Dr Shein amtimua kazi Waziri Himid!

Dr Shein amtimua kazi Waziri Himid!

naona tumekluwa na rais wa kuhudhuria dhifa za kitaifa ugenini kila wiki as if nyumbani ugali hakuna, simtofautishi na mtoto mdogo anayekataa kurudi kwao ili mradi kaona kwa jirani kuna chakula kitamu anachokipenda kimepikwa, hivyo hulazimika kusubiri hadi wapakue
kwa jirani kuna ubwa kwa mharage ya mbeya
 
Nadhani watu wataanza kuelewa Jussa alichokiongea kwenye interview ya CNN, inside afrika, nimepost hapa asubuhi, jamaa anasema zanzibar huru wanaodai ni ccm, pamoja na cuf, so najua Jussa alukuwa anaelewa kuna namba kubwa tu ya wana ccm zanzibar wanaunga mkono ili, so siyo huyo mmoja tu wapo wengi.

Hivi tunawabembeleza wa nini? si waende na nchi yao hawa jamaa??
 
.......mabadiliko ya tabia nchi yanaendelea na mchakato wa kukitafuna kisiwa....suala ni muda...inayoitwa nchi haitakuwapo !
 
kikwete urudi na wanyama wetu siyo utulete story za kusaini mikataba na kutupa matumaini..njoo na raslimali zetu tutakuelewa..
 
Taarifa za magazeti asbh hii nimesikia sheni kafanya mabadiliko kwenye baraza la mawaziri kwa kumwondoa waziri machachari aliyejiweka wazi kutotaka muungano mansour yusuf himid. Hii ina maana gani thinkers?
 
Taarifa za magazeti asbh hii nimesikia sheni kafanya mabadiliko kwenye baraza la mawaziri kwa kumwondoa waziri machachari aliyejiweka wazi kutotaka muungano mansour yusuf himid. Hii ina maana gani thinkers?

Charity begins at home. Tuanze na wewe unaionaje hii?
 
Huo ni mpango kabambe wa kuzima hoja ya muungano wa mkataba. CUF walianza na Jussa, CCM wamemamila na huyu waziri
 
Asante kwa taarifa, ila tu umeniondolea munkari (You have bored me) unapotaja Rais Doctor Shein.

Hivi ni kwa nini mnapenda sana kulazimisha hivi vitu. Ingefaa zaidi basi ungesema Rais Shein, au basi Doctor Shein bila kurudiarudia hiyo Rais Doctor Shein.
 
Asante kwa taarifa, ila tu umeniondolea munkari (You have bored me) unapotaja Rais Doctor Shein.

Hivi ni kwa nini mnapenda sana kulazimisha hivi vitu. Ingefaa zaidi basi ungesema Rais Shein, au basi Doctor Shein bila kurudiarudia hiyo Rais Doctor Shein.

Pole kiongozi lakini ni afadhali huyu ni DR wa kusomea kule yule wa magogoni anayelazimisha U-DR wa heshima nae aitwe hivyo
 
Huo ni mpango kabambe wa kuzima hoja ya muungano wa mkataba. CUF walianza na Jussa, CCM wamemamila na huyu waziri

Muungano wa mkataba ni nini???? JUSA kashindwa kuufafanua mbele ya Warioba, hebu jaribu wewe mkuu kutuelewesha basi
 
Muungano wa mkataba ni nini???? JUSA kashindwa kuufafanua mbele ya Warioba, hebu jaribu wewe mkuu kutuelewesha basi[/QUOTE
Kabla sijakuelewesha maana ya muungano wa Mkataba, nitaanza kufafanua maana ya neno MKATABA
Mkataba ni makubaliano/maafikiano(either kisheria or no) baina ya mbande mbili au zaidi zinapoamua kufanya jambo moja pamoja. Sasa katika hayo makubaliano kunakuwa na terms/conditions ambazo pande zote mbili lazima izifuate.
Muungano wa Tanzania na Zanzibar sio wa mkataba sababu unatawaliwa na matakwa ya wanauchu wa madaraka wa CCM. Leo wakiona mambo yanawaendea vizuri basi hufanya hivi (Mfano mwanzoni ilikuwa kama Rais akitoka Bara, makamu lazima atoke Zanzibar, lakini walipoona CUF inanguvu wakabadili hiki kifungu bila ya matakwa ya wananchi wa pande mbili) laa hufanya vinginevyo. Muungano umekuwa hauleti maana kama Umoja wa CCM na CUF Zanzibar nayo ni mtafaruku vilevile.
Mkataba unaotakiwa ni kufuata makubaliano yote kama tutakapokubaliwa no matter what? huo ndio mkataba ninaoongelea mimi. Pia lazima muungano uwe either serikali MOJA or TATU na lazima uwe wa Uwazi na sio watu wawili wakae chumbani kutumbangia mamilioni ya watanzania kama tulivyoona MUAFAKA wa CCM na CUF
 
