. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #14
  Oct 15, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,315
  Likes Received: 19,463
  Trophy Points: 280
  si waaliichagua ccm wenyewe..?
   
 15. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #15
  Oct 15, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Wakati huo huo.....


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete anaanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku nne katika Taifa la Kifalme la Oman, ikiwa ni ziara ya kwanza ya Kiserikali kufanywa na Rais wa Tanzania katika nchi hiyo.

  Rais Kikwete na ujumbe wake ameondoka mjini Dar es Salaam asubuhi ya leo, Jumatatu, Oktoba 15, 2012, kwenda Oman kuanza ziara hiyo inayofanyika kwa mwaliko wa Kiongozi wa Ufalme wa Oman, Mfalme Qaboos bin Said, ambaye atakuwa mwenyeji wake kwa siku zote nne.

  Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Muscat, Rais Kikwete anatarajiwa kulakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Mheshimiwa Yousef bin Abdullah bin Alawi ambaye ataandamana naye hadi Jumba la Muscat Gate ambako Rais atapokelewa na Mfalme Qaboos. Kutoka hapo wataandamana hadi Kasri ya Kifalme ya Al Alam ambako atapokelewa rasmi kwa heshima zote za Kiserikali.

  Shughuli kubwa ya jioni ya leo ya Mheshimiwa Rais itakuwa ni kufanya mazungumzo rasmi ya Kiserikali kati ya Serikali za Tanzania na Ufalme wa Oman na pia kuhudhuria dhifa rasmi ambayo Mfalme Qaboos atamwandalia mgeni wake kwenye Kasri ya Al Alam.

  Kesho, Jumanne, Oktoba 16, 2012, Rais Kikwete atatembelea Jumba la Makumbusho la Majeshi ya Ulinzi ya Oman, atafungua Mkutano wa Wafanyabiashara wa Tanzania na Oman, atashuhudia utiaji saini makubaliano ya mikataba miwili kati ya nchi hizo mbili, ukiwamo ule wa kuundwa kwa Baraza la Biashara la Tanzania na Oman na ule wa Kuendeleza na Kulinda Uwekezaji katika nchi hizo mbili.

  Jioni, Rais Kikwete atatunukiwa nishani ya juu kabisa ambayo Ufalme wa Oman hutoa kwa viongozi wa nchi za nje ya First Order Medal kwenye Chakula Maalum cha Usiku kitakachoandaliwa na Mfalme Qaboos kwa heshima ya Rais Kikwete.
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Oct 15, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  I hope it is true kwani mkala yangu ya mwishi ilimtaja Shein kuwa Anawaendekeza. Wakitaka muungano wa mkataba watoker ccm na cuf kwanza halafu waanze harakati za kudai uhuru. Lazima afuatie mwanasheria mkuu wa Zanzibar naye.
   
 17. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #17
  Oct 15, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Very true mkuu
   
 18. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #18
  Oct 15, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Rekebisha kwenye red: Mwl Nyerere, mwaka 1985 na miezi michache kabla ya kuondoka madarakani alifanya ziara ya kiserikali nchini Oman.
   
 19. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #19
  Oct 15, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  naona tumekluwa na rais wa kuhudhuria dhifa za kitaifa ugenini kila wiki as if nyumbani ugali hakuna, simtofautishi na mtoto mdogo anayekataa kurudi kwao ili mradi kaona kwa jirani kuna chakula kitamu anachokipenda kimepikwa, hivyo hulazimika kusubiri hadi wapakue
   
 20. F

  FJM JF-Expert Member

  #20
  Oct 15, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mwanasheria mkuu wa Zanzibar ndiye alistahili kuangaliwa kwanza halafu ndiyo wengine wafuate. Huyo amekuwa anawapotosha watu na kwasababu ya cheo chake (mwanasheria mkuu) watu wanadhani anajua anachoongea. Ni yeye alikuja na hoja za muungano wa mkataba kama wa Swiss! Swiss?!
   
Loading...