Wednesday, October 17, 2012

headline_bullet.jpg
Aondolewa rasmi madarakani
headline_bullet.jpg
Alikaidi, akakejeli sasa yamkuta



Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed, Shein, amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri na kumuondoa aliyekuwa Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum, Mansoor Yussuf Himid.

Kwa mujibu wa Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Rais Dk Shein, amemteua Shawana Bukheti Hassan, kuchukua nafasi ya Himid.

Taarifa hiyo haikueleza sababu za kuondolewa kwa Himid katika nafasi hiyo, ingawa wachambuzi wameitafsiri hatua hiyo na msimamo aliouonyesha karibuni wa kutoa maoni ya kuukosoa muundo na mfumo wa Muungano.

Akichangia maoni ya Katiba mpya hivi karibuni, Mansour alisema kuwa Muungano wa sasa unakabiliwa na kasoro nyingi na kupendekeza uanzishwe muungano wa mkataba unaopigiwa debe na Chama cha Wananchi (Cuf).



Mansour alisema pamoja na kwamba msimamo wake ni kuendelea kuwepo kwa muungano wa mfumo wa serikali mbili, lakini Muungano huo unapaswa uwe wa mkataba ili Zanzibar ipate maendeleo ya kiuchumi.

Mansour ambaye ni mtoto wa mmoja wa waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar, Marehemu Yusuf Himid, alisema wazi wazi kuwa halitakuwa jambo baya chini ya Muungano wa mkataba ikiwa kila upande yaani Tanzania Bara na Zanzibar kuwa na kiti chake katika Umoja wa Mataifa (UN).

Alisema haogopi kutokana na maoni aliyoyatoa kwa kuwa ni haki yake na kwamba hata akiadhibiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana na maoni hayo, atakuwa tayari kukabiliana na adhabu yoyote.

Baada ya kauli yake, wanasiasa mbalimbali wa Zanzibar walimtuhumu (Mansour) na wanachama wengine wa CCM ambao walitoa maoni yanayokinzana na sera ya chama hicho ya Muungano wa serikali mbili.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, alisema kuwa mwanachama yeyote wa CCM anayepinga mfumo wa serikali mbili ajiondoe ndani ya chama hicho, vinginevyo atanyang'anywa kadi.

Wakati wa mkutano wa Tisa wa Bunge, Wabunge wa CCM Zanzibar wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Mohamed Saif Khatibu, waliitisha mkutano wa waandishi wa habari na kukitaka chama hicho kuwashughulikia wale wote watakaotoa maoni tofauti na msimamo wa CCM kuhusu Muungano.






 
Kwahiyo Mr. HIMID ni Mtoto wa MUASISI wa ASP? How nice... KIKULACHO KI' NGUONI MWAKO...
Kwanini kuteuana? CCM - CULT!!!
 
wapewe visiwa vyao wao wanadhani tunawamalizia samaki wao
 
Muungano wa mkataba mara ngapi?

Hata muungano wa sasa ni wa mkataba, mkataba ni katiba na articles za muungano.

Semeni katika mkataba mnataka nini?

Na ndoa yao (muungano a.k.a serikali ya umoja wa kitaifa toa vyama vingine vya upinzani) na CUF ni mkataba pia.Sijui itakuweje washinde wengine kwa jamhuri huo umoja utakufa?
 
Back
Top Bottom